Riwaya: Mwanamke Kama Mama Yangu

Dotonho

Member
Jun 25, 2022
21
92
Habari member wa JamiiForums ningependa kuwaleteeni Riwaya ya ndugu mwandishi Kelvin kagambo ili tuelimike na kubuludika pamoja.

========

RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN DONATUS KAGAMBO

SIMU: 0713 48 28 16

FACEBOOK: KEV CLEVER KAGAMBO

SEHEMU YA KWANZA (1)

"Vuta picha ungelikuwa umezaliwa Mwanaume. Je, ungelithubutu kuoa Mwanamke wa sampuli yako?" Nakumbuka hiyo ndiyo ilikuwa sentensi yangu ya mwisho kwake kabla hajarejea Paradiso.

Pengine anaweza asikumbuke nguvu iliyobebwa na sentesi hiyo yenye maneno 12 tu, lakini binafsi naamini ilikuwa ni sentensi yenye nguvu kuu ndani yake. Sentensi ambayo ilikuwa na uwezo wa kubadili yabisi kuwa kimiminika au hata rangi nyeupe kurudi nyeusi.

Ndiyo; na hiyo ni kwasababu sikuzungumza sentensi hiyo kama jinsi mlevi anavyomtongoza baa medi, husema nakupenda licha ya kwamba neno hilo hutokea kwenye ndimi na si moyoni kama inavyohitajika.

Nilizungumza sentensi ile kwa HISIA kali na mguso wa hali ya juu na ndio maana mara tu baada ya sentensi ile nilitokwa na machozi, nikaingia ndani; chumbani, nikajifungia mlango.

Pengine alidhani labda nitaingia ndani na kuchukua kamba ngumu na madhubuti halafu nitajinyonga, lakini mimi si mpuuzi namna hiyo, nijihukumu kwa makosa ya mwenzangu, ni upuuzi ambao kamwe siwezi kuufanya.

Nakumbuka siku ile ilikuwa Jumatatu, kazi zilinibana haswa kiasi kwamba mpaka kufikia majira ya saa tatu za usiku bado nilikuwa kazini. Kwasababu nilikuwa ni Baba wa familia basi ilikuwapo kila sababu ya kuwajulisha wanafamilia yangu kwamba ningechelewa kurejea nyumbani siku hiyo.

Nilichukua simu na kumpigia Ashura--Mke wangu. Simu yake iliita bila majibu na hata niliporudia tena na tena mambo yakawa yale yale.

Sikuwa na hofu wala yale mawazo potofu juu ya Mke wangu. Na hiyo ilikuwa ni kwasababu naifahamu tabia yake ya kuacha simu chumbani wakati mwenyewe akiwa sebuleni.

Nikaendelea na kazi hadi kufikia saa nne nikamaliza. Nitatoka ofisini kuelekea kwenye maegesho ya magari. Nikiwa mbali nikaipata taswira ya ki-gari changu kidogodogo, Toyota Vitz yenye rangi nyekundu ambayo nilinunuliwa na kampuni na kupewa kama zawadi kwa utendaji wa kazi unaozingatia viwango.

Basi nikakiribia na kutoa funguo ambazo mara zote huzifunga kwenye Lux za suruali. Nikafungua mlango huku nikitabasamu.

"Hakika mimi ni mfanyakazi bora na mwenye mafanikio" nikajisemea moyoni na hiko ndicho kilichonifanya nitabasamu.

Lakini ghafla sura yangu ikabadilika, lile tabasamu likayeyuka na ndita zikachukua nafasi.

"Kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke imara nyuma yake" nikasikia sauti ikinambia hivyo na hiyo ndiyo iliyofuta tabasamu langu.

Sikuwa nikikubaliana na sentensi hiyo kwa asilimia 80. Imani yangu ni kwamba si kila mwanaume mwenye mafaniko yupo Mwanamke imara nyuma yake. Sisemi hayo kwasababu ya Ushabiki au kwasababu mimi ni mwanaume, hapana.

Bali nazungumza kitu ambacho nakiishi mimi mwenyewe. Nina kazi nzuri, nina gari, nyumba na hata kipato changu si cha kulenga kwa manati. Yaani hata ingetokea ile kampuni ninayoitumikia ikafirisika leo hii bado ningeendelea kuishi kwa kujitanua kwa kutegemea miradi mingine niliyoianzisha.

Nina kibanda cha Pesa za mtandao, Kibanda umiza ambacho nimemuweka mtu maalum anaonesha mechi za mpira wa miguu na pia namiliki duka kubwa maeneo ya Tabata.

Lakini mafanikio yote hayo Mke wangu ambaye kimsingi ndiye alitakiwa awe mwanamke wa nyuma yangu wa kuhakikisha nafanikiwa hajachangia hata theluthi.

Labda sina bahati kama aliyokuwa nayo Baba yangu-- Mzee Shomari. Yeye alimuoa Khadija, mwanamke ambaye alijitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha Mume wake anafanikiwa.
Jitihada zake zilinifanya nitamani kuoa na MWANAMKE KAMA MAMA YANGU.

Sio kwasababu Mama yangu alikuwa mweupe kama mimi, mwanya mdogo mdogo na vishimo mashavuni pindi anapotabasamu, kucheka au hata anapotamka baadhi ya maneno bali ni kwasababu ya jitihada zake za kufanikisha Baba yangu anaitwa Mwanaume hata anapokuwa nje ya nyumba yetu. Na si kuitwa mwanaume kwasababu ya kuvaa suruali na kuota ndevu tu. Hapana, bali kwa kuwa na kipato cha kukidhi mahitaji ya familia na ziada.

Sura yangu ilibadilka na kurudi kawaida baada ya kugundua kuwa nimetumia dakika mbili na sekunde kadhaa kuwaza mambo hayo. Nikafungua mlango wa ki-gari changu na kutumbukia ndani yake. Nikakiwasha na leo kikawaka bila matatizo ingawa hiyo haikuwa kawaida yake.

Mara nyingi kilikuwa kikinisumbua kwenye kuwaka, hakikuwa na tabia ya kuwaka mara moja unapokiwasha. Ilikuwa ni lazima kukilazmisha au hata kukisukuma kwanza. Nikarudi nyuma (kwa kupiga Reverse) kisha safari ya kuelekea yalipo makazi yangu ikaanza.

Niliendesha kwa mwendo wa taratibu sana kwani niliamini mwendo kasi haukuwa ukifanana na umri wangu; Miaka 30 na kadhaa, pia namiliki familia ya Mke na watoto wawili ambao wote bado wananitegemea. Wanangu wanasoma shule zisizo za Serikali na kwa pamoja nawalipia karo ya zaidi ya milioni moja kwa mwaka.

Hakika mwendo kasi haukunifaa, mtindo wa kuendesha gari kama
mwendawazimu uliwafaa vijana ambao hawakuwa na majukumu namna yangu.

Basi taratibu niliendesha gari yangu huku nikila muziki laini kutoka kwa baadhi ya vijana wa kitanzania walioamua kutumia sauti na akili zao kutuburudisha, kutuelimisha na hatimaye kujipatia kipato. Nyimbo mbili tu za dakika tatu na sekunde kadhaa kila moja zilitosha kunifikisha Buguruni.

Lakini mara manyunyu ya mvua yakatoa habari kwamba punde itanyesha mvua mkubwa, hapo nikaona kila mtu akijitahidi kufanya jihtihada za kuikabili mvua hiyo na punde ikaanza kunyesha.

Ilinyesha mvua kubwa na kunilazimisha kufunga vioo vya ki-gari changu japo nilijua hiyo ingelikuwa ni adhabu kwani AC ya gari yangu ilikuwa haifanyi kazi.
Mara taa za barabarani zikawa za kijani na kunirusu nitembee.

Niliendesha gari na dakika kumi na mbili baadaye niliwasili nyumbani, Kitunda. Ile mvua bado iliendelea kunyesha, tena huku nyumbani ndiyo ilikuwa kubwa zaidi. Nikaegesha gari mbele ya nyumba yangu, nikachukua simu tu na kuacha vitu vingine vyote garini ili visije kulowa. Nikateremka na kukimbia mpaka kwenye mlango wa nyumba, nikafungua kwa kuusukuma kwasababu ulikuwa umesindikwa tu na nikapita mpaka ndani.

'KIMYA' kilinikaribisha, sikusikia sauti ya Mke wangu wala watoto wangu. Nikajitupa kwenye sofa huku nikiita majina ya wanangu.

"Khadijaaa? Ally?" lakini sikupata jibu.
"Ashura Mke wangu nimerudi" nikapayuka hivyo baada ya kuona sikupata jibu toka kwa wanangu lakini sikujibiwa pia. Nikachukua simu na kumpigia Mke wangu mara baada ya kutafuta nyumba nzima bila kufanikiwa kumuona mtu yeyote. Simu ya Ashura nayo iliita bila majibu kama kawaida yake, hofu ikanizidi lakini si mawazo ya kwamba huenda mke wangu yupo kwenye michepuko kwasababu asingeweza kwenda huko kwa kubeba watoto wote.

Nilichanganyikiwa siku hiyo pengine zaidi ya siku yoyote ile duniani. Niliwaza kupiga simu kwa wakwe zangu lakini nayo niliona ni mapema sana, nilihitajika kuwatafuta zaidi na zaidi kabla ya kufikia hatua hiyo ambayo ingekuwa ya mwisho kabisa katika Operesheni yangu.

Nikapata wazo la kutoka ndani na kuelekea nyumba ya jirani kuuliliza. Nikachukua mwamvuli pamoja na tochi na kueleka huko. "Khadija alikuwa hapa siku nzima ya leo lakini aliondoka kwenye saa kumi na mbili za jioni" akanijibu Mama Alphonce, jirani yangu nyumba ya pili kutoka nyumbani; nilikimbilia hapo kwasababu ndiye jirani niliyemzoea zaidi na hata wanangu walikuwa wakipenda kucheza hapo haswa huyu mkubwa—Khadija.

Nilizidi kutoelewa nini kilikuwa kikiendelea, na wala sikutaka kumuuliza zaidi habari za Mke wangu kwani nafahamu jinsi wanawake walivyonatabia ya kuteteana. Hata kama angelikuwa amekwenda baa kuchuna buzi lakini Mama Alphonce angenidanya ili nisijue lolote.

Nikarudi nyumbani tena, nikaingia jikoni sehemu ambayo mwanzo sikuikagua. Hofu ilinizidi mara baada ya kuingia huko kwani nilikuta sahani kadhaa za udongo zimevunjwa, nikaogopa sasa. Nikahisi huenda kuna uvamizi umefanyika nyumbani kwangu.

Haraka nikatoka nje na kurudi tena kwa Mama Alphonce kuuliza lakini hata kabla sijabisha hodi mlango wa choo chao cha nje ulifunguliwa na akatoka Alphonce; mtoto wa miaka saba tu.
"Shikamoo Baba Ally" akanisalimu huku akisulubiwa na ile mvua ambayo mimi haikunipata kwasababu nilikuwa nimejikinga kwa mwamvuli.
Nikamshauri asogee barazani ambapo mvua isigemsulubu naye akafanya hivyo. "Unamtafuta Khadija?" akaniuliza lakini kabla hata sijamjibu kwamba ni ndio au hapana alitiririka.

"Khadija kaenda kumtafuta Ally, kasema kapotea tangu "akanambia lakini kabla hata hajanipa maelezo ya kutosha radi kubwa ilipiga, hapo akamsikia Mama yake akimuita naye haraka akakimbilia ndani na kuniacha nimeganda kama sanamu ya
Askari pale Posta.

Sikuona tena sababu ya kumuuliza kitu Mama Alphonce kwani tayari nilishapa picha ya nini kinaendelea. Kumbe mwanangu amepotea na pengine ndio maana hata nilipompigia simu Mke wangu hakutaka kupokea kwasababu alijua kuna hitilafu nyumbani.

Nikarudi kwangu na kuketi nikiwaza nifanye nini. Nilirudia tena kumpigia simu mke wangu lakini hakupokea kama kawaida yake na hapo nikiwa nimeshjua kwanini hapokei simu yangu.

Wazo la kunyanyuka na kwenda kuwasaka lilinijia na sikutaka kujishauri mara mbili, nikanyanyuka nikiwa na tochi pamoja na mwamvuli tu. Nikafunga mlango kwa funguo na safari ya kuitafuta familia yangu ilianza.

Mitaani hakukuwa hata na watu kwasababu mbili. Kwanza ni ile mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha lakini pia kwetu bado palikuwa ni kitongoji kipya, hakukuwa na watu wengi.

Nilivuka mitaa zaidi ya sita nikiitafuta familia yangu hasa mwananangu Ally ambaye nilipata habari kwamba amepotea. Nikiwa mtaa wa sabu kutoka nyumbani nikamuona mtu mbele yangu, sikumfahamu kwa sura kwasababu sikumuona mtu halisi bali taswira ya mtu kutokana na kule alipokuwako kuwa na giza nene. Lakini pia nilitamani kummulika kwa tochi niliyobeba lakini nikahofia kwamba pengine angechukia kumulikwa kama wengi wachukiavyo.

Lakini kitu nilichogundua kwa haraka ni kwamba mtu yule alikuwa ni mwanamke tena mtoto mdogo, hapo nikatamani awe binti yangu Khadija ingawa ingekuwa ngumu kwasababu niliamini kwamba Khadija ameondoka na Mama yake kumtafuta Ally ambaye inasemekana amepotea.

Mtoto yule alikuwa akitembea kuelekea nilipo, hana mwamvuli japo mvua kubwa ilikuwa ikinyesha. Nilimuonea huruma sana na nikanuwia kumsaidi pindi tutakapokaribiana hata kama si mwanangu.

Taratibu tukakaribiana, akiwa umbali wa mita chache hivi nikapata taswira yake kamili. Ni Khadija, binti yangu; Nikagundua hilo.

Tazama alivyolowana kwa mvua. Nguo chapachapa sambamba na kugongana meno kwa baridi. Usiku huu wa takribani saa sita yu-mwenyewe njiani anatembea, tatizo ni nini?

"Babaaa" alipayuka baada ya kung'amua kuwa aliye mbele ni Baba yake, akanikimbilia na kunikumbatia nami nikampokea huku nikipiga magoti ili kulingana nae, sikujali tope lililotapakaa ardhini, nilipiga magoti na kuchafua suruali yangu ya kitambaa yenye rangi nyeusi lakini yote ilikuwa ni kwasababu ya mwanangu.

"Babaa, Ally kapotea" akanambia Khadija huku sentensi yake ikitoka kwa mtetemeko kutokana na baridi na kilio alichokuwa akikishusha.

Nilijikuta natokwa chozi, na si kwasababu ya kupotea kwa Ally bali ile hali aliyokuwa nayo Mwanangu Khadija, ilinisikitisha kwa kweli. Hana hata viatu, miguu pekua kama Bata ingawa wiki moja tu iliyopita nilimnunulia Yebo-Yebo nzuri za manjano.

Lakini wakati yote hayo yanatokea Mama yao alikuwa wapi? Anafanya nini na mbona hakunijulisha kinachoendelea. Hakunijulisha kwamba mtoto kapotea au hata kupokea simu?

**************************
USIPATE SHIDA YA KUJIBU MASWALI YOTE HAYO, SEHEMU YA PILI ITAKUPA MAJIBU.

UKITAKA KUIPATA RIWAYA HII KWA HALAKA ZAIDI WAWEZA KUWASILIANA NA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.
 
Attachments

  • FB_IMG_16591867722077835.jpg
    FB_IMG_16591867722077835.jpg
    18.1 KB · Views: 26
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN DONATUS KAGAMBO

SIMU: 0713 48 28 16

FACEBOOK: KEV CLEVER KAGAMBO

SEHEMU YA PILI (2)

ILIPOISHIA

Nilijikuta natokwa chozi, na si kwasababu ya kupotea kwa Ally bali ile hali aliyokuwa nayo Mwanangu Khadija, ilinisikitisha kwa kweli. Hana hata viatu, miguu pekua kama Bata ingawa wiki moja tu iliyopita nilimnunulia Yebo-Yebo nzuri za manjano.
Lakini wakati yote hayo yanatokea Mama yao alikuwa wapi?, anafanya nini na mbona hakunijulisha kinachoendelea. Hakunijulisha kwamba mtoto kapotea au hata kupokea simu?.

ENDELEA

"Mama yupo wapi?" nikajikaza na kumuuliza Khadija ambaye bado alikuwa amenikumbatia muda huo huku akiendeleza kilio.

"Sifahamu alipo" akanijibu kwa ufupi jibu ambalo kama lilinieleza kuwa niachane na habari za Mama.
Nilifanya hivyo, nikasimama na kumsimamisha pia na sasa tukaunda jeshi la watu wawili na msako wa Ally ukaanza huku sasa nikifahamu kwamba Khadija hakuondoka na Mama yake.

Nilitembea huku moyo wangu ukiwa na machungu na hasira hasa kwasababu ya Mke wangu. Haiwezekani yote hayo yanatokea anashindwa hata kunijulisha, na si kunijulisha tu bali hata kushiriki katika lolote lile.

"Vituko vyake nimeshindwa kuvivumilia, leo ndiyo utakuwa mwisho wa ndoa yetu. Nitampa talaka ta....." nikawa nawaza hivyo huku tukiongozana na mwanangu Khadija ambaye nilimpa jina la marehemu Mama yangu mzazi lakini kabla hata sijamaliza sentensi yangu Khadija alinisitua kwa yowe kubwa alilopiga.

"Babaa Ally yuleee"

Haraka nikarudisha akili yangu pamoja na macho kuelekea kule nilipooneshwa na Khadija. Ni chini ya mti mkubwa na kweli nikamuona mtu amesimama ingawa sikupata taswira yake vyema kutokana na giza.

Bila shaka alikuwa ni mwanangu kipenzi na wapekee wa kiume --
Ally. Khadija alinichomoka na kukimbilia kule alipomuona mdogo wake aliyesimama chini ya mti pengine kwasababu ya kujikinga mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

Nilishukuru Mungu kwa kufanikiwa kumuona mwanangu. Nikajikuta natimua mbio na kutumbukia kwenye madimbwi kana kwamba nilikuwa siyaoni lakini yote hiyo ni kwasababu ya furaha na upendo nilio nao juu ya Ally; Mwanangu wa pekee wa kiume ambaye pengine angelikuwa ni wa mwisho kwani nilipanga kuwa na watoto wawili tu katika siku za maisha yangu.

Nilimzidi mbio Khadija ingawa ni yeye ndiye aliyeanza kumkimbilia ndugu yake. Lakini niliingiwa na shaka juu ya Ally kwani alikuwa amesimama kana kwamba hakuwa ametuona na kama ametuona basi hatufahamu na endapo anatufahamu basi hatupendi. Amekakamaa kama gogo na asiye na jitihada zozote za japo kutukimbilia.

Sikujali hilo, nilitimua mbio na haikuisha dakika nilimfikia na kumkumbatia kwa upendo mwanangu, lakini hakika sikuweza kuendelea kufanya hivyo hata kwa sekunde tano.
Nilijing'atua na kujiweka mbali na Ally kwa mtindo wa kujirusha huku nikitazama mikono yangu ambayo ndiyo iliyonipa fursa ya kumkumbata mwanangu.

Nikaacha kutazama viganja vya mikono yangu na kutupa jicho tena kwa Ally ambaye muda huo alikuwa akianguka kama mgomba uliokatwa na panga kali.

“Tiiii” alifika aridhini na kishindo kikasikika namna hiyo lakini ajabu hakutoa sauti yoyote ya kuashiria kwamba kaumia.

“Si Ally wangu huyu, si yeye. Mwanangu Ally hana ngozi ya kubanduka namna hii” nilijikuta nimeropoka kutokana na kile nilichokumbana nacho, kwasababu nilipomkumbatia nilihisi ni mwenye ngozi laini na yenye kubanduka mithili ya mtu aliyeungua kwa moto.

Lakini sikuishia pale nilipiga moyo konde na nilitambaa mpaka alipodondokea na kumuinua. Nafsi yangu ikanithibitishia kwamba Yule alikuwa ni mwanangu, nikamnyanyua na kamuweka mapajani muda huo nikiwa nimeketi kwa mtindo wa kupiga magoti huku kooni nikihisi kunasa kwa donge zito.
Punde hiyo dada yake akawasili akiwa na ile tochi niliyoiangusha wakati namkimbilia Ally wangu; akamulika Khadija na kufanya nisiamini kile nilichokiona kwa macho yangu haya mawili.
Mwanangu alikuwa mweusi kama lami au mkaa. Hapa ndipo nilipozidi kusadiki kwamba mwanagu aliungua. Kwanza ngozi kuwa nyeusi namna ile lakini pia ngozi kubanduka kila unapomshika.

Achana na hilo la kuungua, nilikuja kung’amua kwamba nilikuwa matatizoni zaidi ya kawaida mara baada ya kugundua kuwa mwanangu hapumui, amefariki na kamwe sitaishi naye tena duniani.

"Babaa huyu sio Ally" alisema Khadija huku akilia. Hakuwahi kumuona mdogo wake akiwa mweusi mwenye kutisha namna ile hasa ukizingatia mwanagu alikuwa mweupe kama Mimi Baba yake. Alilia mpaka akadondoka chini na kugalagala kwenye tope Khadija kwani hata yeye alikwishafahamu ndugu yake hatunaye tena kiroho.

Nilijikuta nikimuachia mwanangu na kumsaidia Khadija kugalagala, basi tukawa kama wachawi wanaocheza mahepe chini ya mti ule mrefu na mkubwa. Hatukupenda kufanya hivyo bali ni kwasababu ya yale yalitukumba. Tuligundua tumempoteza mwenzetu lakini si kumpoteza tu bali alipotea akiwa si yeye; mwenye muonekano tofauti na mbaya zaidi kati yetu hakuna aliyejua kilichomkumba Ally.

Mtoto wa miaka mitano tu ambaye ukubali ama ukatae hakustahili kufa. Kifo cha Ally kingekuwa ni pigo kwenye maisha yangu lakini kufariki akiwa mtoto wa miaka mitano ni pigo takatifu ambalo sitakaa nilisahau maishani.
Ni mwezi uliopita tu nilitoka kumlipia karo la shule, zaidi ya Shilingi laki 6 ambayo ilikuwa ni ada ya mwaka mzima. Amefariki sasa, ni nani atakayefidia ada hiyo. Nani atavaa sare zake za shule badala yake? Nani atavaa nguo zake za gharama ambazo nilikuwa nikimnunulia kila mwezi ili afahamu kwamba namjali na nampenda na itakapofika siku ya siku nitakapozeeka asiache kunijali pia.

Hata kama umri bado unaruhusu kupata mtoto lakini hakika sitampata Ally, pengo la Ally wangu halitazibika mpaka kuzikwa kwa Dunia.

Mtoto mzuri, mweupe, mrefu mwenye tabasamu zuri na lichekeshalo wakati mwingine kwasababu ya yale mapengo yake ya mapokezi (meno ya mbele) ambayo nakumbuka siku namng’oa meno hayo, aliyachukua na kuyatupa juu ya paa la nyumba na kusema “Kunguru nipe meno ya dhahabu”
Hakika hatokuja kama Ally wangu na hata akija hatofuta maumivu niliyonayo kwa mtindo ambao Ally wangu amenitoka.

Nilisulubika usiku ule, kugalagala chini, kwenye matope na mvua kubwa inapiga. Sikupenda ila ilibidi; Mimi na binti yangu Khadija tulikuwa na kila sababu ya kufanya vile.
Lakini ghafla kilio cha mwanangu Khadija kilikatika, nikajali na sio kujali tu bali hata moyo ulinilipuka.
Nikageuka haraka na kumtazama na mwanangu.

Kimya...

Nilimuona yupo kimya, hatingishiki. Haraka nikamsogelea na kumtingisha lakini hakuonekana kujibu ulizo langu kwa vitendo.
Pengine naye alikuwa amefariki lakini sikutaka kukubali kirahisi namna hiyo, kwanza nafahamu kuwa Mungu si mwenye roho mbaya kiasi hicho, eti amchukue Ally na dada yake pia kwa wakati mmoja. Hapana, hakika Mungu hawezi kufanya hivyo.
Niliendelea kumtingisha mwanangu lakini wapi, hakujibu. Nikamvuta na kumuweka mapajani nikiwa nimepiga magoti. Nikanyoosha mkono hadi ilipokuwa tochi pembeni yetu. Nikainyanyua na kuumulika uso wa mwanangu kipenzi.
Oooh, Mungu wangu! Khadija kafumba macho, hapana hajafa labda amelala.

Nikajaribu kumtingisha labda angeamka lakini wapi.
Tochi nayo ikapinga kuniunga mkono, taratibu ikapungua mwanga wake hatimaye kuzimika kabisa, ikaninyima fursa ya kuiona kwa uwazi sura ya binti yangu, mwanangu wa wa kwanza na wapekee wa kike kati ya watoto wangu wawili.

Ni hivi juzi tu nilipokea ripoti yake kutoka shule, ripoti iliyokuwa ikionesha utendaji wake kimasomo. Alikuwa wa kwanza kati ya watoto zaidi ya 70 wa darasa la pili. Nakumbuka hata Mwalimu wake aliniambia "Huyu mtoto atakuja kutikisa sana sekta ya elimu miaka ya baadae"

Muongo, Mwalimu alikuwa akiniongopea, eti mwanangu atakuwa tishio siku za baadae wakati leo amekufa.
Amefariki na kamwe sitaona tena ripoti yake.
Nilimuachia, nikajikuta mwili umekwisha nguvu na kulegea kana kwamba sikuwa na mifupa. Hata ile mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kwangu ilikuwa ni kama jua kali la kiama. Ilinichoma na kuniunguza haswa. Nililia siku ile kiasi pengine nilimaliza tangi lote la machozi.

Kumbe Mungu hana huruma, kwanini ananitenda hivi. Nitabaki na nani, nani atakayenipokea nikirudi kazini. Nani nitamshushia neti kabla ya kulala wakati Ally amefariki?, nani nitamfundisha hesabu za kuzidisha wakati Khadija wangu hayupo. Nitabaki na nani duniani.

“Mungu kama wewe ni bingwa sana wa kuadhibu watu niue na mimi, nichukue kama ulivyomchua Ally wangu. Nitwae kama ulivyomtwaa Khadija wangu.
Nakuchukia na kamwe sitakuamini tena tangu leo, uliahidi kutupigania na kushambulia maadui wanaotushambulia lakini mbona nini wewe unayetushambulia?.”

*****************************

Nilipofungua macho tu mtu mmoja akanisogelea haraka.
"Umeamka Baba" akaniuliza.
Nikamtupia jicho la udadisi kama nimemsahau na yeye akagundua hilo.

"Bado, bado hujawa sawa. Naona hata kumbukumbu zako hazijarudi" akanambia. Taratibu kumbukumbu alizosema zimepotea zikarudi na kunikumbusha kuwa Mwanamke huyo aliyesimama mbele yangu ni Shangazi yangu. Shangazi Rukia ambaye ni dada wa kuzaliwa na marehemu Baba yangu--Mzee Shomari.

"Shangazi nipo wapi hapa?" nikamuuliza, nilifahamu sikuwa nyumbani lakini sikung'amua ni wapi
"Upo nyumbani" akanidanganya bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo ananijaza hasira, sikuwa nikipenda kudanganywa hata siku moja.
"Kwanini unaninganya, nieleze nipo wapi?" nikamuuliza kwa kung'aka kana kwamba nilikuwa nazungumza na mtoto wangu.
Lakini kabla hajanibu mlango wa chumba kile kilichokuwa na vitanda viwili, kabati dogo na kining'izo cha pazia zenye rangi za kijani, ulifunguliwa na akaingia binti mmoja aliyevalia gauni jeupe. Kwa mtazamo wa haraka niligundua gauni lile ilikuwa ni sare na si gauni la kawaida.

Kumbukumbu zikarudi, nikagundua nipo hospitali.
"Nafanya nini hapa hospitali?" nikauliza kama nataka kupigana na huyo aliyenileta hapo. Nikashusha miguu yangu na kuiweka ardhi hiyo ikiwa na maana kwamba najiandaa kutoka eneo hilo ambalo sikulipenda hata kidogo.

"Tulia Jamal, tulia mwanangu" akanambia Shangazi, sikuleta ukaidi uliokithiri, nikatulia na kumsikiliza.
"Mwanangu naomba utulie, hapa tuko hospitali na punde tutapewa ruhusa ya kurejea nyumbani" akanieleza kwa unyenyekevu Shangazi.
"Kwanini niko hapa?" nikahoji.
"Yote utakwenda kuyafahamu nyumbani naomba uwe mpole na usiye na haraka, si wafahamu haraka haina baraka" akanieleza.
"Ngoja nimuite Daktari tuangalie uwezakano wa kumruhusu" akasema yule Dada ambaye alikuwa amevalia gauni jeupe. Akatoka nje na punde akarejea akiwa na Mama mwingine wa makamo ambaye yeye alikuwa ndani ya koti refu na jeupe.
Akaja karibu yangu Mama huyo, akanishika bega la kulia kwa mkono wake wa kuume.
"Unajisikiaje?" akanihoji.
"Najisikia vyema na sijui kwanini niko hapa" nikamjibu huku nimekunja sura.
"Sawa utaondoka lakini Je, unasikia maumivu yoyote?" akaendelea kunikera kwa maswali yake ambayo sikuona kama yalikuwa na faida yoyote kwangu.
"Mama sijikii maumivu yoyote hebu niachie niondoke zangu mie" nikang'aka.

Basi hapo yule Mama akanyanyuka na kutoka akiwa na yule binti na punde wakarudi pamoja na kuturuhusu kuondoa.

Dereva wa taksi tuliyopanda aliendesha kama nilivyohitaji. Nilimwagiza kuendekesha kwa mwendo kasi ili niwahi kufika nyumbani nifahamu kinachoendelea.
Nilipoteza kumbukumbu kabisa na ndio maana hata nilitaka niwahi kufika nyumbani ili nielewe kilichonisibu.

********************************
UNAIKOSAJE SEHEMU YA TATU YA RIWAYA HII?

KAZI KWAKO UKITAKA KUIPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA ZAIDI WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
Attachments

  • Mwanamke Kama Mama Yangu.jpg
    Mwanamke Kama Mama Yangu.jpg
    18.1 KB · Views: 20
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN DONATUS KAGAMBO

SEHEMU YA TATU (3)

ILIPOISHIA…

Dereva wa taksi tuliyopanda aliendesha kama nilivyohitaji. Nilimwagiza kuendekesha kwa mwendo kasi ili niwahi kufika nyumbani nifahamu kinachoendelea.
Nilipoteza kumbukumbu kabisa na ndio maana hata nilitaka niwahi kufika nyumbani ili nielewe kilichonisibu.

ENDELEA…..

Dalili mbaya nilianza kuziona nje ya nyumba yangu, nilikuta maturubai kana kwamba kulikuwa na msiba, sikutaka kuuliza. Niliteremka kwenye gari kama jambazi na kutoa mbio kukimbilia ndani ili kuhakiki familia yangu kama ilikuwa salama.
Watu waliojaza mikekani chini ya maturubai walinitazama lakini sikuwajali. Nilipita moja kwa moja mpaka mpaka ndani kwangu kama fataki.

Nilipofika sebuleni nilimkuta Ba mkubwa, Baba wadogo wawili pamoja na ndugu zangu wengine wakiume wapatao watatu, sikuwajali pia. Niliekea chumbani kwangu lakini kabla hata sijafika mlangoni walinikimbilia na kunizuia.
"Niacheni" nikawaambia huku nikijaribu kuwaponyoka, wakanizidi nguvu, wakanisogeza hadi sebuleni na kunikalisha kwenye sofa.
"Vipi umetoroka hospitali ama?" akauliza Ba mkubwa.
"Baba sitaki maswali ya kipuuzi, naomba mniache" nilisema hivyo, pengi hivyo labda nimerukwa na akili kwani niliwaita wapuuzi bila kujali kuwa walikuwa walikuwa ni Baba zangu.
"Hali mbaya, Kei kalete kamba" nikamsikia Baba mkubwa akimwambia binamu yangu eti wakalete kamba.
"Baba mkubwa naomba tuheshimiane kwa maana naona unapoelea kubaya. Mnifunge kamba kwami mimi ni Kichaa? Mimi si mwendawazimu, nina akili zangu timamu" nikawaambia hapo nikiwa na hasira kweli kweli.

Pengine hawakunielewa na bado walikuwa na mawazo ya kwamba nimerukwa na akili, nikamuona kei akiinuka na labda alikuwa akifuata kamba kama alivyoagizwa. Punde alirejea akiwa na kamba ya katani mkononi.
"Haya mshikeni vyema" Baba mkubwa akaagiza. Basi wakanikamata na kuniminyia kwenye sofa, wakaivuta mikono yangu kwa nyuma ili waifunge kamba.
Niliumia sana kwa kweli, kwanini mtu timamu kama mimi wanichukulie mwendawazimu kiasi cha kutaka kunifungia kamba. Hizo akili zimeniruka lini na kwasabu ipi?.

Mawazo hayo yakanipa nguvu, nikajikuta nimenyanyuka kama mzimu na kumpiga kiwiko maeneo ya kidevuni yule aliyekuwa kinara wa zoezi lile. Akaniachia na kudondokea pembeni akiugulia maumivu, nikasimama sasa na kumsukuma mwingine ambaye naye alijifanya jemedari pia.
Mara jicho langu likatua pembeni kidogo, hatua kama tano toka pale niliposimama. Kulikuwa na kisu eneo hilo, nikakirukia haraka na kuwatishia huku nikiwasihi wasithubutu kunisogelea. Wakaogopa na kurudi nyuma, hiyo ikanipa upenyo wa kusogea kwenye mlango wa chumba changu na kuchungulia ndani; sikuona familia yangu.

Nikatoka pale na kuingia chumba cha wageni ambacho chenyewe wala hatukukiwekea kitu chotechote.
Hata sijui ni nini kilichonituma kuchungulia humo kabla ya vyumba vingine lakini sikuamini kile nilichokiona.
Nilijikuta nimeduwaa na kuganda kama sanamu. Taratibu kumbukumbu zikaanza kurudi, nikakumbuka usiku wa jana, usiku ambao ulikuwa wa kuumiza zaidi katika siku zote za maisha yangu.

"Wananguuuu" nilijikuta nikipiga yowe namna hiyo mara baada ya ile picha ya jana kunijia. Bila shaka kelele zilitapakaa mpaka nje na kuwasitua watu.
Hata sijui nilijongea vipi kuelekea pale paliponifanya nilie lakini nilijikuta nimewasili.
Nikapiga magoti katikati ya maiti mbili za watoto zilizofunikwa gubigubi kwa shuka nyeupe. Nikafununua shuka kwa huyu wa upande wa kulia, hapo nikajikuta nikilia sana baada ya kumuona Khadija wangu amelala usingizi wa milele, usingizi ambao labda nilipaswa nilale mie kutokana na umri. Sura yake nzuri kama Mama yake bado ilionekana, alinivutia na kunifanya nione hakustahili kufa mapema namna ile.
Nikapiga moyo konde na kufunua upande wa kushoto kwenye maiti nyingine.

Hapo nikajikuta nadondoka na kumlalia maiti, si kwamba nilipenda, Hapana, bali ni hivyo maungo ya mwili wangu yalivyojisukuma. Sikuamini kama yule niliyemuona alikuwa ni mwanangu pia, tena Ally. Kile kitoto kidogo cheupe hivi ambacho kilisifiwa sana na wanafunzi wenzangu niliosoma nao chuo, ni siku zile tulipokuwa kwenye makutano ya chama chetu.
"Jamal mtoto wako mzuri" kila aliyemtazama alinambia huku akimchukua na kupiga naye picha.
Sasa waje leo wamuone jinsi alivyoungua, mweusi na hata muonekano wake ulikuwa kama zimwi. Hakika nisingesifiwa kuwa na mtoto mzuri kama wale walionisifia wangemuona Ally wangu akiwa hivi.

"Pole mwanangu, Mwanaume halii namna hiyo" nikasikia sauti ya Baba mkubwa ikinambia huku mkono wake ukiwa mgongoni mwangu.
Na wengine wakasogea pale na kuninyanyua taratibu tena nikanyanyuka kwa hiari. Sikutaka kuwaacha wanangu pale lakini sikuwa na jinsi, nisingeweza kwenda nao kaburini hata kama ingelikuwaje.
"Pumzikeni kwa amani wanangu" niliwaambia huku nikiwa siamini kiasi cha kutamani hili tukio lisiwe halisi bali filamu moja ya kusisimua kwa maana pindi itakapofika mwisho nitapata fursa ya kupiga soga na wanangu.
Isingeweza kuwa hivyo, Mungu alishasema iwe hivyo na haipingiki.

Wakanichukua na kunirudisha sebuleni, wakanikalisha kwenye kiti lakini nikiwa bado na kilio.
"Nyamaza kwa muda mwanangu nataka kuzungumza nawe" Baba Mkubwa akanambia hivyo. Nilijitahidi kunyamaza na ingawa ilikuwa ni kazi ngumu lakini nilifanikiwa.
"Unakumbuka chochote kuhusu kifo cha wanao" akaniuliza Baba mkubwa.
"Ndiyo" nikamjibu kwa kujilazimisha, sikupenda lakini sikuona budi kujibu ili kujua nini kitaendelea juu ya mazishi.
"Unakumbuka nini?"
"Jana nilirejea nyumbani sikukuta mtu, nilipouliza kwa jirani........." nikaeleza kila kitu kilivyokwenda.
"Sawa, msiba si wako tu ni wetu sote na hapa cha muhimu ni kufahamu jinsi gani tutapanga mikakati ya maziko" akasema Baba Mkubwa na kuendelea.
"Kuhusu wanao kwa kifupi tu ni kwamba jana tulipokea taarifa kwamba umeokotwa chini ya mti wewe pamoja na wanao wakati wakiwa tayari ni marehemu.
Ripoti ya Daktari inasema Ally alipigwa na Radi na Khadija yeye alipata mshituko wa moyo ambao ulisababisha damu kuacha kusambazwaa mwilini na hatimaye kufariki" alinambia Baba Mkubwa.

Niliumia sana, kumbe Ally alipigwa na Radi na pengine ni
kwasababu ya kusimama chini ya mti mrefu lakini Khadija pia alipata mshituko wa moyo ambao nahisi ulisababishwa na kushuhudia kifo cha nduguye.
"Kwahiyo na mkeo yuko wapi mbona hatumuoni?" Akauliza Baba mdogo. Hapo sasa akagusa penyewe, huo ndio ulikuwa mzizi wa matatizo yote ninayokumbana nayo. Kumbe hakuwa amerudi tangu jana.

"Hebu wapigie simu wazazi wake" akaagiza Baba mkubwa na hapo ikaletwa simu yangu, lakini kabla ya kupiga kuna ugeni ukaingia nyumbani.
Watu wapatao sita, Wakwe zangu wote wawili pamoja na mashemeji zangu wakaingia. Waliketi kwenye vipi baada ya salamu na kupeana pole za kutosha.

Walipomaliza tu wakakumbana na swali. "Yuko wapi binti yenu mbona hamjafika naye hapa?" aliwauliza Baba Mkubwa
"Binti gani? Ashura?" akauliza Mkwe wangu wa kiume.
"Ndiyo ni yeye, si ndiye aliyeolewa na mwanetu" akauliza tena Baba Mkubwa hapa akiwa na hasira kidogo.
"Mzee mwenzangu Ashura sisi hatujamuona nyumbani hivi karibuni na tumeshangaa kwanini yeye na Mumewe hajatulisha habari za msiba mkubwa kama huu tena unaotuhusu moja kwa moja. Tatizo nini?"
"Tatizo mwanao haonekani tangu jana na sidhani hata kama ana taarifa ya huu msiba" Akaeleza Baba Mkubwa, mzee mtata kweli asiyependa kuficha mambo yaliyo wazi.
"Hana taarifa, jamani mimi mbona sielewi, mnanichanganya tu" akasema Mama yake mke wangu.
"Wewe mwanamke vipi wewe, tunakuchanganya sisi ama huyo binti yako.,...." akaongea kwa jazba Baba Mkubwa, tayari hasira zilikwishampanda na pengine zilikuwa zimesalia sentensi tatu tu aanze kumwaga matusi.
Baba mdogo ikabidi aingilie suala hilo, alikuwa akimfahamu Kaka yake vyema.
"Hebu naomba tuzungumze kwa mpangilio mzuri wenye kujenga na si hivyo jamani, mimi ninachoona nyie wazazi wa Ashura mngechukua majukumu ya kumpigia simu binti yenu hapahapa ili tufahamu yu-wapi na ikiwezekana tupange na mipango ya mazishi tukazike, sisi ni waislamu bwana hatuwezi kukaa na maiti ndani kwa masaa muda mrefu kiasi hicho tena ukizingatia ni za watoto" akasema Baba mdogo.
Ushauri wake ulifuatwa, Baba mkwe akatoa simu yake na papo hapo akampigia simu mke wangu. Kama kawaida simu iliita bila kupokelewa zaidi ya mara tatu.
Ikawa zamu ya Mama mkwe pia, naye akampigia mwanaye zaidi ya mara tano lakini pia simu haikupokelewa.
"Si mnaona ushenzi wa binti yenu? Na huo si mchezo ulioanza leo tu tangu jana Jamal anafanya kazi kumpigia simu hapokei" akang'aka Baba mkubwa kana kwamba tulikuwa pamoja wakati nampigia.
"Usiseme hivyo mzee mwenzangu, unajua pengine amekumbwa na jambo baya..." akasema Baba Mkwe lakini tena Baba mkubwa akamkatisha.
"Jambo baya wapi? Na mbona hakumuaga Mume wake, hata Quran tukufu ya Allah inafundisha hayo kwamba mwanamke ni lazima amuheshimu mumewe na mwanamke kuomba ruhusa kwa mumeo ni jambo la heshima haswa. Sio mwanamke kama amekunywa supu ya miguu ya kuku, anatembea bila nukta wala koma" akang'aka Baba Mkubwa. Aliwasha moto kwelikweli mle ndani.
"Basi wacha na upande wetu tumpigie tujiridhishe kama hatopokea pia basi tutazika na tutaanza hilo la kumtafuta" akasema Baba mdogo, akatoa simu yake na kumpigia Ashura lakini simu haikupokelewa kama kawaida.
Hapo hata mimi hofu ikaanza kunivaa sasa, nikahisi labda mke wangu amekumbwa na tatizo.

Baba mdogo akapiga tena pia simu haikupokelewa, hata mara ya tatu mambo yakawa yaleyale.
Mara ya nne simu ikapokelewa, wote tukaa sawia kusikia nini kitaendelea kwani hapo simu iliwekwa 'Loud speaker'.
"Haloo" Sauti nzito ya kiume ndiyo iliyotupokea kwenye simu ya Mke wangu.
"Halooo, sijui ni nani mwenzangu" akauliza kwa wasiwasi Baba mdogo kwasababu aliyempigia si aliyopokea.
"Wewe ndiye uliyepiga simu unauliza maswali gani sasa" akasema jamaa huyo kwa ubabe, nikahisi labda ni kibaka alimpora mke wangu simu na labda kumuua au kumjeruhi. Tena pia nikawaza au labda mke wangu alipata ajali na watu wakaota simu yake. Nilikuwa njia panda kwa kweli.
"Mimi nilikuwa nampigia Ashura, mmiliki wa namba hii ya simu" akaeleza Baba mdogo.
"Wewe ni nani yake?" akauliza huyo jamaa tena ni kibabe kweli kweli.

"Kwa kweli sijui niseme ni ndugu yake ama rafiki yake kwasababu tulikutana kwa ajili ya mipango ya kibiashara na akasema nimletee mzigo na sasa ndio nimerudi tangu jana na nimelemletea mzigo" akasema Baba mdogo kwa uongo ambao pengine hakuna aliyeutegemea, uongo wa kiwango cha juu ambao ulikuwa na lengo la kumshawishi yuld jamaa aliyepokea simu atupe data kuhusu Ashura na kweli Baba mdogo alifanikiwa.
"Ngoja nimuite" akasema kumwambia Baba mdogo na hiyo tu ilitosha kuwa sababu ya sisi sote kuamini kwamba mwanaume yule alikuwa na mahusiano na Ashura; mke wangu.
"Baby kuna mtu anatak kuzungumza na wewe kwenye simu" tukamsikia akiita yule Mshenzi wa kiume, eti mwanamke niliyemuoa mie na kupewa kibali na Mungu yeye anamuita 'Baby'.
Iliniumiza sana kwani nilidhalilika ipasavyo, mbele ya ndugu zangu na wazazi wake. Yaani mwanamke niliyemuoa mwenyewe
tena kwa kutoa mahali anafanyia ushenzi wa sampuli ile, iliniuma.

"Nani" tukaisikia kwa mbali sauti yake na pengine wote ilituumiza kwa namna moja ama nyingine.
"Simfahamu lakini sio ndugu yako" akasema yule jamaa. Kauli yake hiyo ikanipa picha ya kufahamu kwamba kumbe alikuwa hapokei simu kwa makusudi ili tusimsumbue.
"Nakuja ngoja nimaliza kupaka hii dawa, maana dozi uliyonipa jana ** wote unawaka moto. Jamani wewe mwanaume kama una ** ya chuma" nikamsikia mke wangu akizungumza maneno makali yenye kuchoma namna hiyo. Maneno yaliyozidi kunidhalilisha kwa ndugu zangu. Ndio kudhalilisha kwani maneno yale yalikuwa yakimaanisha kwamba mimi si lolote si chochote kwenye sita kwa sita. Hilo halikuwa kweli hata kidogo, nilikuwa vizuri kitandani na nina uhakika anafahamu, lakini je unadhani ni nani atakayeamini baada ya kusikia maneno yale? Bila shaka hakuna labda tungelifanya mbele ya kadamnasi na watu wakaiona shughuli yangu.

"Fanya haraka basi laazizi itakatika hii simu" tukamsikia yule Njemba akisema na kusubiri kana kwamba ndio Ashura alikuwa anakuja kuifuata hiyo simu.
Lakini kabla hata hatujapata fursa ya kusikia sauti yake tulisikia kishindo cha mtu kuangua, sote tukaeleza macho yetu ilipotokea sauti na hatukuamini tulipomuona Mama Mkwe wangu yupo chini akigalagala kama mwenye kifafa huku povu likimtoka mdomoni.

***************************
UNAKOSAJE SEHEMU YA NNE....

UKIITAJI RIWAYA HII KWA HUPESI NA NYINGINE NYINGI USISITE KUMPIGIA NDUGU MTUNZI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
Mdgo mdgo sana aseeee
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA NNE (4)

ILIPOISHIA….

"Fanya haraka basi laazizi itakatika hii simu" tukamsikia yule Njemba akisema na kusubiri kana kwamba ndio Ashura alikuwa anakuja kuifuata hiyo simu.

Lakini kabla hata hatujapata fursa ya kusikia sauti yake tulisikia kishindo cha mtu kuangua, sote tukaeleza macho yetu ilipotokea sauti na hatukuamini tulipomuona Mama Mkwe wangu yupo chini akigalagala kama mwenye kifafa huku povu likimtoka mdomoni.

ENDELEA…..

Sote tukakimbilia pale kutoa msaada.
"Mtulizeni kwanza asije akaumia" akaagiza Baba Mdogo na kweli mimi pamoja na wale ndugu zangu wengine tukamtuliza ili asiendelee kujipiga sakafuni.

Naye akaanza kutulia, lakini utuliaji wake haukuwa wa heri. Alitulia mithili ya kuku anayemalizikia kukata roho baada ya kisu kikali kupita shingoni mwake, macho yakamtoka na kuvimba hadi kufikia ukubwa wa limao.
Hakika niliogopa hata kumtazama, muonekano wake ule ulinitisha haswa na nikatamani arejee katika hali yake ya kawaida haraka na mapema.

Hazikuisha dakika tatu akatulia kabisa, hofu ikaniingia na pengine na wenzangu pia. Ulimi ulimtoka nje tena ukiwa mrefu sio kawaida.
"Kalete shuka ndani" nikamsikia Baba mkubwa akimwambia binamu yangu hivyo. Tayari nilishang'amua kitu. Nilishafahamu huu ni msiba. Lazima Mama yake mke wangu atakuwa ameaga dunia.

Pengine labda ni kutokana na mshituko alioupata baada ya kupata habari zinazomuhusu mwanae tena zenye uthibitisho kamili namna ile.
Mume wake alionekana kupagawa zaidi ya watu wote pale ndani, alikaa na kusimama kana kambwa alipewa adhabu ya kufanya hivyo.
Hiyo ikawa ni mara yangu ya kwanza kumuona mtu mzima namna ile akilia, chozi lilimtoka mzee wa watu hadi nikamuonea huruma.
Baba mkubwa akamchukua na kumsogeza pembeni, wakaketi kwenye kochi huku akimpa maneno ya kubasara na kufariji.

Punde binamu alikuja na shuka alilotumwa kuleta. Tukamfunika ili tumbebe tumpeleke ndani kule ilipo miili mingine lakini kabla ya kufanya hivyo simu ya Baba mdogo yule aliyempigia Mke wangu ikaita.

Akaitoa kwenye mfuko wa suruali yake na kuitazama. "Ashura" akatueleza baada ya kugundua kuwa ni Mke wangu aliyekuwa anapiga.
"Nipe hiyo simu" nikamwambia naye akanipa bila kujali. Nikaitazama kwa makini lile jine 'ASHURA' kama jinsi alivyoli-save.
Nikapokea na kuweka sikioni.
"Haloo, nani mwenzangu?" nikaisikia sauti ya mke wangu ikiniuliza. Hapo nikapata picha ya kile kisura chake kisichopitwa na wakati. Kilichopambwa vyema kwa macho legevu, pua ndogondogo iliyochongoka, midomo ya kimo cha kati ilichoreka kwa mtindo wa kopa. Mrefu kidogo, mneme wastani na mwenye umbo la kibantu. Hakika ni mzuri kiasi kwamba nisingeona aibu kumtambulisha kwa mtu yeyote yule.

Fikra zikahama huko, zikarudi usiku wa jana na kunikumbusha maumivu niliyoyapa pindi wanangu walipokuwa wanaiaga dunia, mwanangu Ally alipigwa na radi na kuwa mweusi kama mkaa eti kisa alikuwa amekwenda kumtafuta mama yake ambaye hadi sasa alikuwa huko alipo akifanya ufuska. Tena ufuska wa kusifia utendaji kazi wa wanaume wengine na si mimi mumewe wa ndoa.
"Hapaaanaaa Ashura" nilipayuka kwa hasira, hasira zikazidi nikajikuta nimeirusha ukutani ile simu ya Baba mdogo. Ikaparaganyika na hakika isingepona hata angelikuja fundi kutoka China ili kuitengeneza.
Wote walishangaa kwa kitendo kile nilichokifanya lakini hakuna hata mmoja alijaribu kunilaumu kwani wote walifahamu hali niliyokuwa nayo.

**********************************
Majeneza matatu yalibebwa na watu na safari ya kuelekea makaburini ikaanza. Ndiyo hiyo siku niligundua kwamba naitwa Jamal, nina dhakari (Uume) lakini moyo wa kike. Kwa msiba ule nilishindwa hata kutembea mwenyewe bali kwa msaada. Watu walinipa msaada wa kutembea kwa kunishikiria mpaka makubirini.
Maziko yakachukua nafasi, tulianza na Mwanangu kipenzi Ally. Wakamtumbukiza kwenye mwanandani huku nikimtazama kwa majozi, sikuwahi kuiwaza siku kama hii maishani mwangu. Siku ya kuwazika wanangu badala ya wao kunizika mimi, ni maumivu hakika hasa ukizingatia wanangu ni watoto wadogo sana ambao hawakufika hata balehe.

Zamu ya Khadija wangu ikafika, naye wakamshusha taratibu kana kwamba walikuwa wakimweka pahala pendwa.
Walipomaliza walifukia michanga na haya ndiyo yakawa makaburi ya wanangu.
Lile la Ally, hili la Khadija, sikupenda iwe hivi lakini sikupewa uwezo wa kuzuia.
'Inalilah Wainalilah Rajuun' nikasema dua hiyo fupi kuwasindikiza wanangu.
Tukarudi kwa Mama mkwe ambaye pia alifariki kwa kutokana na ushenzi wa mwanaye, wakamtumbukiza kaburini na kufukia kama ilivyokuwa kwa wanangu na mazishi yakaishia hapo.

*******************************
Ndugu wa familia yangu na ya mke wangu tulijumuika pamoja ili kukubaliana kuivunja ndoa yetu ambayo tayari ilikwishaingia doa.
Hivi unadhani ningeweza kumsamehe Ashura?
Bila shaka hapana, amenifanya niishi kwa mtindo ambao sikuwahi kuuwaza. Amenipa maumivu makali zaidi ya kutokwa na roho, bila shaka hana msamaha kwangu.
Lengo kikao hiki tulichokaa ilikuwa ni mimi kuandika talaka yake na kumkabidhi Baba yake na tangu hapo ndoa ingekuwa imevunjwa.

Lakini ulizuka mgogoro mdogo katika kikao hicho, baadhi ya watu walipinga ile talaka yangu kuipeleka moja kwa moja kwa Walii (Baba wa mke wangu).
"Hakuna Sheria hiyo kokote katika Uislamu, ni lazima asubiriwe aliyeolewa apewe talaka yake halafu yeye ndiye aimpeleke kwa Baba yake" akasema mmoja wa ndugu wa Mke wangu aliyekuwa kwenye kikao hicho.
"Huo Uislamu wako unaousema umeupata wapi, Sheria ya dini imeruhusu hili tunalotaka kulifanya na ndiyo maana sisi tumepanga kulifanya" akadaki Baba Mkubwa kama kawaida yake.
Sasa mgogoro ukakua na kukua, kila mtu alihisi yeye ndiye yu sahihi zaidi ya mwingine kana kwamba walikuwa na dini tofauti.

Tukiwa bado katika vuta nikuvute ile na zogo la aina yake ghafla mlango wa sebuleni ulifunguliwa. Akaingia mtu ambaye alifanya sote tuache ili ligi yetu na kumtazama yeye.
Midomo wazi, macho yametumbuka kwa bumbuwazi kana kwamba tulikuwa tukimtazama binadamu mwenye miguu mitatu.
Binafsi, kadri nilivyokuwa namtazama ndivyo misuli ya mwilini ilivyozidi kunituna. Ni hasira juu yake ambazo zimesababishwa na yeye.
Ghafla akaanza kutokwa machozi akiwa amesimama pale, machozi ambayo binafsi niliyatafsiri kama machozi ya kinafiki na kizandiki.
Ni Mke wangu Ashura, ndiye aliyevamia kikao chetu na kuanza kuvujisha machozi ya kejeli.

"Ashura Mwanangu, kwanini umenidhalilisha namna hii?" Baba yake akamuuliza kwa simanzi. "Kwanini umetenda kama Ibilisi, Allah atakupokea vipi pindi na wewe wakati wako utakapofika?
Sitaki kuamini kama mbali na kukujaza hofu ya Mungu kwa kukulea katika misingi ya dini lakini umefanya uchafu mzito namna hii.

Tazama, leo hii Mimi na Mama yako tunaonekana si kitu katika malezi kana kwamba ni sisi ambao tulikupa kozi ya kutothamini ndoa yako kiasi hiki.
Kwanini umetudhalilisha" akasema Baba Mkwe kwa masikitiko hadi nikamuonea huruma. Akatoa kitambaa chake na kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka wakati akizungumza na bintiiye.
Basi hapo hapo nikaona ndugu wawili wa Mke wakanyanyuka na kuaga kana kwamba wamesusa. Huo ukawa kama ni mwanzo, wote waliosalia wakasimama na kumuacha Baba Mkwe tu kwa upande wa Mke wangu.

"Tazama ndugu wanaondoka, si kwamba hawanipendi bali hawapendi kudhalilika. Familia ya Mumeo itadhalau ukoo wetu wote kwa ushenzi wako mtu mmoja, hatuna kwa kuweka sura zetu kwa jinsi ulivyotenda.
Hata mimi nakuchukia na bila shaka hata Marehemu Mama yako na wanao wote hawakupendi huko walipo na watakulaani milele" akasema maneno mazito namna hiyo ambayo ilikuwa ni kiashirio kwamba kile kilichofanywa na mwanae hakikuwa sawia.

"Baba" tukamsikia akiita Ashura na hapo akili yangu ilikuwa ikitaraji kusikia neno samahani kutoka kwake.
Lakini haikuwa hivyo.
"Wanangu wamefariki?" akauliza kwa sauti iliyoambata na kilio cha kwikwi lakini kabla hata hajajibiwa aliangua kilio kamili.
Nilimtaza hata nikamuonea huruma huku akili yangu ikikosa jibu la swali hili.
'Kumbe alikuwa akiwapenda wanae?"
Nilikosa jibu kwasababu kilio alichotoa sasa hakikuwa cha kinafki kama kile cha mwanzo, kiliashiria kwamba alikuwa akiumizwa na taarifa ile lakini je kama ni kweli alikuwa akiwapenda angethubutu kuwaacha nyumbani na yeye kwenda kufanya ufuska kusipojulikana?.

************************

Wakati namtazama kumbukumbu zangu zikarudi nyuma. Miaka zaidi ya 12 iliyopita. Nikakumbuka ile siku ya kwanza nilipopata bahati ya kumuona binti huyo mrembo.
Ilikuwa ni kwenye kituo cha mabasi cha Mwenge. Nakumbuka nilikuwa natoka Tegeta, nyumbani kwa Baba Mkubwa.
Kituoni nilikuta kundi kubwa la abiria wakisubiri usafiri na wengi walikuwa abiria wa Gongo la mboto na Mbagala.
Nikajiunga nao na kusubiri usafiri wa Gongo la mboto ambapo
ningepanda gari na kuteremka Ukonga.

Pembeni ya pale niliposimama alikuwapo msichana ambaye kwa kumtazama tu niligundua ni mjamzito. Alikuwa akizungumza na mtu kupitia simu lakini punde tu baada ya kumaliza kuzungumza na mtu huyo hali yake ikabadilika. Nikamuoa akikunja sura kana kwamba alikuwa akiugulia maumivu makali, hali hiyo ilizidi na hatimaye akaketi chini huku akijinyongolota.

**********************************

KWA LEO ILA CHA KUFANYA USIKOSE MUENDELEZO WA RIWAYA HII

TUKUTANE TENA KESHO PANAPO MAJARIWA,

UKIITAJI RIWAYA HII KWA HALAKA UNAWEZA KUMTAFUTA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA TANO (5)

ILIPOISHIA……..

Nikajiunga nao na kusubiri usafiri wa Gongo la mboto ambapo ningepanda gari na kuteremka Ukonga.
Pembeni ya pale niliposimama alikuwapo msichana ambaye kwa kumtazama tu niligundua ni mjamzito. Alikuwa akizungumza na mtu kupitia simu lakini punde tu baada ya kumaliza kuzungumza na mtu huyo hali yake ikabadilika. Nikamuoa akikunja sura kana kwamba alikuwa akiugulia maumivu makali, hali hiyo ilizidi na hatimaye akaketi chini huku akijinyongolota.

ENDELEA……

"Dad....." nikataka kumuongelesha lakini kabla hata sijafanya hivyo gari ya Gongo la Mboto iliwasili kituoni na punde abiria wakajazana mlangoni na kuanza kugombea kuingia. Wengine walipitia dirishani nikiwemo mimi ambaye niliacha kutoa msaada kwa yule mwanamke mjazito kwani nilisimama muda mrefu kituoni.
Nilipata siti ndani ya gari, nikawa nimeketi kwa dirishani huku nikimtazama yule mjamzito akiendelea kuteseka mwenyewe bila hata msaada kutoka kwa mtu yeyote mbali na kwamba kituo kilikua na abiria zaidi ya 100.

Kabla gari halijaondoka alikuja binti mmoja mrembo aliyevalia gauni refu la kijani sambamba na ushungi kichwani, akasogea karibu na dada yule mjamzito na kuanza kumuongelesha. Ingawa sikusikia mazungumzo yao lakini nilipata kugundua kuwa dada yule alikuwa akitaka kufahamu tatizo la mwanamke mwenzake.
Baada ya sekunde chache za mazungumzo yao msichana yule akamuacha mwenzie na kuja kugombania gari.
"Na yeye amemuacha pia" nikajiuliza kimoyomoyo bila kupata jibu liliosahihi.

Binti yule aligombani gari tena kwa nguvu kwelikweli, hakujali unadhifu aliokuwa nao cha muhimu kwake ilikuwa ni kuingia ndani ya gari hiyo. Aliwazidi nguvu watu wengine na kupita mpaka ndani, akapata nafasi ya kukaa kiti cha pili kutoka mlangoni.
Baada ya dakika kama tano hivi ule mshikemshike wa kugombea gari uliisha, na hapo ndipo nilipomsikia yule msichana akimwambia konda kuwa 'asiondoe gari kuna mgonjwa anakuja kupanda'. Kisha akamuuita yule dada mjamzito kupitia dirishani.
Taratibu yule dada akanyanyuka na kujivuta hadi garini, akapanda na watu wakajaribu kumpa njia na alipoifikia siti aliyowekewa na kuketi.

"Asante dada yangu umenisaidia kweli, hivi unadhani ningeweza kugombania mie. Ningelala hapa Mwenge leo" akasema mjamzito huyo akimshukuru yule dada aliyemsaidia.
"Usijali kawaida tu" naye akamjibu.
"Si kawaida Dada, hapa kituoni kuna watu zaidi ya 50 lakini ni wewe tu ndiye uliyenionea huruma" akamwambia.
Kweli hata Mimi nafsi ilinisuta, nikajiona niso-utu kwa kukosa kumsaidia dada yule. Lakini mawazo yangu hayakuishia hapo tu, bali yalienda mbali zaidi yakimsifu yule Mwanamke mwenye huruma na moyo wa kutoa msaada kwani alituzidi watu wote tuliokuwa ndani ya gari na biola shaka Mungu alimuandikia swawabu.

*********************************

Moja kati ya masuala yaliyowahi kuwa magumu katika maisha yangu ni kuoa, na ugumu ulikuja pale nilipofikiria ni jinsi gani nitampata mwanamke wa kuwa Mama wa familia yangu.
Mwanamke atakayenijali Mimi na mali zangu, watoto wangu nitakaozaa nae bila kusahau ndugu zangu. Mwanamke mwenye chachu na hamasa ya kuunda familia yenye maendeleo, mwenye kujifunza, anayeambilika na sifa nyingine kedekede ambazo kama nitaanza kuzitaja zote basi hatutofikia lengo la mimi kukutana na ninyi, yaani tutamaliza hata siku nzima ya leo tukiziongelea.

Hakika sifa zote hizo sikuwahi kukutana nazo kwa wanawake kadhaa nilowahi kuwa na mahusiaono nao.
Nilipoona jukumu ni zito sana kwa upande wangu niliomba msaada kwa Baba yangu.
"Unataka kumuoa nani?" hilo ndilo likuwa swali la kwanza kuniuliza mara baada ya kumueleza kuwa nataka kuoa.
"Sijapata wa kumuoa bado na nataka unisaidie hilo pia"
"Yaani unataka kuoa na hata hujajua unamuoa nani? Mbona kituko. Lakini usijali nitamshirikisha na Baba yako mkubwa katika hiki" akanambia.

Haikupita hata wiki nilipokea simu toka kwa Baba Mkubwa.
"Nimepewa habari wataka kuoa?" akaniuliza.
"Ndiyo Baba" nikamjibu.
"Sasa ondoa shaka kijana wangu na wala usihadaike na kwenda kuoa hao wanaowaka huko manjiani, mimi nitakutafutia Mwanamke mzuri sana" akanambia.
Sikuwa na hofu juu yake kwani hata wanawe aliwatafuta wanawake wa kuoa na ni wanawake wazuri ambao hadi leo bado wako nao.

Nakwambia upele ulipata mkunaji, Baba Mkubwa alilivalia njuga suala la mimi kuoa kana kwamba lilikuwa likimpa faida ya moja kwa moja. (malipo). Haziku siku tatu tangu niongee naye akanipigia simu.
"Kazi yako imeshakamilika, nimezungumza na Baba yako na kama utaweza mje kesho kutwa tufanye mazungumzo ya ana kwa ana" akanieleza kupitia simu.
Kweli ikawa hivyo, mimi na Baba tukaongozana hadi tegeta nyumbani kwa Baba Mkubwa.
"Ni binti wa rafiki yangu kipenzi, amesoma hadi kidato cha nne hayo maelimu yenu ya vyuo mimi hata siyafahamu lakini amefika hadi huko.

Pia amesoma Madrasa na ni mwanamke anayeifahamu dini vilivyo na mwenye hofu ya Mungu ndiyo maana nikakuchagulia huyo, lakini kubwa na muhimu zaidi ni kwamba binti huyo bado ni bikra kabisa" akatueleza Baba Mkubwa akinadi sifa za huyo Mke wangu mtarajiwa.
Basi hatukuwa na cha kuchelewesha, mambo yalifanywa haraka haraka na mara baada ya barua kupelekwa ilipangwa siku ya mimi kutembelea kwa wakwe zangu watarajiwa.
Kweli nilikwenda nikiwa Mimi, Baba, Baba Mkubwa pamoja na mtoto Mkubwa wa Baba Mkubwa. Siku hiyo pia ilikuwa mahususi kwa mimi kuonana na Mwanamke ambeye ndiye angekuwa mke wangu.

Tulipokelewa kwa bashasha na wakwe ikiwa ni pamoja na kuandaliwa chakula.
Basi mabinti wa Mkwe wangu wakafanya kazi hiyo, niliwaona mabinti wawili ambao hakika walikuwa ni wazuri haswa lakini sikuwa nikifahamu ni yupi kati yao ndiye atakayekuwa Mke wangu.
Walipofuata chakula jikoni nilimuuliza Baba Mkubwa ambaye yeye ndiye alikuwa akimfahamu.
"Hapo hayupo, ni mzigo wa maana hao unaowaona cha mtoto" akanambia.
Punde nikamuona binti akija hapa sebuleni huku amebeba 'hot pot' kubwa mikononi. Huyu si kati ya wale waliokuwa wakitenga mwanzoni, huyu ni mwingine kabisa na kwa kweli alikuwa ni mrembo zaidi ya wale wengine kiasi cha kwamba niltamani ndiye awe mke wangu.

Akaweka 'hot pot' na kutukaribisha chakula kisha akaondoka.
"Baba, huyu je?" nikamuuliza huku nikiombea aseme ndiye huyu unayetaraji kumuoa.
"Haswaaa, ndiye yeye" akanambia.
Huwezi amini nilijikuta natabasamu kana kwamba niliambiwa 'sasa hii Tanzania yote ni mali yako'.
Nilipagawa kwa kweli, msichana mzuri namna ile halafu tena ni bikra hakika ningefaidi mie.
Nikaanza kuombea Mungu ndoa ifungwe hata muda huo kwa mshawasha niliokuwa nao ambao pengine ulichochewa na matamanio ya kingono tu.

Hata tulipomaliza kula ni yeye ndiye aliyekuja kuondoa vyombo. Hapo nikapata nafasi ya kumuona vyema sana mwanamke huyu na kuzidi kumtamani tena na tena.
Lakini kitu kimoja niligundua kwa Mwanamke huyo ni kwamba niliwahi kumuona sehemu lakini sikumbuki ni wapi.
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu zangu lakini hatimaye jibu lilikuja kwamba binti huyu ndiye yule niliyewahi kumuona Mwenge akitoa msaada kwa yule dada mjamzito aliyezidiwa.
Kwa sababu hiyo nikazidi kumpenda mwanamke huyo nikiamini ni mwanamke anayefaa kuwa Mke.

Ndoa ilifinyika siku tatu baada ya kulipa mahali. Hatukufanya sherehe za kufuru kwani hata misingi ya dini yetu haikuwa ikituruhusu kufanya hivyo. Ilifanyika hafla ndogo tu, watu wakala, wakanywa na mimi nikapewa Mke.

********************************
Sasa Nuru ikaingia ndani ya Nyumba yangu, Mke wangu--Ashura; alikuwa ni Mwanamke ambaye nilikuwa nikimtafuta muda wote. Mwanamke anipendaye na kujua nini maana ya Mume, sikuwahi kujuta hata kidogo kwa kile kipindi cha miaka kadhaa ya ndoa yetu na nilitumaini ingekuwa hivyo hadi kiama.

MIMBA YA KWANZA.
Furaha kamili ndani ya nyumba yetu ilitimia hapa, Mwanaume nilianza kujiandaa kufukia kwa jina langu Jamal na kuitwa Baba fulani.
Hakika mfumo wa maisha yangu ulianza kubadilika hapo kwani nilijitahidi kuwa Baba bora kadri ya uwezo wangu.
Kliniki tulienda wote kama wataalamu wa afya wanavyoshauri. Sikuthubutu kumuacha hata siku moja mpaka ilipotimia miezi 8 ya ujauzito.

Muda wa kujifungua ulipokaribia aliniomba aende akajifungulie kwao. Sikutaka lakini alinieleza kwamba ni vyema kwa mimba ya kwanza akawa karibu na watu wazima ambao watampa muongozo katika kila kitu kuhusu ujauzito.

Nilimtaka asiende kwao na kama ilikuwa ni mtu mzima tu basi nitamuomba Mama yangu aje kukaa hapa nyumbani mpaka atakapojifungua lakini hakutaka kukubaliana na hilo.
Aliniomba na kunisihi akajifungulie kwa Mama yake na hapo nikashindwa kabisa kupinga. Nikampa uhuru wa kufanya kile alichoona ni bora kwake na kwa mwanetu.
Aliondoka na kuelekea kwao na kuniacha mpweke nyumbani. Sikuwa na wakupiga nae stori tena kama ilivyokuwa mwanzo.
Nilikuwa nikimpigia simu mara kadhaa kufahamu anaendeaje yeye pamoja na mtoto aliye tumboni na alinijibu kwamba wanaendelea vyema.

Tarehe 23 ya mwezi wa tano ndiyo siku ambayo Mke wangu alijifungua.
Nakumbuka nilipigiwa simu nikiwa kazini na kupewa taarifa kwamba mke wangu amejifungua mtoto wa kike. Niliwehuka na kuwa mwendawazimu ghafla, muda huo huo nikataka kuacha kazi na kuelekea hospitali.
"Hospitali gani amejifungulia" niliuliza haraka haraka kwani hakunipa taarifa tangu mwanzo walipokuwa wanakwenda hospitali.
"Ni hospitali ya binafsi ya huku huku Tegeta" akanambia Mama Mkwe ambaye ndiye aliyenipigia muda huo.
"Sawa Mama mimi nakuja sasa hivi" nikamwambia huku jasho la furaha likinimwagika.
"Hapana, usisumbuke kuja hospitali, wewe njoo nyumbani tu" akanambia Mama Mkwe.
Hapo kidogo akaniacha njia panda, yaani kwenda hospitali kuiona damu yangu aniambie nisisumbuke, hakika sikumuelewa.
"Hapana Mama, acha nije tu nina hamu sana ya kumuona binti yangu" nikamwambia.
"Tunaruhusiwa muda si mrefu, kwahiyo hakuna haja ya wewe kuja huku" akakazia tena na tena.
Sikuona haja ya kuendea kubishana pale, nilichofanya ni kumalizia kazi kidogo na kutimuka nikiwa na rafiki yangu Maige.

*******************************************
USIKOSE SEHEMU YA SITA KWANI BADO UNA MENGI YA KUYAFAHAMU

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI USIACHE KUMTAFUTA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA KAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

FACEBOOK: KEV CLEVER KAGAMBO

SEHEMU YA SITA (6)

ILIPOISHIA…

Hapo kidogo akaniacha njia panda, yaani kwenda hospitali kuiona damu yangu aniambie nisisumbuke, hakika sikumuelewa.
"Hapana Mama, acha nije tu nina hamu sana ya kumuona binti yangu" nikamwambia.

"Tunaruhusiwa muda si mrefu, kwahiyo hakuna haja ya wewe kuja huku" akakazia tena na tena.
Sikuona haja ya kuendea kubishana pale, nilichofanya ni kumalizia kazi kidogo na kutimuka nikiwa na rafiki yangu Maige.

ENDELEA NAYO…

Tulifika tegeta mpaka nyumbani kwa kina mke wangu lakini hatumka mke wangu wala mwanangu na tulipouliza tuliambiwa kwamba bado hawajarejea hospitali.
Papo hapo nikachukua simu na kumpigia Mama wa Mke wangu ili kufahamu kinachoendelea.

"Tumefika muda mrefu hapa na wanasema bado mko hospitali, kuna tatizo gani?"
"Heee, umefika mara hii!? Bado hatujaruhusiwa" akasema
"Bado!? Basi nielekeze ni hospitali gani nije"
"Hapana usije ndio hapa nipo na daktari anatuandikia karatasi ya kuturuhusu" akanambia.

Hapo sasa nikaanza kuingiwa na wasiwasi, inakuwaje nawekewa kizuizi kumuona mtoto wangu mwenyewe? Au kuna kitu wanajaribu kunificha hawa.
Nikamshirikisha rafiki yangu Maige katika hilo lakini alitumia busara kwa kunitaka nitulie kusubiri na kuona kitakachoendelea.
Nikafanya hivyo, tulikaa pale na mashemeji zangu kwa zaidi ya masaa mawili lakini hawakurudi na kila nilipojaribu kuwauliza Ma-shemeji walinambia kuwa hata wao hawakuwa wakiifahamu hiyo hospitali.

Baadae Baba Mkwe alirejea toka kwenye mihangaiko na kunikuta pale lakini kubwa ambalo lilizidi kunitia wasiwasi ni kwamba hata Baba Mkwe hakuwa na taarifa kwamba mke wangu amejifungua.
"Amejifungua!" alishangaa alipoipata habari hiyo kwa mara ya kwanza toka kwangu "Mbona mimi hawakunambia?" akaongeza na papo hapo akachukua simu na kuwapigia.
"Haloo, upo wapi?" akauliza mara baada ya Mama Mkwe kupokea simu.
"Tupo huku hospitali, Ashura amejifungua" akajibu Mama mkwe kupitia simu.
"Ndiyo unanieleza, Je, nisingekupigia ungenieleza saa ngapi" akaongea kwa ukali Baba Mkwe.
"Hapana Mume wangu ndiyo nilikuwa najianda kukupigi,...." akataka kujitetea.
"Wacha ujinga wewe, rejea nyumbani haraka na kama hamjaruhusiwa useme tufike hapo muda sasa hivi" akang’aka Baba Mkwe, nikajisiki vibaya sana, kusikia mama mkwe akigombezwa namna ile kana kwamba alikuwa ni mtoto mdogo. Niliona chanzo ni mimi ingawa haikuwa hivyo kweli kwani laiti Mke wangu na Mama yake wangetoa taarifa mapema yote yale yasingejiri.
"Sawa nakuja" akajibu kwa unyonge Mama mkwe.
Maongezi mengine yakavamia sebule na yalitafuna takribani dakika 60 hadi Mke wangu na Mama yake waliporejea nyumbani wakiwa na mtoto wangu wa kwanza.

Nilifarijika sana siku hiyo na hata kusahau ile kero niliyoipata kutokana na uzembe uliofanywa na Mke wangu na Mama yake. Hakika nilipata kitoto kizuri hasa na chenye afya njema. Nilijisikia raha nilipokiweka mikononi kwa mara ya kwanza huku nikatamani niendelee kuwa naye muda wote bila kumkabidhi mtu mwingine.
Kwa upande wa Baba Mkwe bado alikuwa na kusisitiza kuhusu ile tabia iliyofanywa na Mke wangu.

"Mimi sijapenda kabisa Mama Ashura, hivi unadhani wazazi wenzetu watatuelewa vipi kwa kitendo cha kutowaeleza kuwa wamepata mjukuu" akasema.
"Nisamehe Mume wangu mimi nitabeba jukumu la kuwapa taarifa kwa namna yoyote ile ili wasielewe kilichotokea" akaeleza Mama mkwe. "Na wewe unisamehe pia Mwanangu" akanambia na mimi.
"Usijali Mama, halikuwa tatizo sana" nikamjibu huku nikijichekesha.
Mishale ya saa ilipogota saa zita za usiku ukawa muda mahususi kwa mimi na Maige kuondoka ingawa bado nilikuwa na hamu ya kuwa karibu na kichanga changu chenye masaa kadhaa duniani. Yaani nilitamani hata kulala palepale.

Tuliaga tayari kwa kuondoka lakini niliahidi kurudi kesho asubuhi kwa ajili ya kujua hali ya mtoto, mke wangu na pia kupanga mipango ya ni lini Mke wangu atarejea nyumbani.
Baba Mkwe alitusindikiza hadi ambapo nilipaki gari langu.
"Mwanangu usifikirie vibaya sana ni mambo ya wanawake tu yale, utusamehe" akanisisitiza Baba Mkwe.
Hapo Mimi na Maige tukaingia garini na safari ya kurudi nyumbani ilianza.
"Sasa hapa nimekamilika kuitwa Mwanaume" nikamwambia Maige tukiwa njiani.
"Hasa" akaniunga
"Yaani unajua nilikuwa nakuonea wivu sana nilipokuwa nakuja nyumbani kwako halafu naona watoto pale"
"Ndio hivyo, katika maisha kuna hatua nyingi sana ila hiyo uliyofikia ni hatua moja wapo tena kubwa kweli kweli.
Ila sasa inakubidi macho yote mawili uyageuzie kwenye familia.

Uweke akiba ya kutosha kumlea binti yako" akanambia maneno yenye hekima sana na hiyo ilikuwa ni kawaida yake. Maige alikuwa ni rafiki yangu ambaye namshirikisha kwenye masuala ya msingi kama haya kwasababu alikuwa ni mtu mwenye kunipa ushauri chanya mara zote.
Baada ya maongezi hayo ukimya ukatekanyara gari lakini Maige akaamua kuutawanisha kwa sentensi moja tu ambayo pia ilinifunua kimawazo kuhusu vitu fulani.
"Hivi unafahamu kama kuna siri fulani Mke wako anaificha. Na anafanya hivyo akishirikiana na mama yake tu, yaani hata Baba Mkwe wako haifahamu" akanambia hivyo.
"Siri!? Siri gani na kwanini unasema hivyo" akanambia kwani nilikuwa sijampata vyema.
"Sifahamu na ndiyo maana imekuwa siri lakini nasema hivyo kutokana na ile picha niliyoiona pale.

Hivi ina maana wewe huhisi chochote? Kwanini Mama Mkwe wako hakutaka kumueleza mtu yeyote kama Mkeo amejifungua?" Maswali mfululizo toka kwa Maige yalianza kuupanua ubongo wangu ambao mwanzo haukuwa ukiwaza ubaya wowote. Nilianza kupata hisia mbaya huku nikijaribu kutuliza akili na kufikiri kinagaubaga ni kipi ambacho sote tulikuwa tunafichwa.
"Au wamehisi kama familia yetu ni wachawi?" nikamuuliza Maige nikitaka ajibu ili nipate mawazo yake.
"Yawezekana, ila sidhani"
"Kumbe unadhani nini?"
"Jamal hebu kuwa na mawazo ya haraka ndugu yangu, unakuwa kama hujapita darasani.

Kama ingelikuwa hiyo ndiyo sababu ina maana Baba Mkwe wako angekuwa na taarifa. Lakini shangaa kwamba hajapewa taarifa na si yeye tu hata wale wasichana mashemeji zako tuliowakuta pale hawakuwa wakielewa ni hospitali gani Mke wako amepelekwa" akanieleza Maige.
Hakika nilifunguka sasa. Nikahisi kuna siri kubwa sana nafichwa, tena si mimi tu bali na watu wote wanaotuzunguka.
Kwanini Baba mwenye mtoto nifichwe kuhusu mtoto wangu. Hakika yahitajika nguvu ya ziada kupata jibu la swali hilo.
"Lazima nimuulize na lazima anipe jibu"
"Umuulize? Sidhani kama atakupa jibu"
"Sasa kumbe nifanyaje?"
"Jamal wewe ni mtu mzima bwana sio kila kitu ufundishwe. Hebu jifunge kutumia ubongo wako" akanambia Maige akimaanisha kwamba nilikuwa na maswali ambayo hayakuwa ya msingi.
Nilinyamaza, nikaendesga gari huku tayari kichwa nikiwa na mawazo juu ya yale niliyokumbana nayo.
"Huna haja ya kujipa mawazo namna hiyo, hili ni suala dogo sana na litakuwa dogo zaidi kama utalifanya taratibu taratibu na kwa udadisi zaidi" akanambia Maige baada ya kunitazama na kugundua ni mwenye mawazo kweli kweli.
Nilimfikisha nyumbani kwake, akaremka na kunipa ruhusa ya kuendelea na safari ya nyumbani kwangu. Niliendesha kwa fujo na hasira na muda mfupi tu nikawasili nyumbani. Nikaingia ndani na kuoga. Kisha nikampigia simu Baba na kumpa taarifa kwamba kajifungua.
"Kajifungua! Lini" akauliza swali ambao nililitarijia toka kwake.
"Ja...ja...jana" nikajibu kwa kujiumauma kwani nilielewa nini kingefuatia baada ya jibu langu.
"Jana? Mbona sisi hatuna habari?"
"Hamna habari? Nilijua mmeambiwa"
"Tumeambiwa na nani?" akaniuliza
"Nilijua mmeambiwa na Ashura au hata Mama yake" nikajitetea.
"Hivi Jamal una akili wewe?" akaniuliza na kuendelea. "Hivi kati yako na Mke wako ni nani mwenye wajibu wa kutupa taarifa kwamba Keo kajifungua?" akaniuliza.
Kweli nikaona waziwazi kuwa nimebugi kuongea vile.
"Samahani Baba" nikajinyong'onyesha.
"Sitaki samahani zisizo na msingi nijibu maswali yangu" akawaka hivyo.
"Ni Mimi ndiye mwenye jukumu hilo"
"Sasa kwanini hukutueleza?" akaniuliza na hakika sikuwa na cha kumjibu. Nikakaa kimya.
"Sasa sikia Jamal, hutaona mtu yeyote kutoka huku anakuja kumuangalia huyo mwanao labda uje na sababu ya msingi ya kwanini hukutupa taarifa mapema" akasema Baba akakata simu.
Namfahamu Baba yangu. Mzee Shomari ni mtu ambaye mara zote maneno yake huwa vitendo. Yaani kama alisema hatokuja basi nisitegemee kumuona hata mara moja.
Niliishiwa nguvu, nikaketi kwenye kochi nikihisi maluweluwe kichwani. Sikujua nifanye nini ili kujinasua kwenye mtihani huu unaoniandama.

Kumueleza Baba hali halisi kwamba hata Mimi sikujulishwa mapema ingekuwa ni tatizo zaidi kwani angehoji ni kwanini iwe hivyo.
Na niseme nisimueleze ukweli basi nisitegemee kumuona yeye wala Mama yangu jambo ambalo sikutaka kuona likitokea.

*************************************************
JAMAL YUPO NJIA PANDA HAFAHAMU AMUELEZE BABA YAKE UKWELI AU LAA?

SEHEMU YA SABA ITAKUPA JIBU KAMILI, USIKOSE

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI WAWEZA MTAFUTA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA SABA (7)

ILIPOISHIA…

Namfahamu Baba yangu. Mzee Shomari ni mtu ambaye mara zote maneno yake huwa vitendo. Yaani kama alisema hatokuja basi nisitegemee kumuona hata mara moja.

Niliishiwa nguvu, nikaketi kwenye kochi nikihisi maluweluwe kichwani. Sikujua nifanye nini ili kujinasua kwenye mtihani huu unaoniandama.
Kumueleza Baba hali halisi kwamba hata Mimi sikujulishwa mapema ingekuwa ni tatizo zaidi kwani angehoji ni kwanini iwe hivyo.
Na niseme nisimueleze ukweli basi nisitegemee kumuona yeye wala Mama yangu jambo ambalo sikutaka kuona likitokea.

SHUKA NAYO…

Nikajaribu kutuliza kichwa na kupembua, nikapata wazo. Niliona ni vyema tu nimueleze ukweli Baba kwani hiyo ingenisaidia hata Mimi kupata kufahamu ni kwanini Mke wangu na Mama yake walificha kuhusu kujifungua kwake.
Nilifahamu ni lazima Baba angezungumza kiutuuzima na wazee wezie na kupatiwa jibu ambalo mimi ingekuwa ngumu kidogo kupewa.

Nikampigia simu.

"Umepata sababu ya msingi?" akaniuliza mara tu baada ya kupokea simu.
"Baba unajua hili jambo ni zito na hatuwezi kulizungumza kupitia simu. Ingependeza kama tungekutana ana kwa ana" nikamwambia
"Uje nyumbani, nipo muda wote" akanambia.
"Sawa nitakuja kesho mapema" nikamwambia kabla sijakata simu na kilichofuata ni kuoga na kupanda kitandani kuutafuta usingizi.

Niliamka asubuhi ma mapema, nikajiandaa tayari kuelekea nyumbani kwa Wazazi kabla ya kwenda Tegeta nyumbani kwa Wakwe zangu. Nilifika nyumbani na nilikaa na Wazazi na nikawaelezea kila kitu kama kilivyotokea.

"Sasa kwanini wanafanya hivyo? Au wanahisi huyo mtoto hatuhusu?" akasema Mama yangu.
"Tusipoteze muda, tufanye twende huko na watueleze kilichofanya wasitoe taarifa vinginevyo mahusiano yetu na wao yataharibika" akasema Baba.
"Hapana Baba sidhani kama hiyo itakuwa ni vyema sana" nikawaambia kwani sikupenda migogoro ijitokeze baina ya familia hizi mbili.
"Ila walichofanya wao ndio chema?" akahoji Mama.
"Mama, si kizuri hata kidogo lakini isifikie hatua ya kuharibu mahusiano. Mtatuweka njia panda sisi watoto na hata huyo mjukuu aliyezaliwa" nikawaambia. Unajua sikupenda hata kidogo kuona mahusiano yetu yanavunjika.
"Mama Jamal hebu jiandae twende" Akaagiza Baba na hapo Mama akaenda kujiandaa na muda kidogo alitoka na safari ya kuelekea Tegeta ikaanza.

Njia nzima mada ilikuwa ni kwanini familia ya mke wangu haikuweka wazi kuhusu hali ya Ashura. Kila mtu alichangia kulingana na mtazamo wake lakini mwisho wa yote ni kwamba jibu la uhakika walikuwa nao wahusika.
Niliendesha gari kwa kasi kidogo na masaa kadhaa tuliwasili Tegeta.

Walitupokea lakini bila shaka walikuwa na hofu juu ya kile walichokifanya. Tulimuona mtoto na hapo Baba nikapewa jukumu la kumpa jina.
"Khadija" nikampa jina la Mama yangu na naamini Mama alifararijika sana.
Lakini kufarijika huko hakukufuta lile suala tulilokuwa nalo, lile la kufahamu ni kwanini Ashura na Mama yake walituficha kuhusu kijifungua kwa Mke wangu.
Kikawekwa kikao kwa ajili ya kupashana kilichopo nyuma ya pazia.
".....Kwahiyo sisi tunataka kufahamu sababu iliyopelekea tusipewe taarifa ya kuja kwa mjukuu wetu" akasema Baba na hiyo ndiyo ilikuwa hoja yake baada ya maelezo kadhaa ya utangulizi.
"Mimi naomba msinielewe vibaya wala kunifikiria tofauti, kilichonifanya nishindwe kuwapa ni kuchanganyikiwa. Unajua Ashura amesumbua sana wakati wa kujifungua na pengine hata angepoteza Maisha" akasema.
"Mbona sioni kama hiyo ni sababu ya msingi kwani nilitegemea sehemu kama hizo ndiyo utukumbuke ili tutoe msaada" akahoji Baba.
"Basi Mimi naomba msamaha wenu wazazi wenzangu"
"Tumekuelewa lakini nashauri tujifunze kuishi vizuri na wengine jamani." akasisitiza Baba na hapo wakafikia tamati.
Mipango mingine ikachukua nafasi ikiwemo ile ya kuhusu Mke wangu kurejea nyumbani pindi mtoto atakapofikisha wiki mbili. Hiyo ilikuwa na maana ya kwamba nitakuwa mwenyewe nyumbani hadi kuisha kwa wiki mbili ndipo mke wanu atajumuika nyumbani na kwa pamoja tutaendelea kumlea mtoto wetu.

*****************************

Hata kama wazazi wangu walikubali kumuelewa Mama Mkwe haikuwa hivyo na kwangu pia. Mimi wala sikuridhishwa na lile jibu na nikahisi kuna kila sababu ya kudadisi zaidi na zaidi ili kupata jibu la kweli na uhakika.

Nilimjulisha na Maige kuhusu kila kitu huku nikitaka anipe ushauri wa mbinu nitumie ili niweze kung'amua ukweli.
"Kama kajitetea hivyo si vibaya ila wewe tafuta uthibitisho. Nenda kwenye ile hospitali aliyojifungulia Mke wako ukafanye udadisi kama ni kweli alikutana ma changamoto kiasi cha kuchanganyikiwa hivyo" akanishauri Maige.
"Lakini Mimi hata hiyo hospitali yenyewe siifahamu ndugu yangu"
"Jamal wewe ni mtu mzima sio kila kitu utafuniwe bwana. Tumia bongo yako" akanambia Maige.
Basi sikuwa na budi kufanya hivyo, ilikuwa ni lazima nitafiti mwenyewe ingawa niliamini zoezi hilio lingetafuna muda mrefu kwelikweli.

********************

Baada ya wiki mbili Mke wangu alirejea nyumbani na tukaanza maisha ya familia yetu tukiwa na mwanetu.
Hakika Khadija alikamilisha furaha ndani ya nyumba yetu. Ni mtoto ambaye alibahatika kupendwa kweli kweli na wazazi wake na bila shaka ni kwasababu alikuwa ni mtoto wa pekee wa kwanza.
Tulimpenda na kumjali na hiyo ilikuwa ni dalili njema ya wawili sisi kuwa na familia yenye amani.

Kubwa ambalo sitaacha kujisifu ni jinsi nilivyokuwa nikiishi na Mke wangu. Yaani nilikuwa nikimsaidia kazi za nyumbani bila matatizo yoyote. Naweza sema hata ungepima ni yupi alikuwa kinara wa kumuhudumia mtoto kati yangu na Ashura basi dhahiri ningeibuka mshindi.
Sikuona ubaya katika hilo, wala sidhani kama kuna ubaya wa aina yoyote kumsaidia mke wako majukumu ya namna hiyo.
Pia furaha iliyojengeka ndani ya familia ilininyima nguvu ya kuanza kufuatilia kwanini Mke wangu hakunijulisha wakati anajifungua. Nilichukulia kawaida tu ikiwa halikuwa na madhara makubwa kiasi labda cha kumjeruhi mtu na vinginevyo.

MIEZI SITA

Hapa ndipo ndoa ilipokuwa ndoano.
Nilianza kushuhudia vituko vidogo vidogo toka kwa mke wangu.
Sekeseke la kwanza kukumbana nalo nilidharau. Sikutaka kumshurutisha nikiamini kwamba hakukusudia.
Lakini sikujua kwamba kwa kufanya vile ilikuwa ni sawa na kujikaanga mwenyewe. Bila shaka tabia ya Mke wangu isingekuwa endelevu kama ningelimuonya lakini kumuacha ilikuwa ni sawa na kumwambia "endelea Mama".

Siku hiyo ilikuwa Jumapili, sikwenda kazini na mara zote hushinda nyumbani siku ya mapumziko kama hivyo. Tulikaa pamoja na Mke wangu lakini mishale ya saa saba aliniomba ruhusa ya kwenda kumuona rafiki yake mara moja.
Nilimruhusu, sikuona sababu ya kumzuia. Akaniachia mtoto na kwenda huko.
Kumbukumbu zangu ni kwamba aliniaga kuwa atatumia dakika sitini tu huko aendeko lakini mambo yalikuwa tofauti.
Tangu saa saba hadi saa kumi sikumuona kurejea. Mtoto naye alilia tena kwa sifa kana kwamba alipanga yeye na Mama yake wanikomoe. Kila nilipojaribu kumbembeleza yeye ndiyo kwanza alikoleza kilio. Nilimpa maziwa lakini hayakupanda. Uji pia ndio kabisa.

Nikajaribu kumuogesha na kumlaza huko ndio akapamba moto.
Nilikasirika kweli kweli siku hiyo na nilipania kumuadhibu Mke wangu kulingana na upuuzi ule alionifanyia.
Alirejea nyumbani saa moja na nusu usiku hiyo ikiwa na maana ya kwamba alitumia masaa zaidi ya manne tofauti na makubaliano yetu. Lakini muda aliorejea alikuta tayari nimefanikiwa kumtuliza mtoto na alikuwa amelala muda huo.

"Khadija kalala?" akaniuliza hivyo mara tu baada ya kuingia ndani.
Huwezi amini, hasira zote nilizokuwa nazo zilipoa na nikajikuta na mjibu kwa upole na ukarimu.
"Ndiyo, ndiyo amelala. Ila alinisumbua aisee"
"Kasumbua eeeh? Ndiyo uanaume huo. Siku moja moja na wewe uenyeke" akanijibu huku akipita na kuelekea chumbani na mimi nikaishia kujichekesha tu na pengine hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana nililothubutu kulifanya.

Dakika tano baadae Khadija aliamka, nikamuita Mke wangu ili aje kumbadilisha nepi kwani bila shaka alikuwa amejikojolea.
Alikuja akiwa na nepi safi lakini kitendo cha kumnyanyua tu mtoto alianza kulia kama aliyepakwa pilipili ya macho. Alilia kilio ambacho sikuwahi kuona akilia hata siku moja.
"Wewe mtoto una tatizo gani?" akauliza huku akimbembeleza lakini haikufaa kitu, Khadija aliongeza kilio mara mbili ya kile alichoanza nacho.
Lakini kitu kilichotuacha hoi na kutushangaza wote ni pale nilipomchukua Khadija kutoka kwa Mama yake, aliacha kabisa kulia.

Binafsi niliona ni suala la kawaida tu na pengine nililikuwa ni kosa sana kufanya hivyo. Nilitakiwa kutilia shaka kwanini hali ile ijitokeze tena mara baada ya Ashura kurudi nyumbani kwa kuchelewa.
Tulidhani kwamba mara baada ya Khadija kunyamaza asingelia tena hata ningemrudisha kwa Mama yake lakini mambo yakawa tofauti. Nilipomrudisha tu akaanza kulia tena mara hii kikiwa kilio cha juu zaidi.

"Wewe mtoto umepandwa na mashetani gani leo" akamuuliza huku akimrudisha kwangu na aliacha kulia mara tu niliopompokea.
Basi siku ikaisha hivyo, Khadija alilia kila Mama yake alipotaka kumbeba na ikabidi nibebe majukumu yote ya kumhudumia.
Nilimlisha, nikamuogesha hata kumbembeleza hadi alipolala.

*************************************
KUNA NINI NYUMA YA MKE WANGU, ENDELEA KUFUATILIA RIWAYA KALI NA UTAFAHAMU NINI NI NINI..

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA UNAWEZA KUMTAFUTA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA NANE

ILIPOISHIA…

Tulidhani kwamba mara baada ya Khadija kunyamaza asingelia tena hata ningemrudisha kwa Mama yake lakini mambo yakawa tofauti. Nilipomrudisha tu akaanza kulia tena mara hii kikiwa kilio cha juu zaidi.

"Wewe mtoto umepandwa na mashetani gani leo" akamuuliza huku akimrudisha kwangu na aliacha kulia mara tu niliopompokea.
Basi siku ikaisha hivyo, Khadija alilia kila Mama yake alipotaka kumbeba na ikabidi nibebe majukumu yote ya kumhudumia.
Nilimlisha, nikamuogesha hata kumbembeleza hadi alipolala.

SHUKA NAYOOOO…

Niliamka asubuhi na mapema ingawa nilichelewa kulala kwasababu ya fujo za Khadija. Nilijianda tayari kwenda kazini, nikatoka nje ya nyumba na kuingia kwenye gari yangu. Niliendesha kuelekea kazini lakini bado nilikuwa na uchovu wa hali ya juu.

Nilifika kazini lakini sikufanya kazi kwa ufanisi siku hiyo kwani nilikuwa nasinzia kweli kweli.
"Leo umekula Kokeini eeh?" aliniuliza Maige ambaye ndiye tulikuwa tunafanya kazi pamoja.
"Wapi ndugu yangu, nimeanza lini mambo hayo?"
"Sasa mbona unafunga magoli ya kichwa" akanambia akimaanisha nasinzia.
"Mtoto Kaka, yaani jana usiku mtoto kafanya visa hata usingizi wenyewe nimepata wa kudokoa"
"Kivipi? Kwani Mama yake hakuwepo?" akaniuliza Maige.
"Alikuwepo lakini alichokifanya huwezi kuamini hata kidogo"
"Alifanya nini?"
"Jana Mama yake aliniaga kuwa anakwenda kwa rafiki yake. Basi aliporudi na kumbeba mtoto kikazuka kizaazaa cha mwaka. Mtoto alilia huyo, hataki kubebwa na Mama yake lakini nikimbeba mie tu ananyamaza."
"Usinambie!" akashangaa Maige.
"Ndiyo hivyo, nakwambia hadi tunalala mtoto kagoma kuguswa na Mama yake basi ikabidi nimuogeshe, nimlishe hata kumbembeleza ili alale likawa jukumu langu" nikamueleza.
"Duuu! Hiyo kali na sijawahi kukutana nayo ila nahisi ni kawaida tu. Au wewe una maoni gani?" akaniuliza kama mtu mwenye kutaka kufahamu kitu toka kwangu.
"Maoni ya nini tena hapo"
"Si jinsi unavyohisi, hauhisi ubaya wowote kuhusu Mkeo hapo"
"Ubaya kivipi, yaani labda ananisaliti?" nikamuuliza.
"Hahahaa, vyovyote tu"
"Hapana, Ashura hawezi kunisaliti wewe. Namuamini sana Mke wangu.

Amezaliwa na kulelewa na watu wanaoifahamu dini na wenye hofu ya Mungu. Hawezi kunisaliti labda nimchokoze" nikamwambia na hicho ndicho nilichokuwa naamini.

Mara nyingi wanawake waliolelewa katika mazingira ya dini sana huwa ni watu wenye kuheshimu sana ndoa zao kwani hofu ya Mungu waliyonayo huwazuia kutenda mambo machafu.
"Kweli, hata mimi naamini hivyo na ndiyo maana nikakuuliza ili kujua kama humuamini mkeo" akanambia na kuongeza. "Mimi ndiye natakiwa kuwa na mawazo potofu namna hiyo kwasababu nimeona mwanamke kama mimi. Tumelelewa ilimradi tukue, tuzeeke na tufe. Hatuna hofu ya Mungu kwa kiwango hicho tena kuchepuka kwetu si dhambi kabisa labda Mkeo agundue" akanambia na sote tukacheka.
"Malizia hiyo kazia unayoifanya sasa hivi ukapumzike, Mimi nitamalizie zilizosalia" akanambia.
Nikafanya hivyo, nilimalizia kazi zangu haraka kisha nakarejea nyumbani mapema kupumzika.

***********************************

Kazi zilitubana kiasi siku hiyo, tulichakalika Mimi na Maige ili kuhakikisha kabla ya saa kumi alasiri tuwe tumemaliza kazi yote.
Majira ya saa nane Maige aliniacha naendelea na kazi yeye akaenda kula ili atakaporejea na Mimi niende.
Kwa bahati alisahau simu yake pale tunapofanyia kazi. Mara simu yake iliita na nilipoitaza ilikuwa ikionesha "Private Number", sikuona sababu ya kupokea lakini aliyekuwa akipiga alipiga tena na tena.

Mwishowe alichoka na akaamua kutuma ujumbe mfupi wa maneno 'SMS' na kwasababu muito wa ujumbe mfupi uliwekwa na Maige ulikuwa ni wimbo wa Bongofleva (wimbo wenye dakika zaidi ya tatu) hiyo ina maana ungeita bila kuacha.
Hiyo iliniboa na kukata hamasa yangu ya ufanyaji kazi na hapo nikaamua kuibofya iki kuikata. Lakini kwa bahati mbaya mambo yalikwenda tofauti na mipango yangu kwani nilikosea kubofya na nikajikuta nimeifungua ile meseji. Na kama unavyofahamu macho hayana pazia nikajikuta naisoma ile meseji.
"Dia ninawashwa, naomba tuonane sawa hivi" ilisomeka hivyo hiyo meseji.

Nikajikuta natamani kumfahamu mtu huyo anayewashwa hasa ukizingatia kwamba Maige hakuwahi kunieleza hata siku moja kama ana mchepuko.
Nafahamu ameoa, ana Mke lakini hana mtoto. Ndoa yao na mke wake imetimiza miaka miwili sasa lakini hawajapata mtoto.
Hata hivyo Maige hakuwahi kunieleza kwamba yeye na Mke wake wana matatizo ya uzazi yanayosababisha wasipate mtoto bali hunieleza kwamba bado hawajapanga kuwa na mtoto. Hiyo hunifanya hata muda mwingine nimuhisi tofauti kwamba huenda hana uwezo wa kupata mtoto au hata labda kuna jambo liko nyuma name silifahamu.

Alirejea dakika kumi tangu kuingia kwa ile 'SMS' na nilimpa taarifa mara tu alipofika.
"Kaka kuna mtu anawashwa kakutumia meseji" nikamwambia lakini hakika nilimshitua kuliko kawaida. Pengine nilikosea kumueleza kwani haikuwa sahihi kusoma meseji au hata kupokea simu ya mwenzio.

"Anawashwa!? Nani?" akaniuliza huku katumbua macho kama kingwendu.
"Private number"
"Private number! Itakuwa kakosea huyo" akasema huku akiinyanyua simu yake.
Akasogea pembeni kidogo kama hatua tatu na nikamuona akiibofyabofya simu yake na kuweka sikioni.
"Halo, nambie" nikamsikia akizungumza hivyo na mtu aliyempigia hivi punde.
"Upo wapi wewe?...palepale kwa siku zote?.....sawasawa nakuja sasa hivi, tena nachukua bodaboda " akaongea hivyo kisha akarudi pale nilipokuwa mara baada ya kukata simu.
"Kaka wewe malizia hii kazi, kuna demu mmoja nilisoma nae kitambo leo ndio kanikumbuka. Ngoja nikamkune" akanambia huku akionekana mwenye haraka na shauku.
Nilimuacha aende kwasababu hatukuwa na kawaida ya kunyimana ruhusa za kishikaji. Akaondoka na kuniacha naendelea na kazi.

Nusu saa tangu kuondoka kwa Maige ilitokea hitilafu ya umeme, ukakatika. Mafundi walithibitisha kwamba tatizo hilo lingedumu kwa zaidi ya saa 12 hivyo hata ningeendelea kuwa pale isingefaa kitu.

Nikaamua kurudi zangu nyumbani tu na kazi ambazo nilizianza ningezimalizia kesho yake mara baada ya mafundi umeme kutatua hitilafu iliyojitokeza.
Niliingia kwe gari yangu na safari ya kuelekea nyumbani ilianza lakini nilipofika Buguruni niliona gauni zuri linauzwa.
Nililipenda na kwasababu nilikuwa nampenda Mke wangu pia sikuona sababu ya kuacha kulinunua kwa ajili yake.
Lilinigharimu elfu thelathini na tano na punde baada ya kununua niliendelea na safari.

Niliwasili nyumbani mapema. Nikaegesha gari nje kama ilivyo kawaida yangu lakini niliposogelea mlango na kutaka kufungua nilikutwa umefungwa.
Mawazo yangu yakanituma kwamba huenda Mke wangu alikuwa ametoka mara moja hivyo ilinibidi nisubiri nje kwasababu sikuwa na funguo.

Huwezi amini, nilikaa pale nje zaida ya robo saa bila kumuona
Mke wangu akirudi. Nikaamua kumpigia simu lakini iliita tu bila kupokelewa kama kawaida yake.
Nilichoka, nikarudi zangu kwenye gari, nikalaza kiti chngu na kujipumzisha huku nikiamini kwamba muda mfupi tu Mke wangu angerejea.
Usingizi ulinipia na nilikuja kushituka dakika arobaini baadae.
Nilikasirika sana baada ya kujikuta nimeamka palepale garini na tena nimeamka mwenyewe bila ya kumuona Mke wangu ambaye nilitaraji atarudi punde tu.
Nilitoka garini na kusogea tena mlangoni na kubisha hodi kwa fujo nikiamini labda Mke wangu alikuwa ndani amelala. Bado sikupata majibu na nilipojaribu kumpigia tena simu bado mambo yakawa yaleyale.

Nikaketi tena mlangoni, hasira zikanipanda na nikanuwia kumuwajibisha kwa hiyo hekaheka anayonipa.
Lakini nikiwa pale ghafla nikasikia sauti ya mtoto mchanga akilia. Nilishituka na kilichonishitua zaidi ni sauti hiyo kutoka ndani ya nyumba yangu halafu pia sauti hiyo kufafanana kabisa na ya mwanangu Khadija.
Nilijikuta nasimama ili kuisikia vyema sauti hiyo na kweli nilithibitisha kabisa kwamba ilikuwa ni sauti ya mwanangu Khadija tena ikitokea ndani kwetu.
Lakini niliingiwa na hofu mara baada ya kwisha dakika moja bila kilio cha Khadija kusikilizwa na Mama yake ambaye kwa sasa nilihisi landa walikuwa ndani wamelala.
Hapana, nilipoona hali ile imekuwa endelevu ilinibidi nifanye jitihada za kung'amua nini kinaendelea ndani.
"Ashura Mke wangu,Ashura" niliita kupitia dirisha la chumba chetu cha kulala lakini bila shaka nilikuwa nafanya upuuzi kwani kama mtu aliyekuwa ndani alikuwa hai basi ingekuwa ni rahisi zaidi kusikia sauti ya mtoto aliyekuwa akilia kuliko ya mimi niliyekuwa naita toka nje.

Pengine ni kupagawa nilikopagawa ndiko kulinituma nifanye vile. Akili za kiume zikanijia ghafla na kunipa wazo la kuvunja mlango ili niingie ndani.
Nikarudi mlango na kuanza kupiga mateke ambayo sidhani kama yalikuwa na msaada wowote kwa kile nilichokuwa nakiwaza.
Nilipoona sifanikiwi wazo jipya likanijia. Nikafikiria kuvunja mlango wa stoo na kuchukua shoka kwani bila shaka ule ulikuwa si imara kama ulivyo huu wa nyumba kubwa.
Basi haraka nilisogea huko na kupiga mateke mawili matatu lakini haukubomoka ingawa ulionesha dalili njema. Nikagundua kuwa kilichokuwa kikihitajika ni mateke yenye nguvu zaidi.
Basi nikarudi nyuma meta kadhaa kutoka mlango na kisha nikaanza kutimua mbio kuelekea, nikaurukia na kuupiga teke moja tu ambalo liliufungua mlango kwa lazima na nikaingia nao hadi ndani.

Haraka nikachukua shoka na kutoka nalo hadi kwenye mlango ambao nilitaka kuubomoa, nikashambulia kitasa kwa mapigo matatu tu ya shoka na mlango ukafunguka.
Hapo sikupoteza hata sekunde moja, nilitupa shoka pembeni na kuingia ndani, chumbani ambapo sauti ya mwanangu Khadija ilikuwa ikiendelea kusikika ikilia. Moyo, roho na akili yangu vyote kwa pamoja vilitaraji ningekuta mwili wa Mke wangu ukiwa mfu kutokana na hali hali halisi iliyokuwa ikiendelea.

Lakini mambo yalikuwa tofauti na nilivyodhani tena kwa asilimia 100, chumbani sikumkuta Mke wangu kama nilivyodhani bali mwanangu Khadija tu akiwa kitandani analilia.
Nilimyanyua na kumbembeleza ili aache kulia naye akafanya hivyo. Nikatoka naye hadi sebuleni na kumlaza kwenye kochi. Nikamvua chupi na 'diaper' (pedi maalum kwa ajili ya watoto) na hakika nilichokumbana nacho kilikuwa ni balaa na pengine ndicho hicho kilichomfanya alie namna ile.

Yaani kinyesi, haja kubwa ya zaidi ya mara bili na haja ndogo ambayo iliisagasaga ile haja kubwa na kutengeneza kama uji uji wa manjano. Kwa kifupi ni kinyaa na uchafu ule ungeweza hata kumdhuru mtoto kama ungelikaa kwa muda mrefu zaidi.
Nikabeba jukumu la kumsafisha mwanangu lakini siwafichi hasira nilizokuwa nazo siku hiyo zilikuwa hazielezeki. Ni hasira ambazo zilipita hata hasira za kawaida na pengine ningeweya kutafuna hata chuma kwa hasira zile.

Hebu vuta picha ungelikuwa ni wewe. Unarejea nyumbani humkuti Mke wako na mbaya zaidi unakuta amemtelekeza mtoto namna ile. Hiyo haitoshi anakupelekea unapata hasara kwa kuvunja kitasa cha mlango kama hivi nilivyofanya mimi, ushishie hapo tu, kumbuka kuna nguvu kazi ambayo uliitumia wakati wa kuvunja mlango wa stoo na kadhalika. Ni maudhi hakika.
Nilipanga kumuadhibu tena adhabu ambayo ingerandana na kosa lake ni kipigo tu na sidhani kama kuna nyingine.
*****************************************************

WAPI AMEKWENDA MKE WANGU TENA BILA KUAGA NA KWA KUMUACHA MTOTO NDANI NA KUMFUNGIA MLANGO , USIKOSE SEHEMU YA TISA YA RIWAYA HII MARIDHAWA ILI KUFAHAMU MENGI.

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA ZAIDI UNAWEZA WASILIANA NA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom