Nafasi ya uongozi (UBUNGE) kama ya kina Waheshimiwa Mnyika, Mtemvu, Ndungulile, Zungu, ni moja na nafasi za juu sana za uongozi katika Jamhuri yoyote ile. Wabunge wanawakilisha MATUMAINI, HOFU, SHABAHA na KIU ya wananchi. Ndio maana nafasi hii inahitaji utashi wa hali ya juu. Mbunge anatakiwa awe na sifa za kiongozi bora (sio bora kiongozi), vinginevyo ataishia kuwa kiongozi mpotoshaji, na anayeongoza au kutoa maamuzi kwa kufuata upepo, huruma kwa wapiga kura wake, pamoja na maslahi binafsi. Mbunge anatakiwa awe na sifa pamoja na:
Waheshimiwa, na hasa John Mnyika - ambapo Ubungo ni Jimbo lako, kwanini haufuatilii suala la Kituo cha mabasi cha ubungo ambako kuna usumbufu na gharama zisizo na sababu kwa wananchi, pengine kuliko suala la kigamboni? Mfano, ili mtu uingie kituo cha ubungo kwa mguu, kwa dakika moja tu kumsindikiza ndugu yako anaesafiri ambae anahitaji msaada kwa sababu ya uzee, au ulemavu au umri mdogo (mtoto wa shule), unatozwa sh 200, je hamuoni kwamba hili nalo ni tatizo? Au ni kwa sababu, tofauti na mapato ya ferry ambayo hayapo chini ya manispaa, mapato ya Ubungo yapo chini ya manispaa ambako kwa nafasi zenu kama wabunge, mnakaa kwenye VIKAO kama madiwani kupitia/kupanga bajeti, na kula posho za vikao?
i.