Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Ni kweli Binti Magufuli
Huyo dada ni mid50, alikwenda akiwa 45 mwaka 2007 alisoma kwa miaka 3 akamaliza ndipo akaajiriwa (kwa sababu ukimaliza tu degree=registered nurse). So ameajiriwa akiwa na miaka 48, lakini mafanikio aliyopata in 5years ni zaidi ya miaka 25 alofanya kazi Bongo. Mimi nimeshafanya kazi miaka 10 kama ofisa wa serikali, sasaivi nina miaka 35 (10 yrs less than her).

Sina sababu ya kushindwa, pia nilishaenda kwa miezi mi3 ila sikupata exposure ya miji mingi kwa vile nilienda tu Melbourne
Mkuu zamia nakuambia kuna watu tumezamia na Form four tu shauri yako. Unafikiri kukamatwa kwa sukari kutakupatia ajira!!!
 
Nimeamini kila jambo njema unalopanga huwa lina baraka za mungu. Jambo mhimu akifika huko awe na tabia zuri kwani atapata marafiki wema na ambao hawatamchoka. Akajishushe kwa lolote atakalokumbana nalo but baada ya muda ataanza kufaidi uvumilivu. Nje kuna fursa asikudaganye mtu pia aweke akili zake kama vile wanajeshi wanaotumwa kwenda vitani so lolote litakalotekea amwachie mungu
Sure mkuu! Ukweli Ni kuwa Upendo na lifestyle ya Kitanzania haipatikani popote duniani, sometimes utamiss life style ya nyumbani but all in all unajua kile kilichokupeleka!
 
Nurses huko kwa wenzetu mnahitajija kama lulu, tena tafuta kazi sehemu ngumu ngumu kama nyumba za wazee,nk. Nenda mkuu tuache sisi tuendelee kupigwa na wagonjwa kisa nimezalisha katoto kamekufa, wakati mama mjamzito alienda kliniki Mara moja, kaswende hakupimwa maana vitenganishi hakuna na hapa labour ward taa hakuna tunazalishia mwanga wa mshumaa...
Nimcheka sana unavyomshtakia huyo ngd
 
Sure mkuu! Ukweli Ni kuwa Upendo na lifestyle ya Kitanzania haipatikani popote duniani, sometimes utamiss life style ya nyumbani but all in all unajua kile kilichokupeleka!
Ni kweli mkuu. Lifestyle ya bongo haipatikani popote pale duniani. Maisha ya kishkaji, maisha ya kijamaa, maisha ya kiurafiki only in TZ. Huku Unaweza kaa hata wiki hakuna wa kuongea nae. Vyakula ndio hovyo kabisa, wasichana warembo na bila gharama wapo bongo. Kiukweli bongo ni ya kipekee. Naishi nje ya bongo karibu two years now lakini sipapendi mpaka najuta kwa nn nilikuja huku. Yaani life la kifala mno
 
Kibongo bongo Mpaka unamaliza bachelor na masters haraka haraka unachezea 29-30 years. okay lets say unaenda Australia kusoma hadi kuwa certified na kuingia kwenye mfumo wa ajira rasmi miaka 8-10. Hapo utakuwa na miaka 40 tayari. Huoni kwamba hiyo miaka 10 ungewekeza hata kwenye kilimo cha biashara ungetoka kirahisi tu kuliko kwenda kujitaabisha na maisha ya kusikia. Tatizo la watanzania hawasemi kwa namna gani wanapigana kufikia walipofika ila wanakuelezea tu mafanikio yao. Kweli nursing inalipa ila huwezi kufika tu Na kufikia mafanikio.
Mtu aliefanikiwa hawezi kukwambia Deeply..... atakupa matamanio tu lkn ukiingia kwenye uhalisia ndio utajua kumbe kakuingiza chaka....Kuna siku nilikuta watu wanamsifia Bakhera kwamba amekuwa tajiri kwa biashara yakushona Viatu...na jamaa mishipa ya shingo imewatoka kupeana hope nimecheka sana!,.......Nilichogundua kwenye maisha iwe ni Biashara kuajiriwa ukiambiwa changanya na zako
 
mkuu kama kweli unataka utusue maisha tafadhali nenda katika nchi zifuatazo Shelisheli Ipo Africa,st Vincent And Grenadies,british Virgin Island Zipo Marekani Kaskazin Bila Kusahau Cape Verde Nakuhakikishia Ukirud Baada Ya Miaka Miwili Kama Hujajenga Magorofa Matatu Kwa Mpigo Mimi Fala..
Kuna fursa gani?
 
Ni kweli mkuu. Lifestyle ya bongo haipatikani popote pale duniani. Maisha ya kishkaji, maisha ya kijamaa, maisha ya kiurafiki only in TZ. Huku Unaweza kaa hata wiki hakuna wa kuongea nae. Vyakula ndio hovyo kabisa, wasichana warembo na bila gharama wapo bongo. Kiukweli bongo ni ya kipekee. Naishi nje ya bongo karibu two years now lakini sipapendi mpaka najuta kwa nn nilikuja huku. Yaani life la kifala mno
Wapo aina ya Wabongo wengine wana enjoy lifestyle ya ukimya hawapendi kujichanganya mtaani, Hawa hawapati shida kuishi maisha ya upweke abroad, but wale walioishi maisha flani ya Uswahilini kujichanganya mtaani, wataona shida kwao kuishi abroad..

Komaa mkuu coz labda ushatengeneza channel huko, siku unaamua kurudi mazima bongo sio kuja kuanza moja tena!
 
Ngoja nimalizie michakato yangu huku, then nirudi zangu home Tz nifanye maisha pasipo pressure wala stress.
Kwakifupi kwa muda ambao nimejaribu kuzunguka nchi kadhaa kama expert worker, bado nakiri wazi kwamba home Tz bado kuna opportunity nyingi sanaaaaa ambazo kiukweli mtu ukiamua kuweka bidii na kujitumia kwa dhati lazima ukue na Good life aiseeee.
Tatizo linalo tutafuna sana waTanzania ni uvivu, kupenda kuomba, kuwa tegemezi na shortcut.
Swala la uvivu kweli lipo lkn pia wapo watu Serious wanapiga kz bt hawafanikwi cz Income ni ndogo Nch yetu Watawala wamewekeza kwenye SIASA tu
 
Swala la uvivu kweli lipo lkn pia wapo watu Serious wanapiga kz bt hawafanikwi cz Income ni ndogo Nch yetu Watawala wamewekeza kwenye SIASA tu
Kwani......
Unapo sema kwamba mshahara ni mdogo au kipato kidogo, hapo unamaanisha ni pesa ngapi hiyo?
Hili swali nimekua nikiwauliza watu wengi sana, lakini sijawahi kupata jibu sahihi.
 
Wapo aina ya Wabongo wengine wana enjoy lifestyle ya ukimya hawapendi kujichanganya mtaani, Hawa hawapati shida kuishi maisha ya upweke abroad, but wale walioishi maisha flani ya Uswahilini kujichanganya mtaani, wataona shida kwao kuishi abroad..

Komaa mkuu coz labda ushatengeneza channel huko, siku unaamua kurudi mazima bongo sio kuja kuanza moja tena!
Toka nimekuja huku mambo yangu yote yamesimama. Fursa zangu zote naona zipo Dar. Nina jishughulisha na kulima. Kama unavyojua wabongo, ukimuachia kitu unakuta manyoya tu. Wenzangu nakuta wamesonga sana kimaendelea. Bongo fursa zipo. Nje ya nchi ni mbwembwe tu
 
Hivi huko Tz hizo opportunity ni zipi? Wewe umesema ni expert worker, kwa nn uajiriwe ikiwa kweli unaona hizo opportunities? Mfano ukifanya nn unaweza kuwa na net saving ya m10 guaranteed kila mwezi kwa Tz?
Tatizo letu watz tunadharauliana sana hasa MTU aliebahatika kufanya kz NJE yaani anaona walioko huku wote ni bongo lala.....
 
Dah umeongea hadi umenivunja moyo kwenye ndoto zangu za kujiajiri. Haya we nenda Mungu akutangulie ila ukifanikiwa tu ninaomba unikumbuke kwenye ufalme wako. Utatupatia muongozo wale wa ungwini tufanyaje japo me nilipenda sana niende Canada.

Mkuu hakuna shaka, nimeshaungwa na group moja la waTz mix na Wakenya wa huko jimbo mojawapo..so naona tu nazidi kua karibu na kufanikiwa. We fanya unaloamini kua ni mafanikio, mimi nimeona kwa macho na nataka nijaribu, siachi kazi katu nachukua likizo bila malipo, ikitokea tu vimegoma au tz imekua nzuri narejea tu. Asante sana kwa mchango wako, I promise nitafufua huu uzi siku moja na kuappreciate zaidi ya leo, God bless your endeavors
 
kweli kabisa mkuu, yani nafananisha haya maisha kama biashara, mwenzako anawaza aanzeje wakati wewe unaona haifai. Bongo ni pazuri sana kwa kitu kimoja tu...social life. Na nchi nyingi za kimaskini pia ziko hivyo..social interaction inakua kubwa sana. Kwa hilo nakuunga mkono 100/100, Lakini upate pesa labda hata holiday moja uende hata Cape town kutembea na familia utakufa unaota tu labda uwe fisadi au mla rushwa. Lakini kwa hii TGS E2 yangu mafuta tu kwenye gari, luku, bado, vifurushi vya mitandao...inafika tarehe 17 hoi bin taabani.

Nina kaka angu yuko Berry Spring Michgan, kaenda tu kusoma na mkewe mbongo na walikua wanalipwa sh 700,000 (combined), lakini walipoamua kwenda kwa akina Nyani Ngabu kwa miaka 3 wameshainvest zaidi ya milioni 200 hapa Bongo. Na wanamiss sana maisha ya bongo...lakini kiuchumi dahh inategemea sana na mawazo yako unadefine vipi kufanikiwa
Asikudanganye mtu bana, bongo bado pazuri sana. Hapa nina mkakati wa kuacha na kashule kenyewe nirudi zangu bongo nikakomae na maisha yangu. Ukitoka nje ya nchi fursa nyingi zinakupita hivi hivi. Nachukia kukaa nje ya nchi muda mrefu. Nimetembea nchi nyingi lakini sikuwahi kuwaza hata siku moja eti nizamie kabisa huko au nitafute paper au sijui nifanyeje ili nisirudi bongo? Mimi napenda bongo hata iweje hadi kufa nitaipenda daima. Nikikaaa miezi 3 bila kuona bongo land naumwa kabisa.

Kila mtu na fursa zake, wewe unaweza kuziona lakini mwenzako anaweza asizione. Kila mtu na mtazamo wake, wewe unaweza ona bongo panalipa, mwenzako akaona maisha yapo nchi nyingine za watu. Haya ndio maisha yetu, na waliposema dunia ni msongamano hawakukosea, maana huyu anakwenda, yule anarudi, huyu analia, yule anacheka, huyu analala yule anaamka. Fanya ile kitu roho yako inapenda mkuu. Usisikilize mineno ya watu. Huo ndio mtazamo wako na ndio maisha yako. Don't give it up. Woga wako ndio umaskini wako. Kila la kheri
 
Toka nimekuja huku mambo yangu yote yamesimama. Fursa zangu zote naona zipo Dar. Nina jishughulisha na kulima. Kama unavyojua wabongo, ukimuachia kitu unakuta manyoya tu. Wenzangu nakuta wamesonga sana kimaendelea. Bongo fursa zipo. Nje ya nchi ni mbwembwe tu
Usidaganye watu kwa kuangalia matokeo negative yaliyokupa. Kama ni mbwembwe ataona mbele ya safari.
 
Tatizo letu watz tunadharauliana sana hasa MTU aliebahatika kufanya kz NJE yaani anaona walioko huku wote ni bongo lala.....
mkuu kuna mtu amedharau kwani? nadhani jamaa alitaka tu hizo OPPORTUNITY NYINGI ni zipi kama sio kupeana no sweat? au kulima nyanya chungu au pilipili hoho?ndio fursa, na bahati mbaya tunaoshabikia hizo opportunity unakuta tumeajiriwa, au katika hizo kazi tunakwepa kodi, kuonea wengine kwa 'kuwaibia'...anyway ni mawazo tu
 
Toka nimekuja huku mambo yangu yote yamesimama. Fursa zangu zote naona zipo Dar. Nina jishughulisha na kulima. Kama unavyojua wabongo, ukimuachia kitu unakuta manyoya tu. Wenzangu nakuta wamesonga sana kimaendelea. Bongo fursa zipo. Nje ya nchi ni mbwembwe tu
Uko nchi gani mkuu?
 
Ulileta uzi ili upate ushauri na msomi hua anapokea advice then anafanya analysis kupata conclusion.. sasa kama ulitgemea usipate ushauri negative unanipa waswas na elimu yako kwa sababu haiwezekani muuza genge pale tandale anafamilia,ananyumba na anasomesha hawazi kutoka lakin ww unaingiza 1.5m monthly unawaza maisha magumu. Writing may judge enough.wewe si 1.5m earner per month ni sifa tu.

Sawa mkuu umesomeka, asante sana uwe na wakati mzuri huko ulipo. Kumbuka nimeomba exposure tu kwa walio Australia kwa maana ya uzoefu, ofcourse inaweza kuwa hata sehem nyingine ikawa na mchango kunipa uzoefu wa ninakotaka kwenda. Ishu ya sifa inatoka wapi tena? kwani tunajuana hapa Jf mzee? after all mm ni new member humu sijajuanana mtu yeyote wa kuqualify kunisifia. Nadhani una inferiority tu sijaona sifa yeyote eti kwa sababu ya kuearn 1.5m/pm wakati kuna watu wapo Tz na wanapata m36/mwezi..hizo zitakua sifa za kijinga haaaaaaa
 
mkuu kuna mtu amedharau kwani? nadhani jamaa alitaka tu hizo OPPORTUNITY NYINGI ni zipi kama sio kupeana no sweat? au kulima nyanya chungu au pilipili hoho?ndio fursa, na bahati mbaya tunaoshabikia hizo opportunity unakuta tumeajiriwa, au katika hizo kazi tunakwepa kodi, kuonea wengine kwa 'kuwaibia'...anyway ni mawazo tu
Ha ha haaa....eti....kulima Nyanya na Pilipili hoho
 
Back
Top Bottom