Nasumbuliwa sana na mke wa mtu alienidhamiria bila kuchoka, nawezaje kumfanya ajue haitawezekana bila kuvunja urafiki wetu?

Nasumbuliwa sana na mke wa mtu alienidhamiria bila kuchoka, nawezaje kumfanya ajue haitawezekana bila kuvunja urafiki wetu?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,450
Kuna binti mmoja, ni mke wa mtu, lakini ananiumiza kichwa sana siku hizi. Mume wake alimfungulia duka kubwa tu awe anakuwa bize, na kwa kuwa hata mimi nina duka katika mitaa hiyo, tulianza kuzoeana kama majirani. Kila nilipopita na kumuona, sikusita kumsalimia na mara nyingi tulikuwa tunapiga stori chache. Kadri muda ulivyokwenda akanizoea sana, hadi nikikosa kupita huanza kutafuta sababu yoyote ili niende kumuona. Sasa hivi hali imebadilika kidogo, maana ameanza kuonyesha wazi kwamba ananipenda sana.

mara ya kwanza alikuwa ananipa signals ila nadhani utani kumbe yeye kazama deep sana

kawa wazi mno kuhusu hisia zake kwangu

Anajua kabisa nina mke lakini hajali na kwa kutia msisitizo aliwahi kunitumia hadi clips za Engonga akijitetea dunia imeharibika ila nilishajua hesabu alizopiga,

najitahidi sana ku back off lakini kadhamiria,

niwe wazi, angekuwa mjanja labda ningefikiria kuchepuka lakini ni mweupe sana upstairs, nimemdadisi bado ni mgeni sana kwenye ishu nzima ya uchepukaji, hata simu yake pattern ni nyepesi sana, kwangu ni jambo ambalo halitawezekana kabisa.

nawezaje kumfanya aelewe haiwezekani bila kuumiza hisia zake na tuendelee kuwa marafiki tu ? maana ninajua wazi nikikubali tu lazima tunaswe na kumkwepa ni ngumu kwasababu nina ofisi eneo hilo na lazima kila siku nipite mchana au jioni.
 
Hakupendi huyo ili uniamini we Mshtukizee umwambie mkapime afyaaa utakuja kunishukuru🙏🙏
 
Ni mke wa mtu huyu binti, katika kuzoeana nae kwenye duka alilofunguliwa na mme wake, ametokea kunipenda sana.

mara ya kwanza alikuwa ananipa signals ila nadhani utani kumbe yeye kazama deep sana

kawa wazi mno kuhusu hisia zake kwangu

najitahidi sana ku back off lakini kadhamiria

hata kama ningekuwa na nia nae ya kuchepuka nisingeweza, bado ni mgeni sana hata kuficha meseji hajui, ni rahisi sana kujulikana, kwangu ni jambo ambalo halitawezekana kabisa.

nawezake kumfanya aelewe haiwezekani bila kuumiza hisia zake na tuendelee kuwa marafiki tu ?
Uendelee kuwa na urafiki na mke wa mtu unamaanisha nini?

Fisi ukisikia anacheka, elewa anasherehekea mawindo.

Kwa binadamu ukimuona ama kumsikia akilaani jambo lolote ili wenzie wasilifanye, ima kulaani umalaya ama mahusiano yoyote yasiyofaa, yakupasa umfuatilie binadamu huyo kisogoni kwake, hatua kwa hatua, waalah utagundua mengi maovu kumhusu.

Una umri gani kushindwa kuelewa njia za kumkwepa Ibilisi?

Mwenzetu nadhani unasherehekea ushindi, sawa, lakini dhambi hiyo usituhusishe na sisi, bakia nayo mwenyewe.
 
Baki njia hiyo hiyo mkuu, utajiepusha na mengi. Kuwa kama Yusufu, alikimbia mbio ndefu ili asimchape mke wa bosi wake.
 
Acountability na rejection ni mambo mawili ambayo yanawashinda wanawake. Ukimwajibisha au ukimkatalia hitaji lake mwanamke hawezi kukubali with no hard feelings.

Kwa hiyo scenerio yako jua tu ukamkatalia anachotaka na urafiki unakufa. Hauwezi kumkatalia mwanamke na akaendelea kuwa friendly kama mwanzo. Kuna kasehemu kwenye moyo wake atakutengenezea uadui.

Women can't handle accountability and rejection like men.
 
na ndio maana nakuwa careful sana kwenye mazungumzo ili asije kuyatumia kunigeuzia kibao au hata yakivuja nisiwe mhanga

Lakini pia namuonea hutuma mwanaume ataekuja kuchepuka nae anaweza kufumaniwa kirahisi sana kwa sababu huyu binti bado ni mgeni sana kwenye kuficha clues na footprints
 
Kamsemee kwa babaake
Huyu ni mke, ni ishu nzito kidogo

Ingekuwa ni girlfriend ningeenda kwa jamaa yake, hata Suma G aliawahi kuimba

Mshikaji demu wako, ananitaka
Mshikaji demu wako, anachemka
Kila nikipita mimi ananifata
Kila akinionaa, ananiita ita...
 
Attachments

😅😅😅JF bhana, Kila mwanaume humu anashobokewa na pisi Kali/ mke wa mtu, eniwei hii alkasusu ni ya moto sana mkuu and by the way acha uzinzi.
 
Huyu ni mke, ni ishu nzito kidogo

Ingekuwa ni girlfriend ningeenda kwa jamaa yake, hata Suma G aliawahi kuimba

Mshikaji demu wako, ananitaka
Mshikaji demu wako, anachemka
Kila nikipita mimi ananifata
Kila akinionaa, ananiita ita...
Kwamba akiwa mke hana baba?
 
Acountability na rejection ni mambo mawili ambayo yanawashinda wanawake. Ukimwajibisha au ukimkatalia hitaji lake mwanamke hawezi kukubali with no hard feelings.

Kwa hiyo scenerio yako jua tu ukamkatalia anachotaka na urafiki unakufa. Hauwezi kumkatalia mwanamke na akaendelea kuwa friendly kama mwanzo. Kuna kasehemu kwenye moyo wake atakutengenezea uadui.

Women can't handle accountability and rejection like men.
Mkuu inawezekana sema kijana akili yake haiko vizur.

Cha kufanya yeye asimzingatie huyo mwanamke na ajifanye bwege tu kama haelewi kitu atafanikiwa.
 
Back
Top Bottom