Natembea na mume wa mtu

Natembea na mume wa mtu

missa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
360
Reaction score
193
Hi wanajamii,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 ninaomba ushauri wa kuweza kunisaidia kuondokana na tatizo nililo nalo la kutembea na mume wa mtu.

mwaka 2000 nilianza form one kwenye shule moja ya misheni, nilipofika huko kuna wakaka waliokuwa wanavolunteer kufundisha watoto wa form 1$2 baada ya masomo,wao walikuwa ni form 3 $ 4 wenye performance nzuri. sasa kama mnavyojua form one hadi form four wengi wao ni wanakuwa kwenye foolish age, sasa katika hao wakaka wa form 3 waliokuwa na desturi ya kutufundisha akaanza kunisalandia japo mi ndo kwanza nilikuwa na miaka 15 (form one).

Tukaenda hivo ikafika mahali nikamkubali kwa akili zangu za kitoto ili aendelee kunifundisha mana kwa wakati huo nilikuwa sina idea yoyote kuhusu mapenzi na wala nilikuwa sijawahi ku do, basi tukaendelea na mapenzi hayo ya kitoto ambapo yeye alikuwa akinitomasa tomasa to mwilini ula hakuwahi kunifanya chochote kwa wakati ule, japo shule nzima ilijua na walimu walijua na watu walianza kututania sana shule mana yeye alikuwa anajulikana sanapale shule.

huyo mkaka alipofika form four mwanzoni wazazi wake wakamuhamishia shule nyingine ili akamalizie huko,hata alipohama tuliendelea kuonana mana hakuhamishiwa mbali,na hapo ndo tukazidi kupendana zaidi huku ahadi yetu ni kutofanya mapenzi hadi tutakapoowana., alipomaliza form 4 tena wazazi wake wakamtafutia seminary nje ya mkoa akasome five na six,wote tulisikitika mana kipindi hicho kwa mwanafunzi kuwa na simu ilikuwa si rahisi zaidi ni barua tu,hali ikazidi kuwa ngumu japo tulipendana sana.Alipofika seminary mawasiliano yakakatika na hata alipomaliza wazazi wake wakapropose akae huko huko wao wanataka asome short coz wakati anasubiri kwenda chuo.

Baada ya hapo tukapotezana kwa miaka kadhaa na mimi nilipofika advance nikapata mpenzi ambaye tulisomaga nae o level na anajua historia yangu na my first boyfriend,baadae nikafanikiwa kufika chuo kikuu, nilipokuwa mwaka wa pili field nikakutana na my first boyfriend yuko na kaka yake wanatafuta suti ya harusi na huyo boyfriend wangu wa kwanza aliponiona na kaka yake walishtuka sana mana hawakutegemea na wiki hiyo ndo alikuwa anafunga harusi mwaka (2009),basi akaniuliza uli nimekutafuta sana?wote tukabaki tunashangaana tu lkn bado kila mtu alikuwana ishara za kumpenda mwenzake.basi tukapeana namba za cm lakini kwa wakati huo ye alikuwa ni mfanyabiashara na mimi mwanafunzi wa chuo.

baadae tukawa tunawasiliana ila yeye akawa anasisitiza sana tuonane tuongee,mi nilijitahidi sana kumkwepa mana nilijua ye ameshao nami nina mpenzi,baadae akaniuliza kuwa amesikia nina uhusiano na mtu fulani ambaye ye ana mfahamu,mi nikamwambia ukweli, nilipomwambia ukweli akamtafuta huyo mkaka akamuuliza nae akamwambia ni kweli.
lakini kwa bahati mbaya huyo boyfriend wangu wa pili nikiwa namaliza chuo (2010), ye akaoa kimya kimya,nilipotaka kujua sbb akasema kwao wamesema asinioe sbb nimemzidi elimu ye ni form 4 mi chuo ivo nitamsumbua huko mbeleni. boyfriend wangu wa kwanza ambaye tayari ndo mume wa mtu akamfuata boyfriend wangu wa pili kuwa amesikia kuwa ameniacha wakati tulishwahi kufanya mapenzi (amenitoa virgin) kwanini aniache? akamjibu kuwa hawezi kuishi na mwanamke aliyemzidi elimu so ameamua kuoa.

Baadae nilipoanza kazi pa nikapa mpenzi mwingine nae pia nikagundua hana true love yuko after money nikipata tatizo anakaa mbali nami basi tukaachana.wakati wote huo boyfriend wangu wa kwanza(mume wa mtu kwa sasa) alikuwa anafuatilia maisha yangu ki ukaribu huku akidai hawezi kuacha kunipenda maisha yake yote, sasa baada ya kuachana na huyu wa mwisho yeye akaanza kutoroka kwa mke wake anasafiri na kunifuata mkoa ninaokaa,anamuaga mkewe anaenda kwenye biashara anakuja kwangu toka january mwaka huu nimejikuta kwenye mapenzi mazito na huyo boyfriend wangu wa kwanza ambaye kwa sasa ni mume wa mtu na ndoa yake ina miaka 4 na ana mtoto mmoja,kila nikijaribu kumuuliza kama ana tatizo lolote na mkewe anasema wanaishi vizuri tu ila anasema anaona bado roho yake inanipenda sana anashindwa kujizuia na kilichovunja uhusiano wetu ni umbali tu na anasema hata ndugu zake wanajua kuwa bado ananipenda hata sometimes anapokuwa anakuja kwangu baadhi ya ndugu zake wanajua.

sasa wanajamvi wenzangu nisaidieni ushauri nifanyeje mana ndo nazidi ku fall zaidi japo nilikuwa nampenda ili nilipoona ameoa nikaamua kumwachia mungu,lakini naona kama limekuwa jaribu kwangu mana namuonea huruma mke wake japo ye ndo aliingia anga zangu lakini maadamu hana matatizo naona yeye ni innocent kwanini nitoke na mumewe japo,,japo nimempa warning huyu mwanaume asimfanyie vituko mke wake na aendelee kumuheshimu, na mimi simchokozi kwa namna yoyote ile yule mkewe.

jamani nipeni ushauri nifanyeje mana toka mwaka jana sina boyfriend wala mchumba zaidi ya huyu mume wa mtu ambaye ndo alikuwaga boyfriend wa kwanza sasa tumerudiana ye akiwa mume wa mtu tayari.
 
Aisee pole sana !
Unasema umemwambia asimfanyie vituko mke wake ! hakuna kituko kibaya kama hicho unachofanya ! uNgemwambia endela kumdanganya mke wako !HEBU TAFAKARI MANENO HAYA ULIYOANDIKA!
,lakini naona kama limekuwa jaribu kwangu mana namuonea huruma mke wake japo ye ndo aliingia anga zangu lakini maadamu hana matatizo naona yeye ni innocent kwanini nitoke na mumewe japo,,japo nimempa warning huyu mwanaume asimfanyie vituko mke wake na aendelee kumuheshimu, na mimi simchokozi kwa namna yoyote ile yule mkewe.

NAKUSHAURI UPIGE MOYO KONDE HUYU MTU ATAKUHARIBIA MAISHA YAKO ! KUNA WANAUME WENGI WANATAFUTA WACHUMBA ...TULIA UTWAPATA!
 
Kama ni waislam uolewe mke wa pili.....
Siyo lazima awe muislam. Kwani wakristo wangapi wana mke zaidi ya mmoja? Kama vipi nyie halalisheni tu, mkafunge ndoa ya bomani. Sioni ubaya katika hilo. Hii habari ya mke mmoja ni sheria ya kanisa tu, haina madhara yoyote kiimani. Kwa uelewa wangu wa biblia, ni askofu tu ndiyo amezuiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.
 
Amka leo anza kutafuta mchumba tena ikiwezekana tangaza hapa JF. Utaishi kwa short course mpaka lini? Swali ni mpaka lini? Au unataka aje akupe mimba na kufuta ndoto yako ya kupata wa peke yako aka Mume? ( kwa maelezo yako inaonesha kabisaa hamtumii condom)
 
Jitahidi uachane nae. Unapokuwa nae watu wanaokupenda na kutaka kukuoa unawazuia. Ni vizuri ukawa mwenyewe ili watu wanaotafuta wachumba waweze kukufata.
 
Mkewe hakuingia anga zako bali wewe, kwa kuwa walipokutana hamkuwa katika mahusiano na wala hukujua huyu jamaa yuko wapi, achana na mume wa mtu ni sumu. Au umeamua kuwa spare tyre?
 
Hiyo ni dhambi, jitambue,Maneno yangu hapa yasipite bure, kwani ni maneno ya Roho Mtakatifu,Geuza shingo yako,usiufanye mugumu moyo wako,TUBU NA UACHE DHAMBI,MUME WAKO ATALETWA NA MUNGU.
Hima Geuka..
 
Achana na mume wa mtu, mbona wanaume wapo engi tu?

Hebu fikiria mkewe akiyajua hayo itakuwaje?

Hebu fikiria kuhusu mtoto aliye naye atakaa kwenye mazingira gani,
Ilihali kwasasa wanaishi kwa furaha na amani.

Jipe moyo na wewe utampata aliye wako kwani huyo siyo wako.
 
Siyo lazima awe muislam. Kwani wakristo wangapi wana mke zaidi ya mmoja? Kama vipi nyie halalisheni tu, mkafunge ndoa ya bomani. Sioni ubaya katika hilo. Hii habari ya mke mmoja ni sheria ya kanisa tu, haina madhara yoyote kiimani. Kwa uelewa wangu wa biblia, ni askofu tu ndiyo amezuiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.
wazo zuri sana!tekeleza hili
 
Hiyo ni dhambi, jitambue,Maneno yangu hapa yasipite bure, kwani ni maneno ya Roho Mtakatifu,Geuza shingo yako,usiufanye mugumu moyo wako,TUBU NA UACHE DHAMBI,MUME WAKO ATALETWA NA MUNGU.
Hima Geuka..
Man, there are already 1 million more women than men in Tanzania. Ukisema uamini kwamba kila asiye na mme basi mme wake ataletwa, hawa milioni moja zaidi watatoa wapi hao waume? Mungu alikuwa na makusudi ya kuwafanya wanawake kuwa wengi zaidi kuliko wanaume. Waache wabanane kwa hao hao wanaume wachache, kama Mungu angejua hiyo ni dhambi basi angewaumba wanaume na wanawake kwa idadi sawasawa.
 
adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie. Vijana tuko wengi mjini na kazi zetu ila hatuonekani, loh!

we mwache mwenzio kapenda kuwa uhawara kugegedwa mchana tu usiku mpaka mume asingizie safari tena na mwenzie anacheo cha mrs yeye hawara a.k.a kimada, nyumba ndogo, kipozeo na kadhalika na usomi wake wote huo kipindi cha baridi anapopata shida wakati mwenzie kakumbatia hata baridi haijui
njoo kwangu mimi mwenyewe single and searching check avatar mwanamke wa kitz haswa
 
Ushawahi kutolewa busha la kike ww? Nadhani bado, basi endelea kuendekeza mali za watu tu.

Sent from my BlackBerry 9530 using JamiiForums
 
Kwanza Pole sana kwa kuingia kwenye mahusiano na mume wa mtu,
Unafurahia uhusiano wa kujifichaficha? Ungependa kuwa na future ya aina gani na huyo mume wa mtu?
Kama nyie waislam wenzangu nendeni mkamwombe bimkubwa uolewe mke wa pili.....kama sivyo jipe moyo mwache sababu atakuja kukuacha wewe na kurudi kwa mkewe wakati muda ushaenda
Anakupotezea muda huyo ohoooooooo
 
Back
Top Bottom