kante mp2025
Member
- Nov 11, 2022
- 7
- 13
Stamara wajada ni msingi kwenye kila kitu tunachokifanya, Kama wanasiasa wasemavyo vijana tujiajiri huku wao wakiendelea kukaa maofisini na wengine wakiroga waendelee kubaki kwenye hizo nafasi.
Kijana wa kimaskini nikasema ngoja nirushe ndoana katika ulingo wa biashara ndogo ya mtaji wa kawaida usiozidi laki tano.
Baada ya kusoma vitabu vya mashujaa wa ulimwengu wa biashara kama guru Robert Kioyasaki, na kupitia nondo za wakuu mbalimbali kama ontario nikajisemea kwa hizi maarifa nikirusha ndoana lazima inase
Basi bhana baada ya kumaliza masomo kwa kuwa mipango na maarifa nilikuwa nayo nikaingia kwenye biashara ya mitumba maana mataikuni walinitonya kuwa ni biashara ambayo bei unajipangia wewe kutokana na mteja aliyekuja.
Ukikosa stamara wajada katika biashara kuangukia pua ni kitendo cha kufumba macho na kufumbua , Ugeni katika biashara hiyo uliniponza vibaya sana kwani badala ya kwenda kuchagua nguo moja moja, nikaingia mzima mzima kwa kununua balo zima nikaambiwa hili ni first grade nikawapa pesa nikapewa mzigo kutoka mji mmoja mkubwa kwenda nao huko ndichi.
Shauku ya kujua yaliyomo ndani ilikuwa kubwa nilipofika tu geto nikasema jambo la kwanza ni kufungua kujua yaliyomo yamo,😁Kwa kweli ukisikia suprise basi nilipigwa suprise hadi miguu ikaishiwa nguvu na kuamini stamara wajada ni muhimu sana robo tatu ya viwalo vilikuwa kama zile nyanya masalo,😁kuna suruali zilikuwa zimetoboka, shati hazina kola, nililia kwa mayowe.
Nilipompigia mkuu wa wakuu aliyeniuzia kujua ananisaidiaje simu ikawa haipatikani, nikafunga safari kumrudia kesho yake nikakuta pamefungwa nilipoulizia wenyeji wakasema kahama muda mfupi uliopita😁
Nikajua bush boy nishaingizwa mjini, nikagugumia maumivu stamara wajada ikanisaidia zile nguo ikabidi nizipige mnada wa hasara kwa kuuza hata kwa mia mbili kwa mia tatu ikarudi hela kama ya kula kuku watano na bia kreti moja.
Nikagundua kwenye hii dunia sio kila mtu ni mfanyabiashara acha wengine tuendelee kuwa wateja😁Sema nawaheshimu sana wajasiriamali na wafanyabiashara bila stamara wajada biashara hutoboi.