Nilidhani mabinti wa dukani wanafanana, najuta kumpoteza binti aliekuwa ananifanya niagize mzigo kila wiki, nimebadili wawili ila biashara inasua

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
muda mwingi nipo kazini hivyo dukani naacha msaidizi.

Kwa miaka miwili mfululizo duka lilikuwa na wateja wengi na nilidhani mimi ndie mjanja nilieumiza kichwa kuchagua eneo zuri, kuweka bei, kuweka bidhaa original, n.k. yani niliona mimi ndio genius, kila baada ya wiki 2 mzigo ulikuwa unakata inabidi niagize, Daftari la mauzo lilikuwa linameremeta kwa kurasa zilizojaa mauzo. pesa za dukani nilikuwa nazitenganisha kwa mafungu ya milioni, simu za wateja wenye hasira hazikukauka mzigo ulipokata,

Ni kwa kipindi cha miaka miwili nfululizo mambo yalikuwa bampa to bampa, binti akaja kupata mimba na akaondoka, muda mchache baadae aliolewa na kuhama mkoa.

Binti alikuwa kaishia form 4 nikaona acha nijiongeze niweke waliosoma chuo hata kozi za secretary, hotel, tourism, n.k. maana huwa wanagusia masomo ya biashara... LOOOH! Biashaea imedorora sanaaaa.

Mabox yamekusanya vumbi, kukaa siku mbili tatu bila kuuza imekuwa kawaida, oesa nazitenga kwa mafungu ya laki, pesa za mauzo zinaishia kwenye mshahara, chakula, usafiri wa binti anaeuza duka.

nimebadili binti nimeweka mwengine kuna nafuu lakini mauzo bado ni ya kusua sua, mzigo hadi uishe inapita miezi mitatu
 
Duh, kweli nakubaliana kidogo na wadau wanaosema ishu ya nyota. Mimi dukani kwangu nnakaa masaa manne kwa siku, masaa mengine anakaa mkewangu. Nikiwepo mimi wateja wengi huniulizia 'yule dada yuko wapi'? Nawajibu ametoka kidogo, halafu wanaondoka, yaani akiwepo mkewangu anauza sana tofauti na mimi
 
Wenye elimu wezi,dharau kwa wateja pia wanapenda maisha makubwa kuliko uwezo wao
Hapana mkuu, nina ushuhuda kuna kijana mwenye degree alikuwa anauza duka la simu, acha kabisa ule moto, kiduka kidogo tu lakini simu kama 30 zinatoka kila wiki.

Bosi wake mkojo ulikuwa unambana akisikia kaenda interview,

ni baada ya mimi kupata mkasa unaofanana nikaanza kuunganisha dots,
 
Sio nyota, akili ya kibiashara mkuu.

Kuna wadada ukiingia tu dukani kwake unajua tu huyu anajielewa...

Anawafanya wateja wengi wasimuwazie mawazo ya ngono ngono, ukiweka mwenye nyodo kila kijana atataka ampitie.
 
Sio nyota, akili ya kibiashara mkuu.

Kuna wadada ukiingia tu dukani kwake unajua tu huyu anajielewa...

Anawafanya wateja wengi wasimuwazie mawazo ya ngono ngono, ukiweka mwenye nyodo kila kijana atataka ampitie.
kuna kitu nami nigusie, kuna siku alizinguana na mteja wa muda mrefu aliekuwa anaependa kushushiwa bei alimuwashia moto, mimi nikamwambia sio vizuri wateja watatukimbia, yeye aliniambia sipendi mteja mwenye dharau aishie zake,

mwili ulinisisimuka kuona jinsi anavyojiamini kwamba hata bila huyo mteja mambo yataenda tu.
 
Hili suala limenikuta mkuu, tangu nimtumue kijana kwa sababu za kukosa uaminifu, biashara imekufa kabisa.

Zamani kwa week nilikuwa nafunga hadi 1M, sahv kwa week nikifunga hela nyingi basi ni laki.. kupita siku 4 bila kuuza ni kawaida sana hadi nawaza niuze duka nihamie bishara nyingine
 
Hili suala limenikuta mkuu, tangu nimtumue kijana kwa sababu za kukosa uaminifu, biashara imekufa kabisa.

Zamani kwa week nilikuwa nafunga hadi 1M, sahv kwa week nikifunga hela nyingi basi ni laki.. kupita siku 4 bila kuuza ni kawaida sana hadi nawaza niuze duka nihamie bishara nyingine
ukiwa na kijana mwenye nyota yake hata akikuibia usimfukuze. hakikisha tu haui mtaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom