Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Asikudanganye mtu bana, bongo bado pazuri sana. Hapa nina mkakati wa kuacha na kashule kenyewe nirudi zangu bongo nikakomae na maisha yangu. Ukitoka nje ya nchi fursa nyingi zinakupita hivi hivi. Nachukia kukaa nje ya nchi muda mrefu. Nimetembea nchi nyingi lakini sikuwahi kuwaza hata siku moja eti nizamie kabisa huko au nitafute paper au sijui nifanyeje ili nisirudi bongo? Mimi napenda bongo hata iweje hadi kufa nitaipenda daima. Nikikaaa miezi 3 bila kuona bongo land naumwa kabisa.

Kila mtu na fursa zake, wewe unaweza kuziona lakini mwenzako anaweza asizione. Kila mtu na mtazamo wake, wewe unaweza ona bongo panalipa, mwenzako akaona maisha yapo nchi nyingine za watu. Haya ndio maisha yetu, na waliposema dunia ni msongamano hawakukosea, maana huyu anakwenda, yule anarudi, huyu analia, yule anacheka, huyu analala yule anaamka. Fanya ile kitu roho yako inapenda mkuu. Usisikilize mineno ya watu. Huo ndio mtazamo wako na ndio maisha yako. Don't give it up. Woga wako ndio umaskini wako. Kila la kheri
 
kaka jibu kwa Jerrymsigwa umejibu wewe... nilimjibu yeye alivyouliza biashara ya kufanya. sio wewe kaka..

wewe ni jembe sana nimekukubali wazo lako

Mkuu kwanza ninashangaa jinsi unavyoona uamuzi wangu ni uoga au uvivu. Kiufupi hata nia tu ya kuthubutu kufanya hili ni ujasiri tosha, kwa miezi michache hiyo niliyonja kukaa huko nilipata ORCHE card, forklift Licence, High Rigid Licence na first aid course..kwa vile mwenyeji wangu alipenda nichangie kdg rent.

Kiufupi niko exposed kwa kiasi kikubwa tu, ila nimeomba uzoefu wa wenzangu hasa walioko huko majimbo mengine na kama kuna mabadiliko kdg maana kipindi naenda Kelvin Rudd ndio alikua Pm. Dhiki na shida inapunguza sana uchaguzi wa kazi ambazo tuna passion nazo mkuu, mm ningependa kua mwana mazingira lkn je what is my fate after getting 60? Kama maDr na maProf waliotusomesha nao wanalalamika maisha magumu sasa kwa nini na mm nikae katika mstari huo huo wkt nina miaka 25 ili nifike retirement?

Kiufupi I want to start with nursing to pursue my 'environmental mgt career' baada ya kua qualified nurse ila ukiomba visa kwa hizo degree za bongo ili upate kazi utakesha
 
Ndugu ,

Katika maisha kujaribu ni kitu kizuri sana tena kujaribu kwa tahadhari ni vema zaidi. Meaning take risk with your eyes wide open.
Kwa mtazamo wangu watanzania wengi bado tu waoga sana na hii ni kutokana na mazingira tuliyokuzwa nayo. Kuajribu vitu, kusafiri, kubadili kozi, kazi , sehemu ya maisha isnt a thing we are used to see. Kama malengo yako ni makubwa kuliko unachopata na kila ukiproject unaona bado kazi ya bongo haifai, I encourage you to try other places. Ila fanya uchambuzi yakinifu wa kutosha . Kuinvest 20+ Million si hela kubwa sana kukimbiza ndoto yako.
jipe nchi mbili ufanye comparison ya kutosha na tafuta washauri wazuri ambao unahisi wanakwambia ukweli. Ingia kwenye expat forums za hizo nchi uone foregners wanasemaje?
I highly encourage you to chase your dream , its better to try and fail than just sit and complain.
 
bablai. Kama umeshindwa kutusua hapa bongo. Basi hata uende marekani huwezifanikiwa.

Wazungu wanatoka majuu wanakuja kutusua bongo Alafu wewe unazubaa!

Kwanza lazima uzijue changa moto za nchi za wenzetu.

Usipate matumaini ya Abunwasi ukajikuta unakwenda kuangukia pua.

Kwanini usijipange hapa hapa bongo kwenye kilimo cha kisasa?

Mshaara wako ukijipanga ukatafuta mashamba. Mbeya na morogoro, unatusua ndani ya mwaka 1 mkuu wangu.

Tatizo la watanzania wengi hawapendi kutafuta taharifa na kutembelea mikoani kuona fursa mbali mbali.

Jipange mkuu, huna haja ya kwenda kwa wazungu, utabarikiwa hapa hapa.
 
Don't lose your focus. keep chasing your dreams bro.

Engage your mind, Listen to your heart, then take-off !

Notably however, in your such endeavors, YOU must learn to expect the unexpected coz LIFE is full of surprise.

-Kaveli-
 
Mkuu unauzoefu wa nchi gani kati ya izo?
Mkuu British Virgin Island Nimeishi Tangu Nina Umri Wa Miaka 20 Lakini Nimetusua Even If Elimu Yangu Ni Ndogo Sa Hivi Nimerejea Home Maisha Yangu Yakiwa Na Uafadhali Kidogo Nimeishi Kwa Miaka Kumi From 2000 Hadi 2010 Ni Kanchi Kadogo Chenye Watu 50000 Tu Lakini Kila Raia Mambo Supa.Nchi Hii Ipo Chini Ya Malkia Wa Uingereza Ni Kuzuri Mno
 
kiongozi hizo inchi kuna fursa zipi zinapatikana huko mfano zinazohusu biashara na ajira
Nimeishi British Virgin Island Kwa Miaka Kumi Mfululizo Kaka Yangu Ndio Alonipa Ujanja Wa Kuishi Katika Nchi Hizo.Mimi Niliajiriwa Kwenye Kampuni Ya Mafuta Ya Bp Nchini British Virgin Island.Fursa Ni Nyingi Tu Kama Kuajiliwa Katika Makampuni,madaktari Na Mainjinia Wanahitajika Sana Nchini Humu Kuna Madaktari Raia Wa China Na Malawi Wengi Sana Karibu Mkuu
 
Aah bob nursing ni kwere sanaa wanapiga hela ya ajabu huko UK.

Nlikua napiga shule wakat flan UK. Nurses wana earn £ 22 to £ 25 per hour......kuna madem waki nigeria nilikua nao UK mabinti wadogo tu (Age 25 - 27) ni ma nurse wana hela kiseng*......

They live good kwa kazi ya nursing walifanyaga makeke wakapata ma indefinite leave to remain in UK....madem hao kila december wanaenda states or the carribean kutalii kula bata for 2 weeks or 3 (ni vishua alaf hawana majukumu wanangoja ndoa tu).

Last Christmas nimewacheki insta na fb wako Carlifonia wanakula life. Daaah aisee. Coursea za science Europe/States zinalipa sanaa yani tena ukiwa bado jankee mpaka uje kutulia akili aah ushagonga sana na madem wa kila aina. Tehe
 
Mkuu nitakujibu ila lengo la post ni kupata uzoefu wa walioko huko au kujua tu maisha yapoje. Dar-O'Tambo 4Hrs, O'Tambo-Perth 13hrs, Perth-Geelong 3hrs..route yangu hiyo ninavyokumbuka, ila huenda kuna njia yenye kutumia muda mdogo au zaid ya huo

Dar-Dubai 5 hrs, Dubai Perth 10 hrs.
 
Wakuu baada ya kumaliza chuo miaka kadhaa na kuhangaika kupata masters degree naona bado future yangu haiko salama ikiwa nikiwa naishi hapa Tz. Kupata mshahara wa 950,0000 na allowance ya 600,000 kila mwezi naona inaishia kuishi maisha ya hand to mouth. Sasa umri unaenda, na hakuna cha maana kinafanyika, na mzee Magu amebana mno hata hakuna deal kabisa, naomba msaada wa ushauri tu kwa wale wenye uzoefu wa Australia, na sio kwingine au kutoa kejeli zisizojenga kwani.

Mpaka nimefikia uamuzi huo wa kwenda huko kwa wazungu kwa sababu nina jirani yangu hapa alikwenda akasoma (Bachelor of nursing na akawa registered nurse), na bahati nzuri akapata PR na anafanya kazi ya nursing salary yake kwa saa ni aud 59 (90,000 tsh) na weekend (sunday) ni aud 118/hr (180,000 tsh). Expenditure zake ni aud 500/week rent, groceries ni aud 150-200/week, gas aud 70-80/week.

Haki ya nani huyu dada anajenga bonge la ghorofa hapa jirani, pamoja na kuwa amenipa clues tu chache na kuona positivity yake bado naomba michango yenu.

Asante sana, nikifanikiwa nitarejea kutoa ushuhuda
Kama mdada anakojozwa ikamuongezea kipato vipi wewe?kaka usikurupuke ukarudi unapaka lip sticks...
 
Sina uzoefu na Australia ila mkuu zamia tu. Mwanzo mgumu sana ila usitegemee utapewa ushauri positive hapa. Omba mungu na jikabidhi kwake na atakusaidia. Lolote ngumu katika safari yako usikate tamaa wengine ndo hivyo tena tunabadiri border tu maana hamna namna. Kuzamia yataka ujasiri na siku ukianza safari ndipo utawaza sana kwa nini umezamia!? Nani atanipokea? Je ni mtu mwema!? Lakini ukishatua tu utashangaa unakuta Watz kibao tu. Nipo South ila misele ya kwenda na kugeuza Botswana si issue sana
 
Mkuu kwanza ninashangaa jinsi unavyoona uamuzi wangu ni uoga au uvivu. Kiufupi hata nia tu ya kuthubutu kufanya hili ni ujasiri tosha, kwa miezi michache hiyo niliyonja kukaa huko nilipata ORCHE card, forklift Licence, High Rigid Licence na first aid course..kwa vile mwenyeji wangu alipenda nichangie kdg rent.

Kiufupi niko exposed kwa kiasi kikubwa tu, ila nimeomba uzoefu wa wenzangu hasa walioko huko majimbo mengine na kama kuna mabadiliko kdg maana kipindi naenda Kelvin Rudd ndio alikua Pm. Dhiki na shida inapunguza sana uchaguzi wa kazi ambazo tuna passion nazo mkuu, mm ningependa kua mwana mazingira lkn je what is my fate after getting 60? Kama maDr na maProf waliotusomesha nao wanalalamika maisha magumu sasa kwa nini na mm nikae katika mstari huo huo wkt nina miaka 25 ili nifike retirement?

Kiufupi I want to start with nursing to pursue my 'environmental mgt career' baada ya kua qualified nurse ila ukiomba visa kwa hizo degree za bongo ili upate kazi utakesha
Mkuu nakufatilia toka post yako ya mwanzo, huwa nipo interesting na thread kama zako, Mimi pia ninao ujasiri huo na by October nasepa nje kucheki fulsa, usipoteze muda kumjibu mdau kama ulivyofanya believe me watu wa aina hiyo hawezi kwenda hata Kenya kucheki fulsa, usipoteze muda na negative thinking za watu hapa, wewe jari positive thinking coz ndo zitakusaidia, binafsi na support uamuzi Wako, wewe nenda mkuu sio Siri kuwa nje fulsa Ni nyingi hasa za kutengeneza mitaji!
Kwenda nje inahitaji ujasiri na sio kila mtu anao, kuna watu wanaondoka wakiwa na mazingira magumu Kweli na wanatoboa, sembuse wewe ambaye naona uko vizuri financial, jichanganye mkuu!
 
Kama mdada anakojozwa ikamuongezea kipato vipi wewe?kaka usikurupuke ukarudi unapaka lip sticks...
Ni vizuri kama ushauri hauna unapita tu taratibu haya mambo ya kuwaza negatively hayatakusaidia chochote. Kila binadamu ana ndoto zake na malengo take hata akienda na kukosa tayari atakuwa amejifunza jambo mhimu sana maishani. Watanzania tuna roho mbaya sana japo kimataifa tunaonekana wapole na wakarimu
 
Mkuu nakufatilia toka post yako ya mwanzo, huwa nipo interesting na thread kama zako, Mimi pia ninao ujasiri huo na by October nasepa nje kucheki fulsa, usipoteze muda kumjibu mdau kama ulivyofanya believe me watu wa aina hiyo hawezi kwenda hata Kenya kucheki fulsa, usipoteze muda na negative thinking za watu hapa, wewe jari positive thinking coz ndo zitakusaidia, binafsi na support uamuzi Wako, wewe nenda mkuu sio Siri kuwa nje fulsa Ni nyingi hasa za kutengeneza mitaji!
Nimeamini kila jambo njema unalopanga huwa lina baraka za mungu. Jambo mhimu akifika huko awe na tabia zuri kwani atapata marafiki wema na ambao hawatamchoka. Akajishushe kwa lolote atakalokumbana nalo but baada ya muda ataanza kufaidi uvumilivu. Nje kuna fursa asikudaganye mtu pia aweke akili zake kama vile wanajeshi wanaotumwa kwenda vitani so lolote litakalotekea amwachie mungu
 
Ni vizuri kama ushauri hauna unapita tu taratibu haya mambo ya kuwaza negatively hayatakusaidia chochote. Kila binadamu ana ndoto zake na malengo take hata akienda na kukosa tayari atakuwa amejifunza jambo mhimu sana maishani. Watanzania tuna roho mbaya sana japo kimataifa tunaonekana wapole na wakarimu
Ulileta uzi ili upate ushauri na msomi hua anapokea advice then anafanya analysis kupata conclusion.. sasa kama ulitgemea usipate ushauri negative unanipa waswas na elimu yako kwa sababu haiwezekani muuza genge pale tandale anafamilia,ananyumba na anasomesha hawazi kutoka lakin ww unaingiza 1.5m monthly unawaza maisha magumu. Writing may judge enough.wewe si 1.5m earner per month ni sifa tu.
 
Back
Top Bottom