Nataka kuanza kwenda kanisani

Nataka kuanza kwenda kanisani

Dada Latifa, dada latifa!! Umewaza vyema sana kuamua kwenda kanisa, mi nasema kubadili mfumo wa maisha. Lakini dada Latifa, naomba tutambue kwa kitengo cha kanisa ni cha Mungu mwenyewe na siri zote za namna kanisa linavyo operate azijua Mungu mwenyewe, Tena hekima na busara ya kuchagua mahali pako sahihi pa kwenda kuabudia amekupa (kwani ni kweli ameshakuambia wapi uende kumuabudu) Mungu mwenyewe.Tambua Roho mtakatifu aliyekupa neema ya kukupeleka Kanisani tayari ameshakuelekeza ni kanisa lipi sahihi la kwenda, isipokuwa tu wewe unasitasita kuisikiliza na kuitii sauti yake ya kwanza iliyokuelekeza vyema.(ikumbuke sauti ya kwanza iliyokuambie uende kanisani ilikwambia kanisa lipi?). Sauti hizi za Jf ni sauti za pili tena na ya shetani imeingilia kati ili kukusahaulisha ile sauti ya kwanza, na pia kuwatukana watumishi wa Mungu ili ujazwe dharau tena juu yao na kubadili mawazo yako mazuri. ITII SAUTI YA ROHO MTAKATIFU (ILE YA KWANZA), KISHA NENDA KANISA ILIYOKUELEKEZA PASIPO KUSITASITA WALA KUJIHOFU USIJE UKAGEUZA MNARA WA CHUMVI KAMA MKE WA RUTU!! Ubarikiwe sana!
kama hakumbuki hiyo sauti ya kwanza?
 
N
nashukuru sana naubarikiwe, basi nitaenda moja wapo ila sasa lipi?
Kichwa kinanigonga bado.

Ndio maana Latifah nikakwambia hii ni sauti ya pili tena na Ibilisi ameingilia kati, tazama mtu anapokushauri kuwa kanisa ni Kkt, Catholic na Anglicana tu, hii ni ajabu sana na ni sawa na Mungu alivyonena; HEKIMA ZA WANADAMU KWAKE NI UPUMBAVU MTUPU. Kwa mfano mtu anaposema hayaamini makanisa ya KIROHO hii ni ajabu sana kwa sababu Mungu ni Roho na Wamwabuduo wapaswa kumwabudu katika Roho na kweli, sasa kama haamini makanisa ya Kiroho huyu anaamini makanisa ya KIMWILI. Mimi ni Muumini mzuri wa KKKT, lakini kwa kuisoma vema Biblia najua ubora na udhaifu wa Dhehebu langu na vile vile ubora na udhaifu wa madhehebu mengine yakiwemo ya Pentekoste.Kuhusu dhehebu kuongozwa na mtumishi fulani hiyo isikutatize, kwani Bwana Yesu alizikuta Taasisi Kubwa za Kidini lakini nyingi kati ya hizi zilipinga mafundisho yake hadi zikamuua msalabani lakini wanafunzi watiifu wa YESU mmojammoja ( sio chini ya dhehebu au Taasisi fulani ya kidini) aliachiwa kazi ya kueneza Injili iletayo wokovu duniani kote na walifanya hivyo hata hayo madhehebu makubwa yalipowatesa na kuwaua( mfano Petro, Stefano, Paulo, Yohana n.k) Hivyo basi narudia kukusihi kuwa KANISA LA KWANZA NI WEWE MWENYEWE AMBAYE ROHO MTAKATIFU AMESHASEMA NA WEWE NA KUKUELEKEZA UENDE KATIKA KANISA LINALOHUBIRI INJILI ILETAYO WOKOVU( inayobadilisha maisha yako kutoka katika vifungo vya dhambi na kukuweka mbali na dhambi) iwe ni pentekoste, kkkt, anglicana, sabath, catholic n.k ilimradi unasikia sauti ya Mungu inakuelekeza hapo na kukuacha na AMANI TELE MOYONI. Ubarikiwe sana kwa uamuzi sahihi !
 
Nimeupenda ushauri wako.
Na sabato pia ni kanisa lenye misingi mizuri.

Ni ushauri mzuri sana lakini nakushauri uutathmini kwa maandiko ya Biblia kinyume na hapo ni Busara tu za mwanadamu ambazo Mungu ameziita UPUMBAVU!! Kwa sababu unashauriwa na MTU, usiende kwa watumishi wanaojiita MITUME; Lakini Neno linasemaje, "Kanisa linajengwa chini ya Misingi ya MITUME NA MANABII" Na pia Usiende kwa watumishi wanaohubiri sana utoaji! Nakukumbusha tu kwamba usiposisitizwa na kufundishwa vyema kuhusu UTOAJI NA NAMNA YA KUTOA, Amini usiamini hutatoa na usipotoa Hapo ibada ni batili, kumbuka Mungu amekataza kabisa kujaribiwa na MTU, lakini sehemu moja tu ameruhusu for purpose amesema; "Nijaribuni Kwa Matoleo Muone kama Sitafungua Madirisha ya Mbingu na kuwamwagia Mibaraka tele..." Lakini pia baraka za Baba yetu wa Imani zilikuja Kwa kutoa (tena mwanae Isaka wa Pekee) na Yesu Mwenyewe akajitoa sadaka kwa ajili yetu, hivyo kupinga makanisa yanayosisitiza utoaji tafakari kwanza na Muulize Roho Mtakatifu atakufunulia namna ya kufanya.Na ukishauriwa Kupiga makanisa yanafanya Miujiza tafadhali Roho mtakatifu na akupe hekima ya kutambua miujiza ya Mungu na ile ya Kishetani, kwani Maandiko yako Wazi kuwa Yesu Kristo tunayemfuata hakuwahi kuhubiri pasipo kutenda miujiza ili kuwavuta wasioamini waamini baada ya kuyaona matendo Makuu ya Mungu kupitia kwa Mtumishi wake, kadhalika hata mitume wake aliowaacha nao hawakuwahi kuhubiri Injili chukwuchukwu ila iliyoambatana na ishara na maajabu ili kuwavuta wasioamini waokoke na kutubu dhambi zao.Unaonaje mtumishi anapokusisitiza kila siku kuwa Yesu anaokoa na kuponya halafu katika utumishi wake hata siku moja hujawahi kushuhudia akiokoa(kumtoa mtu katika maisha ya dhambi) wala kumponya walau Mgonjwa wa mafua tu!!? Roho Mtakatifu na akutafakarishe na hili pia kabla ya kufanya uamuzi.UBARIKIWE SANA!
 
Tunashukuru kwa ushauri wako.
Ila ningependa kukuuliza, hivi unadhani kuibuka kwa haya makanisa mengi mengi . . . sababu ni uponyaji wa kiroho pekee???

Na vipi kuhusu hiyo miujiza unayoizungumzia . . . kwani wale manabii wa uongo waliotabiriwa hawawezi kuifanya??
Thanks.

DISCLAIMER
No hard feelings, no harm, no insult intended or any other malicious thought.
It is just for a simple reasoning.
 
Thanks a lot, hilo kanisa halina
branch huku mabibo au river side hata?

Mkuu vipi, Mzee wa Upako yuko pale pale karibu nawe, usafiri wa mabasi upo kuanzia Riverside hadi kanisani kwake, sasa unataka kwenda wapi zaidi? Lakini andaa salary slip kama ni mwajiriwa au leseni ya biashara na malipio ya kodi ya serikali, kama ni dent andaa uthibitisho wa mkopo unaopokea toka HESLB, nyaraka hizi zitasaidia ukokotoaji wa 10% ya Mungu. Nakutakia ibada njema.
 
Ukristo ndo dini sahihi ya kumpeleka mtu mbinguni ila huku nako shetani kajisajili. Please dada yangu mi nakushauri mtafute ndugu mkristu mfano mama mchungaji na akushauri vzr ili mfanye kwanza maombi nae ili Roho Mt aseme nawe wapi ukamwabudu Mungu ktk roho na kweli. Usiogope, Kristo aliyeweka nia hii njema moyoni mwako atakutetea. Hongera kwa kuwa sasa hauko mbali na Mbingu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
jamani kwaanae jua anijuze niko more than serious pls

wewe unavutiwa na lipi maana umevutiwa mda mrefu eg, roman, lutheran, anglican, morovian, sabato, nakadhalika alafu ndio tujue unaanzia wapi.
 
Mkuu vipi, Mzee wa Upako yuko pale pale karibu nawe, usafiri wa mabasi upo kuanzia Riverside hadi kanisani kwake, sasa unataka kwenda wapi zaidi? Lakini andaa salary slip kama ni mwajiriwa au leseni ya biashara na malipio ya kodi ya serikali, kama ni dent andaa uthibitisho wa mkopo unaopokea toka HESLB, nyaraka hizi zitasaidia ukokotoaji wa 10% ya Mungu. Nakutakia ibada njema.
Cheap is expensive
 
Ukristo ndo dini sahihi ya kumpeleka mtu mbinguni ila huku nako shetani kajisajili. Please dada yangu mi nakushauri mtafute ndugu mkristu mfano mama mchungaji na akushauri vzr ili mfanye kwanza maombi nae ili Roho Mt aseme nawe wapi ukamwabudu Mungu ktk roho na kweli. Usiogope, Kristo aliyeweka nia hii njema moyoni mwako atakutetea. Hongera kwa kuwa sasa hauko mbali na Mbingu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Mhh haya
 
wewe unavutiwa na lipi maana umevutiwa mda mrefu eg, roman, lutheran, anglican, morovian, sabato, nakadhalika alafu ndio tujue unaanzia wapi.

labda nikuulize, mazingaombwe ulimaanisha nini? maana efatha kuombewa watu wakadondoka ni swala la kawaida sana sasa labda inawezekana nimekuelewa vibaya.
 
labda nikuulize, mazingaombwe ulimaanisha nini? maana efatha kuombewa watu wakadondoka ni swala la kawaida sana sasa labda inawezekana nimekuelewa vibaya.

Ooh nimetaja Efatha kwa vile hujalitaja hapo, kuhusu mazingaumbwe nina maana mimi nia yangu sio kwenda kanisani kwaajili ya kuonyeshwa miujiza miujiza wakati jinsi ya kuomba mwenyewe sijuhi maneno ya ushuhuda ndani ya neno la Mungu sina yani silijui neno, sasa hata nikifanyiwa hiyo miujiza siitakua kazi bure tuu sinitakua kilasiku mimi ni mtu wakutafuta miujiza, Nafikiri mwanzilishi wa miujiza alikua YESU KRISTO na aliifanya ili watu wamwamini sasa mtu kama mimi tayari nimeshamwamini YESU KRISTO kwanini nisifundishwe jinsi ya kuomba ili niwe naomba mwenyewekama ni hiyo miujiza itakuja tuu kwakuomba pekeyangu ?
 
Karibu sana... Ni maombi ya wote wanaokutakia mema uishi matendo mema tu.

Ila fahamu haya ndugu;

Hakuna Dini iliyokamili kwa asilimia 100
Hakuna dhehebu lililokamili kwa asilimia 100

Kanisa/Msikiti kwa maana ya kawaida ni sehemu (kama jengo tu) ambapo watu wenye imani moja hukutana kwa imani moja.

Si Dini ndiyo itakayokupeleka mbinguni/peponi
Si Dhehebu ndilo litakalokupeleka mbinguni/peponi

Ni matendo yako mema na uhusiano wako mzuri na Mungu wako tu ndiyo tiketi yako.

Kila la kheri
 
Nami naungana na mkuu Kanga nenda TAG REVIVAL KINONDONI pale hutajuta ama vipi jaribu kutembelea siku moja kama ratiba ulivyopewa au nicheki nikuelekeze zaidi
 
Nimeamua kuwa mkristo natafuta kanisa lakiroho nianzekwenda maeneo ya mabibo hosteli. Sio kanisa la mazingaumbwe noo kanisa la kuijenga roho yangu na uhusiano mzuri na Mungu mwenyezi

Kuijenga roho??,hapa sielewi kabisa kwan roho imekuwaje mpaka ijengwe? Na nani kakwambia kanisa ama msikiti ni suluhisho la matatizo ya roho??,kuwa huru ili uone amani ya moyo,unachofuata huko ni nidham ya uoga na Hofu ya anayeitwa mungu,ambayo hata hivo haitakusaidia bali kukufanya kuwa na halu ya wasiwas zaidi moyon,na miungu ipo ya aina nyingi sasa sijui huyo umfuatae wewe niy upi huko kanisani ama yule wa MUSA asiyeonekana??,
 
Nimeamua kuwa mkristo natafuta kanisa lakiroho nianzekwenda maeneo ya mabibo hosteli. Sio kanisa la mazingaumbwe noo kanisa la kuijenga roho yangu na uhusiano mzuri na Mungu mwenyezi

Acha kuchezea watu wazima akili, kama vipi peleka hili swali lako Facebook. Hapa kila mtu ana imani yake na anafuata nyumba yake ya ibada na anaamini yupo sahihi kuwepo kwenye nyumba hiyo husika ya ibada, hivyo lazima akushauri uende kwake na mwisho wa siku utabaki kuzunguka zunguka tu. This is a platform of great thinkers stop playing with minds and faith of the people. Najua huna lolote wala huna shida na kujua kanisa nia yako ni kuona malumbano tu hapa.
 
Back
Top Bottom