Hongera idara ya elimu sekondari halmashauri Bunda kwa mabadiliko ya mtihani wa mock kidato cha pili na kidato cha nne

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
200
431
Hii sasa ndio mikakati madhubuti ya kuinua kiwango cha ufaulu katika halmashauri.Hili jambo lina mana gani kwa walimu na wanafunzi?

Tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma ambapo mtihani wa ukamilifu (mock) ulikuwa unafanyika kati ya mwezi may au agosti ambapo miezi ya awali wanafunzi hawakuweza kujisomea ipasavyo na hata baadhi ya walimu kutofundisha kwa nguvu zote ambapo ni tofauti na mwaka huu ambapo ufundishaji wa nguvu umeanza katika mashule mbalimbali tangu zianze kuenea taarifa za awali kwamba mtihani wa mock kwa vidato vyote viwili.

Kwa hili nawaunga mkono mkono, kikubwa ni kuhakikisha tu mtihani unakidhi tu vigezo vyake vyote husika, validity na reliability!Kwangu mimi Kwa hili nawapa 💯.
 
Back
Top Bottom