Dodoma: DC wa Chamwino, Gift Msuya ajeruhiwa kwenye ajali baada ya gari lake kugonga treni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,106
Msuya.jpeg

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gifty Msuya amejeruhiwa baada ya gari alilokuwa amepanda kugonga treni eneo la Iyumbu Jijini Dodoma walipokuwa wakitoka kwenye sherehe.

Sherehe hiyo iliyofanyika juzi usiku Novemba 28 ilikuwa ni kwa ajili ya kupongezana kwa Mkoa wa Dodoma kushika nafasi ya kwanza kwenye mbio za Mwenge mwaka 2023.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye yeye na dereva wake walipata majeraha mwilini, amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Alipoulizwa leo Novemba 30, 2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Dk Semistatus Mashimba amethibitisha DC huyo kupata ajali.

Hata hivyo, Dk Mashimba amesema hawezi kuzungumza zaidi kwa kuwa yupo kwenye kikao.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, hakupatikana baada ya simu yake kuita bila majibu.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika zinasema Msuya alipata ajali hiyo saa 1:00 usiku wakati akirejea nyumbani kwake baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo iliyofanyika mjini Dodoma.

Taarifa hizo zinasema baada ya sherehe kuisha, Gifty walitumia barabara ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili watokee barabara kuu ya Morogoro eneo la Ihumwa, lakini wakati anavuka reli ya kati ndipo alipogonga treni.

"Alikuwa na dereva wake, bahati mbaya wakati wanavuka daraja la reli ya mwendo kasi ndipo walipopata ajali maana waligonga treni waliyokutana nayo wakati wanavuka,” kimesema chanzo hicho.

Chanzo hicho kimesema hali ya DC huyo inaendelea vizuri kwa sababu pamoja na kuumia, hakupata majeraha mabaya isipokuwa michubuko na maumivu kidogo ambayo yamesababisha alazwe kwa uangalizi zaidi.

IMG_8368.jpeg


Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu wa wilaya ya Chamwino mh Gify Msuya na Dereva wake wamelazwa hospital ya Benjamin Mkapa baada ya Kupata ajali

Gari ya DC Msuya iligonga Treni eneo la Iyumbu wakati wanatoka kwenye sherehe za kusherehekea Dodoma Kuwa mshindi wa kwanza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru

Source: Mwananchi
Hawa jamaa na hayo magari ya Serikali huwa wanajiona sana wakiwa barabarani, sasa hilo ni fundisho - wakimaliza kutibiwa washtakiwe kwa kusababishia hasara shirika letu la reli.
 
Unatamani useme Sheria za reli zirekebishwe, ila ukikumbuka mwendokasi WA madereva wa STK unakosa upande wa kusimamia.

Niseme tuwe makini barabarani, mara nyingi mwendokasi ndio chanzo cha ajali, dereva akiwa katika speed ya kistaarabu ni rahisi kufanya maamuzi sahihi....mwendokasi unakunyima nafasi ya kufanya maamuzi.

Pole nyingi Kwa majeruhi
 
Mkuu wa wilaya ya Chamwino mh Gify Msuya na Dereva wake wamelazwa hospital ya Benjamin Mkapa baada ya Kupata ajali

Gari ya DC Msuya iligonga Treni eneo la Iyumbu wakati wanatoka kwenye sherehe za kusherehekea Dodoma Kuwa mshindi wa kwanza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru

Source: Mwananchi
Kazi ipo mbuzi wa bwana heri shamba la bwana heri!
 
Endapo reli zitaendelea kukatiza barabara za waenda kwa magari, ajali hizi hazitaisha...

Kwa wenzetu endapo inatokea reli na barabara za magari zinakutana, huwa yanawekwa geti, mataa na kengele ambavyo huikinga reli na kutoa ishara pindi treni linapokuwa karibu kupita
 
Hiyo gari yao ilikuwa mafuta sana nadhani kiasi cha kushindwa kupunguza mwendo au kusimama kabisa baada ya kuona treni kwa mbele ikizingatiwa kuwa kuna zaidi ya mita 50 kati ya daraja la sgr na mgr.

Pole nyingi kwa majeruhi
 
"Kwa bahati mbaya waligonga treni" lakini kama angekuwa mtu mwingine asiyefahamika tungesoma na kusikia kauli za "Uzembe wa dereva" au "alilewa sana akashindwa kulimudu gari" au " mwendo Kasi" n.k

Halafu ajari imewapata watu wawili lakini anayeripotiwa ni mmoja.. Kwanini? Tunayo safari mdefu ktk kuutambua utu wa mtu nje ya kipato na nafasi yake

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom