Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Pumbavu kama hili utakuta lipo kwa shemeji kazi ni kubadili chanel, utakuta limekimbia kijijini huko halijawahi hata kuuza karanga hajui lolote kuhusu ugumu unaowakuta wakulima na wafanyabiashara...
Hivi wewe lipumbavu hapa aliedharau uhusiano na mwenzie ni nani tz au Kenya?
 
kwani unalima kwa ajiri ya kenya!!!

unafikiri kenya wakianza kulima na wao utamuuzia nani mahindi??
Kenya hawana ardhi mkuu,sisi ndo basket of food for east and central Africa,Ila tu tumekosa viongozi wa kutuongoza ili tuwe a real basket of food for our majiranis
 
Wakulima Walime, Watanzania tule kwani Kenya tu ndo wanamatumbo peke Yao?.. Viongozi wetu sio wajinga na sisi Watanzania tupunguze uoga, changamoto kidogo tu mshaanza kupost Mabandiko, Kama hawanunui wao tutauza kwingine watakapo hitaji, ikishindikana tuuziane humuhumu Maisha yaendelee mi hua hainingii akilini kununua debe la Mahindi 20,000 wakati mengine yanapelekwa Kenya huko.. hii Ni Vita ya kiuchumi na Kenya wameshaona Kuna uwezekano wakageuka koloni la Tanzania.. Punguzeni Uoga Vijana, maendeleo hayaji bila changamoto.. Sengwile Makamanda!!
C unaona vilaza wanaochangia? Hii nch ina mabogaz mengi hayajitambui.
 
Sisi ni watu wa ajabu sana yaani tunashindwa kutafuta masoko tunasubiri mpaka anayejifanya kuwa soko kuu atujambishe halafu wanasiasa wanshupalia kana kwamba wao wanaathirika wakati wanakula kwa maneno masoko ya bidhaa za kilimo yako mengi sana tatizo tumejibweteka tunasubiri wakenya watoke kwao waje kununua kwetu sisi tunashindwa kutafuta masoko kuna Comoros, sudan, msumbiji Congo na Tanzania yenyewe
 
Tanzania na Kenya wala hakuna tatizo...

Tatizo ni hawa mabeberu wanataka kutufarakisha na majirani...

Kisa Kenya imekula pesa za covid na imekubali chanjo... kwa hiyo wanaitumia kuleta mtafaruki na Tanzania kisa...

Tanzania imekataa kuchukua pesa za covid na haitaki chanjo...
 
Kwa hiyo wewe unataka wakenya wafanye wanachotaka wao siyo?? Subiri tunapiga stop bidhaa zao zote kuja TZ tuone nani ataumia zaidi.
Jamani hivi dunia ishakua kijiji, na wote tutaishi kwa kutegemeana mpendwa msiende, na uadui au ushabiki kama wa Simba na Yanga ktk mambo msingi ya kiuchumi hayatupeleka popote...mambo ya kutunisiana misuli kwenye ulimwengu wa free market economies hayana nafasi tena, labda kama mnataka kurudi nyuma tena kwenye siasa zilizoshindwa za kikomunisti.
 
Mtoa mada umekula mahindi yenye sumu, hata kufikiri kwako ni dhaifu.
 
Kenya, jifunzeni kutoka kwa Japan. Kwa miongo mingi Japan iliipita jirani wake yaani China katika maendeleo ya kiuchumi. Hivyo hivyo Kenya iliipita Tanzania.

Na kama ilivyo Japan yenye sasa za kibepari dhidi wajamaa China, Kenya pia ilikuwa na mrengo wa kibepari tangu uhuru huku Tanzania ikifuata siasa za ujamaa na hatimaye kama ilivyo China ikauboresha ujamaa wake ukawa sasa mfano wa ujamaa wa kibepari.

Kijiografia pia Japan ni kadogo sana kwa China kama ilivyo Kenya kwa Tanzania. China ilikuwa dude lililosinzia "sleeping giant". Hatimaye dude likaamka, likazinduka usingizini. Tanzania imeshaamka.

Japan sasa ni mtoto kwa China. Inamhofu China. China imeitupa mbali Japan. China sasa haishindani na "mchovu" Japan. Inamtafuta na iko inampita superpower wa dunia, Marekani. Japan yenyewe inajijua nguvu zake ndogo, inajipendekeza kwa China ili ibaki na amani dhidi ya jirani mwenye nguvu, China.

Ni muda mwafaka sasa Kenya ijifunze kwa ufasaha hili somo la China-Japan, dude la Afrika Mashariki limeshaamka na Kenya icheze vizuri karata zake ili iwe salama kiuchumi, kisiasa, kijamii dhidi ya jirani mwenye nguvu.

Busara muhimu: Mwenye nguvu mpishe, usishindane naye. Usipige ngumi ukuta.
 
Nafikiri na sisi tulichangia baada ya kuchoma viranga vyao mpakani kwa sababu ya kutokukidhi viwango au labda kuna mengi nyuma ya pazia ambayo hajawekwa wazi
Magu amewashika pabaya sana nowadays, c unajua jamaa ni madalali wa malighafi za Tz, ss sleeping giant imeamka mali zake inauza yenyewe hapo ndipo kunapowauma cz wao mali zao ni chache na kanchi kao 3/4 ni kame
 
Kuna clip nimeiona inaonyesha wakulima wa kenya wakilaumu ofisi ya makamu wa rais wa nchi yao, kuwa ndiye yeye na group lake wameagiza mahindi kutoka nje, ndiyo wao wanalima mahindi heka 500,000 huko congo brazavile ili wayauze kwa wananchi wa kenya.

Nashindwa kuelewa ni only urasimu wa nchi yao katika ofisi tajwa ndiyo inapelekea mahindi yetu kuharibiwa soko au ni zile chochoko na wivu wao kwa tz tangu enzi mlima knjaro upo kenya?

Mimi naona Tanzania tumekuwa soft mno kwa hawa jamaa, wametuingiza vidole vya pua mara zote na sisi tunapata baridi kuwarudishia. ni wakt sasa wa sisi ku'act aggressively dhidi yao katika kujibu hili. Kutokana na umoja wetu, ilifaa wazir wao husika angechek na wazir wetu husika juu ya ubovu wa hayo mahindi, na kuhus hicho kinachoitwa sumu kwny mahindi kabla hawajaenda public kutuchafua.

Hivyo basi tanzania katika kujibu hili, ipige marufuku bidhaa zote kutoka kenya ikiwepo malory yao. fukuza balozi wa kenya hapa nchini, rudisha balozi wetu nchini kisha close border zote kati yetu na wao. huu upuzi wao umezidi, kuna kipindi walipga marufuku malory yetu kuingia kenya kwa kisingizio cha korona, lakn malory yao yanaingia tz bila kuzuiwa, sasa unajiuliza kwann hawaogopi madereva wao kuja kuambukizwa wakija huku?

Ila kuna jingine, pengine wanatumika katika kututia pressure ingine, ili tuone kila kitu ni hovyo ili ajenda ya chanjo ya korona nayo ipate kasi. kenya ni majirani wa hovyo sana, wao wanategemea sana soko la bidhaa zao hapa nchini, na sisi tukizipiga marufuku watayumba katika viwanda hivyo kupelekea tukae mezani tukubaliane, waandike gazeti lingine la kuomba sorry kwa uzito ulele walio tuchafua, walipe fidia kwa wakulima wetu na wafungue tena soko lao la mahindi kutoka kwtu.

Zaidi, lawama kwa tiss katika dawati la intelligence ya economy, walifaa walione hili la wao kuagiza mahindi mengi nje kabla, nia yao ya kuzuia na kutuchafua kabla, kisha kuja na njia ya ku counter hili tukio.
 
kuna clip nimeiona inaonyesha wakulima wa kenya wakilaumu ofisi ya makamu wa rais wa nchi yao, kuwa ndiye yeye na group lake wameagiza mahindi kutoka nje, ndiyo wao wanalima mahindi heka 500,000 huko congo brazavile ili wayauze kwa wananchi wa kenya..
Wamesema mahindi ya Tz yana sumu kuvu inayosababisha kansa, je ni kweli hayana hilo limethibitishwa na mamlaka za Tz? maana Tz kwa siku za karibuni imekuwa ikifanya vituko/uwongo wa kijinga kwa mfano watu wanapimwa korona wanapewa vyeti hawana lakini wakifika nchi wanayoenda wakipimwa wanakutwa nayo mifano ipo ingi tu!

Haya nyavu za uvuvi na vifaranga vya Kenya vilichomwa moto, je hapo Tz haikuwa imewaharibia soko lao hao wakenya? Ifike hatua Tz iwe smart kwenye issue za diplomasia ya uchumi, Tz ijue kwenye issue za uchumi hakuna huruma huruma na hivi si Tz imekuwa ikikataa kununua sukari toka Uganda?

Badala yake inaona bora iagize toka nchi zingine za mbali? Hivi si Tanzania bara ilishakataa kuagiza sukari toka Zanzibar ilhali ya kuwa Zanzibar ilikuwepo? chanjo Watz watachanjwa tu ni suala la muda tu japo wapo wachache sana hawatokubali kwa sababu za kidini n.k lakini walio wengi watadai chanjo na serikali yenyewe itasarenda.
 
Wamesema mahindi ya Tz yana sumu kuvu inayosababisha kansa, je ni kweli hayana hilo limethibitishwa na mamlaka za Tz? maana Tz kwa siku za karibuni imekuwa ikifanya vituko/uwongo wa kijinga kwa mfano watu wanapimwa korona wanapewa vyeti hawana lakini wakifika nchi wanayoenda wakipimwa wanakutwa nayo mifano ipo ingi tu!
nakubaliana na usemayo mkuu, nafikir ni muda muafaka wasisi kama tz kujitathimini kwny baadhi ya maswala kama hilo la sukar nk. ijapokuwa yapo ambayo tulimalizana nao kama hilo la vifaranga.

swali ni kuanza tena kwa hizi chokochoko zao, kama mahindi yetu yamegundulika na hili tatzo huko kwao, wao wakenya walishindwa nn kuwasiliana na tanzania privately kabla ya kwenda hewani?

hapa inabidi tujiridhishe madai yao kama yana ukweli, ikiwa kweli sumu hiyo imekutwa ama ipo kweny mahindi yetu, basi kuanzia mkrugenzi hadi boss wa tbs mpakani wafukuzwe na wapelekwe mahakamani kwa kuruhusu mahindi substandard kuuzwa nje. ikiwa la mahindi hayana shida, basi ni kuita balozi wetu arudi nchini, fukuza wa kwao. funga boda na kuzuia bidhaa zote kutoka kenya kwa muda usio na kikomo. wao wanauza zaidi kwetu bidhaa nyingi kuliko sisi tunavyo uza kwao...

ishu yetu ya kukiri korona ipo au haipo nchini, siyo swala la siasa baina yetu na wao wakenya, zaidi ni swala la tz na ulimwengu wote
 
Kenya sasa hivi wanakimbizana na nchi za ulaya kwenye kilimo. Afrika wameshampiga bao south na misri kitambo, hawa vijana wanashinda jukwaa la siasa hawasomi yanayojiri kenya na nje ya tz matokeo yake ndio haya
Sasa umekuwa mwongo.

Kilimo gani wanachokimbizana na ulaya?

Chai?, ulaya hawalimi chai. Makampuni makubwa yanayolima chai ni ya walowezi waingereza.

Maua? Mkenya gani analima maua kama sio kampuni za ulaya.

Mahindi? Mkulima wa mahindi Uasini Gishu, Kitale na sehemu zote za Rift Valley sasa hivi wanatelekeza mahhindi kwa sababu ardhi imechoka ile mbaya, pamoja na kupewa ruzuku ya mboleakila mwaka!

Sasa tueleze wewe unayedanganya hapa bila aibu, hao wakenya wanalima kitu gani kutuzidi.

Ngoja nikusaidie sehemu moja, ambayo ni uzembe wetu tu, lakini na yenyewe tukiweka juhudi kidogo muda si muda tunawatupilia mbali - Maziwa - uzalishaji wa maziwa..., lakini na wenyewe sasa Uganda anawaliza, halafu wewe unakuja kusifia hapa na kuwalinganisha na ulaya?
 
Unaweza ukiwa umeandika ukweli, ila ili tuweze kuwapita Kenya, tunahitaji fikra za raia wa Tanzania zibadilike, fikra za viongozi wetu nazo zibadilike hasa wale walioko kwenye ngazi za maamuzi waache kukwamisha kwa misha mambo bila sababu za msingi.

Mimi nampongeza sana muheshiwa Rais, yeye kama mkuu wa nchi amejitahidi sana kutubadilisha fikra sisi wa Tannzania katika mambo mbalimbali, mara nyingi amekuwa akituhamasisha tuchape kazi tulipe kodi huku akituondolea ile dhana tuliyokuwa tumeizoea kuwa nchi yetu ni masikini, mara kadhaa amekuwa akituambia kuwa nchi yetu ni tajiri.

Nchi yetu imeingia kwenye uchumi mdogo wa kati, lakini bado viongozi na wasimamizi wa taasisi mbalimbali wanafikra zile zile za uchumi wa zamani, kifupi sio wa bunifu kabisa, na wakati mwingine wanawakwamisha wale wanaonekane kuwa na fikra chanya za kimaendeleo kwa kutumia mamlaka yao, ukitaka kutumbua hilo angalia ni mara ngapi kwenye msafara wa Rais tunaona wananchi wakilalaikia matatizo mbalimbali ambayo yangeweza kutatuliwa hata na mkurugenzi, diwani au balozi?.

Juzi Morogoro Mh. kabaini ufisadi kwenye kodi ya vizimba vya soko jipya na haya mambo yapo karibu nchi nzima, sasa jiulize hali inakuwaje huko ambako Mh. Rais hajafika kufanya ziara. Embu tujiulize ndugu zangu, nchi imeingia kwenye uchumi wa kati shule zinakosa hata madawati au vyumba vya madarasa eti mpaka Rais au waziri mkuu aanze kufuatilia wakati tunamiti ya kutosha kabisa, hapo ujue tunabaadhi ya viongozi waliopewa mamlaka ya kusimamia taasisi fulani sio wabunifu yaani wao kila kitu wanataka serikali kuu ije ifanye, wanashindwa kutumia nguvu zao za kiushawishi kutatua kero ndogo ndogo zinazo ikabili jamii.

Ili nchi iweze kuendelea inahitaji mabadiliko makubwa ya science na techolojia. Mtaani kuna wabunifu wengi sana ambao kama wangetumika vizuri na taasisi za elimu ya juu hasa vyuo kama Arusha Tech, DIT na MUST na shule za ufundi basi tungeanza kutengeneza bidhaa zetu na kuanza kutatua baadhi ya kero kwenye jamii, lakini wizara yenyewe sidhani kama imeshawahi hata kuwadhamini katika tafiti zao.

Wakenya wao wameshajanjaruka siku nyingi hivyo wao hata akija kiongozi yeyote wanaenda na speed ile ile. Sisi watanzania tulio wengi bado hatujiamini amini hivi tunajihisi bado tupo katika maisha yake ya zamani, hivyo kama tunahitaji kuwapita wakenya basi tubadilike haswa.
 
Back
Top Bottom