Nashauri Serikali iajiri Walimu wenye ufaulu wa daraja la kwanza au la pili kwenye vyeti vya elimu ya sekondari(Kidato cha nne na sita)

Umepata division one au Two af wahitaj kuajiriwa??? Nadhani akili unazo nyingi mno usiipe mzigo serikali kukulipa ilihali waweza kuiingizia mapato zaidi....... pambana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I agree with you...

Walimu walipaswa huwa na payscale sawa na majudge!

yes walitakiwa walipwe Zaidi...

hii ingewa attract watu makini, wenye uwezo mkubwa kufundisha na wenye uwelewa kubwa,in terms of qualifications,...

sio kama sasa hivi,ualimu ni kwa wale failures ,,,ni kama label vile,ukichukua ualimu inaonyesha Marks zako huko nyuma zilikua kwa mbinde...

yaani katika jamii yetu uwalimu=failure in academic achievement.

we have to change this attitude,

ba tutafanya hivyo pale ambapo walimu watapewa mishahara inayostahili,na pale ambapo Fani ya uwalimu imefanikiwa kuchota walimu ambao wako competent,wana qualifications sawa na profession nyingine kama doctor,lawyer etc

Serikali ibadilishe vigezo vya kuombea uwalimu,waweka tighter system,waliofaulu tu ndio waruhusiwe kufundisha
Hahaha Judge ana degree moja, mshahara wake mkuuubwa, allowances za kumwaga, Gari na Dereva anapewa, Nyumba nzuri pia ulinzi. Sasa sikiliza Mwalimu , hata angekuwa na PhD kama Muheshimiwa Magufuli, utasikia anasubiria kupandishwa madaraja.Mshahara kupanda mpaka atishie anaacha kazi.
Huwa nasema ualimu haujawahi kuwa na mtetezi duniani, hii hoja mnaiumiza bure muiache tu.
 
Hahaha Judge ana degree moja, mshahara wake mkuuubwa, allowances za kumwaga, Gari na Dereva anapewa, Nyumba nzuri pia ulinzi. Sasa sikiliza Mwalimu , hata angekuwa na PhD kama Muheshimiwa Magufuli, utasikia anasubiria kupandishwa madaraja.Mshahara kupanda mpaka atishie anaacha kazi.
Huwa nasema ualimu haujawahi kuwa na mtetezi duniani, hii hoja mnaiumiza bure muiache tu.

mnhhh
 
nimeguna sababu sijakuelewa
Nimesema Judge ana degree moja lakini mshahara wake na yale tunaita marupurupu yanatisha, ukija kwa mwalimu mshahara kiduchu, na hata kupandishwa mshahara mpaka chama cha walimu kipige kelele au watishie kugoma.
 
Nimesema Judge ana degree moja lakini mshahara wake na yale tunaita marupurupu yanatisha, ukija kwa mwalimu mshahara kiduchu, na hata kupandishwa mshahara mpaka chama cha walimu kipige kelele au watishie kugoma.

Life is not fair....

Wangeweka mshahara na marupurupu Mengi kwa walimu,inge attract watu makini
 
Kuna ufaulu, alafu kuna kipaji kwenye kufundisha.

Unaweza kua na GPA kubwa sana, ukawa na div 1 au 2 lakini bado ukakosa uwezo wa kumuelekeza mtu.

Kwahiyo division au gpa bado sio kigezo peke yake cha kumfanya mtu kua competent kwenye ualimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio div1 or 2
Kinachotikiwa walimu nao wawe na enterview kama fani zingine hapo ndo utajua kama mwl yupo vzr ama la!
Coz utakuta mwl mwinge yupo right ktk vyeti na ana one ama two but skills za kuamisha knowledge kwenda kwa mwinge ili na yeye apate one ama two hana, je, huyo mwanafunz atapata hayo madaraja?
Lkn pia wapo hata waliopata div4 lkn akawa na larger skills ya kuhamisha knowledge kwenda kwa mwingne na akayapata hayo madaraja. Mtu kupata div4 au 3 haimaanishi kwamba yupo vibaya coz zipo sababu nyingi zilizomfanya spate hayo madaraja.
Kwang Mimi sio kigezo cha MTU aliyepata one ama two ndye anaweza kuamisha hizo skills kwa mwanafunz ili nae spate hayo maharaja.
 
unachoongea hata mimi nakubaliana nacho, kwenye Chemistry O level tulikuwa na mwalimu aliyefaulu na alikuwa na jitihada za kufunsisha alianza na sisi toka tukiwa form two mpaka tunamaliza form four, matokeo yetu katika wanafunzi 42 'F' zilikuwa mbili tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu aliye pata division one na two anazo mbinu za kufauru mtihani, mbinu za kufauru mtihani hatusomei chuoni, mbinu za kufauru mtihani anazo yule mwalimu aliye fauru mtihani huo. Tutumie walimu wenye ushuhuda


kumbe nawewe ni kilaza! siyo kufauru ni kufaulu
 
mshauri kwanza mama ako apunguze kuzaaa haya mengine naona yako juu ya uwezo wako!!
Naishauri Serikali yangu iajiri Walimu wenye division two na One kwenye vyeti vyao vya kidato cha nne (olevel) na kidato cha sita (Alevel) kwenye shule zetu za Serikali, kwa sababu Walimu hawa ndio wenye mbinu za kujisomea na kufaulu mtihani. Ikiwaajiri hao watawapatia Wanafunzi wetu mbinu za kujisomea na kufaulu mitihani.

Naishauri pia Serikali yangu ijaribu kuwachukua Wahitimu wa vyuo vikuu walio somea fani mbalimbali walio faulu vizuri kidato cha nne na sita (division 2 na division 1) wakafundishe shule za Serikali kwa sababu wanazo hizo mbinu za kujisomea na kufaulu mtihani. Wawalipe mshahara ule ule wa kawaida.

Ili Serikali iweze kushindana na shule za binafsi (private) iajiri Walimu wenye uwezo (competent teachers), ambao kiukweli kuwapata ni ngumu sana katika kada ya ualimu, wanafunzi wengi wanao somea ualimu ni wale wenye ufaulu mdogo (division three).

Mimi ningelikuwa Mwalimu wa Serikali Mwanafunzi wangu asingepata F, kwenye somo langu, kwa sababu Serikali huwa inachukua wanafunzi walio faulu sana mtihani wa darasa la saba, kinacho tokea ni kwamba walimu wao ndio wanao waharibu mpaka wanafeli kwasababu walimu wengi kule hawana material kichwani.

Nitoe tu ushuhuda huu kipindi tunafundisha shule moja ya binafsi (private), tulikua tukimpata mwanafunzi anayetoka shule ya serikali kuja shule yetu, tunahesabu hiyo ni A, kwasababu mwanafunzi wa serikali huwa analewa haraka mno akipata mwalimu mwenye uwezo.

Asilimia 90 ya shule za binafsi (private) zinachukua wanafunzi wasio elewa haraka (slow learners) lakini kwasababu wana walimu wenye uwezo (competent teachers), wana wabadili wanafunzi hao wanapata one, na two. Walimu wengi wa private ni wale wenye one na two, katika mitihani yao ya olevel na advance, ni walimu wenye historia fulani ya kujituma kimasomo wakiwa shuleni wanasoma, mwanafunzi mwingine historia tu ya mwalim inatosha kumfaurisha.

Mimi nae ongea nimewahi kufundisha private, na hicho ndicho nilicho kiona. Serikali inatumia walimu walio feli mno, mwalimu aliye feli, huyo maana yake hakuwa na bidii wakati anasoma, kwa hiyo hawezi kuwavisha roho ya bidii wanafunzi wake.

Mwalimu aliye pata division one na two anazo mbinu za kufauru mtihani, mbinu za kufauru mtihani hatusomei chuoni, mbinu za kufauru mtihani anazo yule mwalimu aliye fauru mtihani huo. Tutumie walimu wenye ushuhuda.

Mwalimu aliye pata S au E ya physics au math au chemistry, au history advance huo hana mbinu za kufaulu mtihani, hivyo hawezi mshuhudia mwanafunzi akafaulu mtihani.

Wanafunzi wengine wanapo fundishwa na mwalimu aliye perform vizuri nao wanapata hamasa wanasoma kwa bidii ili wanafaulu.

Ni hayo tu.
Ahsanteni sana
Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa bahati mbaya O level na A level hakuna kozi la strategies za kujisomea haijalishi una one au two.... Hayo yote utayatakuta chuo ukiwa unasomea taaaluma ya ualimu....tafadhali one au two haina msaada kwenye taaluma ya ualimu..... Knowledge base ya mwalimu ndio msingi wa ualimu....
Kama hujaelewa nitakuandikia notes
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom