Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Wadau, mimi ni mteja wa Zain tangu mwaka 2004. Niliponunua simu nilipewa sim card ya Voda kama offer ikiwa na shilingi 1,000/- na baada ya mwezi mmoja nilihamia Tigo (Mobitel wakati huo) baada y kuona kuwa Vodacoma wako ghali sana. Mwaka 2004 nilipoteza simu na hivyo niliponunua simu nyingine nikaamua kuhamia Celtel baada ya kuona mahali nilipokuwa mandao wa Mobitel unasumbua.
Baada ya Celtel kubadilisha jina na kujiita Zain, walituandikia wateja kwa sms kuwa wanakuja na mfumo mpya wa bonasi badala ya ule wa zamani kwa ajili ya wateja wao waaminifu (loyal customers). Baada ya kuingizwa kwenye hilo daraja la loyal customer kuanzia Novemba, Zain wakaja na mfumo mpya wa bonasi za kulazimisha ambazo ndo zinanifanya kutaka kuhamia mtandao mwingine. Kwanza walianza kutuandikia wateja sms kuwa ongeza 40,000/- kabla ya tarehe fulani upate bonasi ya shilingi 12,000/-! Kwa kweli mfumo huo unanikera na juzi nimepokea sms nyingine ati niongeze shs 40,000/- kabla ya tarehe 26 Dec ili nipate bonus! Ilinudhi sana maana nilidhani ni sms ya muhimu. Zamani Celtel ukiongeza airtime kwa muda fualni unatumiwa sms kuwa umepewabunus ya shilingi kadhaa na si kushawishiana kutumia ili upate bonus kama sasa.
Mfumo wa sasawa kupata bonus na hasa kunitumia sms ati niongeze shs kadhaa kabla ya tarehe fulani ili nipate bonus umekuwa kero kwangu maana sioni sababu ya kunishawishi kuongeza matumizi ati nipate bonus.
Wana JF nimeazimia kuachana na Zain, Je, nihamie mtandao gani ambao ni bora zaidi?