Natafuta mwanamke aliyeachika na mwenye watoto

umri wangu ni mkubwa kwa hiyo huwezi ukawa na mtu ambaye maisha yake anawaza mtoko mara TAARAB, DISKO nk , kwanza maendeleo, mengine baadaye. na kama wote tutakuwa na watoto ni rahisi watoto wakatuunganisha na hakuna atakayefanya upuuzi kwa mwenzake kama cheating n.k , as far as kuna miradi ya kuungalia for the future of our childrens

Kama nna miaka 50 na nina vigezo vyote hivyo na pia mzuri hatari. Niku pm?
 
Cc: uvugizi
Hujaleta mrejesho kama umeshampata mke uliyekuwa unamtafuta!!! Ni vema JF ikapewa credit kama mambo yamekwenda sawa jamani!!! Matangazo ya bure hata senti hulipi zaidi ya muda wako hapa.

Niwie radhi nime'edit somewhere.
 
Last edited by a moderator:
Sasa kwa nini utangulize kumtajia majukumu atakayopambana nayo kabla hata haujamjua? Je ukimpata mwenye kazi yake ya kuajiriwa ambaye hataweza kusimamia hiyo miradi utamkataa? Nakushauri utafute kitu kimoja baada ya kingine,mke kwanza halafu ndipo mtaongea namna ya kuendesha maisha yenu kwa ushirikiano.

Naona ameamua kuweka vigezo na masharti ya kuzingatiwa hadharani ili akijitokeza mtu awe anajua anachokiendea
Kila la heri ndugu
 
umetaja biashara zako, vipi kuhusu tabia zako?
tabia utajua tu baada ya kuniona si kwamba mtu anaweza akajiingiza kichwa hata mimi sintopenda kumkosea binadamu mwenzangu , nina imani kwa umri huo wote hatudanganyiki , isitoshe nimempata mama mmoja ni muungwana sana nataraji mambo yataenda vizuri , changamoto ni kuwa na yeye ana miradi yake na vime match kataika harakati zetu . god bless JF na wote members wa JF
 
Huyo aliekwenda na pressure nadhani hata over weight inatokana na stress!!! Vp tabia zako?!
Ndugu kwa maisha haya ya familia hakuna kitu kinatesa kama kufiwa na mke , mama , baba, na wengineo kwangu haiumi sana kama mke, kwani anatesa sana hasa unapoangalia watoto wako
 
Yupo jamaa mmoja kila akioa wakeze hufariki hivi hili huwa ni tatizo gani?till now ameamua aishi mwenyewe.

Hili huwa ni tatizo linabase sana kwenye imani ya kikwetu kama wakati wa utoto ulianza kuota meno ya juu kabla ya meno ya chini kama ni mwanamke ni kwamba waume zake watakuwa hawamalizi round wanakufa na kama ni mwanaume wake zake watakuwa wanakufa tu. So sijui connection ya meno na ndoa labda wanasayansi ya imani waje waeleze zaidi. Ila ndio ukweli
 
JF si mchezo mtu katangaza hata miezi miwili haijapita keshapata mtu na keshajua ni muungwana! Aisee tahadhari sana kuhusu watoto, usije ukadhani umepata kumbe umepatwa. Ila nakutakia kila la kheri katika harakati zenu za kufuga mang'ombe na makuku. Ulezi wa kulea watoto vyema mkiupa kipaumbele.
Aliyeachika, kwanini sio mjane? Inawawezekana kilichamfanya wenzio wakashindwana na wewe kikakushinda pia.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Unasaundi kama kilanja vile!

Halafu kama unatafuta operations manager siyo mke, anyway kila la kheri
 
Back
Top Bottom