Nataka kumuacha mke wangu

Nataka kumuacha mke wangu

Maamuzi ya talaka yaweke pembeni kwanza,then nenda kwa kiongozi wa dini yako mwenye uelewa wa mambo ya ndoa na talaka, atoa ushauri kwa mujibu wa imani yako
 
Wanajamvi, ni kama wiki tatu hivi tumebahatika kupata mtoto wa kwanza lkn kabla wife hajifungua nilimpeleka kwa mama yangu kwaajili ya huduma baada ya kujifungua, ndo ilikua mara yake ya kwanza kwenda kuishi na mama mkwe, cha ajabu kwa kipindi chote alichokaa nae ameonesha utovu wa nidhamu mkubwa.

Hivyo nimedhamilia kuachananae muda tu atakapo pata nguvu. Hivyo wanaojua sheria za ndoa na jamii naomba mnijuze ni sheria gani inaweza kunibana ktk hayo maamuzi yangu.

Asante nawasilisha tafadhali.
Imeandikwa
wataachana na baba na mama zao
wawili mtaambatana.
Sasa wewe hukuachana na mama yako.

Wanajamvi, ni kama wiki tatu hivi tumebahatika kupata mtoto wa kwanza lkn kabla wife hajifungua nilimpeleka kwa mama yangu kwaajili ya huduma baada ya kujifungua, ndo ilikua mara yake ya kwanza kwenda kuishi na mama mkwe, cha ajabu kwa kipindi chote alichokaa nae ameonesha utovu wa nidhamu mkubwa.

Hivyo nimedhamilia kuachananae muda tu atakapo pata nguvu. Hivyo wanaojua sheria za ndoa na jamii naomba mnijuze ni sheria gani inaweza kunibana ktk hayo maamuzi yangu.

Asante nawasilisha tafadhali.

Siku hizi kuoa ni kujitimizia tendo la ndoa na hakuna upendo wa dhati juu ya mkeo au mmeo! Ni ajabu mkeo kumpeleka kwenu eti akazalie huko! Ulioa ili upeleke kwenu! Sijaona japo katika agano la kale katika kitabu cha biblia mahala ambapo mke akitaka kujifungua anaenda kwao! Vibaba vya siku hizi ni viruka njia tu!! hata hadhi ya huo ubaba ni mashaka matupu! macho juu juu na viburi kibao! Huyo mama yako hajawahi mkosea ndugu na baba yako? mbona yupo na anaishi? Elimu ya shetani inatawala vichwa vya vibaba vingi na havina hata aibu kuja kuelezea ushetani na uibilisi wao!
 
Mke kama mnaelewana wawili yatosha, Kama wamekwazana mshauri mkeo amuangukie Mama yako. Myamalize all in all wewe hujaolea Familia wala ukoo ulioa kwa matakwa yako binafsi. Kama mtoto aliye zaliwa ni wa kwako yatosha, Ucmuache bint wa watu akaenda kuteseka na kichanga kisio na hatia.
THINK OUT OF THE BOX.

He is in the box now.
 
Mkuu Fedora
Sijaoa lakini ninachojua hao watu wawili hawachangamani (mke na mama mkwe). Kwanza katika hali ya ujauzito mke alihitaji matunzo na wajawazito huwa wanamabadiliko ambayo hata mume hukasirika sembuse mama mkwe ambaye hajui utamu wake??
Fikiri kabla hujaamua, huo udhaifu ulitakiwa kuujua kabla hujamuoa na uukubali kwamba utaweza kuuvumilia na hautakusumbua sasa wewe kama uliangalia tako ndio matatizo hayo. Wewe ndio umekosea sio yeye kaa nae mvumilie na tako si analo?

Asante,
Sitaki kujua sana haya mambo ya tako km analo au la ila ukweli ambao naanza kuukubali ni huu wa kuyajua udhaifu kabla sijamuoa, na nilijitahidi kufanya hivyo lakini lol! Kumbe nilikosea. Je siwezi kujinasua hapa niliponaswa kwa utaratibu mzuri tu?
 
Mh Asante kwa huu ushauri japo na yeye wakati wa uchumba hakua na tatizo la kum-disqualify, ila baada ya miezi kadhaa ndani ya nyumba akaota mapembe
Kama hakuwa hivyo, hujawahi kufikiria inaweza kuwa ni spiritual attack? Jaribu kuexplore upande huo kabla ya kuachana.
Utapata mwingine utkatemuona anafaa lkn ukimuoa anabadilika.
 
Kama hakuwa hivyo, hujawahi kufikiria inaweza kuwa ni spiritual attack? Jaribu kuexplore upande huo kabla ya kuachana.
Utapata mwingine utkatemuona anafaa lkn ukimuoa anabadilika.

Spiritual attack?? Sijawahi kufikiria hii kitu
 
Kuna makabila hapa TZ ambayo kiutamaduni kama mke wa kijana wao anajifungua, basi kijana atampeleka mkewe kwa wazazi wake(wazazi wa mke) ili akale uzazi huko. But gharama zote zitakuwa juu ya mume na familia ya mume! Kwa maana hiyo, binti atakula uzazi kwa mama yake mzazi na sio kwa mama mkwe wake!

Huu uzi umenionyesha kwamba huu ndio utamaduni mzuri!...yaani wakati wa uzazi binti aende kwa wazazi wake waliomzaa kwani huko atajisikia huru zaidi kuliko kwa mama mkwe!

Wanajamvi, ni kama wiki tatu hivi tumebahatika kupata mtoto wa kwanza lkn kabla wife hajifungua nilimpeleka kwa mama yangu kwaajili ya huduma baada ya kujifungua, ndo ilikua mara yake ya kwanza kwenda kuishi na mama mkwe, cha ajabu kwa kipindi chote alichokaa nae ameonesha utovu wa nidhamu mkubwa.

Hivyo nimedhamilia kuachananae muda tu atakapo pata nguvu. Hivyo wanaojua sheria za ndoa na jamii naomba mnijuze ni sheria gani inaweza kunibana ktk hayo maamuzi yangu.

Asante nawasilisha tafadhali.
 
Asante kwa ushauri wako lakini nilimpeleka kwetu baada ya wazazi wake kunikatalia kwa kusema mila haziruhusu. Pia ujinga alioufanya huko hata kwangu alishafanya na nikamkataza lkn hakusikia

Mkuu sasa utaacha wangapi, Kumbuka Mama yeye tayari ana familia yake na wewe hii ndio familia yako inatakiwa uilinde kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote na ikiwezekana kwa dam yako. leo unamwacha mke na mtoto fikilia dingi na yeye angekufanyia hivyo those days wewe bado kadogo. Ndoa ni ya watu wawili. ndugu hawahusiki kabisa kwa sababu mwisho wa siku watoto wale ni wako si wa ndugu zako. Sikatai ndoa huwa zinavunjika lakini isivunjike kwa sababu ya ndugu kuwe na sababu zenu tu.
 
Back
Top Bottom