Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Kua na msimamo mkuu,kama wewe na mwenzio mmeamua hivyo bas ni fresh, sherehe yenu iwe honeymoon yenu
unajua ni kasumba tu kwa baadhi ya waafrika kwamba lazima lisherehe likubwa na wakat you can do something good and simple for both of you
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Ndoa kanisani sherehe ni anasa tu mnatumbua milioni 20 kwa masaa machache watu wakishaondoka mnaendelea kula ugali wa kulumangia
 
Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Hao wanaokushangaa.... ukiwapelekea kadi za michango wanalalamika chini chini....!!! Binadamu bhana...!!!
 
Mkuu tuko pamoja.... Hiyo ni namna nzuri sana

Fanya hivi... Alika ndugu jamaa na marafiki wote hapo kanisani, baada ya ibada mnapata kama robo saa ya kuabudu na kusifu kwa shangwe kuu ndani ya kanisa

Baada ya hapo mnapiga picha za ukumbusho nje ya jengo la kanisa kisha kila mtu atawanyike kwenda kwao. Itakua poa sana mkuu usijali

Ntakucheki PM
Asante sana
 
Mi nmeshawai kuona hyo ni nzur kama huna hela ya kutosha na utak lawama watu wameondoka na bajaji wakarud na miguu na pete zao wakaendelea na kaz zao kama kawaida
 
Mimi nilifunga ndoa wilayani, tukaenda nyumbani kuwajulisha majirani basi. Mimi ni mlala hoi ila hata ninazo mambo ni yaleyale, pesa ya sherehe napanua vimradi vyangu. Mchango wa kusaidiana shida mbalimbali natoa kadiri ya uwezo wangu
 
Wanaume wengi hawapendi mambo ya sherehe sometimes hawa dada zetu ndio wanaforce sana.
Mkuu uko sahihi..mimi mwenyewe hiyo kitu ya sherehe ndo big problem...nilimwambia sherehe sio ishu...cha msingi ni pale kanisani Mungu kubariki kupitia mtumishi wake

..akanigomea anasema eti yeye ataonekanaje kwa wenzake?eti mwanadada ana siku mbili muhimu mbili siku ya kufa na siku anayo olewa.....

Yaani shida tupu!
 
Harusi ni chanzo pia cha kuharibu kilichounganishwa. Nakumbuka kushuhudia Sherehe moja kule kusini ndoa iliyofungwa mchana ilikuja kuvunjika ukumbini. Simply bibi harusi kumbe alikuwa na mchepuko hadi dakika ya mwisho. Wakati wa kutoa Zawadi ilishangaza Zawadi zote zinaingizwa kwenye gari la hawara. Hakika harusi ile ingekuwaje DAR, Kiu na Ijumaa weekenda wangepata stori ya wiki nzima.

Achana na Sherehe. Wanawake ndio wanashinikiza sana mambo ya harusi. Kwake ndoa sio muhimu. Anachowaza ni harusi tu. Anataka awatambie wenzie. Ndoa za kimya kimya ndio hudumu sana na zina upendo wa hali ya juu.
 
mh!wanawake kumbe wanabadilika atiiii!!!!
hii mada hakuna mwanamke anayeonesha kumpinga mtoa mada!!!!wakti wao ndo huwa wanawatesa vijana wa watu kwa kupenda ufahari!!

jamaa mpango wako na utimie!
mi nilioa mwaka 2014 kwa sherehe kubwa ili nimfurahishe mwanamke but ndoa yetu haikumu mwaka 2015 ilivunjika!

cha muhimu ni cheti cha ndoa baasi,sherehe ya ndoa ni sawa sawa kabisa na birthday ya mwanao,kwa hiyo haina umuhmu na ni USHAMBA MKUBWA!
 
Safi Mkuu kuchangishana imepitwa na wakati,bora ukapiga part ya kimya kimya kuepuka usumbufu usiokuwa na maana yoyote.
 
Wakati nafunga ndoa Padre alisema ndoa ya kweli na Mwenyezi Mungu anayo itambua ni makubaliano ya wausika wawili, hivyo yeye ana bariki tu.

Fanya kile kinachofaa kwa nyie wawili na sio kutazama upande wako au upande wa watu wengine.
 
Back
Top Bottom