Nataka kufunga ndoa bila sherehe

Hii imekaaje wazee mwezi December nataka kufunga ndoa KKKT Mbezi Dar. Sasa watu wananishangaa kwanini sichangishi na wala siwaambii.

Mchungaji wangu ameniambia kazi yake ni kufungisha ndoa hayo ni ziada,
Hii imekaaje? Au mimi ndio wa kwanza kufanya hivi?
Safi sana. Imekaa poa.
 
Atakuwa bidada huyoo...mwanamke ndoa bila harusi anaona ni matusi makubwa kwake!

Watu tumetofautiana asee....nilivyo na uchungu na hela, halafu kirahisi rahisi ikalipiwe ukumbi, sijui Gari la kutubeba, kunywesha watu bia! Mume wangu hajafanya huo upuuzi nikamvumilia!
Wewe ndio tunaendana nakuja inbox nataka sana nimetafuta kwa mudamrefu wa aina hii
 
Mbona hiyo nzuri tu mkuu mimi sijaoa bado ila muda ukifika hata harusi sitafanya ni kutoa mahari tu maisha yanaendelea.
 
Nilishaapa, sichangii harusi ya MTU, na sitachangiwa yangu. Maziea hayo kwenye ndoa. Wakichangisha ya matibabu kwa mgonjwa na elimu nitafanya kwa moyo mmoja.
 
Back
Top Bottom