Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Inawezekana mkuu, Mimi nikikumbuka yakwangu mbaka nacheka.
Nilishtukizatuu watu wakashangaa ninafungandoa wakaja kanisani ilenatokatu naingia kwenye kimeochangu na wife naona watu rundo wananipigia vigelegele na magari yananifuata sijui ilikuwaje wengine nikawakuta home dah nilishangaasana.

Walinilaumu sana, wakajichangisha michango ya gafla waka nunua gambe sherehe ikawa hapohapo nyumbani hadi saa saba usiku maana kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndio walikuwa wakipigiana cm na kuongezeka.
Kwakweli sikuamini.
Mimi nimchangiaji mzuri wa harusi za wenzangu lakini yangu sikutaka kusumbua mtu nikaamua kufanya kimyakimya.
 
Mkuu uko sahihi sana, Mimi mwenyewe tarh 28 mwezi huu nafunga ndoa kama yako, mke wangu ni mwalimu hivyo kuwachangisha watu ni kuwasumbua tu, mungu akubaliki sana mpendwa
Ayaaa
Mkuu mimi mwenyewe nataka kufanya hivyo mwenzi wa 12
Chek na uyu
Safiii saaana mkuu..nakuunga mkono..hata Mimi nipo njiani kufanya hivi hivi..mungu akusimamie mlitimize
Kumbe mko weng
Mbona poaw tu Hiyo Kiongozi wanguu mm mwenyewe mwakani nafanya hvyo, na sio kwamba fedha sina but naona ni usumbufuuu tu mambo mengne tunacomplicate sana shereheee , fedha na muda oia
Wanaume vyuma vimekaza naona ubunifu mpyaaa
Kuna jamaa yangu kafunga juzi tulienda kanisani watu kama 10 mpaka padri alishangaa maana hapakua na shangwe lolote lkn padri alisema amependa iyo staili na kwenye mahubiri yake alisema ndoa ni watu wawili na wazamini wao mengine ni mbwembwe lkn kibaya yule jamaa yangu alichangisha watu
Aya sasa
Mkuu achana na sherehe Ni gharama tu ambazo baadae unajuta Kama unataka mke achana na sherehe mtasherehekea chumbani
Wachek na hawa
Mimi mwenyewe nataka kama hiyo pale kibangu
Magu noma
Hata mimi nataka kufunga ya hivyo, ila mama watoto kagomea, nilimwambia sipo tayari kwa sherehe maana sina hela akiwa tayari kufunga ya kimya anijulishe.
Aseee
Duh! Ngoja na mimi nikaoe aisei make kujipanga na harusi hatimaye uhenga utanikutiliza sasa..!
Akili zimekaa sawa tunabana matumiz
Ndio mpango wangu huo, nitaenda kufunga ndoa. Tukimaliza tunaenda zetu honeymoon, watu wanaosubiria sherehe wakafanyie kwao.
Hata ww
Funga tu mkuu, hata mimi muda si mrefu nafunga ya namna hiyo.
Usijal
Wewe una fikra kama zangu sema muoga tu.
Usiogope sema ogopa sababu ya kuogopa
Mimi pia mwez wa 10 napiga ivoivo biashara za kuanza kulipa madeni baada ya harusi cztak..
Duh
Kumbe wenye mawazo ya aina yako tupo wengi,ubarikiwe na azma yako mkuu
 
Hiyo ndiyo akili. Maana sasa vurugu za kadi zimeanza kwani nina7 mpaka sasa na Desemba ndiyo inasogea sijui zitafika ngapi maana zinazidi kumiminika na kiwango cha chini kwa kadi moja ni 100000
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii...

Upo sawa kabisaa bro, hata mimi nategemea kufanya hivyo wakati ukifika. Nitafunga ndoa ya kimya kimya/isiyokuwa na gharama kubwa.

Binasfi sioni maana ya kufunga ndoa ya milioni 15-20+ kwa ajili ya kulisha na kunywesha watu!

Mfano:
Gharama ya ndoa ni milioni 15,000,000/- kulingana na mahitaji na mapendekezo ya bwana na bibi harusi, hapo lazima Bwana harusi atatoa milioni 3-5.

Kumbuka, huwezi kutaka harusi kubwa kwa kutegemea michango ya ndugu jamaa na marafiki tuu! Lazima uwe na kianzio.

UZURI WA NDOA YA KIMYA KIMYA

1. Hela yako utafanyia mambo mengine ya mandeleo

2. Haina stress ya kuchangisha na kufatilia watu kila mara

3. Hauhitaji kukopa ili ujazie bajeti

4. Hutojutia ikiwa ndoa itakuwa ngumu huko mbeleni

5. Ukiwa na milioni 1,2,3 au 5, unawachukua watu wako wa karibu, mntafuta sehemu mnajipongeza mambo yakwenda vizuri.
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Unaisoma namba kwa visingizio. Anyway ndoa inafungwa hata bila sherehe
 
Safi sana !! Vijana sasa badilikeni. Michango ya nini? Weka tu vihela vyako kwa expenses za honeymoon basi. Sana sana kama ni sherehe iwe kwa wakwe na watu wa karibu sana - wasizidi ishirini. Piga tu picha za ukumbusho inatosha. Usitake michango kabisa. Watu wanasema wanakuchangia milioni 25 lakini WALIOKUCHANGIA WANAZILA ZOTE WAO. Wanakuacha bila kujali hata kumega kidogo kukulipia kodi ya nyumba. Kama ni kukuchangia kwa nini hizo walizochanga wasikupe? Waseme tu wanachangishana ili wale na wanywe kwa kisingizio wamekuchangia wewe.
 
Ayaaa

Chek na uyu

Kumbe mko weng

Wanaume vyuma vimekaza naona ubunifu mpyaaa

Aya sasa

Wachek na hawa

Magu noma

Aseee

Akili zimekaa sawa tunabana matumiz

Hata ww

Usijal

Usiogope sema ogopa sababu ya kuogopa

Duh
We jamaa ni noma sana duh
Ulivyoquate .
Maisha yamebadilika
 
Atakuwa bidada huyoo...mwanamke ndoa bila harusi anaona ni matusi makubwa kwake!

Watu tumetofautiana asee....nilivyo na uchungu na hela, halafu kirahisi rahisi ikalipiwe ukumbi, sijui Gari la kutubeba, kunywesha watu bia! Mume wangu hajafanya huo upuuzi nikamvumilia!

Kulaaaaa LIKEEE
 
tatizo ni huyo bibie atakuelewa au vip,maana hawa wadada wanatakaga kuvaa shela ili kuringishiana
 
Aisee ulijuaje maana hata mimi pia huwa sipendi complications maishani.Ikibidi hata nisichangishe watu kabisa, Ila nahisi bibie lazma agome wanawake hawa wana kasumba ya kutambiana.
Hapa hesabu video & photoshoot kali, ukumbi mkali, gari ya kifahari ya kutubeba on the event havikwepeki aisee.
Afanye "Bridal shower" ambazo huwa hazituhusu kwa kweli. Harusi ni mipango ya mwanaume. Hapa simama. Hizi sherehe zingekuwa biashara tungekuwa mamilionea. Jinsi unavyosumbuka kisaikolojia mpaka hiyo sherehe ifanikiwe. Hapana. Ifike wakati tubadilike. Tatizo hawa wenzetu wanataka kuonekana!
 
Kaka angu alifanya sherehe ya harusi yake kwa gharama ya milioni 50...mpaka Leo anajuta!

Umesema milioni 50,000,000/-
AU NIMESIKIA VIBAYA?!!!

Alikuwa pedeshee ndama au pedeshee kuku?!!! Ana moyo MKUBWAAA!!!

Natania lakini daaa...nilioni 50 ni hela nyingi aisee!!! Kuichoma moto kwa usiku mmoja ni HARAMU na kejeli kwa Watanzania wengi.

Hata kama ilikuwa ya kuchangiwa, wasimamizi walitakiwa watengeneze bajeti angalao ya milioni 30, nyingine wawakabizi au wawanununilie chochote cha maana.

ANAJUTA KWA SABABU HAKUJIPANGA AU BIBIE ALIMJAZA UJINGA! Maana mwanamke ana nafasi kubwa sanaa ya kumjenga au kupoteza mwanaume.

HAIJALISHI MWANAUME NI MJANJA AU NI...HUO NDIO UKWELI.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom