Acheni kulalamika. Serikali iko mbioni kurekebisha miundo mbinu ya reli, michakato wa kununua treni mpya imeshafikia pazuri, mikakati iko safi. Bajeti kidogo imepungua lakini hata hivyo, jitihada za kuwasiliana na wafadhili zinaendelea vizuri, wakati huo huo mawasiliano kati ya serikali na mwekezaji mpya karibu yanafika mwisho. Bahati mbaya serikali haijajua muda kamili ila inatarajiwa kuwa kabla ya 2061 (50yrs). Tusiwe na hofu ajali haitatokea, na kama itatokea kabla ya utekelezaji wa mpango mkakati na kuua mamia ya watu hiyo ni mapenzi ya Mungu, hata hivyo serikali itatoa ubani kwa wafiwa. Msisikilize malalamiko ya Wapinzani.