Nataka kuanza kwenda kanisani

Nakushauri ukamuone Mama Zungu (Rwakatare), Zungu Kakobe, Zungu Mwingira, kama hawa hauwataki pale Mabibo karibia na baa ya Rangers kuna wale waNigeria (wakimashaka) wanahubiri neno la Mungu pia tena wana maajabu ya balaa kama vile nyoka anakutoka tu ghafla mfukoni, mtu kuanguka (msanii) toka juu ya mti huku akilia alitumwa na Mungu kuna wanigeria watamsaidia kuokoka ndipo akaja pale. Mbona makanisa ya hajabu yako mengi tu. Kama unataka ni pm nije nikuchukue nikupeleke ila mwezi ujao kwani kwa sasa niko mbali kidogo.

Mkuu umenichekesha sana..
 
makanisa kwaajili ya mazingaumbwe siyataki wala ya kulipa hela ili Mungu ajibu sitaki. Nataka kanisa dogo lenye imani ya kweli na unyenyekevu kwa Mungu

Hebu nenda pale Emaus Centre Ubungo, ukaonane na watumishi wa kweli wa Mungu..
 
ni kweli ila nataka kushirikiana na wenzangu kwenye ibada

Basi kama ni hivyo jiunge na jumuiya ili muwe mnasali kila siku na kuomba ila haya makanisa ya kishikaji (Ya wazungu wa sembe) watakulostisha tu na kukufirisi kila kitu huku mitume wenu/wao wanakula raha na kuwacheka kuwa wamepata wajinga wengine.
 
Nimeamua kuwa mkristo natafuta kanisa lakiroho nianzekwenda maeneo ya mabibo hosteli. Sio kanisa la mazingaumbwe noo kanisa la kuijenga roho yangu na uhusiano mzuri na Mungu mwenyezi

Latifaa; imani yapaswa iwe ndani yako na siyo kanisa flani, anza kuamini kwanza ndani ya moyo wako. Pili, kanisa ni nahala na wenzio wenye imani inayorandana, haina ubishi ili kumuona Mungu tunahitaji kujifunza neno lake tena kwa imani. Kukutana na wenzio ili kumtukuza Mungu na kumsifu ni jambo jema zaidi mbele za Mungu kwani inaonyesha umoja na mshikamano wetu mbele za Mungu. Hivyo basi kwa anslysis yangu ndogo ni bora kwenda kwenye makanisa yalio na misingi ya kumtumikia Mungu kwa usminifu, japokuwa baadhi ya wanaoyaongoza wana madhaifu ya kibinadamu, makanisa hayo ni Lutheran, Anglikana na Roman Catholic, sina uhakika na Pentecost. Makanisa ya kiroho siyo mabaya ila hayana system ya uongozi hivyo ni rahisi kwa kiongozi ama viongozi wake kurubuniwa na shetani na hivyo shetani kuchikua nafasi ndayi ya makanisa hayo. Kwanini nasema hivyo? Mskanisa mengi ya kiroho ni mali za watu binafsi, kwamfano kanisa la mama Lwakatware, Mzee wangu Kakobe na kaka yangu Mzee wa upako Lusekelo kwa uchache tukiwataja. Lakini Romani, Anglicans, na Lutheran ni system na hakuna mwenye umiliki na wala siyo Mali ya mtu flani bali mfumo maalumu wa watu kukutana kwa ajili ya kusifu na kuabudu wenye mfumu maalumu wa uongozi unawekwa kwa waamini wenyewe.
Nihitimidhe kwa kusema, kanisa halitskufikisha mbinguni bali imani yako mbele za Mungu na kufuata maagizo ya mwenyezi Mungu kama alivyoagiza. Makanisa yanakusaidia kuikuza tu hiyo imani yako lakini hayana nafasi kubwa ya kukuhakikishia afya yako kiroho.
Nauhakika na naamini kwa sehemu kubwa, japo mi ni mkisto, hata huko ulipokuwa awali, tuseme labda ulikuwa muislamu, ukitenda mema, ukafuata maagizo ya Mungu kwa mwanadamu na kuamini kwa uaminifu, basi pepo na mbingu ni vyako hakuna wa kukuzuia. Hakuna dini bora kuliko nyingine idipokuwa niko tofauti sana ni zile zinazomilikiwa na watu binafsi kama nilivyotangulia kusema hapo awali.
Note: misingi ya dini ya kiisilamu inafanana kwa karibu na Lutheran, catholic, Anglicans tofauti ni namna ya kuabudu tu.
 
nashukuru sana naubarikiwe, basi nitaenda moja wapo ila sasa lipi?
Kichwa kinanigonga bado.
 
kanisa alisaidii...ni imani yako tu, RC roman catholic au KKKT, ndio makanisa
 
Wabongo bana; mtu anauliza jamani kuna mtu yeyote anayejua hoteli nzuri ambapo naweza kupata chakula kizuri maeneo ya Mabibo na Riverside hapa? Watu wanaanza kuuliza "kwani huwezi kupika?"; "Kwanini unataka kula hotelini?" 'Hongera mwaya kwa kutafuta chakula kizuri"; "Kwani chakula chako hakiivi" na wengine kama vile hawajasoma alichouliza wanasema "kuna hoteli nzuri Chalinze"!!

Grrrrrrr... kama unajua kanisa ambalo linakidhi au linaweza kukidhi mahitaji ya mtoa mada toa ushauri. Vinginevyo; fanya kama mimi tu sepa!
 
latifa, kama ni mwanafunzi hapo mabibo hostel, wasiliana na uongozi wa TAFES AU CASFETA, huwa kuna mabasi ya kuchukua wanafunzi na kuwarudisha kwenda kanisa la TAG, victory christian centre tabanacle, kanisa lipo mbezi beach kawe. kama ni mkazi wa hapo mabibo, nenda kanisa la TAG Sahara lipo barabarani kama unaelekea mabibo mwisho ukitokea ubungo maziwa, au TAG Ubungo karibu na NBC ubungo, au nenda kinondoni TAG Revival church. Roho yako itachengwa vizuri.
 
Kwanini msianzishe Kanisa la Wanachama wa JF? Nna uhakika wapo wachungaji humu, wainjilisti, wanakwaya n.k; mnasali kwa Skype na kutoa sadaka kwa Paypal... LMAO...
 
latifa, kama ni mwanafunzi hapo mabibo hostel, wasiliana na uongozi wa TAFES AU CASFETA, huwa kuna mabasi ya kuchukua wanafunzi na kuwarudisha kwenda kanisa la TAG, victory christian centre tabanacle, kanisa lipo mbezi beach kawe. kama ni mkazi wa hapo mabibo, nenda kanisa la TAG Sahara lipo barabarani kama unaelekea mabibo mwisho ukitokea ubungo maziwa, au TAG Ubungo karibu na NBC ubungo, au nenda kinondoni TAG Revival church. Roho yako itachengwa vizuri.
ok nashukuru je mtandao wakijamii unaozungumzia maswala ya imani kwa wa kristo upo? Iwe wa dhehebu lolote la kikristo
 
Nimeamua kuwa mkristo natafuta kanisa lakiroho nianzekwenda maeneo ya mabibo hosteli. Sio kanisa la mazingaumbwe noo kanisa la kuijenga roho yangu na uhusiano mzuri na Mungu mwenyezi

Latifa sidhani kama utakuja kuandika thread nzuri na yenye mashiko kama hii,hakuna zitafanan bt sio hiii,
Hongera sana sana sana....unajua ukiwa na Mungu unakuwa na amani sana,unajua shetani anatusumbua sana,na tuna jua yeye hatima yake ni moto,lini tutasema imetosha?
Haijalishi ulikuwaje la msingi ni kutubu,

let me tell one thing:
hakuna binadamu ambaye hatendi dhambi,hata watakatifu,the good thing ni kuwa wao huwa wanatubu sana pindi tu wanapokosea,unapotubu una achilia nguvu na furaha kuwa juu yako,ni kama ulikuwa na li kitu mwilini sasa linaondoka au kuyeyuka....
watu wengine wanahisi wakiamua kusali ni ku miss mambo mazuri,starehe,jamani kwa Mungu hakuna starehe,hata duniani mbona zipo tu,hujazitafuta tu.
Nakuombea sana sana Mungu akulinde na akupe Nguvu na imani zaidi.
Kumcha Mungu ndio chanzo cha Maarifa."mithali"
 
Kila post niisomayo hapa ndani, napata picha ni kwa kiasi gani imani ya Kikristo ambavyo imeyumbishwa.
Hakuna hata mmoja amwaminiye mwenzake, zaidi aaminiye nyumba ya ibada ya mwenzake.

Yesu Kristo alipokuja ulimwenguni, alikuja kwa missions nyingi ila moja ni kulijenga Kanisa Jipya tayari kwa unyakuo.

Baada ya Yesu kuondoka ulimwenguni, kazi ya kuliendeleza kanisa aliicha kwa mitume 12 ambao walizunguka duniani kote kueneza yale yote waliofunzwa na Yesu.

Wengi ambao sio wafuatiliaji wa Biblia huwa wanasahau kuwa hata Mitume walipokuwa wakieneza Injili walikuwa wakifungua makanisa sehemu mbalimbali walizokuwa wakizuru. Mfano mdogo ni Nyaraka za Paulo Mt kwa makanisa mbalimbali. Hivyo wingi wa makanisa kwa sasa si jambo la ajabu.

Ushauri...
Biblia yatuambia, "Wamwabuduo Bwana, inawapasa kumwabudu katika Roho na Kweli...". Hivyo binafsi sina jibu moja kuwa nenda kanisa fulani, zaidi zingatia hayo maneno ndani ya mabano.
 
Nimeamua kuwa mkristo natafuta kanisa lakiroho nianzekwenda maeneo ya mabibo hosteli. Sio kanisa la mazingaumbwe noo kanisa la kuijenga roho yangu na uhusiano mzuri na Mungu mwenyezi

Karibu sana SDA, ingia iliyoko karibu na wewe, na hapo ulipo ipo utabarikiwa sana!!!
 
Hivi kuna kanisa linalofundisha kutenda dhambi? kama makanisa yote yanafundisha kutenda mema basi aamue mwenyewe wapi aende.
Imeandikwa "anayezania kuwa anayo dini anajidanganya maana sitakuja kuhukumu dini ya mtu bali matendo"
Dini ya kweli isiyo na mawaa mbele za Mungu ni hii -kuwasaidia yatima na wajane na kwenda kuwatembelea wafungwa na wagonjwa na kuwaombea hapo utakua umemaliza na ndicho Yesu Kristo alikuja kukifanya hapa duniani na hakuwa na dhehebu maalum.

Hizi dini ni itikadi tuu za watu na siyo imani kama unavyofikiria dini ni sawa na utaratibu fulani tuu ambao watu wameamua kuufuta hawa utaratibu wao ni huu na hawa utaratibu wao ni huu basi nandio maana zinapishana, kwahiyo usiumize kichwa sana
Ila sikuhizi nimesikia kuna madalali wa imani wamefungua makanisa yao kwakupitia jina la makanisa fulani ili wapate kibali, nawako kibiashara kama bishara zinginge kwahiyo ukienda kwa hao ili ufanikiwe inabidi uwe na hela utoe ili ubarikiwe nao.
 
Labda kama utaniruhusu nikupe namba ya simu ya mtu ambaye yupo hapo dar then akupeleke coz mm cpo dar latifa

Dada Latifa, dada latifa!! Umewaza vyema sana kuamua kwenda kanisa, mi nasema kubadili mfumo wa maisha. Lakini dada Latifa, naomba tutambue kwa kitengo cha kanisa ni cha Mungu mwenyewe na siri zote za namna kanisa linavyo operate azijua Mungu mwenyewe, Tena hekima na busara ya kuchagua mahali pako sahihi pa kwenda kuabudia amekupa (kwani ni kweli ameshakuambia wapi uende kumuabudu) Mungu mwenyewe.Tambua Roho mtakatifu aliyekupa neema ya kukupeleka Kanisani tayari ameshakuelekeza ni kanisa lipi sahihi la kwenda, isipokuwa tu wewe unasitasita kuisikiliza na kuitii sauti yake ya kwanza iliyokuelekeza vyema.(ikumbuke sauti ya kwanza iliyokuambie uende kanisani ilikwambia kanisa lipi?). Sauti hizi za Jf ni sauti za pili tena na ya shetani imeingilia kati ili kukusahaulisha ile sauti ya kwanza, na pia kuwatukana watumishi wa Mungu ili ujazwe dharau tena juu yao na kubadili mawazo yako mazuri. ITII SAUTI YA ROHO MTAKATIFU (ILE YA KWANZA), KISHA NENDA KANISA ILIYOKUELEKEZA PASIPO KUSITASITA WALA KUJIHOFU USIJE UKAGEUZA MNARA WA CHUMVI KAMA MKE WA RUTU!! Ubarikiwe sana!
 
Back
Top Bottom