Nape, naamibi unajua kwamba JF ni chombo kikubwa sana cha habari ambacho mtu anaweza akatoka au akaangamia kutoka alipo ikitegemea na jinsi anavyoichukulia.
Bila kujalisha kama ni kweli hauna kadi au kama unayo, me nadhani hoja iliyoletwa ni rahisi sana na ambayo ina majibu mafupi tu, (1) Ni kweli sina kadi (2) Nina kadi ya ccm namba xxxx tawi la xxx ya mwaka xxx ili watu wanaokuonea wivu Mheshimiwa sana Nepi waone walipokosea.
Lakini kitendo cha wewe kujichekesha katika hoja nzito kama hii ambayo binafsi nimeacha hadi kufanya kazi nikitafuta uthibitisho wake, umenisikitisha sana, sijui kama hii username ni yako au kuna mtu amejibu kwa niaba yako. Sitaki kuamini kama kiongozi mwenye nafasi kubwa ktk chama ya uenezi anaweza akajichekesha katika hoja nzito kama hii, unataka wanachama wako wa ccm waelewaje na wale wa chadema wasemaje?
Watch your words Nepi, usipokaa makini, JF itakutoa ktk nafasi uliyonayo, sipendi tu kuwa mtabiri.