Nashauri Serikali iajiri Walimu wenye ufaulu wa daraja la kwanza au la pili kwenye vyeti vya elimu ya sekondari(Kidato cha nne na sita)

Umepata division one au Two af wahitaj kuajiriwa??? Nadhani akili unazo nyingi mno usiipe mzigo serikali kukulipa ilihali waweza kuiingizia mapato zaidi.......
pambana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha Judge ana degree moja, mshahara wake mkuuubwa, allowances za kumwaga, Gari na Dereva anapewa, Nyumba nzuri pia ulinzi. Sasa sikiliza Mwalimu , hata angekuwa na PhD kama Muheshimiwa Magufuli, utasikia anasubiria kupandishwa madaraja.Mshahara kupanda mpaka atishie anaacha kazi.
Huwa nasema ualimu haujawahi kuwa na mtetezi duniani, hii hoja mnaiumiza bure muiache tu.
 

mnhhh
 
nimeguna sababu sijakuelewa
Nimesema Judge ana degree moja lakini mshahara wake na yale tunaita marupurupu yanatisha, ukija kwa mwalimu mshahara kiduchu, na hata kupandishwa mshahara mpaka chama cha walimu kipige kelele au watishie kugoma.
 
Nimesema Judge ana degree moja lakini mshahara wake na yale tunaita marupurupu yanatisha, ukija kwa mwalimu mshahara kiduchu, na hata kupandishwa mshahara mpaka chama cha walimu kipige kelele au watishie kugoma.

Life is not fair....

Wangeweka mshahara na marupurupu Mengi kwa walimu,inge attract watu makini
 
Kuna ufaulu, alafu kuna kipaji kwenye kufundisha.

Unaweza kua na GPA kubwa sana, ukawa na div 1 au 2 lakini bado ukakosa uwezo wa kumuelekeza mtu.

Kwahiyo division au gpa bado sio kigezo peke yake cha kumfanya mtu kua competent kwenye ualimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio div1 or 2
Kinachotikiwa walimu nao wawe na enterview kama fani zingine hapo ndo utajua kama mwl yupo vzr ama la!
Coz utakuta mwl mwinge yupo right ktk vyeti na ana one ama two but skills za kuamisha knowledge kwenda kwa mwinge ili na yeye apate one ama two hana, je, huyo mwanafunz atapata hayo madaraja?
Lkn pia wapo hata waliopata div4 lkn akawa na larger skills ya kuhamisha knowledge kwenda kwa mwingne na akayapata hayo madaraja. Mtu kupata div4 au 3 haimaanishi kwamba yupo vibaya coz zipo sababu nyingi zilizomfanya spate hayo madaraja.
Kwang Mimi sio kigezo cha MTU aliyepata one ama two ndye anaweza kuamisha hizo skills kwa mwanafunz ili nae spate hayo maharaja.
 
unachoongea hata mimi nakubaliana nacho, kwenye Chemistry O level tulikuwa na mwalimu aliyefaulu na alikuwa na jitihada za kufunsisha alianza na sisi toka tukiwa form two mpaka tunamaliza form four, matokeo yetu katika wanafunzi 42 'F' zilikuwa mbili tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu aliye pata division one na two anazo mbinu za kufauru mtihani, mbinu za kufauru mtihani hatusomei chuoni, mbinu za kufauru mtihani anazo yule mwalimu aliye fauru mtihani huo. Tutumie walimu wenye ushuhuda


kumbe nawewe ni kilaza! siyo kufauru ni kufaulu
 
mshauri kwanza mama ako apunguze kuzaaa haya mengine naona yako juu ya uwezo wako!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa bahati mbaya O level na A level hakuna kozi la strategies za kujisomea haijalishi una one au two.... Hayo yote utayatakuta chuo ukiwa unasomea taaaluma ya ualimu....tafadhali one au two haina msaada kwenye taaluma ya ualimu..... Knowledge base ya mwalimu ndio msingi wa ualimu....
Kama hujaelewa nitakuandikia notes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…