Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

Aslan Hatun

Senior Member
Aug 31, 2021
104
352
Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.

Nilihamishwa kikazi kutoka Dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikuwa mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na Dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.

Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikuwa anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.

Nilikuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kuwa wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokuwa zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mimi mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.

Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia simu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.

Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kuwa yawezekana nimeshakanyaga waya.

Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)

Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba.

Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama ni kujifungua basi itakuwa mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa

Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana (mtoto wa kiume, ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)

Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mimi nasema kama mimi ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mimi nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitumika ndio kwa mbaali wakapunguza.

Jina hili limeendelea kuitwa na kutajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo, mimi nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo.

Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kufanana na wakubwa zake Wala mimi Wala yeye mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha.

Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kugombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawa imetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lakini moyoni naumia Sana.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi, huwa nakuwa na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokuwa yangu.

Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mimi hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba.

Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kuwa mimi uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili, nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mimi aniache nilee watoto wangu wawili

Naombeni USHAURI WENU wadau mwenzenu, niko dilemma.

NB: Matusi nisingependelea kuyaona
 
Jul 3, 2014
95
226
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Umefanya maamuzi mazuri na sahihi kwa muda huu. Afya yako ya akili ni muhimu zaidi vilevile utulivu wa nafsi. Umri wako wa 35 years bado una kesho nyingi za ujijenga kiuchumi wako na watoto.

Hakupitiwa na shetani ila timing yake ilikuwa mbaya.

Pole sana comrade.
 

44mg44

JF-Expert Member
Jun 16, 2019
1,082
1,046
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Kwanza kabisa tuliza akili yako na ukubali kuwa Jambo Kama Hilo limetokea, kama wewe ni mvumilivu, vumilia tu, nifanye Kama hujui, Kama huwezi kuvumilia basi mtimue tu huyo wife wako!

Maana angekuwa na akili angefanya uzinzi bila kupewa mimba, namaanisha angechukua tahadhari ili asipewe mimba, lakini kitendo cha kuamua kufanya hivyo hivyo mpaka mimba juu hapo kakudhalilisha Sana aisee!!

Ndoa kaidharau Sana.
 

HS CODE

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
268
706
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Kisaikolojia binadamu akikumbana na changamoto, huwa kuna hatua ya kuikataa au kutoikubali, asipokuwa makini inaweza kupelekea maumivu makali yatakayosababisha kujidhuru au kumdhuru aliyemsababishia.

Kwa sasa, wakati unaendelea kutafuta ufumbuzi, nashauri umrudishe mwanamke na mwanae ambaye amekiri sio wako kwao au mpeleke mbali usikoweza kumfikia kwa urahisi. Lengo ni usalama wako, wake na wa mtoto.
 

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
51,656
64,250
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Nilihamishwa kikazi kutoka dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikua mwaka 2019 ikabidi wife na
Pole sana mzee ila wahenga walisema kitanda hakizai kharamu! Usiharibu familia yako haya mambo yapo tangu enzi na kuna jinsi wazee wali-handle haya mambo! Watafute!
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
21,202
28,025
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018. Nilihamishwa kikazi kutoka dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikua mwaka 2019 ikabidi wife na
Wanawake ni washenzi sana. Kwa kweli kitendo cha kugegedwa mpaka unapata mimba ni dharau kubwa sana kwa mume. Yaani huyo mwanawane wala usiangalie nyuma... achana nae kabisa. Dah watu wanagegeda na kunyunyuzia mbona kabisaaa.

Hapa ndio unapo amini bora ugegede malaya hutapata ngoma kuliko kugegeda mke au gelofrend
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
46,312
78,133
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018...
Ukijua tu Saikolojia ya Mwanamke yoyote kuwa hawezi Kukuvumilia pale ukiwa mbali na kwamba hata Wao ni Binadamu na wana Nyege na kuhitaji Kuliwa wala huwezi Kuhangaika nae au Kuhoji kama Mimba uliyomkuta nayo ni yake au yangu Mimi Msela ( Bachela wa Kudumu ) GENTAMYCINE, ila utavumilia na Kufa na Tai Shingoni ili Maisha mengine yaendelee.
 

ChoTar11A

Member
Aug 5, 2022
5
6
Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Pole sana mkuu uamuzi ulochukua simbaya lakini msamee mkeo mlee watoto coz watoto wataishi pasina furaha ikiwa mama yao hatakuwepo nyumbani kama vip huyo mtoto akikua umri furani mkeo ampeleke mtoto kwa baba yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

104 Reactions
Reply
Top Bottom