Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Jan 7, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Nafasi ya uongozi (UBUNGE) kama ya kina Waheshimiwa Mnyika, Mtemvu, Ndungulile, Zungu, ni moja na nafasi za juu sana za uongozi katika Jamhuri yoyote ile. Wabunge wanawakilisha MATUMAINI, HOFU, SHABAHA na KIU ya wananchi. Ndio maana nafasi hii inahitaji utashi wa hali ya juu. Mbunge anatakiwa awe na sifa za ‘kiongozi bora' (sio ‘bora kiongozi'), vinginevyo ataishia kuwa kiongozi mpotoshaji, na anayeongoza au kutoa maamuzi kwa kufuata upepo, huruma kwa wapiga kura wake, pamoja na ‘maslahi binafsi'. Mbunge anatakiwa awe na sifa pamoja na:

  · Consistency au uthabiti katika maamuzi na utendaji, na sio leo hili, kesho lile.
  · Upeo na uelewa wa mambo anayoyasimamia au zungumzia kwenye umma.
  · Ujasiri wa kuwaambia hali halisi wapiga kura wake, bila ya uwoga.
  · Uwezo wa kutofautisha baina hoja/maamuzi ya kisiasa na yale ya kimantiki.
  · Msimamo usiobadilika/kuyumba kutokana na upepo wa kisiasa.
  · Ujasiri wa kusimamia kitu anachokiamini/maamuzi magumu.
  · Uwezo wa kufikiri kabla ya kufanya maamuzi muhimu/kutoa kauli au msimamo mbele ya umma.

  Katika sakata la Magufuli na nauli feri, ni dhahiri kwamba wabunge wetu hawa - Waheshimiwa Mnyika, Mtemvu, Zungu, Ndugullile, Mnyika na wengineo, wamepwaya katika sifa nyingi hizi. Kwa nafasi zao, wameonyesha ukosefu wa uthabiti (consistency) katika kauli/maamuzi yao, wamekosa upeo, wamekosa ujasiri wa kuwaambia ukweli wapiga kura wao bila ya uwoga, washindwa tofautisha hoja/maamuzi ya kisiasa na ya kimantiki, wameji expose kwenye mazingira ya kuweza badili misimamo yao siku za mbeleni, wameshindwa kuwa na ujasiri wa kuunga mkono maamuzi ya kimantiki ya magufuli, na wameshindwa kufikiri kwanza kabla ya kutoa kauli nzito kwa umma/wapiga kura wao. Ndio maana, kwa haya yote, Magufuli amewapiku, ingawa wanajidanganya mbele ya umma, kwamba wao ndio wapo sahihi, na magufuli ndio hayupo sahihi. Nitafafanua.

  Feri ya Kigamboni ni kivuko ambacho kinaendeshwa kwa ruzuku kubwa sana ya serikali (yani government subsidy). Sina uhakika kama waheshimiwa wetu hawa wanalielewa hilo. Vinginevyo watumiaji wa kivuko kile wangekuwa wanalipa nauli kubwa sana kama kivuko kingekuwa kinaendeshwa na sekta binafsi, au hata kwa ubia kati ya sekta binafsi na serikali (yani Public –Private Partnership).

  Waheshimiwa wabunge Mnyika na wengineo, kwenye sekta ya usafiri wa umma (madaladala) ambayo ipo chini ya soko huru, na kusimamiwa na Sumatra, mtumiaji wa chombo cha usafiri (daladala) kutokea Feri hadi Posta, anatozwa shillingi 300 (mia moja zaidi ya nauli ya Feri ya sh.200). Ikumbukwe kwamba umbali kutoka Feri Hadi Posta ni kama Kilometa 3, hivyo mtu ukiamua kutembea, unaweza kufanya hivyo. Kwa maana nyingine, ni hiyari kwa mtu kulipa nauli ya sh. 300 au kutembea. Lakini wengi huwa wanaamua kulipa sh.300, na shughuli za uchumi zinaendelea.

  Lakini suala la kivuko cha ferry ni tofauti. Kivuko cha Feri hakiendeshwi na kanuni za soko huria. Umbali wa kivuko kile ni takribani kilometa moja kutoka upande mmoja hadi mwingine. Na tofauti na umbali kutoka Feri hadi posta ambao mwananchi ana hiyari ya kuchagua kati ya kutembea au kulipa nauli ya dala dala ya sh. 300, mwananchi hana hiyari kuchagua kupanda pantoni au kuongelea. Hivyo, lazima mwananchi alipe shillingi 200 kuvuka upande wa pili. Lakini ni muhimu nikasisitiza hili: miaka ya nyuma, serikali ilikuwa inatoa huduma ya kivuko kuanzia asubuhi hadi saa sita usiku. Lakini kwa sababu ya kujali wananchi wake, ikaamua huduma ile itolewe masaa 24. Tusisahau kwamba huduma hii ilitolewa kwa masaa 24 kwa kipindi kirefu sana kwa nauli ya shillingi 100. Na pia tusisahau kwamba pantoni lile likiwashwa asubuhi, halizimwi tena, hivyo kupelekea gharama za uendeshaji kuwa kubwa mno, in terms of fuel consumption (mafuta ya diesel). Sasa katika mazingira haya, Mheshimiwa Mnyika na wengine, tatizo lipo wapi serikali ikiamua kuongeza nauli kwa shillingi mia moja?

  Waheshimiwa wabunge Mnyika na wengineo, tuseme basi serikali inajitahidi kukamilisha daraja la kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa eneo lile. Je, mtakuwa na consistency katika hoja zenu? Kwani ni dhahiri kwamba, Daraja likikamilika leo, litakuwa na urefu wa kilomita sio chini ya saba (kati ya 7-10), na ramani zinaonyesha kwamba litaanzia maeneo ya Kurasini na Kushukia maeneo ya Kibada. Umbali huu wa kilometa saba, ni karibia mara saba ya umbali kutokea Feri hadi Posta ambako watu wanalipa nauli ya daladala sh.300. Daraja likikamilika, ni wazi usafiri kwa umma kutoka kurasini (DSM) hadi kibada (kigamboni), utaendeshwa chini ya kanuni za soko huria (madaladala), na wasafiri watalipa sio chini ya sh.300. Muhimu zaidi ni kwamba wananchi watakuwa na uhuru wa kuchagua kutumia daladala (chini ya soko huria) au pantoni (iwapo economics za pantoni zitakuwa bado zinaruhusu). Je, waheshimiwa wabunge, tuseme kwamba wananchi wafanye mgomo juu ya nauli ya kuvuka daraja kwa daladala (chini ya kanuni za soko huria) kwa sh. 300 au zaidi, mtakuwa upande gani, wa Sumatra au Wananchi? Ikumbukwe pia kwamba hili daraja kushukia Kibada haina maana msafiri amekamilisha safari yake kwenda upande wa pili wa feri, kwani umbali kutokea Kibada hadi upande wa pili wa feri (kigamboni) ni karibia kilometa 18. Sasa ukimjulisha umbali wa kivuko cha daraja (kilometa 7) na umbali wa Kibada hadi upande wa pili wa feri (kilometa 18), tunapata jumla ya umbali wa kilometa sio chini ya 25. Je, nauli mpya ya daladala chini ya soko huria kwa umbali wa kilometa 25 itakuwa sh 200 kama ya kivuko? Jibu ni hapana.

  Waheshimiwa wabunge, kuna wakati bunge letu tukufu liliunda kamati maalumu kuchunguza gharama za uendeshaji wa kivuko cha kigamboni ili kubaini changamoto zilizopo, lengo likiwa ni kutafuta njia za kuboreshwa huduma ile kwa wananchi. Nyinyi kama wabunge mlikuwepo bungeni kuweza kuhoji mengi sana, lakini hamkufanya hivyo, na badala yake mnakuja kuyahoji masuala ya mapato barabarani. Kwa mfano, ripoti ya bunge ilibaini kwamba mapato kwa siku ni 9,000.000 (shillingi milioni tisa - enzi za nauli ya shillingi 100); Ripoti ile ikaendelea kusema kwamba ziada (yani surplus) kwa mwezi ni shillingi milioni tano. Lakini kamati ile haikutoa takwimu juu ya gharama za uendeshaji, na badala yake, ikatoa taarifa za masalio kwa mwezi. Sasa hoja yenu kwamba kuna ufisadi katika ukusanyaji wa mapato, kwanini hamkuijadili bungeni wakati kamati ile inatoa ripoti yake? Waheshimiwa wabunge, mngekuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuhoji ongezeko la Magufuli la sh 200 leo iwapo tu mngekuwa makini bungeni, kuhoji takwimu juu ya gharama za uendeshaji kwa siku katika kivuko cha ferry ni zipi. Au pengine hamkuwepo bungeni, au hamkuwa na upeo wa mbali, vinginevyo mlipoteza fursa nzuri sana, ambayo ingeweza kutuokoa na sakati hili linalochanganya wananchi. Wapiga kura wenu ni muhimu wakagundua uzembe wenu huu.

  Kwa vile kamati ya bunge haikutoa takwimu juu ya gharama, nimejaribu kutumia nyingine ili angalau tupate makisio ya gharama kwa siku na kubaini yafuatayo i.e. if we work backwards: Mapato kwa siku sh. 9,000,000 (chini ya nauli ya sh.100) ; Masalio (surplus) kwa mwezi, sh.5, 000,000 (chini ya nauli ya sh.100). Hii ina maana kwamba masalio/surplus kwa siku ni Sh. [5,000,000] GAWANYA KWA [SIKU 30[, ambayo inatupa Sh. 166,666 kama masalio/surplus kwa siku. Hivyo basi, gharama kwa siku itakuwa: [Sh. 9,000,000] TOA [Sh. 166,666], ambayo ni sawa na na Sh. 8,833,333 kwa siku.

  Waheshimiwa wabunge, kwa kutumia simple economics peke yake – gharama za kuendesha kivuko hiki ni 98% ya mapato kwa siku. Sasa tukianza kuangalia suala la kupanda kwa gharama za bidhaa muhimu kama mafuta n.k, JE, ni haki kweli kumshambulia magufuli, kisa, amepandisha nauli kwa sh. 100, hivyo kufanya masalio kwa siku yawe sh.333, 332 (laki tatu), badala ya Sh. 166,666? Inawezekana kinachoogopesha wabunge hapa ni the fact kwamba nauli imepanda kwa asilimia 100, kwani ulilitazama suala hili ki-asilimia, bila ya kuwa makini, kitakwimu, ongezeko la asilimia 100 ni kubwa sana. Vinginevyo, kwa sasa, shillingi mia moja ya kitanzania ni karibia na SENTI SITA katika dollar za kimarekani. Waheshimiwa, sote tunajua jinsi gani bei ya mafuta katika soko la dunia imekuwa inaongezeka kila kukicha. Serikali ilianza kutoa huduma ya kivuko kwa masaa 24 kwa kipindi kirefu sana kwa nauli ya Sh.100. Je, mnajua ilikuwa inatoa ruzuku kiasi gani? Na imechukua muda mrefu sana kabla serikali kupandisha nauli kwa shilling mia zaidi (sawa na SENTI SITA za kimarekani), katika kipindi ambacho bei ya mafuta duniani imepanda kwa mamia zaidi, ya hiyo senti sita ya dollar.

  Kuna hoja pia kwamba Magufuli hakufuata Sheria, Je ni sheria ipi iliyo muhimu zaidi ya ile iliyopitishwa na Bunge ambalo nyinyi ni wawakilishi wetu - THE FERRY ACT ambayo ukiitazama, utabaini kwamba Magufuli na washauri wake, wameifuata mstari kwa mstari kabla ya kufikia uamauzi wa kuongeza nauli kwa shillingi 100? Waheshimiwa, na hasa John Mnyika - ambapo Ubungo ni Jimbo lako, kwanini haufuatilii suala la Kituo cha mabasi cha ubungo ambako kuna usumbufu na gharama zisizo na sababu kwa wananchi, pengine kuliko suala la kigamboni? Mfano, ili mtu uingie kituo cha ubungo kwa mguu, kwa dakika moja tu kumsindikiza ndugu yako anaesafiri ambae anahitaji msaada kwa sababu ya uzee, au ulemavu au umri mdogo (mtoto wa shule), unatozwa sh 200, je hamuoni kwamba hili nalo ni tatizo? Au ni kwa sababu, tofauti na mapato ya ferry ambayo hayapo chini ya manispaa, mapato ya Ubungo yapo chini ya manispaa ambako kwa nafasi zenu kama wabunge, mnakaa kwenye VIKAO kama madiwani kupitia/kupanga bajeti, na kula posho za vikao?

  Kwanini huwa amhoji sheria zinazotumika na Sumatra kupandisha nauli za daladala ovyo? Au ni kwasababu mna imani kubwa sana kwamba soko huria huwa halifanyi makosa, na badala yake makosa hufanywa na serikali tu? Ni dhahiri kwamba kwenye usafiri wa umma ulio chini ya soko huria (daladala), wapo waheshimiwa wengi wenye maslahi binafsi. Vinginevyo, hata kwenye suala la nauli za mateksi, bajaji, ilitakiwa wabunge pia waibane serikali isimamie hilo, sio kuwaachia wamiliki wa vyombo hivi kuwaburuza wananchi watakavyo. Hata nchi za wenzetu, nauli za mateksi sio za makisio, ni kwa mujibu wa sheria.

  Ushauri:
  · Ongezeni juhudi katika kujenga hoja zenye mantiki, na mjifunze umuhimu wa kukwepa maamuzi ya kisiasa pale pasipotakiwa, vinginevyo mtachanganya wananchi.
  · Elimisheni wapiga kura wenu kwamba uamuzi wa Magufuli ni sahihi, na toeni ahadi kwao kwamba mkienda bungeni mwisho wa mwezi huu, mtaenda kuhoji kamati husika kuhusu suala ambalo mlilizembea kweney vikao vilivyopita - takwimu juu gharama za uendeshaji wa pantoni kwa siku, ili muwe na legitimacy ya kuhoji mnayohoji leo juu ya shilling 200, vinginevyo, hamna that legitimacy as we speak.
  · Ibabeni serikali juu ya misamaha ya kodi kwa mwaka ambayo inakaribia asilimia 20 ya bajeti nzima ya mwaka, na muelekeze suala la subsidy ya kigamboni huko, sio kwa magufuli.
  · Litazameni suala la market failure kwa makini ili muelewe mapungufu, sio juu ya Ferry pekee, bali hata madala dala, bajaji, na mateksi.
  · Vinginevyo, kama hamridhiki, nyinyi ndio watungaji wa sheria zetu, fuateni ushauri wa Magufuli kwamba, pengine Manispaa zichukue jukumu la kuendesha Ferry ili muelewe economics zake, kwani huko mkiwa kama sehemu ya madiwani, pengine mtatusaidia kutuondolea siasa kwa jambo ambalo limejaa mantiki tupu.
  · Na Mwisho, Magufuli anastahili kuomba msamaha kwa kauli zake zilizokosa ustaarabu, lakini hastahili kubadilisha msimamo juu ya ongezeko la nauli, kwani uamuzi wake ni sahihi.
   
 2. Painstruth

  Painstruth Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ndio mnapokosea....Magufuli alitoa kauli ile baada ya kuzomewa! hakuna anayesema wananchi waombe msamaha kwa kuzomea.......
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Teh!teh! sana tu ni kama wanaotaka kufika mbinguni ilhali hawataki kufa,
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi,
  Leo umeanishika haswa pale ambapo siku zote mimi huwapima viongozi wetu kama ni wanasiasa ama vijaa tu waliokimbilia siasa baada ya kuona wana uwezo wa kuwasaidia Umma.. Sifa ilizoziweka hapo juu vijana wengi sana hawana na wapo CCM, Chadema na CUF kwa sababu kila mmoja wao anaamini kichwa chake mwenyewe...

  Flip-Flop kwao siii mapungufu kisiasa bali inategemea na upepo..wapo vijana wanaoamini kabisa kwamba JK anaweza kufanikiwa ama ana malengo mazuri ikiwa juhudi kubwa zitafanywa kuongeza uzalishaji wakati miundombinu hakuna, Uwajibikaji hakuna, na kibaya kuliko yote Miiko na maadili hakuna...Ila kwa fikra zao wanafikiri wao kwa kupenyeza na kusimamia maswala haya wanaweza leta mabadiliko. Hizi ni ndoto za mchana na kutofahamu SIASA..
   
 5. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Heading yako kwanini isiwe Nauli Feri: Mtemvu, Hata Wewe? au Nauli Feri: Ndungulile, Hata Wewe? au Nauli Feri: Zungu, Hata Wewe? au Nauli Feri: Wabunge, Hata nyie?, ,
   
 6. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Yani upo sawa kabisa..Na isitoshe kuna viongozi wenig washatoa kauli za jabu mbona mnamkomalia Magufuli peke yake?Mnamuonea wivu ni mchapakazi au?
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ingekuwa ni wabunge wa CCM peke yake, pengine nisinge hoji kwani tumewazoea wabunge wengi wa CCM (sio wote), kuja na matamshi ya ajabu ajabu. Mnyika ni mtu makini sana kutumbukia katika sakata lillojaa mantiki kuliko siasa, na hilo ndilo limenigusa zaidi.
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,568
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu Mnyika kazi unayo! Njoo uweke hali ya hewa sawa,kuna kitu hakijakaa vema Mheshimiwa!
   
 9. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumsubiri kuna siku atakuja kutoa ufafanuzi.
   
 10. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nakupongeza sana mchambuzi kwa kuchanganua jambo hili nafikiri hawa wabunge, wananchi na mh, makugufuli kila mmoja amepata sehemu yake iliyomgusa ktk issue hii ya nauli ya kivuko. Nilichogundua na ambacho wanasiasa wetu wanalenga ni kura tuu ndo hata mambo ambayo wanapaswa kuwaambia wapiga kura wao wanashindwa, tutapumbazwa sana na wanasiasa wa namna hii katika kutimiza malengo yetu.
   
 11. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mchambuzi heshima mbele

  Asante sana kwa makala yako iliyojaa hekima na mambo mengi uliyoyachambua kwa kina. Kwangu mimi sishangai hata kidogo nauli kupanda kwani hata nchi zilizo endelea wana tabia hiyo ya kupandisha nauliu kila inapobidi. Kwa mfano kwa watu wanaishi Uingereza watakubaliana na mimi kuwa kila mwaka huwa wanapandisha nauli kwa wastani wa 2%. Na ongezeko hilo la nauli linakuja na ongezeko za uboreshaji wa miundo mbinu, nikiwa na maana ya mabasi, tubes, vivuko n.k.

  Sasa tuje hapo kwetu, swali la kwanza la kujiuliza je ongezeko limekuja na uboreshaji wa kivuko?

  Je uendeshaji wa kivuko kwa takwimu zako ni milion 90, je hapo ni kabla au baada ya gov subsidy?

  Je ongezeko hilo linakuja na ongezeko la kipato cha mwananchi?
  Kwa hiyo mkuu kuna maswali mengi yakujiuliza yasiyo na majibu.....nami naungana na mbunge wangu mh J J Mnyika kupinga hili ongezeko na kuhoji uhalali wa Magufuli kuongeza hizi nauli

  J J Pikadili
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kwa mamntiki hiyo mkuu unashauri wananchi wapige mbizi???
   
 13. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kaka bosi wako akikukaripia kwa ufanisi mbovu na ww huwa unamkaripia nini?
  wanchi ndio bosi wa Magufuli, so wana kila haki ya kumkaripia kwa ufanisi wake mbovu
   
 14. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hapa bado sijaona hoja ya msingi kwa wanaomshutumu Mnyika akiwa kama mwakilishi wa wananchi..
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Hayo ni maswali ya msingi. Kabla ya kuangalia uboreshwaji wa huduma, mapato ya wananchi, n.k, ni muhimu kwanza tuwe na takwimu juu ya gharama za uendeshaji wa kivuko kile, ambazo wabunge walizembea kuzihoji huko bungeni, na badala yake kuja kutupiga blah blah kwenye vyombo vya habari. Na ndio maana hoja yangu ya msingi ni kwamba kina Mnyika et al. hawana legitimacy kuhoji hayo barabarani. Hawana takwimu zozote zinazowasaidia kujenga hoja kwamba ongezeko la sh. 100 ni kubwa sana; Mbaya zaidi, walizembea kuhoji kamati ile ya bunge kuhusu gharama za uendeshaji wa kivuko kile. Kutokana na mapungufu hayo, hawana legitimacy, na wamekurupuka kwa msukumo wa kisiasa huku mantiki ikiwasuta. Warudie ile kamati ya bunge kwanza. Na mtu sharp kama Mnyika lazima kwa sasa analijua hilo, sina uhakika kuhusu wengine.

  Magufuli ana mapungufu mengi kama kiongozi, lakini ni dhahiri kwamba Magufuli sio kiongozi wa 'kupurupuka' katika maamuzi.
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135


  Tanzanians in totality: subjectivity all the time, hakuna anayetaka kuona positive side..What is the issue here?
   
 17. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wasipige mbizi, wasubiri mwekezaji watakayepanga naye nauli za kivuko
   
 18. c

  cilla JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Muwenaakili yakutafuta usahihi wa mambo sio mnaropoka.1 elewa ubungo sio lazima uingie na kwamsafiri ni bure 2.sumatra wao hupandisha kwasababu huangali faida kwa wafanya biasha .na serekali huwa haifanyi biashara kwa maana hiyo haina hasara.serekali yenyewe hukusanya nakutumia ndio maana katika vitabu vyao wana income na expendure lakini mfanya biashara expt,income na lost (hasara)3.kivuko nisawa na daraja na nihuduma ya jamii 4mwenye crueser analipa 2000 mwenye mikokoteni 1800 ni sawa hilo.5.Bakresa aliomba asimamie yeye kivuko nawatu wasinge lipia isipokuwa magari tu kwanini serekali walimkatalia.6.magufuli jimboni kwake aliomba kivukoni wananchi wasilipe ila halimashauri ikasema tunakitegemea sana kwa mapato ya halimashauri je yy naye alikuwa mjinga?pale kunaulaji na serekali imefilisika na inatafuta vyanzo vipya si waweke wazi tu.7.kwasiku wanakusanya milion 9 faida milioni 5 kwa siku mnaona ni kidogo? wanaolipwa pesa nyingi sa pale ni master 2 tu.tumieni bongo
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Una hoja lakini kuna vitu unavi over look katika sakata hili; na pia ni muhimu ujisahihishe kwamba kamati ya bunge ilisema surplus KWA MWEZI, SIO KWA SIKU, ndiyo hiyo Shillingi MILIONI TANO.
   
 20. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  si kila ahudhuriaye kikao amekubaliana na maamuzi ya kikao

  lkn ukweli nadhani pesa nyingi zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache kwani hatuoni maendeleo

  pia kiwango kinchopendekezwa ni cha juu sana, kwa wenye magari itabidi wapaki kigamboni wasipitishe kwenye pantoni kwani watahitaji si chini ya shilingi 3600 kila siku kuvusha magari,je hii sawa, kwa kipato gani
   
Loading...