Napendekeza siku ya Kumbukizi ya Hayati Magufuli tuandamane na mabango hadi kaburini ili kuhiji na kuonesha hisia zetu

Kweli ukiwa mnyonge na akili yako inajaa unyonge.
Kama US, China na Russia vitu vimepanda bei huku bongo kwanini visipande?
Jambo jingine ni kwamba akili yako Haina akili unawaza umachinga tu badala ya kuwaza mbali. Sheria ziliwekwa na ndizo Samia kazifuata, hairuhusiwi kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi kibiashara.
Magufuli aliwatumia nyie wajinga kujizolea umaarufu.
Angekuwa na nia njema angefuta zile sheria mnazohisi haziko sawa maana alikuwa na authority hiyo.
Alikuwa anawainjoi tu.
Mbona kuna sheria nyingi alizibadili ili aendelee kubaki madarakani kiurahisi?
Kwa ufupi wewe ni lofa,
Nadudia wewe ni lofa
Lofa
Jipige kifua, sema mimi ni lofa
 
Mfumuko wa bei ni janga.

Tuache hayo nina swali nje ya mada.
Huku mitaani hakuna soda ya Pepsi nasikia tatizo ni kukosekana kwa sukari.

Tetesi ni kuwa kuna upungufu mkubwa wa sukari ya viwandani na ya majumbani.

Hii habari ni ya kweli? Kama ndivyo serikali inamkakati gani kutatua tatizo?
Kama kiwanda kikubwa kimeshindwa kuagiza nje sisi inatuhusu nini? Mpaka stock inaisha mmekaa tu kusubiri samia abebe migunia kuwaletea hapo kiwandani?
 
Kwa hiyo unataka kwenda na mabango kaburini kwa Rais aliye mfu, lakini huna nia ya kwenda na mabango ikulu kwa Rais aliye hai....!!!
 
Shangazi yako amekopa trillion 10 ndani yamiezi sita ili kujengea matundu ya choo kenge wewe.
Watanzania tunashida ya kufikiri kwa kutumia mihemko.Hayati Magufuli alikopa akanunua ndege,akajenga flyover, akajenga SGR,akajenga Bwawa la Nyerere .huwezi kulinganisha na anayekopa kujenga madarasa na kujenga vyoo ili watoto wa kike wakipata mimba waendelee kusoma mfumo rasmi.unless kama kodi zetu zinaenda kumalizia miradi mengine yenye tija kwa taifa
 
Huku jimbo jirani kabisa na kaimu ardhi hatuna maji siku ya tatu leo.

Huku umeme tena ni majaliwa washa zima imezidi.

Hatukuyaona haya enzi za Magufuli, Ila kaburini kwake siwezi kwenda nendeni nyie vijana

Ijapokuwa wengine alituumiza ila sasa tunaumia zaidi.
Swala la umeme ni ukame ndio chanzo hilo ndilo jibu sahulihi , ukame wa sasa hakuwahi tokea tangu 2015
 
Mfumuko wa bei ni janga.

Tuache hayo nina swali nje ya mada.
Huku mitaani hakuna soda ya Pepsi nasikia tatizo ni kukosekana kwa sukari.

Tetesi ni kuwa kuna upungufu mkubwa wa sukari ya viwandani na ya majumbani.

Hii habari ni ya kweli? Kama ndivyo serikali inamkakati gani kutatua tatizo?

We nyumbani kwako hamtumii sukari mpaka usikie kwa jirani?
 
Watanzania tunashida ya kufikiri kwa kutumia mihemko.Hayati Magufuli alikopa akanunua ndege,akajenga flyover, akajenga SGR,akajenga Bwawa la Nyerere .huwezi kulinganisha na anayekopa kujenga madarasa na kujenga vyoo ili watoto wa kike wakipata mimba waendelee kusoma mfumo rasmi.unless kama kodi zetu zinaenda kumalizia miradi mengine yenye tija kwa taifa
Yaan hapo wewe ndio unajiona huja hemka!? Basi we nawe ni tatizo

Unashangaa kujengwa madarasa kwa hiyo ulitaka watoto waendelee kukaa 200 kwa darasa moja?
 
Bado ni mwaka mpya maana hata watoto hawajaenda shule bado.

Pamoja na yote natambua juhudi na kazi kubwa inayofanywa na rais wetu mpedwa mama Samia kwa kuhakikisha usalama wa nchi na kuifikisha Tanzania sehemu fulani.

Kwa sehemu yangu nakupongeza sana mama na hiyo inathibithisha kuwa kweli mama zetu mnaweza. na wale ambao wamefikia mahali kuachia ngazi za juu za uongozi nao pia nawapongeza maana wametumia haki yao kikatiba bila kuharibu amani ya nchi yetu maana amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko mtu mmoja au nafasi walizonazo.

Pamoja na yote mimi kama mwananchi wa chini kabisa huku ambaye natafuta mkate wangu jua kali kwa maana ya machinga na kibarua. ni ombi langu kuu, kwamba kwa vile mwaka umeanza hivyo naamini kutakuwa na ratiba ya kiserikali ya kumbukizi ya aliyekuwa rais wa awamu ya tano ambaye kwa sasa ni marehemu.

Napendekeza kumbukizi hiyo ifanyikie Chato palepale alipolazwa lakini pia uwepo utaratibu wa uhuru wa watu kutoa maoni yao ya hisia bila kupigwa kwa njia yoyote ile hasa ya mabango na vyombo vya habari visichuje habari.

Yaani kuwe na maandamano ya amani kwa wale wote tutakaoweza kufanya maandano hadi eneo litakalotengwa kupokelewa maandamano hayo.

Moja kati ya hisia zangu ni pamoja na kutaka kujua marehemu aliwezaje kudhibiti mfumko wa bei kama mafuta, sabuni na chakula hali ambayo kwa sasa ni kama imekuwa ni kama imeshindikana.

lakini pia hisia zangu nitaonesha, marehemu aliweza kumudu kuwacha machinga mjini na bado mambo yakaenda sawa tu hali ambayo kwa sasa limepita fagio la kata mtaji na kuyumbisha watu hao kwa kuwahamisha hali yeye marehemu aliweka usawa.

Mwisho naamini kuwa watu wengi wanaweza kuwa na mambo mengi ya kumkumbuka marehemu hivyo kupitia maandamano hayo kila mmoja anaweza kutoa hisia zake kama sehemu ya kumkumbuka marehemu.
Au muandamane mpaka ahera kabisa, na msirudi kabisaa! #kulenyai
 
R.I.P Magu...kifo hakichagui nyie wapambe wake kama mnataka kumfuata aliko nafikiri mmechagua njia sahihi coz hata Magu angekua hai angewafanyia hivyo coz alikua hapendi maandano.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom