Nashauri Serikali iajiri Walimu wenye ufaulu wa daraja la kwanza au la pili kwenye vyeti vya elimu ya sekondari(Kidato cha nne na sita)


H

Hashimu lwenje

Senior Member
Joined
Oct 2, 2017
Messages
165
Likes
128
Points
60
H

Hashimu lwenje

Senior Member
Joined Oct 2, 2017
165 128 60
Naishauri Serikali yangu iajiri Walimu wenye division two na One kwenye vyeti vyao vya kidato cha nne (olevel) na kidato cha sita (Alevel) kwenye shule zetu za Serikali, kwa sababu Walimu hawa ndio wenye mbinu za kujisomea na kufaulu mtihani. Ikiwaajiri hao watawapatia Wanafunzi wetu mbinu za kujisomea na kufaulu mitihani.

Naishauri pia Serikali yangu ijaribu kuwachukua Wahitimu wa vyuo vikuu walio somea fani mbalimbali walio faulu vizuri kidato cha nne na sita (division 2 na division 1) wakafundishe shule za Serikali kwa sababu wanazo hizo mbinu za kujisomea na kufaulu mtihani. Wawalipe mshahara ule ule wa kawaida.

Ili Serikali iweze kushindana na shule za binafsi (private) iajiri Walimu wenye uwezo (competent teachers), ambao kiukweli kuwapata ni ngumu sana katika kada ya ualimu, wanafunzi wengi wanao somea ualimu ni wale wenye ufaulu mdogo (division three).

Mimi ningelikuwa Mwalimu wa Serikali Mwanafunzi wangu asingepata F, kwenye somo langu, kwa sababu Serikali huwa inachukua wanafunzi walio faulu sana mtihani wa darasa la saba, kinacho tokea ni kwamba walimu wao ndio wanao waharibu mpaka wanafeli kwasababu walimu wengi kule hawana material kichwani.

Nitoe tu ushuhuda huu kipindi tunafundisha shule moja ya binafsi (private), tulikua tukimpata mwanafunzi anayetoka shule ya serikali kuja shule yetu, tunahesabu hiyo ni A, kwasababu mwanafunzi wa serikali huwa analewa haraka mno akipata mwalimu mwenye uwezo.

Asilimia 90 ya shule za binafsi (private) zinachukua wanafunzi wasio elewa haraka (slow learners) lakini kwasababu wana walimu wenye uwezo (competent teachers), wana wabadili wanafunzi hao wanapata one, na two. Walimu wengi wa private ni wale wenye one na two, katika mitihani yao ya olevel na advance, ni walimu wenye historia fulani ya kujituma kimasomo wakiwa shuleni wanasoma, mwanafunzi mwingine historia tu ya mwalim inatosha kumfaurisha.

Mimi nae ongea nimewahi kufundisha private, na hicho ndicho nilicho kiona. Serikali inatumia walimu walio feli mno, mwalimu aliye feli, huyo maana yake hakuwa na bidii wakati anasoma, kwa hiyo hawezi kuwavisha roho ya bidii wanafunzi wake.

Mwalimu aliye pata division one na two anazo mbinu za kufauru mtihani, mbinu za kufauru mtihani hatusomei chuoni, mbinu za kufauru mtihani anazo yule mwalimu aliye fauru mtihani huo. Tutumie walimu wenye ushuhuda.

Mwalimu aliye pata S au E ya physics au math au chemistry, au history advance huo hana mbinu za kufaulu mtihani, hivyo hawezi mshuhudia mwanafunzi akafaulu mtihani.

Wanafunzi wengine wanapo fundishwa na mwalimu aliye perform vizuri nao wanapata hamasa wanasoma kwa bidii ili wanafaulu.

Ni hayo tu.
Ahsanteni sana
Mungu ibariki Tanzania.
 
M

mbuyamore

Member
Joined
Oct 25, 2018
Messages
17
Likes
12
Points
5
M

mbuyamore

Member
Joined Oct 25, 2018
17 12 5
Hashimu lwenje,

Una div two unaandika upupu wa aina hii. Tambua kwanza hao waliosomea ualimu ndio hao wanaofundisha shule za private unazosifia na wengine wanafundisha part time private wakiwa wameajiriwa serikalini.

Kama hujui pia kuanzia mwaka 2015 sifa za kujiunga ualimu zimebadilika, diploma na certificate ya ualimu unaingia ukiwa na div one hadi three pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gwankaja

gwankaja

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Messages
3,660
Likes
3,983
Points
280
gwankaja

gwankaja

JF-Expert Member
Joined May 16, 2011
3,660 3,983 280
Uko sahihi ila wale waliochemka kupata div 1 na 2...watapinga!!
 
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
8,835
Likes
10,912
Points
280
Age
27
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
8,835 10,912 280
Mbona mwenye division four haruhusiwi kusomea Ualimu level ya Certificate na Diploma.

Kama huamini cheki guidebook ya level ya Diploma na Certificate kwenye kusomea Ualimu
Wanaruhusiwa mkuu. Check qualifications. Wanataka five passes na kuendelea. Haijalish una division gan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Messages
4,909
Likes
3,590
Points
280
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2015
4,909 3,590 280
Hapo uliposoma kwenye four passes umeona kuna Education(Ualimu).
Hata zamani kada zingine ilikuwa four passes ila Ualimu ilikuwa mwisho division four ya 28(yaani Seven passes) sasa wewe sijui umeona wapi?

Mimi naweza kuleta ushahidi hapa hakuna mtu anasomea Ualimu kama hana division one hadi three.
Kwa kada zingine zote ni four passes.
Wanaruhusiwa mkuu. Check qualifications. Wanataka five passes na kuendelea. Haijalish una division gan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Messages
4,909
Likes
3,590
Points
280
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2015
4,909 3,590 280
Wewe ni mtu mbishi tu,uliza au lete ushahidi kupitia Guidebook ya Certificate na Diploma ya Ualimu.
Nitakupa list ya vyuo wanavyofanya hivyo. Si uwongo. Akiwa na cheti na hizo marks o level anaingia diploma. Kuna vyuo vinafanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Messages
4,909
Likes
3,590
Points
280
Madihani

Madihani

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2015
4,909 3,590 280
Nitakupa list ya vyuo wanavyofanya hivyo. Si uwongo. Akiwa na cheti na hizo marks o level anaingia diploma. Kuna vyuo vinafanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiwezekani kwa Diploma in Education.(Lazima one hadi three).
Labda unaongelea Diploma zingine
 
A

Aspatam

Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
47
Likes
30
Points
25
A

Aspatam

Member
Joined Oct 26, 2018
47 30 25
kuelewa kitu kunatokana na utayari wa mjifunzaji..afu pia mwl habebi maarifa aliyo nayo na kuyaingiza kichwan mwa mjifunzaji bali anamuwezesha mjifunzaji kuelewa ..
 
E

E and E

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Messages
572
Likes
405
Points
80
E

E and E

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2017
572 405 80
Mkuu mdogo wangu ana division 3 lakini kwenye hesabu B physics B je huyu nae pamoja na three yake ni kilaza?
 
1SKY

1SKY

Member
Joined
Aug 1, 2018
Messages
49
Likes
23
Points
15
1SKY

1SKY

Member
Joined Aug 1, 2018
49 23 15
Kwa wanaofuatilia mpira kidogo mfano Alex Ferguson ajawahi kushinda Uefa akiwa mchezaji lakini amefanya maajabu akiwa kocha Thierry Henry aliwahi kushinda Uefa akiwa mchezaji ila kwenye ukocha chali.
Kujua mbinu za kusoma ni tofauti na kujua mbinu za kufundisha.(japo unaweza ukajua zote mf Zidane)
Mtu anaweza kujifunza zaidi katika kufeli kuliko kufaulu.
Mi nadhani njia pekee ya kupata walimu bora ni kuwa na namna ya kuwapima uwezo (kama interview kabla ya kuajiriwa)
 
M

Mashona

Member
Joined
Sep 18, 2018
Messages
76
Likes
122
Points
40
M

Mashona

Member
Joined Sep 18, 2018
76 122 40
Nimechoka sana baada ya kusoma andiko la mtoa HOJA, nakumbuka mwaka 2004 nilipohitimu kidato cha nne baada ya kutoka matokeo ya kidato cha nne nilienda kuangalia matokeo husika katika shule ya sekondari AZANIA

Kwa wale waliosoma na kahitimu kidato cha nne miaka hiyo watakumbuka mfumo huo wa kuangalia matokeo, tulipofika pale na baada ya kuangalia matokeo kwenye mlango wa kutokea kulikuwa na walimu wanne wa Shule ya FEZA BOYS walikuwa wanauliza umepata division gani kwenye matokeo yako ukiwambia una division three au two walikuwa wana kwambia Kwa heri

Ila kwa wale waliokuwa na division one walikuwa wanachukua information zako na kukuahidi kwamba kuna shule yetu tunataka kuianzisha tunaomba mawasiliano ya mzazi /mlezi wako kwa ahadi ya kusomeshwa bure kwenye shule yao na ni kweli waliwachukua wanafunzi wengi wenye ufaulu wa division one na matokeo ya kidato cha Sita ya mwaka 2007 ambayo ndo yalikuwa ya kwanza kwa shule hiyo yalikuwa mazuri sana na ndiyo yaliyoiweka kwenye RAMANI ya ubora wa shule hiyo, hivyo dhana kusema kwamba shule za PRIVATE inachukua wanafunzi wasio na uwezo sio sahihi kabisa
 
free lander

free lander

Member
Joined
Nov 7, 2018
Messages
87
Likes
56
Points
25
free lander

free lander

Member
Joined Nov 7, 2018
87 56 25
I think swala la kufeli sio la walimu peke yake,

mie naona mazingira yanachangia,

boresha mazingira ya shule za serikali utaona matokeo chanya,

boresha maabara,

ongeza vitabu

,punguza kazi za shule kama kilimo

wanafunzi wa concentrate na masomo peke yake.

.utapata positive results

...mimi ni mmoja ya watu nisioamini uwezo wa kiakili ni unarithishwa,

mie naamini MAZINGIRA yakiboreshwa mtoto wa shule za kata ana uwezo sawa na wa Marian Boys...
Bado na stress za nyumbani na mtaani, kufaulu pia ni kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
free lander

free lander

Member
Joined
Nov 7, 2018
Messages
87
Likes
56
Points
25
free lander

free lander

Member
Joined Nov 7, 2018
87 56 25
Ndugu, wewe unayesema ukipewa wanafunzi uwafundishe hawatopata "F" haujui kuandika kwa ufasaha, umerudia kuandika kimakosa neno "faulu" kwa kuliandika "fauru", ziada umerudia kuvunja neno moja na ukatoa mawili mara kadhaa " nae ongea" badala ya "ninayeongea" (wanapo fundishwa=wanapofundishwa), na umeunganisha maneno mawili kutengeneza moja "kwasababu" badala ya "kwa sababu"..
Hayo ni kwa uchache sana, hivyo basi wewe nawe yakustahiki kuwa katika hilo kundi la walimu wasio na weledi na kwa ukweli mweupe na mweusi wewe haustahili kuwa mwalimu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanajiitaga walimu wa sayansi na namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
free lander

free lander

Member
Joined
Nov 7, 2018
Messages
87
Likes
56
Points
25
free lander

free lander

Member
Joined Nov 7, 2018
87 56 25
I agree with you...

Walimu walipaswa huwa na payscale sawa na majudge!

yes walitakiwa walipwe Zaidi...

hii ingewa attract watu makini, wenye uwezo mkubwa kufundisha na wenye uwelewa kubwa,in terms of qualifications,...

sio kama sasa hivi,ualimu ni kwa wale failures ,,,ni kama label vile,ukichukua ualimu inaonyesha Marks zako huko nyuma zilikua kwa mbinde...

yaani katika jamii yetu uwalimu=failure in academic achievement.

we have to change this attitude,

ba tutafanya hivyo pale ambapo walimu watapewa mishahara inayostahili,na pale ambapo Fani ya uwalimu imefanikiwa kuchota walimu ambao wako competent,wana qualifications sawa na profession nyingine kama doctor,lawyer etc

Serikali ibadilishe vigezo vya kuombea uwalimu,waweka tighter system,waliofaulu tu ndio waruhusiwe kufundisha
Hata maslahi yakiongezwa tatizo litabaki kuwa stereotyping, walimu wanachukuliwa kama watu waliofeli ila walimu waliopata I & II wapo wengi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ze Heby

Ze Heby

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2012
Messages
4,251
Likes
2,487
Points
280
Ze Heby

Ze Heby

JF-Expert Member
Joined May 20, 2012
4,251 2,487 280
Ulichokisema ni kweli

Mwanafunzi gani aliepata one alieenda kusoma ualimu kwa mapenzi yake mwenyewe?

Ni aidha,alikua anataka mkopo au alikosa kozi alizozipenda
Sema utapingwa sana lakini ilitakiwa iwe MWIKO kwa mwanafunzi mwenye 3 na kushuka chini kusomea ualimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,274,286
Members 490,649
Posts 30,507,316