Nataka kufunga biashara yangu naomba ushauri

Introverted

Member
Oct 25, 2022
8
15
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani.

Wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizuri lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder.

Usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndiyo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi.

Chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache!

Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani.
 
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani. wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizur lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder,usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi, chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache! Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani
Umeweka kinga hapo?
 
Ninaelewa changamoto ulizopitia katika biashara yako ya mgahawa na ninaweza kutoa ushauri kadhaa kwa kuzingatia hali yako:

  1. Tathmini Gharama na Mapato: Kwanza, ni muhimu kufanya tathmini ya kina ya gharama na mapato yako. Kujua vizuri gharama zako na ni kiasi gani unachopata kutoka kwenye biashara itakusaidia kuelewa kama unaendelea kupata hasara au faida. Unapaswa kuwa na rekodi sahihi za mapato na matumizi.
  2. Tathmini Bei: Inaonekana kubadilisha bei ya ugali kulikuwa na athari hasi kwa biashara yako. Unaweza kufikiria kurudisha bei ya ugali kwa kiwango cha awali (1500/=) au kupunguza kidogo ili kurudisha wateja wako. Pia, unaweza kufikiria kutoa ofa au punguzo kwa wateja wanaonunua kwa wingi au kwa mara kwa mara.
  3. Ubora wa Huduma: Hakikisha unatoa huduma bora kwa wateja wako. Unaweza kuangalia jinsi ya kuboresha huduma yako ili kuwavutia wateja. Pia, kuwa na orodha yenye aina mbalimbali za chakula inaweza kuvutia wateja wengi zaidi.
  4. Usimamizi wa Gharama: Punguza gharama zisizo za lazima na ongeza ufanisi. Hakikisha unapata bidhaa kwa bei nzuri kutoka kwa wauzaji wako, na hakikisha kuwa unapunguza upotevu wa chakula.
  5. Matangazo na Ukuaji: Jaribu kutumia njia za matangazo kama mitandao ya kijamii, matangazo kwenye eneo lako, au ofa za kuvutia ili kuwavutia wateja wapya. Unaweza pia kufikiria kutoa huduma ya kujifungia chakula (takeaway) au kufanya usambazaji (delivery) ili kufikia wateja wengi zaidi.
  6. Usimamizi wa Madeni: Punguza kukopa kadri unavyoweza na jua jinsi ya kusimamia madeni yako vizuri. Ikiwa madeni yanazidi kuwa mzigo, unaweza kujaribu kupata mkakati wa kulipa deni hilo polepole.
  7. Kufanya Maamuzi: Hatimaye, fikiria kwa uangalifu ikiwa biashara hii bado ina faida au la. Inaweza kutokea kuwa ni wakati wa kubadilisha mkakati au hata kufikiria biashara nyingine inayoweza kufanya vizuri zaidi.
Ni muhimu kukumbuka kwamba biashara inaweza kuwa na changamoto, lakini pia inaweza kuleta mafanikio makubwa. Kwa kuzingatia tathmini ya kina na kufanya marekebisho sahihi, unaweza kuboresha hali ya biashara yako. Pia, usisite kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa biashara au washauri wa kifedha ikiwa unahitaji msaada zaidi.
 
Huenda wateja hawakufuata chakula bali walikufuata wewe. Walivyoona 'hucheki na kima',
Umenikumbusha, Nanukuu maelezo ya mdau: Inasemekana, kuwa biashara za Baa/vinywaji (Pombe/Bia) - Hii ni kanuni namba moja. "Weka warembo na wabadilishe kila baada ya muda fulni." hakika biashara yako itakuwa kwa kasi
 
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani.

Wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizuri lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder.

Usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndiyo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi.

Chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache!

Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani.
Shusha bei upate faida kidogo wakati unajipanga.. Biashara ya chakula ina changamoto sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe ni dini nyingine zaidi ya ulokole nenda kwa waganga ukaloge! Kama ulikuwa unabeza ulokole ujue kule kuomba na kukemea kwa Jina la Yesu na damu ya Yesu kabla na baada ya biashara katika maeneo yote ya ardhi na mipaka ya biashara na wateja na vyombo vya biashara, na sahani na maji (yaani kila kitu) kukisafisha na kukitakasa kwa damu ya Yesu (of course mambo ni mengi ya kujifunza katika kuomba) ndo mlango wa kufanya biashara ukaona wateja, pesa zako zisiibiwe na wachawi wa chuma ulete, uepushwe na mabalaa ya nuksi na mikosi itakayopelekea faida kwenda huko kama magonjwa, misiba, huruma za kijinga kama kukopesha, kukopwa, michango ya harusi na makusanyiko ya kijinga sijui jumuia, vikoba! Kwa ufupi kuwa ng'ang'ari achana na makanisa uchwara ya eti toa zaka, sadaka (hawa ni matapeli). Hata hivyo kutoa sadaka ni muhimu ili Mungu aendelee kuilinda biashara lakini changamoto unatoa sadaka katika madhabahu hipi? maana makanisa na watu wanaojiita watumishi wa Mungu ni mapandikizi ya shetani hata ukiwapa sadaka unajenga ufalme wa shetani. Nakusaidia nikupe madhabahu moja ambayo imenisaidia mimi (Mwalimu Christopher Mwakasege) kupitia namba za tigopesa/mpesa unaweza kujifungamanisha na hii madhabahu ni nzuri (uliza moyo wako ukiona una amani toa hapa) ni mahali sahihi utamuona Mungu. Acha mambo ya kuomba kijingakijinga kama walokole mapandikizi ya shetani kuwa kero kwa waliokuzunguka. Omba kisirisiri katika maeneo ambayo watu hawakuoni au hawajui kama unaomba hata ikibidi (mkeo/mmeo) hasijue kwasababu kikulacho kiko nguoni mwako, nk., n.k, Nimejitahidi kuandika haya kwasababu nimeona unahitaji msaada na mimi nilipitia hapa! Mengine omba Roho mtakatifu yuko karibu atakusaidia! Mwisho! Hamua moja kufuata uchawi au kuokoka nje ya hapo sahau kufanikiwa katika jambo lolote liwe kazini, shuleni, ndoa, mahusiano yako na hapo ndani ya familia, mtaani, biashara n.k
 
Achana na wanaosema ulozi, kifupi huja fanya analysis ya wateja wako, mtaani, km biashara yako haiko naeneo ya serikali basi ujue bei ya 2000 ni kubwa.

Mtaani ugari maharage buku, wao wanaangalia quantity sio quality, ndo mana wanawekewa hamira,

Si either uendane nao au utafute sehemu inayoendana na biashara yako.

Nasisitiza hapo hakuna uchawi,
 
Hapana huko atapotea mazima.. Mchawi bei hapo.. Watu wa uswazi hawataki ubora wanataka wingi kwa bei kitonga.. Ugali mboga 3 wanataka kwa buku jero.. Akishusha bei watarudi wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Ashushe bei hivyo vitu kaviokota? Lazima auze bei ya soko! Of course na akili ya biashara lazima ifanyekazi! Mungu anasema kuweni na maharifa "umetakataa maarifa mimi nami nimekukataa". Ukitaka kufanya biasha pia lazima huwe na maharifa juu ya sehemu hipi ufanye biashara ya aina gani? Wewe unafanyabiasha katika jamii ya watu masikini wa pwani unategemea kutoboa? Nenda mbezi mwisho tafuta kisehemu (bure) anza kuuza hivyo vyakula. Hakuna kodi cha muhimu ni mahali pa kuifandhia hivyo vifaa vyako ndo utalipia
 
Mimi ni kijana wa miaka 22 nimemaliza chuo mwaka huu nina degree ya kodi, baada ya kumaliza chuo kuna sehemu ya biashara nilipata ya mgahawa iko pwani.

Wiki mbili za mwanzo biashara ilienda vizuri lakini baada ya hapo kila tukipika chakula kikawa kinabaki maana kwenye suala la wateja baada ya kupika nlikua nazunguka kuchukua oder.

Usafi nilizingatia sana ila suala ambalo lilikuja kuniangusha nahisi ni kwenye bei maana chakula tulikua tunauza 1500/= ndiyo bei za huku baada ya mwezi ilibidi ugali niuze sh 2000 kutogana na gharama ambazo tulikua tunazitumia kwenye mboga, tangu tupandishe bei ya ugali mambo yamebadilika watu hawaji kula chakula kinabaki cha kutosha wale wateja nliokua nawafata wamerudi kwa watu wao walipokLesua wanakula zamani maana hapa nimezungukwa na mama ntilie kama watatu hivi.

Chakula kinabaki kingi inabidi niwe nakopa naongezea kwenye biashara ila madeni yanazidi kuongezeka nimekata tamaa na hii biashara ya chakula na hata nkisema niache!

Sijui nifanye nn jamani ni wiki mbili kila siku wali unabaki kama kilo mbili na ugali unakuta inabaki kama sahani saba hivi nisaidieni binti yenu jamani.
Lesson: badiliko la bei, badiliko la maokoto
 
Mchawi bei Tu hapo mkuu , maswala ya uchawi usijarbu kuamini mkuu utateseka Sana , Acha akili ifanye kazi , akili ikikuambia kwamba hili ni tatizo basi lifanyie kazi , usiidharau akili ukakimbilia maswala ya cheap solution za waganga utakuwa confused...hyo biashara nishawahi fanya na nilifukuza Wafanyakazi wote wa kike , nikabakiza mmoja tuu binti bandidu Yule anapiga kazi kisawa sawa , wengine wote wa kiume...

Ule mtaa walinikubali mpak Leo nikipita huwa wanataka nifungue tena mgahawa , kitu kingine kama unaona kushusha bei ili uendane na wala Hoi wa hapo mtaani ni miyeyusho basi lenga kundi Fulani Tu la wateja , kuna wateja wao wanataka huduma Bora tuu , haijalishi mtoa huduma ni Nani wao hawajali , hao ndo uwatengeneze , itachukua mda Ila utawapata
 
Labda umeingia kwenye mtengo;
Kuna mpango wanakuwanao mamantilie. Wanakubaliana wote(eneo husika). Mfano bei ya ugali 2000. Chai 200.
Wanaanza utekelezaji. Kati yao watauza ugali 1500 na chai 100 au bei waliokubalia wanapunguza kidogo badala ya kupandisha.
NB. Wale watakaokuwa na msimamo wa bei waliokubaliana kwenye kikao mara nyingi huwa wanafunga au kudorora sana kwa biashara zao.
 
Ashushe bei hivyo vitu kaviokota? Lazima auze bei ya soko! Of course na akili ya biashara lazima ifanyekazi! Mungu anasema kuweni na maharifa "umetakataa maarifa mimi nami nimekukataa". Ukitaka kufanya biasha pia lazima huwe na maharifa juu ya sehemu hipi ufanye biashara ya aina gani? Wewe unafanyabiasha katika jamii ya watu masikini wa pwani unategemea kutoboa? Nenda mbezi mwisho tafuta kisehemu (bure) anza kuuza hivyo vyakula. Hakuna kodi cha muhimu ni mahali pa kuifandhia hivyo vifaa vyako ndo utalipia
Sijasema atoe bure nimesema ashushe bei.. Nimekwambia uswazi hawataki ubora (quality) wanataka wingi (quantity)
Kuna michele inauzwa kilo 1500 mpaka 1800 nk
Kuna uchafu mwingi kwenye biashara ya chakula ukitaka upate faida.. Vingi sio halali
Wengi hununua nyama za wizi machinjioni
Samaki ni wale waliokaa zaidi ya siku 3
Kuku ni wa wizi ama vibudu
Nyanya ni zile salo nknk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom