Nape asusia kikao cha CCM

Nape asusia kikao cha CCM

CCM ya sasa kila mtu ni msemaji wa mwisho chamani.

Ugonjwa wa saratani ya rushwa ikishapenya kwenye uongozi wa juu chamani ndio kama hivo heshima kutoweka kabisa na kila mtu kuenenda tu na lwake. Nasema mwenyekiti asiyejiheshimu kabisaaa hana tofauti hata kidogo na baba mtu mzima mwenye mji wake lakini bado ni LIKOJOZI KITANDANI.

Hata hivyo, mambo ya mafisadi tuwaachie magamba wenyewe watajiju ila ndio kama hivo wananchi tumeshaelewa wote hadi mwenyekiti wao wa taifa na unafiki wake unavyokua ni zaidi ya mzigo wa misumari ya moto kwa sehemu kubwa ya wanachama wake na uvundo huo huo sasa kusambaa nchi nzima.

Kiongozi yeyote akiwa ni kigeugeu mbaya sana, ila akiongezea na tabia wizi na uporaji wa mali ya umma kama hivi sasa hadi hapo havumiliki tena!!


ndugu Nape alitaka kufanya press conference na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC lakini alizuiwa na wakubwa wa CHAMA kuwa hakuna haja hali iliyopelekea Nape kususia kikao cha viongozi wa Chama na habari zaidi nilizopata ni kwamba amerejea Dar mapema zaidi hata kabla ya wenzie kutawanyika.
 
This is rather sad; hivi kweli tatizo la CCM ni NAPE. As a matter of fact Nape angepewa pongezi na kuungwa mkono na wana CCM wanaotaka mabadiliko ya kweli. Alichokifanya Nape hadharani hakijawahi kufanywa na kionogozi yeyote wa CCM. Wengi wa wale wanaojiita viongozi au wanajionesha kuwa niviongozi hawajawa na ujasiri wa kusimama na kuiita limau limau na chenza chenza! Tangu mwanzo wa sakata hili sikuwahi kusema lolote juu ya Nape lakini ukweli ni kuwa Nape amefanya kilichowashinda wengi na kama aliamua kuondoka kwenye vikao vyao pia ni uamuzi wa akili kwa sababu kwanini watu wakae mahali ambapo hawawezi kusimamia walichokisea. Kama watu wote wenye nguvu Tanzania wanakutanika kwenye chumba kimoja halafu wanashindwa kuchukua uamuzi ambao wanajua walipaswa kuukua bado wanaonekana wamefanya la maana?

Hivi kweli mnataka kusema ndani ya kundi zima la watu wa Kamati Kuu na NEC hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wakujibu hoja zinazodaiwa kutolewa na Lowassa, really? Nape hata akijiuzulu kesho, atakuwa amejionesha kuwa amethubutu kufanya kilichomshinda fisi.

Kaka unaweza kusema Nape ni kijana aliye jitahidi na labda wapenda mabadiliko ndani ya CCM wangempongeza. lakini uthubutu wake ulikuwa ni dhaifu na wa kukurupuka ninasema hivi kutokana na maelezo yafuatayo

EL alituhumiwa na tume ya akina mwakyembe, na hata baadae akajiuzulu kutoka ktkt nafasi yake. tangu kujiuzulu kwa EL, zaidi ya uchunguzi wa akina mwakyembe, hakuna chombo cha maadili ndani ya CCM kiliwai kumchunguza au kumhoji EL kuhusiana na utendaji wake mbovu kuhusiana na richmond, kumbuka ushahidi wa kwanza wa sababu za kumhoji ingekuwa ni ripoti ya richmond ambayo ipo bungeni. EL alijaribu kukanusha juu ya ushiriki wake wa moja kwa moja ktk richmond. lakini watendaji wa kuu wa CCM walikaa kimya. mpaka pale wapinzani walipoendelea kuzomea hayo maovu ya richmond wakitaka serikali iwaadhibu viongozi waliohusika na richmond, ndipo serikali ikaona iwa "fool" wananchi kwa kuhamisha hii kitu na kupeleka kwenye chama but this deliberately with "surface actions". kwakuwa ilikuwa ni "surface" ndiyo maana chama hakikutaka kuchunguza tuhuma zilizo mkabili EL, badala yake chama kikawa kinaongea na EL na wenzake kupitia media.kwasababu kilichokuwa kinafanyika kilifanyika kwa makusudi, na Nape ametumiwa kwenda kuongea mtaani juu ya kuvua gamba-yeye akidhani amepewa heshima kumbe anadhalilika. hata ungekuwa wewe kaka Mwanakijiji, usingejivua madaraka ndani ya chama , pasipo kusomewa mashtaka na hatimaye hukumu. El hajawai somewa mashtaka na chama, kwanini ajidhalilishe kwa kuachia ngazi?. nae Nape leo akiambiwa atoe ushaidi wa makosa ya EL, na adhabu anayostahili ndani ya chama kwa mujibu wa taratibu za chama anaweza kutoa?.
ninamwona Nape ni kijana dhaifu na asiye makini, huwezi kujenga maadili ya chama kwa kuzungumza kwenye media eti kisa wewe katibu mwenezi, haiwezekani . tuwe wakweli, Kaka Mwana kijiji unafahamu mgogoro wa ndani ya Chadema wakati ule wa uchaguzi, wakati Mh. Kabwe anataka kugombea uenyekiti, si uliwaona walivyo handle mambo yao?walikuwa wanalopoka ovyo kama hiki chama chetu CCM?. nape hana tofauti kubwa na yule katibu wa CCM aliye staafu juzi hajui anachokifanya. I would expect a creative and innovative Nape, one whose thinking is based on logic and not intuition!. nasema hivi kwasababu ktk mahubiri ya magamba , Nape alikuwa anatumia hisia na siyo logic. EL aliyafahamu mapungufu yote yaliyopo ktkt kushughulikia tuhuma zake. na sasa EL anatumia u mbumbumbu wa Nape kutafuta kufuta ukweli wa tuhuma zake.
kwenye NEC kusingepatikana mtu wa kumpongeza Nape kwakuwa wanajua Nape anatolewa sadaka, aidha walishafahamu hilo siku nyingi. lakini lililo kubwa ni kuwa hawana nia ya mabadiliko, CCM inalelewa na vyombo vya dola na siyo mission yake kwa wananchi.

kumbuka nilikwambia pasipo na kiongozi makini , hali haiwezi tulia. Jambo laweza kuibuliwa na yoyote, lakini kiongozi lazima awe na uwezo wa kulimaliza na kulifunga, hatimaye kuendelea na mengine. mpaka sasa mgogoro wa makundi na magamba una gharimu CCM, kumbuka migogoro hii inatumia pesa,inatumia muda, wanakaa vikao kujadili yasiyoisha, hawana muda wa kujenga chama, hawana muda wa kupanga maendeleo, na wao ndo "wameshika hatamu" – na nchi yetu haiwezi kuendelea
 
Nape amekumbana na tatizo lile lile ambalo wengine tumeliona muda mrefu uliopita - CCM haibebeki, haikoleki na mtu yeyote anayejaribu kuiokoa anaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa zaidi. Kwa sababu tazizo la CCM ndani ni zaidi ya watu (personalities) na ni zaidi ya maslahi (interests) na kwa kweli kabisa ni zaidi ya matamanio (ambitions). Tatizo lake limefungamana moja kwa moja na tunu, mitazamo, na itikadi ya Chama. Haiwezekani kuisafisha CCM bila kugusa huku. Ndio maana mwisho wa siku naamini kama Nape aliyoyoasema aliamini yalikuwa sahihi na kuwa alikuwa anasimamia maamuzi sahihi ya Chama na dhamira yake ikimthibitisha anabakiwa na uchaguzi mmoja tu - kutoka kwa heshima.
 
Nape amekumbana na tatizo lile lile ambalo wengine tumeliona muda mrefu uliopita - CCM haibebeki, haikoleki na mtu yeyote anayejaribu kuiokoa anaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa zaidi...

... Ndio maana mwisho wa siku naamini kama Nape aliyoyoasema aliamini yalikuwa sahihi na kuwa alikuwa anasimamia maamuzi sahihi ya Chama na dhamira yake ikimthibitisha anabakiwa na uchaguzi mmoja tu - kutoka kwa heshima.



Mkuu,
Naheshimu sana mawazo yako. Hasa pale uliposema kuwa hukuwahi kuzungumzia kuhusu Nape.

Ukweli upo wazi. Ccm haiwezi kubadilika na haiwezi kubadilika kabisa pale anayeongoza mabadiliko anapokuwa ni kijana. Nape alieelezwa hayo tangu awali. Akaishia kujibu wanaomtahadharisha kwa mipasho na taarab. Leo yamemkuta. Alikuwa anahubiri mafisadi wajivue gamba (kitu ambacho wapenda mabadiliko/maendeleo tunakikubali) leo yeye ndiye anatakiwa kuvuliwa gamba. Laiti angesikia sauti zilizokuwa zinamshauri, leo yasingemkuta!

Sasa anatakiwa kufanya maamuzi magumu. Aondoke kabisa kwenye hicho chama maana imedhihirika kwamba wana mtazamo tofauti. Hiyo ndio njia pekee itakayomrudishia hesima yake kisiasa. Otherwise atapotea kabisa kwenye ulingo wa siasa na anayoyaamini yatakuwa yamekufa nae!
 
Nilishawahi kusema humu ndani ya JF kuwa watanzania bado hawajawa huru na bado tunapigania demokrasia. Ukiisaliti demokrasia ya Tanzania especially kwa miaka hii, na yenyewe pia itakusaliti. It's just a matter of time Nape atadai kuwa ni victim...watch.
I'm prepared to be corrected.
 
Hamu sina wana jf kumbe wengi wenu Nape alikuwa akiwaboa sana hasa anapomtaja EL?
 
Kwa wenye negativity dhidi ya Nape pasipo kujali UKWELI [REALITY] ya mwenendo mzima wa Matendo ya CCM dhidi ya TAIFA hakika subilieni TUTAWATAFUTA KUWAKUMBUSHA MANENO YENU HUMU NDANI, ILI MKANE MLICHOONGEA MSISAHAU MANENO YA MTOTO WA BABA WA TAIFA KUWA RACHEL NINI?

Mheshimiwa Mwenyekiti sina tatizo na kaka Yangu Lowasa lakini ulipomuinua Mkono Uko Monduli site [Wananchi] wakasema HIKI NI NINI?
Mheshmiwa Mwenyekiti nampenda Ndugu yangu Chenge wanamuita Mzee wa Vijisenti hilo Mimi Sina Hakika Nalo ulipomuinua Mkono huko Maswa site [Wananchi] wakasema HIKI NDIO NINI?

Mheshimiwa Mwenyekiti anakotembele Rostam Mimi Nisifiki na Naye afiki Mimi nilipo, ulipomuinua Mkono uko IGUNGA site [Wananchi ] wakauliza HIKi NINI?

Sasa nyie mnaoshabikia PUMBA [Kisa Wanachadema] mnatupa shaka sie tusio wananchama wa chama chochote kweli nyie ni wapenzi wa Nchi.
Tunawasubilia manake kwa wanaojua michezo ya CCM tegemeeni Chochote Kipya wakati wowote.Time will tell.

Mi nna ushauri mmoja tu kwako..jifunze kuandika!!manake ulichokiandika hapo juu hakika hakieleweki..loh!
 
kinyonga.jpg sifa mojawapo ya wana ccm unatakiwa ufanane na huyu kiumbe nape kesho utamusikia
 
Hamu sina wana jf kumbe wengi wenu Nape alikuwa akiwaboa sana hasa anapomtaja EL?

Binafisi sikuwa nakwazika bali nilikuwa ninamuona Nape kama mmoja wa wasanii na waganga njaa ambao wakishapewa ulaji wanatulia na kuanza kuimba mapambio ya kusifia mfumo kwamba ni mzuri sana.

Kila siku huwa ninasema kwamba huwezi ku-isolate ufisadi wa individuals ndani ya CCM kwa kuwa viongozi wengi kama sio wote ni wanufaika wa ufisadi, wameshiriki kwa njia moja au nyingine, ama individually au kama Chama. Ndo maana kesi za EPA zimebaki kuwa ni masimulizi tu na haswa kwa wanufaika waliozipeleka kwenye chama.

Nape alitaka kupata umaarufu kwa "Operation Vua Magamba" sasa naona imegoma. Ili kumuonyesha kwamba uongozi wa CCM ni Gamba Kuu, alipigwa stop na CC asiende Igunga kwenye kampeni na ilihali yule aliyejivua gamba akipewa nafasi ya kushiriki kwenye kampeni. Hilo lilikuwa ni tusi kubwa sana kwa Nape na baada ya hapo alitakiwa kuwa makini.

JK baada ya kuona chati ya CCM imepanda ghafla, alitamka kwamba, "kile anachosema Nape, ni maelekezo yenye baraka kutoka kwenye uongozi wa juu wa CCM". Nape alikuja hapa na kujitapa kwamba tumemsikia Mwenyekiti kwa kinywa chake.

Ili kuonyesha kwamba alikuwa na dhamira ya kweli ya kupambana na mfumo huo aachie ngazi kwa kuwa kile alichokuwa akiwaahidi vijana kwamba amedhamiria kukishughulikia kimemshinda na sasa kibao kinamgeukia. Yeye alikuwa anawatuhumu mafisadi na sasa nao wamemgeuzia kibao kwamba anawapaka matope na kuwatukana.

Nape na akina Samweli Sitta, Mwakyembe, Kilango, Sendeka, Lembeli, Manyanya na wengineo wanaotumia kete ya kupambana na ufisadi, ni wanafiki tu. Hakuna mpambanaji wa kweli ndani ya CCM, wengi wao ni waganga njaa tu na wachumia matumbo.
 
ndugu Nape alitaka kufanya press conference na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC lakini alizuiwa na wakubwa wa CHAMA kuwa hakuna haja hali iliyopelekea Nape kususia kikao cha viongozi wa Chama na habari zaidi nilizopata ni kwamba amerejea Dar mapema zaidi hata kabla ya wenzie kutawanyika.

Namsikitikia ila hayo ndiyo malipo anayopata kwa kutokuwa na akili za kutosha.
 
Kijana alifanya kile alichoamini, na ambacho watanzania wengi wakiongozwa na wapinzani pia waliamini kuwa ndicho kilichoiangusha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kijana aliongea kwa moyo kwa kuamini, na wengi waliamini kuwa ukombozi pekee wa CCM ni kuwaondoa watu ambao wamekuwa wakitumia madaraka waliyonayo kwa manufaa yao binafsi. Kuondoka kwa akina Makamba ilikuwa kama changamoto na ufunuo mpya kwa watu wote walioamini kama ambavyo Nape alikuwa akiamini. Nguvu ya chama na kukubalika kwa chama kwa wananchi na kupunguza nguvu ya upinzani ni kusafisha chama kwa kuwaondoa watu wote waliokipaka chama matope, watu waliosababisha CDM ikawa na nguvu katika uchaguzi wa mwaka 2010, na watu waliosababisha mgawanyiko mkubwa katika kura za maoni mwaka 2010. Kwa wanaoelewa na hata uongozi wa juu wa CCM unakiri kabisa kwamba matatizo yanayokikabili CCM yanatokana kwa kiasi kikubwa na mambo hayo. Sasa kijana alisahau watanzania wengi ni Njaa tu. Nilikuwa nikisoma magazeti kuwa pesa ilitembea, pesa ilitumika, na CCM ni pesa na kwa mwenye nazo CCM ndio mtawala wa Chama. Nape na wenzake walikuwa wanatumia pesa za chama, na hawa wengine wanatumia pesa za nani? Mzee MMJ naafiki na ushauri wako wa mwisho kuwa ndugu huyu ananjia moja tu iliyobakia, je anaweza kuifuata njia hiyo? Ni njia ngumu sana kwa mtu mwenye ndoto za kisiasa. Kuna ndugu zetu waliwahi kufukuzwa CCM sasa ndio hao, they came back, how did they do that? and what do they stand for now? Hata hivyo haki wakati wote huwa inashinda siku za mwisho, tutacheza sana libeneke sasa hivi lakini Chama chochote cha siasa kitashinda kama kitakonga nyoyo za wananchi. Madhumuni ya chama cha Siasa ni kushika dola, na sio rahisi kila wakati yatumike mabavu, ulaghai au njama ili kufikia adhima hiyo, itafikia kipindi CCM wataona umuhimu wa wananchi, hope this will happen before it is too late.
 
Ndio maana mwisho wa siku naamini kama Nape aliyoyoasema aliamini yalikuwa sahihi na kuwa alikuwa anasimamia maamuzi sahihi ya Chama na dhamira yake ikimthibitisha anabakiwa na uchaguzi mmoja tu - kutoka kwa heshima.
Mwanakijiji kutoka CCM kunahitaji uaminifu sifa ambayo sidhani kama Nape anayo, kutoka CCM kunahitaji kuwa jasiri sifa nyingine ambayo sidhani kama Nape anayo, kutoka CCM kunahitaji utulivu wa mawazo sifa ambayo mtu mkurupukaji kama Nape nina hakika hana na kutoka CCM kunahitaji uwajibikaji ambao Nape ameonyesha si mara moja kuwa hata dalili yake hana.

Ndani ya CCM hivi sasa naamini hakuna mtu hata moja mwenye sifa hizo na kama alikuwapo ameshaathirika kiasi cha kupoteza hata kile kiduchu alichokuwa nacho awe kiongozi wa chama, kiongozi wa serikali au mwanachama wa kawaida. Mtu yeyote ambaye anaamini kuwa wakifukuzwa watu wawili watatu, CCM itatakasika hawezi kuwa na hekima ya kutoka CCM kwa heshima.
 
Mkuu,
Naheshimu sana mawazo yako. Hasa pale uliposema kuwa hukuwahi kuzungumzia kuhusu Nape.

Ukweli upo wazi. Ccm haiwezi kubadilika na haiwezi kubadilika kabisa pale anayeongoza mabadiliko anapokuwa ni kijana. Nape alieelezwa hayo tangu awali. Akaishia kujibu wanaomtahadharisha kwa mipasho na taarab. Leo yamemkuta. Alikuwa anahubiri mafisadi wajivue gamba (kitu ambacho wapenda mabadiliko/maendeleo tunakikubali) leo yeye ndiye anatakiwa kuvuliwa gamba. Laiti angesikia sauti zilizokuwa zinamshauri, leo yasingemkuta!

Sasa anatakiwa kufanya maamuzi magumu. Aondoke kabisa kwenye hicho chama maana imedhihirika kwamba wana mtazamo tofauti. Hiyo ndio njia pekee itakayomrudishia hesima yake kisiasa. Otherwise atapotea kabisa kwenye ulingo wa siasa na anayoyaamini yatakuwa yamekufa nae!

Tatizo atoke aende wapi? Shida wengi bongo hatuna option B. Namshauri akomae humohumo apigane kiume na apambane nao kisawasawa vinginevyo atasahaulika kwenye medani za siasa za bongo.
 
Elimu + utashi ni vitu muhimu katika maisha ya leo ya binadam.Hivi ummpa fursa ya kujitambua na kutenda kulingana na hali iliyopo.CC na NEC waliomo wengi aidha wanakosa elimu ama utashi hivyo kutizama matumbo yao pamoja na ombwe la uongozi.

Siamini katika usafi wa Lowassa hata kidogo.Ni nini mtu huyu anachotaka kwetu sisi? Kuwa RAIS? Hapana tunapaswa kumuogopa kama ukoma maake tamaa aliyonayo si dhahiri kwamba ana nia ya dhati kuwatumikia watanzania.Huu ni uchu uliopita kiasi,kwani ali-resign ili atokee mlango wa nyuma? If that is the case hapa kuna tatizo tena kubwa.

Hakuna anayethubutu kuprove kuwa Lowassa ni msafi zaidi ya kudai samaki mmoja akioza uoza wote!Taarifa ya tume ya Mwakyembe ni ushahidi tosha na iwapo anabisha/kupinga juu ya hayo alete utetezi wake against Mwakyembe tume na si bla blaa za kisiasa ili kupata huruma toka kwetu.Typical agenda ili kuwa juu ya hali ya kisiasa nchini,ghafla akaibuka na mambo yake binafsi hundred percent na kusahau juu ya Taifa kwanza huu si ubinafsi ni nini? Eti anajisafisha na kuungwa mkono na wezi wenzake kama Sumaye.

Binafsi naitizama CCM,CC na NEC yake kama wanacheza ngoma wasio ijua.Nadhani ni wakati wa kufa kwake kwani sikio sasa halisikii dawa.Huwezi kutoa maamuzi rahisi rahisi kwa gamba la Lowassa etal.Kamati ya Maadili inauwezo wa kuchunguza madhambi ya Lowassa zaidi ya kamati ya akina Mwakyembe? Au ni njia za kutafuta huruma za kisiasa na kuwapumbaza watanzania.

Hapa sijaafiki juu ya yaliyotokea ndani ya CC na NEC ya CCM, to me its a biggest disappointment i had ever seen na ni fedhea kwa wenye nia njema na chama pamoja na nchi kwa ujumla.Kikwete tuambie juu ya hiyo hidden agenda yako na Lowassa na wala si ''ukigeu geu'' wa huku Nape tuko pamoja (diamond jubilee) upande mwingine Lowassa hatukukutana barabarani.Msingi wa maamuzi magumu si ''kucheka cheka'' kwani body language means a lot.

Ilikuwa muhimu kushughulikia matatizo haya sasa ili kama ni kuvurugana kuonekane mapema na kudhibitiwa before 2015.Ushauri wa jaji Bomani kuwa CCM isubiri uchaguzi wa mwakani ili iweze kujisafisha ni sawa na kutokipa kidonda dawa na kuacha kiendelee kuoza.

Ni dhahiri uchaguzi mwakani ndani ya chama ni timu ya ushindi, hivyo hapa ndipo mafisadi watatumia fedha zao kupanga safu ya kutimiza matakwa yao.Hili ni pigo kwa Chama pamoja na wazalendo wa nchi hii.

Nape simlaumu sana ila nae kajisahau kupita kiasi hasa baada ya kupanda juu.Siku moja nimezungumza nae na nilichokibaini ni kuwa si kiongozi bora na ni kijana tu kwenye upepo wa siasa.Madaraka aliyopewa anayaona ni makubwa kiasi cha kujitenga na vijana wenzake ''eti aliniambia ,kama ni ushauri nataka kumpa nimpe kupitia facebook ama ani assign mtu wa chini yake kwani yeye yuko busy sana''.Huyu ni kijana anayejiita mpambanaji katika dunia ya changamoto kama hii anayedhani ukosoaji ni upinzani tu.

Majibu yake hata humu Jf ni ya kejeli na yasiyoendana na hadhi yake kwa maana ya nafasi aliyonayo.Real ni ya mtaani kabisa.Huyu sina comment sana nae, ngoja asonge kwa silaha aliyonayo uwenda akashinda vita hiyo isiyo na maono.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Saturday, 26 November 2011 07:45[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
gamba-vip.jpg
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, jana, juu ya maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika kwa siku mbili mkoani Dodoma.Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara Pius Msekwa Picha na Edwin Mjwahuzi

CHASEMA KUJIVUA GAMBA,VITA YA UFISADI VIKO PALEPALE

Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM),
kwa mara ya kwanza kimekiri hadharani kuwa mbio za Urais wa mwaka 2015 ni miongoni mwa mambo yanayokitikisa na sasa kinachukua hatua za kuwadhibiti makada wake wenye nia hiyo ili harakati zake zisikiathiri.Kadhalika, CCM kimesema dhana ya kujivua gamba kiliyoiasisi iko palepale na kwamba utekelezaji wake unaanza mara moja kwa kuwachukulia hatua wanachama wake wote wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari jana Mjini Dodoma kuwa si vibaya makada wa chama hicho kuanza kufikiria urais wa 2015 lakini tatizo ni njia ambazo zinatumika katika harakati hizo."Sisi hatuna shida na watu hao kwa kuwa ni haki yao, lakini lazima watumie njia sahihi ambazo hazitaleta shida kwa chama na tumeona iko haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa kupata mgombea urais ambaye hatatokana na fedha isipokuwa akubalike kwa uwezo wake wa kujenga hoja, itikadi yake na kile anachokiamini," alisema Mukama.

Mukama alikiri kuwa mbali na mbio za urais 2015, pia CCM kinateswa na siasa za makundi ambayo yamekuwa yakitumika kushambuliana, kinyume cha maadili yake.Alisema CCM kinachukua hatua za kukabiliana na makundi ambayo misingi yake hujengwa katika chaguzi za ndani ya chama, na kwamba watahakikisha hilo halitokei wakati wa uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika mwakani.

"Kwa maneno ambayo tuliyatumia tulisema, hii kansa ya kupangana safu inaweka mtu ambaye hata sifa wala hana habari kabisa na matatizo ya wananchi, wala haumii lakini anapanga safu… lazima tuondokane na kansa hii ili tupate viongozi wanaojali na wanaohangaika na maisha ya wavuja jasho wa nchi hii," alisema.

Kujivua gamba
Kuhusu suala la kujivua gamba, akimaanisha kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali ukiwemo ufisadi na rushwa, Katibu Mkuu huyo alisema kati ya maazimio 26 yaliyotolewa na NEC Aprili mwaka huu, Azimio namba 27 "linahitaji kutekelezwa haraka iwezekanavyo."

"Dhana hiyo ya kukipatia chama chetu sura mpya ndiyo iliyopewa jina la kujivua gamba na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa imekwishatengeneza mpango wa utekelezaji wa uamuzi huo,'' alisema Mukama.Alisema katika kikao chake kilichomalizika juzi,
NEC imeamua kuwa viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama walipaswa kujipima na kujitafakari wenyewe na ikibidi wachukue hatua jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa.

Alisema Azimio hilo liliwalenga viongozi katika ngazi zote za chama kuanzia taifa hadi tawi na kilichokusudiwa ni kujenga utamaduni wa kusimamia maadili ya viongozi na wanachama wake.

"Takriban miezi saba baada ya Azimio hilo kupitishwa, bado hatujapata mwitikio wa kuridhisha kutoka kwa viongozi wa ngazi yoyote wa chama chetu ambao ni walengwa wa azimio,'' alisema na kuongeza:"Bila shaka sasa wakati umefika wa chama kutekeleza ile sehemu ya pili ya azimio husika kwa kuwawajibisha wahusika, lakini utekelezaji wake hauna budi ufanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa ndani na kanuni za CCM za uongozi na maadili.'

'Msingi wa mpango wa kujivua gamba umejengwa katika azimio la NEC linalosema: "Viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa maslahi ya chama, wasipofanya hivyo, chama kiwawajibishe bila kuchelewa."Lakini tangu kupitishwa kwa mpango huo Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Igunga na Ujumbe wa NEC huku wengine wakiwa kimya.

Mukama alisema sehemu ya pili ya azimio hilo inayosema:
"Wasipofanya hivyo chama kiwawajibishe bila kuchelewa," ndiyo msingi wa NEC kurejesha suala hilo kwa Kamati Kuu na kwamba sasa litafanyika katika ngazi zote.Alisema NEC imeziagiza kamati za siasa kupitia kamati za ulinzi usalama na maadili kwa ngazi zote kuanza mara moja, mchakato wa kutekeleza azimio hilo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama.

Alisema NEC iliagiza kazi hiyo kufanyika haraka bila kuchelewa na baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, taarifa zipelekwe kwenye vikao vya kikatiba vya uamuzi kwa hatua za utekelezaji.

Alisema chama hicho kitahakikisha kwamba ajenda hiyo haitekwi na makundi yanayokinzana na kwamba lengo zima ni kuhakikisha kwamba CCM kinaongeza uwezo wa kusimamia mambo yake na Serikali zake zote.

"Lazima kifike mahali (CCM), kiwe na uwezo wa kuzisimamia na kuhakikisha kwamba Serikali zinatekeleza matakwa ya wananchi na siyo vinginevyo, ndiyo maana watu wanajiunga na vyama kwani huwa wanatarajia watapata utetezi," alisema Mukama.

Kuhusu vurugu na migomo ya vyuo vikuu CCM kiliagiza Serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo na kuitaka kusimamia sheria inayokataza uendeshaji wa shughuli za kisiasa katika taasisi za elimu nchini.

Kimetaka wanafunzi na watumishi wabanwe ili waendeshe shughuli hizo nje ya taasisi husika.Kuhusu suala la Nishati nchini, Mukama alisema NEC imeiagiza Serikali kuhakikisha kuwa inapunguza bei za mafuta na hasa ya taa ambayo yanatumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini.

Juzi, Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, waliwashambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakisimamia mpango wa kujivua gamba.

Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, pale alipowataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia zaidi ya dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Taaaaaaaaaaarrrrrrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaatttttttttttttttttiiiiiiiiiiiiiiiibbbbbbbbbbbbbbbbbuuuuuuuuuuu?

Kwa wenye ufahamu huu ndio mwanzoooooooooooo.!!!!!!!!!!!!!1
 
Nape amekumbana na tatizo lile lile ambalo wengine tumeliona muda mrefu uliopita - CCM haibebeki, haikoleki na mtu yeyote anayejaribu kuiokoa anaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa zaidi. Kwa sababu tazizo la CCM ndani ni zaidi ya watu (personalities) na ni zaidi ya maslahi (interests) na kwa kweli kabisa ni zaidi ya matamanio (ambitions). Tatizo lake limefungamana moja kwa moja na tunu, mitazamo, na itikadi ya Chama. Haiwezekani kuisafisha CCM bila kugusa huku. Ndio maana mwisho wa siku naamini kama Nape aliyoyoasema aliamini yalikuwa sahihi na kuwa alikuwa anasimamia maamuzi sahihi ya Chama na dhamira yake ikimthibitisha anabakiwa na uchaguzi mmoja tu - kutoka kwa heshima.

Uko sahihi kaka,option ni yake sisi wengine ni kumuunga mkono tu ila sio yeye tu yupo mzee wangu chiligati huyu ana heshima sana sasa leo kuvunjiwa heshima ndani ya kikao ni aibu kwake.Nilichosikia kama ni kweli mkiti amekubali kuwachukulia hatua za kinidhamu wakina chiligati basi watoke mapema tena kwa heshima zao.
 
Back
Top Bottom