Simulizi yako iko very clear, nakuonea huruma, haya yamewakumba wengi katika maisha. Ikimbie zinaa, unachofanya ni chukizo mbele ya Mungu aliyekuumba (Amri ya sita), Kumbuka unaingilia ndoa ya watu (Ndoa na iheshimiwe na watu wote).
Wewe bado ni kijana sana, mrudie Mungu wako kwa dhati kabisa naye atakubaliki na utapata aliyewako wa pekee ili mkapate kuoana na kuishi pamoja kama mume na mke mkitenda yampendezayo Mungu (Mapenzi ndani ya ndoa) naye atazishusha baraka zake juu yenu.
Jaribu kupiga picha kama wewe ndio ungelikuwa unaingiliwa hivyo ndani ya ndoa yako ingalikuwa vipi dada na mwisho huyu mpenzi wako unayemuita no 1, ipo siku mtaachana na hapo hakika muda utakuwa tayari umekwisha enda sana dada, please usije kumbumbuka shuka ili hali kumekucha.
Piga moyo konde upate kuyatenda mapenzi ya Mungu, achana na mambo ya kufurahisha mwili kwa kipindi kifupi cha maisha yako hapa duniani then ukabaki na majuto kwa kipindi kirefu cha maisha yako hapa duniani na baada ya hapa duniani.
Kama huyu mpenzi wako no 1, kama unavyomtaja anaweza kumsaliti mke wako wa ndoa, hakika jua ya kwamba ipo siku atafanya hivyo kwako tena jeuri kubwa, so is better kukata mahusiano sasa na upate kuwa huru na kuweza kufungua milango kwa mpenzi mpya na mume mtarajiwa,maana kwa jinsi hii sio rahisi hata mtu akikuapproach utamkataa coz already you are full occupied with somebody who is not yours in real.
Fanya uamuzi sahihi juu ya maisha yako dada.