Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 44,310
- 105,133
media inawanafki wengi at least saizi wamepunguzaNyie akili kubwa si mnasemaga hamsikilizi redio, media house ni biashara hivyo wengi wape!
hip hop ni wanamziki wasio shoboka na promo (hapa simzungumzii lunya)
kuna kipindi nikki aliwachana wale majamaa walikua wanajiita wakali wa media yani wao ndio wanao request ngoma za wasanii, tena kunawatu mpaka waliajiriwa hadi kwenye kitengo cha wakali wa media yani zile meseji za request zilikua zinapitia kwao
yaani hao ndio walikua wanachagua ngoma gani ipigwe ipi iachwe, kuna ngoma hata kama imeombwa mara nyingi ila kwasababu zao binafsi hawaipigi
kunawatu walikua wana request ngoma za kina nikki mbish, nash na wasanii wengine wa tamaduni
kuna jamaa mmoja alishawahi kupewa makavu na nikki anaitwa evans chua, huyu mwamba alikua ana request kazi za nikki mbishi sana. Sasa kuna siku jamaa akamuibukia nikki kwamba ampe mtonyo ili aendelee kugonga nyimbo zake
Nikki akamchana akamuuliza "hizi ngoma una request kwa mapenzi tu au mimi nilishawahi kukuomba uwe unazi request" jamaa akasema "hamna bro mbona wakina madee wanafanya hivyo mbona fresh"
Kumbe machizi wakitoa ngoma wanatenga kibunda kwamba huyu anashikishwa buku 10 ya vocha ili kuhakikisha ndani ya week ngoma ishakua hit na baada ya wiki mbili ngoma inakua ishakua hit inajitegemea yenyewe hapo haina haja ya ku request ishaingia kwenye rotation