Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi
Haya mambo ya mtu kusikia sauti, sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, haya ni mambo ya ulimwengu wa Roho.

Hii ni thread ya maono tuu ya unabii, sio utabiri, sio trends readings, ni unasikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kuambiwa sababu na huwezi kuuliza, hivyo nami naomba kuwaeleza tuu sauti niliosikia na naomba msiniulize kitu kwasababu sio mimi ni sauti za "Voices from Within", yaani sauti toka ndani yako!, the inner you. The inner you ya kila mwanadamu ni YEYE aliyemuumba na kumpa uhai, ila sometimes yeye ambaye siye YEYE, huweza kujipenyeza kule inner na kutoa sauti, ukadhani ni YEYE kumbe sio YEYE bali ni yeye tuu!.

Leo nilikuwa naandika bandiko fulani humu JF, ndipo ghafla nikaisikia sauti (voices from within) kuwa Rais wa JMT kwa mwaka 2025 should be a man kwa kipindi kimoja, then 2030 ndipo tuje na mgombea mwanamke!.

Sauti hiyo inamaanisha inamtaka Rais Samia awe ni Rais wa JMT kwa kipindi kimoja tuu cha mpito cha awamu moja hadi 2025 na afuatiwe na rais mwanaume atakaye kaa kwa kipindi kimoja hadi 2030 sasa ndipo tuje na mgombea mwanamke!.

Sauti hiyo maana yake inamaanisha ni Rais Samia yeye mwenyewe willingly anatakiwa kujiandaa kisaikolojia kuwa ni rais wa awamu moja, na kumuandaa mtu wa kumkabidh urais awamu yake ya pili ya miaka 5 yake iliyobakia ya 2025 - 2030!.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, hakuna mwana CCM yeyote anayeruhusiwa kùomba fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kwa pande zote mbili za muungano. Mgombea urais wa CCM kwa 2025 kwa huku bara ni rais aliyepo madarakani sasa, Rais Samia na kwa Zanzibar ni Dr. Mwinyi, kwasababu wote wiwili hii ni awamu yao ya kwanza!. Hivyo utaratibu wa CCM ni ule wa zengwe la kutoa fomu moja tuu!.

Kama sauti hii nilio isikia ni sauti ya ukweli ya kwake YEYE, hii inamaana, ni ujumbe kwa Rais Samia, ama Rais Samia yeye mwenyewe ameisha ambiwa na YEYE, ama YEYE ameanza kutuambia kwanza sisi wengine wa kutangazia umma ili kuanza kuwaandaa Watanzania kisaikolojia kuhusu 2025.

YEYE huwa ana mtindo kwa baadhi ya mambo, kuwaambia watu wengine kwanza kabla hajawaambia wahusika wenyewe, mfano mzuri ni huu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli wakati huyu aliyeezwa haya ilikuwa ni 2014, by that time hata JPM alikuwa bado hajaambiwa kuwa ni yeye 2015!. Hivyo kuna uwezekano hata sauti hii ya bandiko hili, usikute hata Rais Samia mwenyewe bado hajaambiwa hili na YEYE, ila kama ni sauti yake YEYE mwenyewe halisi, then na Rais Samia pia ataambiwa!.

Hivyo namshauri Mama aendelee na maadalizi ya 2025 kwa kujiandaa yeye kama yeye, lakini pia afanye na maandalizi ya kuisubiria hiyo sauti ya uthibitisho kuwa 2025 yeye Rais Samia ndiye aliyepangiwa na YEYE, kama ni yeye ndiye aliyepangiwa na YEYE, then 2025 ni yeye Samia.

Lakini kama ataisikia hii sauti, sio vibaya kama atajiandaa na kumuandaa mtu wa kumpokea, kwa maoni yangu, Dr. Hussein Mwinyi atatufaa sana, hivyo namuomba Rais Samia akiisikia sauti, amuombe Dr. Hussein Mwinyi, kwa uchaguzi wa urais wa 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu ya pili ya Mama Samia kwa yeye kukubali kuwa rais wa JMT kwa awamu moja tuu.

Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndipo sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakaye kuja kugombea urais wa JMT kwa 2030, na kwa maoni yangu, Mwanamke huyu sii mwingine yeyote zaidi ya Dr. Tulia Akson Mwansasu, Spika wa sasa wa Bunge la JMT.

Japo Tanzania, tulipania 2025 twende na mgombea mwanamke, na mimi niliunga mkono hoja hii Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
kama hii sauti ni yake YEYE kweli, then inamaanisha kwa uchaguzi wa 2025, Tanzania tuna mgombea mmoja tuu Mwanamke, yaani the one and only ambaye ama anatakiwa na YEYE apumzike ampishe mgombea mwanaume, ama ...

Japo sio sio lazima kusema kila unachosikia, kwa sababu sometimes sio kila unachosikia kwenye the voices form within ni sauti kutoka kwake YEYE au ni maono, sauti nyingine ni sauti za kina yeye tuu na sio sauti yake YEYE!.

Hata yale maono ya kwenye ndoto, sio kila ndoto ni maono kutoka kwa Mungu, kuna ndoto nyingine, ni ndoto za shetani kama ile "ndoto ya Lema", ukisikia sauti ukahisi inaweza isiwe ni sauti ya Mungu, au ukiota ndoto ya jambo fulani la ajabu ajabu ukahisi jambo hilo sio la kheri, sio lazima uliseme, ila ukilisema lina faida moja, kufanya maandalizi ya kabla!.

Mfano ni tangu ile August 14, 2014 nilipoelezwa rais ajaye wa Tanzania ni Magufuli, na nilielezwa sababu za kwanini ni Magufuli, nami nikaeleza humu kwa rais wetu ajae ni Magufuli lakini hizo sababu za kwanini ni Magufuli, japo nilielezwa lakini mimi sikuzisema humu!. Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, hivyo hiyo 2014 wakati nikisema hayo, unaweza kukuta hata JPM mwenyewe alikuwa hajui kuwa ndiye yeye!.

Hivyo hata sauti hii niliyoisikia leo, 2022, kuhusu 2025, usikute hata Mama Samia mwenyewe bado hajui kuwa 2025 sii yeye kwasababu yeye bado hajaelezwa na YEYE kuwa sio yeye, na ndio sababu ni Rais Samia ndiye aliyependekeza 2025 twende na mgombea Mwanamke kumaanisha ni yeye!.

Unaweza kuta aliyepangiwa na YEYE kuwa rais wetu 2025 ni Mama Samia mwenyew, baada ya kuingia by default kuwa rais wa JMT kwa awamu hii ya kwanza, sasa anajipanga kuendelea awamu ya pili, properly kwa kuchaguliwa na jura za Watanzania, ila kugombea kwake ni kupitia ule mserereko wa CCM , huku Dr. Mwinyi akiji set for his second term in Zanzibar kwa mserereko wa CCM na wala hajui kuwa kuna sauti inamtaka yeye ndiye aje awe rais wa JMT, 2025!, hivyo maono kama haya, yanasaidia sana kuwaandaa watu kisaikolojia!.

Hata ile siku niliyoisikia sauti hii
Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... Spika Job Ndugai hakujua kuwa yeye hatakuwa Spika, wala Dr. Tulia hakujua kuwa yeye ndiye atakuja kuwa spika ajae!.

Hata ile siku namzungumzia huyu DC, Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam DC mwenyewe alikuwa hajui, na watu humu wakanidhania mimi ni mtu wa kule naniliu na kudhani nimeleta za jikoni!.

Hili la Mwinyi kuja huku, sio la sauti, hili ni langu tuu, maana usikute pia ni mpango ya YEYE, kumfanya huyu jamaa Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii maana
wakati nikiandika hayo, Dr. Shein alikuwa hajui, hivyo hata saa hizi ninapoandika hapa, usikute huyu jamaa wala hajajijua kuwa yeye ndiye anapaswa aje awe rais ajaye wa Zanzibar!. Hii nibkufuatia dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyika Zanzibar kwa miaka na miaka, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda lakini sasa kwavile Samia ni mpenda haki, msema haki na mtenda haki, for the first time in Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964, uchaguzi wa 2025 unaweza kuwatendea haki!.

Hitimisho
Kwa vile mimi ni Msukuma, naweza kutuhumiwa ni sehemu ya Sukuma Gang wasiotaka Samia aendelee 2025 to 2030. Naomba kwanza niwathibitishie I don't believe hiki kitu kinachoitwa ,"The Sukuma Gang" kina exist in reality!, hakuna kitu kinachoitwa Sukuma Gang, ni just a fictitious group in mind za watu waliofilisika kimawazo!.

Mimi ni Msukuma na sio Sukuma Gang, ila pia ni Mimi ndio nilimtabiria Samia urais wa JMT toka 2017, Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
nikamshauri Blaza asigombee 2020 ampishe Samia, but no one takes me seriously, kama sauti hii!, you never know, kama JPM angeusikiliza ushauri wa bandiko hili Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” nilishauri
Wanabodi,
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu.

Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa. Kwa jinsi alivyo na sauti safi, tamu na laini yenye lafudhi ya Kizanzibari, akiongea, utatamani asimalize kuongea, utatamani aendelee tuu kuongea, ukijumlisha na yale macho...!, sijui hata akitaka kugomba, atagomba kwa sauti gani na macho gani maana...!.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Huyu Mama ana Virtues karibu zote na baadhi yake ni hizi nilizozitaja humu.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
probably ange...

Mwaka 2020 nikasema humu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
nilisema
Wanabodi,

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Amezungumza mengi na kumalizia kwa kusisitiza Muungano ni jambo jema, tuulinde na kuuenzi.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Hivyo it's up to Mama, to decide, kuutafuta ukweli wa sauti hizi, au kuzipuuzia na kuendelea na mipango yake ya 2025.

Kuna kitu pia nimeambiwa ni kwa nini Mama amuombe Mwinyi, ila sio lazima kusema kila kitu. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Hivyo mpaka umelisikia hili nimelisema, ujue lina maslahi kwa Taifa.

Kitu muhimu ni nimesikia sauti, nimesema nilichosikia, mimi nimetimiza wajibu wangu!.

Mungu Mbariki Rais wetu Samia aisikie Sauti YAKO!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
(Mzee wa Sauti, "The Voices From Within)

Baadhi ya Mchango very objective
Nikisoma katikati ya maandishi naona Pasco huna imani na huyu Mama.

Nikirejea uandishi wako wa siku nyingi humu na uzoefu wako wa siasa za ndani ndani huko naona tayari upepo wa nchi haupo pamoja na Mama 2025..

Na nikimwangalia Mama mwenyewe naona kabisa hana nguvu wala ushawishi wa kulazimisha kuendelea baada ya 2025.

Hasa akiambiwa mrithi wako huenda akawa "nduguyo" basi Mama hatakuwa na nongwa kabisa.
Mkuu idawa , kwanza asante sana kwa mchango wako na uwezo wako wa kunisoma in between the lines, ila naomba nikuhakikishie, it's not my making, it's the voices from within!.

Sikukisema vyote nilivyo ambiwa, na hiyo sauti labda nikivisema vyote itasaidia kwa kuvi mitigate kabla ya 2025 ili Mama aendelee.

Kinachonifanya nisiseme kila kitu ni kwasababu kauli nyingine huumba!. Nisije nikasema humu, halafu yakatokea ya kutokea tukaaanza kunyoosheana vidole!.

Hata mimi kujiunga JF nikauli za wana JF ile 2008 nikiwa naendesha bike Morogoro Rd mitaa ya Manzese, kuna mwana JF akanianzishia uzi humu kuhusu uendeshaji wangu wa bike.

Kilichofuata hata wiki haikupita... mimi chali!. Uzi ule wa kwanza ukafutwa na kupandishwa uzi huu
Pascal Mayalla apata ajali..... na ndipo nami nikatua rasmi humu JF na baada ya mwaka nikatoa shukrani
Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
from then mimi ni mtu makini sana
naamini kwenye nguvu ya kauli Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu Kiongozi Tunayemtaka!. Mdomo Huumba!.

Mimi ni muumini kuwa humu jf tuna manabii wetu wa ki jf jf TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!

Pia humu JF tuna wanga wengi tuu Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

P
Mchango mwingine very objective
P,
Sijakuelewa wewe ni mwandishi kweli ukumbe very complicated kuelewa. Mimi kazi yangu ni opposite kama analyst ni kurahisisha vitu! Kwa ufupi sijaelewa ujumbe wako na tofauti ya Yeye na Yeye😂
Japo JF mwanzo was meant to be the home of great thinkers, great mind who discuss ideas, those who can read and think, but as times go by, simple minds who discuss people wakajazana humu, ordinary mind who discuss events nao wakajazana humu, hivyo sasa jf ni home to everyone, simple minds, ordinary minds na great minds, ukipandisha bandiko linalohitaji great mind to digest, only the great mind ndio wataelewa unazungumzia nini, simple minds na ordinary minds wataishia chaka.

Kwa kukusaidia wewe and the like minded people wa level yako, bandiko hili Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Maana yake
  1. Marais wa nchi hupangwa na YEYE.
  2. JPM yeye alipanga kumalizia awamu yake ya pili lakini YEYE akampangia kazi nyingine na badala yake ndiye akatuletea Samia.
  3. Hivyo Rais Samia hakupanga yeye kuwa rais wa JMT bali alipangiwa na YEYE.
  4. Urais haupangi wewe, kazi yako ni just to wish, Ila ili uwe wewe na wish yako itimie, ni lazima iwe imepangwa na YEYE.
  5. Rais Samia alipoulizwa na Kikeke kama atagombea 2025 alijibu vizuri kuwa mambo ya 2025 tumwachie mpangaji Mungu.
  6. Kwa vile Tanzania hatukuwahi kuchagua rais Mwanamke, Kwa Samia imetokea tuu kwa kudra za Mungu, then lets wish 2025 tusimame na mgombea Mwanamke.
  7. Nikasema mwanamke huyo, sio lazima awe ni Rais Samia, bali ni yule aliyepangiwa na YEYE.
  8. Hivyo kama 2025, ni Samia ndiye aliyepangiwa na YEYE, then who are we to say no?.
  9. Hivyo kama yeye ndiye aliyepangiwa na YEYE, then 2025 ni yeye.
  10. soma tena
  11. Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, ila Mungu huweza kulikatiza chaguo lake wakati wowote na kumchagua mwingine, hii haikuanza leo, toka enzi za Nabii Musa, alikatizwa hakuingia nchi ya ahadi Caanan, kwa sababu fulani. Everything happens for a reasons anazojua Mungu mwenyewe, hivyo hata Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania labda hadi 2025 ni Mungu tuu mwenyewe anajua. Kama Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema nasi hapa katikati kabla ya 2025, kwasababu hata JPM, hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, vivyo hivyo kwa Samia 2025, ni Mungu tuu pekee ndiye ajuaye amepanga nini, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa sasa wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua utaratibu wa CCM, anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if kama ndivyo Mungu alivyopanga.

    Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is shure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha lazima mwanamke huyo awe ni yeye!. Hivyo ni busara kwa rais wetu Samia, hili la ugombea wa 2025, asilizungumze zungumze sana kwa sasa, ni vyema akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na yale ya Kimungu tumuachie Mungu mwenyewe.

    Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

    Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

    2025 Twende na Mwanamke!.

    Paskali
Hivyo wakati tukisubiri 2025 huku tukienda na Samia, hivi visauti sauti sasa ndio vinaanza. Kwa vile no one is certainly sure of tomorrow, na hakuna uthibitisho wa hizi sauti , voices from within kama ni sauti ya YEYE au yeye, ukisikia sauti inakuambia kitu, kama kitu hicho kinasemeka, kiseme, ili kijulikane, kama ni kizuri kipepewe, kama ni sio kizuri kitafutiwe jinsi.

Natumaini nimeeleweka.
P.
 
Back
Top Bottom