Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Fanya hima mkuu,wengi watakuiga baadaye.
wengi wanakufa na tai shingoni kwa kukosa
mtu wa kulianzisha,ukishaanzisha wengine
wataunga tela.Lakini hakikisha umekubaliana na mwali wako.
 
That is a Good Idea, Kufanya masherehe makubwa ni shoo tu lakini kama nyote mmepatana na mwapendana kwa dhati hiyo ni Nzuri sana
 
Ahsanteni kwa michango yenu na mungu awabariki,nitaleta mrejesho nimepanga kufanya hivyo tar 9 December
 
Hakuna tatizo mkuu ila cha msingi mkeo nae awe na idea kama yako vinginevyo kuna ka nuksi katamea taratibu na hutakijua hadi upate tatizo kwenye hio ndoa.

Kila la kheri mkuu.
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Wazungu wenyewe waliobuni maswala ya ndoa kufungwa kanisani huwa wanaenda wanne tu kanisani then pete ikivalishwa wanasepa zao sisi ma ngedere tunacomplicatisha mpaka magari ya matangazo ,ukumbi wa mil kadhaa mara gari la matangazo,mara chereko cherereko damn it inaudhi kichizi
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?

Huna maamuzi?
 
Wanaume wengi sana wangependa kufanya hivi....tatizo ni vigumu sana kupata mdada ambaye atakubali hii. Wengi wamefanya sherehe ili kuwaridhisha wenza wao ama wazazi
 
Mkuu uko sahihi..mimi mwenyewe hiyo kitu ya sherehe ndo big problem...nilimwambia sherehe sio ishu...cha msingi ni pale kanisani Mungu kubariki kupitia mtumishi wake

..akanigomea anasema eti yeye ataonekanaje kwa wenzake?eti mwanadada ana siku mbili muhimu mbili siku ya kufa na siku anayo olewa.....

Yaani shida tupu!

Kaka mimi mwenyewe nilijaribu kutoa suggestion ya kutofanya sherehe, the lady alikuja juu sana kukawa na ugomvi mkubwa. Na akasema kabisa kama sina mpango nae nimwache mapema. Akadai hio ni kumdhalilisha....na machozi juu. Sijawahi kuelewa hizi sherehe kwann zinakua na umuhimu sana kwa wadada.
Hili swala la sherehe limewatoa sana jasho rafiki zangu. Most of the time the couple hawa enjoy kabisa huo ucku, ni kuwafurahisha tu watu ndani ya masaa machache kwa gharama zaidi ya millioni 25.
 
Na engagement day( kuvarishana Pete ya uchumba ) - kuna umuhimu wa sherehe.

Vipi kuhusu SEND OFF- Kwa mwanamke , napo sherehe inaweza kupita kimya kimya

Naomba mawazo yenu juu ya hilo
 
Na engagement day( kuvarishana Pete ya uchumba ) - kuna umuhimu wa sherehe.

Vipi kuhusu SEND OFF- Kwa mwanamke , napo sherehe inaweza kupita kimya kimya

Naomba mawazo yenu juu ya hilo

Mimi nadhani vyote havina umuhimu wa sherehe, labda hafla fupi
 
Back
Top Bottom