Natumia Excel kutengeneza taarifa na kuzichambua Katika njia mbalimbali ili ziweze kukusaidia kufatilia maendeleo kwenye biashara yako

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
Ndugu habari
Mimi ni kijana mwenye ujuzi na excel sasa nmeona pengine naweza kuufanya ujuzi huu kuwa huduma na kupata chochote kinisadie hapa na kule.

Nina ujuzi na excel na ninaweza kutumia katika namna mbalimbali ili kuweza kusaidia kutatua changamoto tofauti tofauti.

Wee mfanya biashara ambaye una maduka yako ungependa kujua kwa mwezi au robo mwaka mauzo yako yanendaje kipi unauza sana na unauza kwa kiasi gani, bidhaa gani ndo zina dominate mauzo yako katika eneo na taarifa nyingine nyingi lakini hata kulinganisha hesabu za taarifa na ZA kwako au kijana wako ili kujua kama amna wizi au kuna mashaka ya upotevu.

Hii itakusaidia wee kujua nini hasa wateja wanapenda eneo ulipo na nini hawapendi ninii ulete sana nini ulete kiasii.

Lakini pia itakusaidia kufahamu taarifa ZA muda mrefu kama kipindi cha mwaka mzima , vipindi mbalimbali vya mwaka nini unauza sana ili uelewe ikifika muda flani bidhaa flani zinapendwa zaidi eneo nilipo kwahiyo napaswa kuwa na stock ya kutosha.
Na pengine wewe ni mwalimu unatafuta njia ya kuwa una pima maendeleo ya ufundishaji wako na mabadilko ya kila mwanafunzi ili kupima ufanisi wako na impact yako kwao pia tunaweza kuandaa njia ya kulipima pia Hilo.

Lakini pia una changamoto mbalimbali zingine ambazo uko nazo na unahitaji kuwa na njia ya kuona progress yake kwa taarifa inayoeleweka.iwe kaziini kwenye biashara na maeneo ya uzalishaji unaweza kuniambia mimi nikafikiria solution na kukueleza kama tunaweza leta jawabu na kukusaidia.

Nitafanya kazi kwanza na kukupa mrejesho ukiipenda ndo utafanya malipo kadri ya makubaliano, ukinidhulumu sitakuwa na la kufanya, natafuta kujenga uaminifu tu ndomana sitaki malipo ata nusu kabla ya kazi.

Nb. Mimi ni mwanafunzi tu hii ni kama part time nayotaka inisaidie kupata mahitaji madogo madogo.

Asanteni nisaidieni kijana wenu.
 
Jaribu kucheck sites za freelancer kama upwork, fiverr etc,ziko nyingi tu, mind you competition ni kubwa so usiombe na kazi zenye malipo makubwa,ikiwezekana anzia chini ili ujenge profile kwanza thn baadae ndio utakuja kucharge hela kubwa.
 
Back
Top Bottom