Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Nataka kwenda Australia kutafuta maisha

Ebana australia naitamani sana,ila sitaki kwenda kinjaanjaa.ngoja niwe mtamu inshaalah nkafanye ka vekeshen walau ka tuwiki tumoja
 
bongo tambarare wapi kaka. mbona hali hoi tu. fikiria miaka 10 ijayo utaweza kumsomesha mtoto wako shule private za maana?
 
bongo tambarare wapi kaka. mbona hali hoi tu. fikiria miaka 10 ijayo utaweza kumsomesha mtoto wako shule private za maana?


Mambo mazuri yapo mbele. Twe'nzetu Mkuu, usiniache.

Bongo giza hakuna mwanga, ukipata visa pasua anga !

-Kaveli-
 
Ndo kwenu lakini,hata kama umepata nafasi ya kusepa usipaletee dharau,maana ndo pamekutunza mpaka umepata ujanja wa kusepa

Hahaha sure home ni home tu aiseee Blessings hiyo uni iko kweli au ni Univ of Queensland? Nina wsws na data zako huenda ni fake hujapata admin hapo UQ, CRICOS provider ya UQ ni ngap?
 
mkuu kama kweli unataka utusue maisha tafadhali nenda katika nchi zifuatazo Shelisheli Ipo Africa,st Vincent And Grenadies,british Virgin Island Zipo Marekani Kaskazin Bila Kusahau Cape Verde Nakuhakikishia Ukirud Baada Ya Miaka Miwili Kama Hujajenga Magorofa Matatu Kwa Mpigo Mimi Fala..
Mkuu ya kweli haya?
 
Mkuu tujuze mpango wako umefikia wapi? Mimi nnatamani kujaribu maisha Canada, bado sijapata mtu wa kuniongoza!!

Mtafute rais wa wabeba maboksi atakupa mchongo - Nyani Ngabu
Ila kuwa makini na the toughest Sherrif in the Americas kama huna papers
 
Wakuu baada ya kumaliza chuo miaka kadhaa na kuhangaika kupata masters degree naona bado future yangu haiko salama ikiwa nikiwa naishi hapa Tz. Kupata mshahara wa 950,0000 na allowance ya 600,000 kila mwezi naona inaishia kuishi maisha ya hand to mouth. Sasa umri unaenda, na hakuna cha maana kinafanyika, na mzee Magu amebana mno hata hakuna deal kabisa, naomba msaada wa ushauri tu kwa wale wenye uzoefu wa Australia, na sio kwingine au kutoa kejeli zisizojenga kwani.

Mpaka nimefikia uamuzi huo wa kwenda huko kwa wazungu kwa sababu nina jirani yangu hapa alikwenda akasoma (Bachelor of nursing na akawa registered nurse), na bahati nzuri akapata PR na anafanya kazi ya nursing salary yake kwa saa ni aud 59 (90,000 tsh) na weekend (sunday) ni aud 118/hr (180,000 tsh). Expenditure zake ni aud 500/week rent, groceries ni aud 150-200/week, gas aud 70-80/week.

Haki ya nani huyu dada anajenga bonge la ghorofa hapa jirani, pamoja na kuwa amenipa clues tu chache na kuona positivity yake bado naomba michango yenu.

Asante sana, nikifanikiwa nitarejea kutoa ushuhuda
mbona wenzako tunatusua hapa tz ,tatizo wengi mnataka kuajiliwa , mimi nipo shamba fursa zipo kibao kuingiza kwa siku
250000 ni kitu kidogo sana fursa ya kilimo ,ufugaji na upandaji wa miti kwa ajlli ya mikopo kwenye mabenki.mimi kadgree kamoja ka mlimani kananisaidia sana kuwa na upeo mkubwa wa kujifunza zaidi,acheni uoga wa maisha,

maisha ya mjini yana changamoto m sana kwa maisha hsa hay ya magufuli
 
Kondoomwema! nionyeshe mkulima wa Tanzania japo mmoja tu aliyeweza hata kununua PASSO kwa kuuza mazao yake!! Msimuamini Masanja na stori zake zile, haiwezekani uwe msanii eti utusue kwenye kulima MPUNGA!! Vijana hawa wanatumika sana na Viongozi wao DINI!! Australia (Brisbane) Beibiii!!! Here I Come.
 
Back
Top Bottom