Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Nakuunga mkono100% kazi yakukusanya michango si mchezo kipindi hiki
 
Mkuu, nilisimamia harusi ya kijana mmoja anasoma UDM ilikuwa simple sana, haikuwa na michango wala nini, kijana baada ya kutoka kanisani, hafla ilifanyika uwanja wa maonyesho wa mal Nyerere tena nje siyo ukumbini, watu walidhani ni kikao cha harusi baada ya kujua ni sherehe ya harusi walisogea kuona maana hawakuamini. Nilimpongeza sana kijana yule kwa kumuambia watu tunasoma kujikomboa kifikra na siyo kufanya mumbo kwa kukariri, tunakuwa watumwa wa mawazo ya watu. Tukatae.
ni kweli mkuu aisee tuache kukariri
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Safanya linalowezekana hali ni tete!
 
Sheria ipi mkuu? Labda kwa upande mwingine; Ila kwa Wakristo hakuna Sheria; Neno la Mungu linasema ivi Ukiwa na Neema uko juu ya Sheria, Simply ni kwamba ukiwa na Neema ya Mungu Sheria haikusumbui.

Labda useme ni Sherehe ni Utamaduni na sio Sherehe ni Sheria.
Hata ktk uislam hakuna sheria ya ndoa ni sherehe hakunaaa
Ni wahusika,mashahidi na mawalii wa ndoa tu (baba au kaka wa kutoa tamko?
 
Sheria ipi mkuu? Labda kwa upande mwingine; Ila kwa Wakristo hakuna Sheria; Neno la Mungu linasema ivi Ukiwa na Neema uko juu ya Sheria, Simply ni kwamba ukiwa na Neema ya Mungu Sheria haikusumbui.

Labda useme ni Sherehe ni Utamaduni na sio Sherehe ni Sheria.
Tena kiislam hizi ndoa za kichamungu
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Usichangishe, fanya harusi kwako ila angalia mimi yalinikuta haya:
Nilifunga ndoa sitaji wapi ila sikuchangisha, nilimwambia kila mgeni aje na chupa yake ya wine. Nilikuwa na vyakula, vinywaji sisemi mengi maana majanga yalitokea ila ndo hivyo ndoa ilifungwa na sherehe ilifanyika. Wavamizi hawakosi hata ufanyeje tena wabaya kuliko ungealika. Wengi Mungu kawahukumu lakini kwa ubaya waliotufanyia walitanguia ila wazazi wetu wa pande zote walipata chakula ila kilichobaki kiliibiwa na wasaidizi waliojifanya marafiki pamoja na vinywaji vyote.
 
Mimi mwenyewe sikuwahi kuchangisha mtu, ila waliona aibu wengine wakaleta mwenyewe.

Na kwakua ilikuwa sio ya mchango nilifanyia nyumbani kawaida sana, na watu wakala na kunywa.

NOTE:

- Kwasababu hakukuwa na michango sikupata malalamiko ya aina yeyote zaidi ya sifa.
- Watu wote sasa hawanipi kadi as wanajua SITAKAA NICHANGIE KAMWE HARUSI.
 
Hiyo ni poa lakini km unajiweza Fanya sherehe ili iwe ni kama kumbukumbu yako kimaisha.lakini pia inabidi MKE wako aweameridhia usije ukawa umemkwaza maana wanawake wengi wanaamini ndoa bila sherehe ni kama wameporwa
 
Nawafahamu wengi wamefanya hivyo. Unakwenda kanisani baada ya ibada unakuwa umeandaa sehemu ya kupata dinner watu wachache mnafurahi na maisha yanasonga mbele kama waliofunga ndoa zenye sherehe za mamilioni kwa siku moja.
 
Ujinga huo, we put money on long term investments...Mwambie apambane na hali yake, ufahari huo sionagi maana yake!
Namwonea huruma mnoo he's my blood brotha

.....kingine ni mtu peace mnoo, akiwa na hela ujue shida zako zimeisha kwa mda!
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Uko sawa, sherehe ni mbwembwe tu hazina kizuizi ktk kufunga ndoa. Tena ndoa ikiisha unamwambia na mkeo tangulia nyumbani mimi naenda kuangalia mpira.
Nimeipenda sana hiyo.
 
Back
Top Bottom