Walikataa kumzika babangu eti sikuwa natoa sadaka - mrembo afichua mbona haendi kanisani

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
Walikataa kumzika babangu eti sikuwa natoa sadaka - mrembo afichua mbona haendi kanisani.
---
Katika miaka ya hivi karibuni, idadi kubwa sana ya Wakristu wameacha kuhudhuria mahubiri kanisani, wengi wakiwa na sababu zao binafsi na wengine ikiwa ni kutokana na uzoefu walioshuhudia kutoka kwa wahubiri au waumini wenzao.

Lakini je, umewahi sikia watu wakizungumzia sababu zao za kuacha kwenda kanisani?

Mrembo mmoja kupitia mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter amewashangaza wengi baada ya kuhadhithia sababu yake ya kuacha kwenda kanisani, licha ya kuwa alikuwa ni muumini asiyekosa ibada kila wiki siku za nyuma.

Kulingana na mwanadada huyo aliyetambulika kwenye Twitter kama @Miss_ezeani, marehemu babake alikuwa Mkristo mcha Mungu na alijitolea maisha yake yote kumtumikia Mungu na kulipa haki zake hadi alipopatwa na ugonjwa ambao uliathiri mapato ya familia.

Alisimulia jinsi baba yake hangekosa kwenda kanisani kwa lolote na alijulikana sana na washiriki wa kanisa hilo.

Hata hivyo, jambo la kustaajabisha ni kwamba baada ya kifo chake, kanisa hilo lilisema mtu huyo alishindwa kulipa baadhi ya hela za maendeleo ya kanisa, hivyo hawatakuwa sehemu ya maziko yake.

Aliongeza kuwa mambo mengine yalifanyika ambayo yalimpa sababu za kutosha za kuacha kuhudhuria kanisa, lakini maendeleo baada ya kifo cha baba yake yalikuwa kiboko cha mwisho ambacho kilivunja mgongo wa ngamia.

“Baba yangu alifariki; walitishia kutomzika hadi tulipe malipo yake. -Alikuwa mwanachama hai sana kabla sijazaliwa. Alipenda kanisa kupita maelezo. Afadhali apelekwe kanisani akifa kuliko kuruka Jumapili. Alichangia sana, KILA njia. Kila mtu alijua ugonjwa wake uliimaliza benki yetu, hivyo basi, kudorora kwa sadaka yake. Walakini… Pamoja na mambo mengine hata hivyo, hiki kilikuwa kiboko cha mwisho,”
@Miss_ezeani aliandika.

Alifichua haya kutokana na swali lililotumwa kwenye Twitter na Instablog9ja, likiwauliza wafuasi wake: "Ni nini kilikufanya uache kwenda kanisani?".

Je, wewe una sababu ya kutoenda kanisani?
 
Back
Top Bottom