Hii ndiyo sababu kwanini mtaji wako unashindwa kukua

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,154
4,520
Habari zenu wadau

Leo nimekuja hapa nataka niwashirikishe sababu zinazofanya biashara nyingi kushindwa kukua na Nini cha kufanya ili biashara yako ikue

Nipo kwenye biashara kwa muda mrefu Kuna mengi nimejifunza kipindi naanza biashara nilikuwa nayumbisha sana mtaji mtaji kushindwa kukua Kuna mambo nilikuwa nakosea bila kujua nakosea inaweza ukawa unajinyima ili mtaji ukue lakini wapi unaishi maisha local ili mtaji ukue lakini wapi

Baadae nikaja kupata somo kumbe Siri ya utajiri sio ubahili kama wahenga walivyosema. Siri ya utajiri ni kuwa na elimu ya kazi/biashara unayoifanya. Hakuna kitu muhimu kama elimu kwenye biashara

Turudi kwenye mada yetu kwanini biashara yako inashindwa kukua ipo hivi wote tunaelewa ili biashara ikuwe ni lazima utengeneze faida kwahiyo biashara yako kushindwa sababu kubwa ni kwamba haupati faida toshelevu

Kuna jambo nimelifanyia utafiti kwa wafanyabiashara wengi wanajua somo la kufanya mauzo na kuongeza wateja lakini wengi hawajui somo lakutengeneza faida

Kuna njia mbili zitakazokuwezesha kupata faida

1. Kuwatumia wateja wachache wakuzalishie faida
hii inawafaa sana wafanyabiashara wadogo

1. Kuuza bidhaa zenye mzunguko mkubwa dukani
Njia hii inawafaa wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji

Tuangalie sasa makosa wanayoyafanya wafanyabiashara wadogo. Kosa kubwa nikufanya biashara ya mzunguko sababu bidhaa nyingi zinazopendwa dukani huwa na faida ndogo bidhaa nyingi zenye mzunguko dukani huwa hazina faida bidhaa nyingi zinazouliziwa sana dukani hazijawahi kuwa nafaida

Ni bora kumzingatia mteja anaye uliza bidhaa yenye faida kuliko wateja 20 wanaouliza bidhaa zinazopendwa sana

Kwanini uwaache wateja 20 na umzingatie mteja mmoja anayeuliza bidhaa yenye faida kubwa ipo hivi hili wengi hawalijui mteja mmoja anawakilisha mahitaji ya wateja 10 ukiwa na watatu ujue una wateja 30 Hawa ni wateja wengi sana kwenye biashara ukiweza kuwatumia vizuri

Ukiwazingatia wateja wengi utauza mauzo makubwa lakini ni ngumu kufikia lengo la faida hii nazani kwa wafanyabiashara mnalijua utakuta miaka inaenda lakini biashara haikui sababu kubwa ni hii njia hii inawafaa wafanyabiashara wakubwa wanaokopesheka na bank

Wakati washindani wako wanakimbilia kujumua bidhaa zenye kupendwa sokoni wewe unajumua bidhaa zenye faida mwisho bidhaa hizo zitakuwa chache sokoni hivyo kufanya thamani yake kuongezeka zaidi na kuziuza bei kubwa kwa wateja wako wachache
 
Back
Top Bottom