Bado ni mwaka mpya maana hata watoto hawajaenda shule bado.
Pamoja na yote natambua juhudi na kazi kubwa inayofanywa na rais wetu mpedwa mama Samia kwa kuhakikisha usalama wa nchi na kuifikisha Tanzania sehemu fulani.
Kwa sehemu yangu nakupongeza sana mama na hiyo inathibithisha kuwa kweli mama zetu mnaweza. na wale ambao wamefikia mahali kuachia ngazi za juu za uongozi nao pia nawapongeza maana wametumia haki yao kikatiba bila kuharibu amani ya nchi yetu maana amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko mtu mmoja au nafasi walizonazo.
Pamoja na yote mimi kama mwananchi wa chini kabisa huku ambaye natafuta mkate wangu jua kali kwa maana ya machinga na kibarua. ni ombi langu kuu, kwamba kwa vile mwaka umeanza hivyo naamini kutakuwa na ratiba ya kiserikali ya kumbukizi ya aliyekuwa rais wa awamu ya tano ambaye kwa sasa ni marehemu.
Napendekeza kumbukizi hiyo ifanyikie Chato palepale alipolazwa lakini pia uwepo utaratibu wa uhuru wa watu kutoa maoni yao ya hisia bila kupigwa kwa njia yoyote ile hasa ya mabango na vyombo vya habari visichuje habari.
Yaani kuwe na maandamano ya amani kwa wale wote tutakaoweza kufanya maandano hadi eneo litakalotengwa kupokelewa maandamano hayo.
Moja kati ya hisia zangu ni pamoja na kutaka kujua marehemu aliwezaje kudhibiti mfumko wa bei kama mafuta, sabuni na chakula hali ambayo kwa sasa ni kama imekuwa ni kama imeshindikana.
lakini pia hisia zangu nitaonesha, marehemu aliweza kumudu kuwacha machinga mjini na bado mambo yakaenda sawa tu hali ambayo kwa sasa limepita fagio la kata mtaji na kuyumbisha watu hao kwa kuwahamisha hali yeye marehemu aliweka usawa.
Mwisho naamini kuwa watu wengi wanaweza kuwa na mambo mengi ya kumkumbuka marehemu hivyo kupitia maandamano hayo kila mmoja anaweza kutoa hisia zake kama sehemu ya kumkumbuka marehemu.