Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Habari hizi zina TIJA ipi kwa taifa letu. Niliisha mshauri huyu ndugu afanye kazi ya KUKIENEZA chama chake (umri bado anao) la sivo aripoti kwenye vyombo vya usalama nchini. Mie kama ningekuwa mwandishi wa habari hii SIO habari kwa wananchi.
 
Hii habari imeenea sana vyo vikuu tangu siku nyingi na inaonekana CCM ndo wanaipata leo, na inasemekana na mambo ya kweli, kwa wale ambao hamshabikii mambo kuna haja ya kuchukkua tahadhari kuliko kutanguliza ushabiki.


Vyuo vikuu gani, mbona hapa chuo kikuu hakuna habari kama hii?

Acha kushabikia mambo yanayopikwa na wanasiasa wasio na sera alafu mwishowe aliyechonga tuhuma anawalalamikia wenzake kwa kumwachia zigo, hiv video hawajashoot?
 
*Ni kuhusu mauaji, Chadema, CCM vyashikana uchawi
*Mpango wa Nchimbi na Kinana kukutana waandaliwa


WAKATI Chadema wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inakihujumu, tuhuma nyingine nzito zimeibuliwa dhidi yake. Tuhuma hizo ni zile za mipango ya mauaji, ambako CCM kinadai kuwa kimebaini mpango wa siri unaoratibiwa na chama hicho kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.

Hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa nchini kushutumiana hadharani juu ya tuhuma nzito kama hizo. Wakati CCM ikidai kuwa na ushahidi juu ya tuhuma za sasa, Chadema wamekuwa wakidai kuwa tuhuma kama hizo na nyingine ni mpango wa kutaka kukidhoofisha baada ya kuona kuwa ni tishio kwake.

Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, aliibua tuhuma nyingine nzito alizodai kuwa na ushahidi nazo dhidi ya Chadema mbele ya mamia ya wananchi aliokuwa akiwahutubia mjini Makambako na vitongoji vyake.

Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa CCM imedhamiria kukishughulikia Chadema dhidi ya tuhuma hizo, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, anaelezwa kupanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mkoani Ruvuma kuangalia jinsi ya kushughulikia tuhuma hizo.

Nape akizungumza na wananchi hao, alidai kuwa mpango huo unawahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.

“Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya Chadema, ni kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika miji minne, ikiwemo Makambako.

“Lengo la maandamano hayo ni kuibua vurugu zitakazosababisha mauaji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida, ili kutafuta umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.

“CCM inapenda kuwaambia Watanzania popote pale walipo, wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung’oa kucha watu. CCM haiko tayari kuona nchi inaingia katika shimo la mauaji ya kupanga hata kidogo.

“Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua miji ya kufanya maandamano yao ambayo yataambatana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako, Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha, wilayani Kilombero,” alisema Nape, huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakuwa tayari kuona kile alichodai kuwa mauaji yakitokea tena nchini, kama ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.

“Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano ya Morogoro yaliyosababisha kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya mauaji inayopangwa na Chadema kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.

“Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingiza vijana maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.

“Haikupita muda alikufa kijana wa Kitanzania bila hatia, huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao, huku wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao kweli wana uchungu na nchi hii, kwa nini hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano,” alisema Nape.

Kutokana hilo Nape, alisema kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa sasa ni kwenda mjini Songea ambako atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kumueleza juu ya mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa ili atoe ufafanuzi wa shutuma hizo, lakini simu yake iliita bila majibu, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake hiyo ya kiganjani pia hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, naye hakujibu chochote.


Source: Mtanzania la leo 2/6/2013
nape ni mbu wa mambulula,anadanganya wananchi wasiokuwa na upeo ki fikra,lakini kwa sisi great thinkers na watanzania wengi ambao hivi sasa hawadanganyiki hawezi hata siku moja,Nape ni mbulula kwa sababu anafahamu kabisa kuwa ni ccm na polisi wake ndiyo huanzisha vurugu katika mikutano na maandamano yote ya CHADEMA ambayo huwa ya amani,wanafanya mauaji kwa makusudi kisha wanasema CHADEMA ni chama cha vurugu,uongo mtupu,nape anajisumbua,huenda anatisha watu wasijitokeze kwenye maandamano au mikutano itakayoandaliwa na CHADEMA,lakini ajue kwamba kwa sasa wananchi hawababaishwi na uongo na hawaogopi polisi,people's power,
 
CCMafisadi na mzee wa Tembo na Nepi wanapanga kuua sasa askari katika mkutano yoyote watakayofanya CDM ili ionekane kuwa CDM ndio wameua. Kama ilivyotaka kutokea Arusha jana ndio mikakati iliyobaki. Lakini sio mikakati mizuri yani kuua raia wako kwa ajili ya matumbo yao kweli wengi watafungwa haitajalisha kutoka chama gani. Ninachoomba mungu atusaidie tupate katiba nzuri ya Tanganyika yetu hapa ndio watapatikana wauaji wote. Nepi sijui atakimbilia wapi mwaka ujao wakati Fisadi Lowasa atakapoteuliwa kuwa mgombea wa urais wa ccmafisadi labda wataelekea ADP
 
Hatudanganyiki.ccm ndiyo inayoandaa fujo kwenye mikutano ya chadema ili kionekane ni chanzo cha fujo.laikini kiini cha fugo ni ccm.Pia matamushi ya nape yanalenga kuzuia mikutano ya chadema kwa kuipaka matope kuwa itasababisha vifo.

Nape ni kijana lakini anaabudu chama badala ya watanzania.Tambua nape hata shuleni kulikuwa na wajuzi zaidi yako haiwezekani ukawa na akili kuliko watanzania wote.

tukubali kila mtanzania anaweza kuongoza nchi hii kutoka chama chochote.kila chama kikipoteza mwelekeo lazima kiondoshwe madarakani. jiandaeni 2020 labda mtafikiliwa kurudi madarkani.Angalia kwa makini wamebakia wangapi na vilemba na kofia za ccm.
 
Mimi naona ccm ishughulikie hotuba ya sugu aliyosoma bungeni iliyowataka serikali ichukue hatua dhidi ya wauaji na wanaotesa watu.serikali ya ccm ikichukua hatua hizo nadhani suala zima la nani anaandaa mauaji litaisha maana mzizi wa fitina utakatika.
Kama kweli muandaaji wa mauaji na mateso ni CDM inakuwaje anakuwa mstari wa mbele kutaka wauaji wachukuliwe hatua? Na je kwa nini serikali ya ccm haikubaliani na wazo hili la kuchukua hatua,hapa kuna nini?
Watanzania tusipozinduka usingizini,tukaendelea kudhani kuwa ccm ya nape ni ile ya Mwalimu tumekwisha.CCM ya Mwalimu ilikuwa ya azimio la Arusha ,HII ya nape ni ya azimio la Zanzibar ndo maana inaitwa nambari wani
Mimi nampongeza nape kwa jambo moja muhimu analolifanya au kwa kujua au kutojua kwamba analamba matapishi yake maana yule aliyemuita gamba ndiye anayemfagilia njia kuelekea 2015
 
hawa wamechanganyikiwa jamani wanatapa tapa Mungu wangu inusuru tanzania na hawa ambao wanajianda kutokabidhi dola kwa chadema


Haha ha ha CCM mwaka huu mtapasuka msamba ha ha ha na bado mbona nape atapata kisukari na BP akiwa bado mdogo? CCM kwisha kazi. Jamani mazishi ya CCM hayawezi kusubili 2015 yanaanza mwezi huu mwisho 2014 Serikali za mitaa. Mbona ra
 
Hivi kweli Nape unawakusanya Wazee na vijana kisha bila aibu unaanza kuwahutubia mambo ya uongo,fitina na uchochezi kiasi hicho bila hata aibu? Umewadharau kiasi gani watu wa Makambako? Tabia za aina hiyo huwa zinafanywa na vijana ambao hawakupata malezi bora ya wazazi wao tuu. Mtu aliyepata malezi bora hasemi uongo mbele ya watu wazima kiasi hicho,pole sana Katibu mwenezi kivuli wa Chadema.
 
Tatizo la CCM wanafikiri watu wa vijini hwawpati habari za uhakika kupitia kwenye mitando na vyombo vingine vya habari. JF yenyewe ina wasomaji zaidi ya milioni moja. Jaribu kuona kila uzi utakuta memba 20 wageni zaidi ya elfu moja. Mjitathimini mbadilike propoganda haijengi chama . Tekelezeni ahadi zenu
 
hawa wamechanganyikiwa jamani wanatapa tapa Mungu wangu inusuru tanzania na hawa ambao wanajianda kutokabidhi dola kwa chadema

kuchukua dola mpaka uwe msafi mkuui chadema labda wanataka kuchukua paundi.
 
Mkuu sasa inavyosemekana ni kwamba kumbe LWAKATARE ndiye alikuwa aongoze kazi hiyo na baada ya kukamatwa ikabidi warudi kujipanga na kutafuatwa kijana ambaye anaweza kusimamia vizuri kazi hiyo, mpaka sasa inasemkana yule jamaa aliyejiengua CCM kule tanga na kujiunga na CHADEMA ndiye aliyekabidhiwa jukumu hilo wakati ambapo LWAKATARE bado hajatoka lupango

Hili ndio tatizo la AKILI ZA KUSHIKIWA. Lazima ukariri kama Kasuku.
 
Walikuja na propaganda ya udini, madhara yalipozidi tofauti na walivyotarajia wakaduwaa.
Sasa wanakuja na la mauaji, nalo likileta impact kama swala la udini, pia watatoa macho kama wamefumaniwa.
 
Ahsante Nape kwa kutufungua macho watanzania. Inabidi sasa vyombo vya dola vifuatilie tuhuma hizo na wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria
 
CCM Wakubali tuh kwamba zama zao sasa zimefikia ukingoni,kufeli kwa sera zao na wananchi walivyowachoka wao wanatupia lawama kwa wapinzani,

Haya sasa mauaji yaliyofanyika huku Mtwara ya kina mama na watoto tena kwa kupigwa risasi na polisi ikiwa na nyumba zao kuchomwa moto na polisi yamefanywa na harakati za chadema pia??,Upuuzi sana huu,na 2015 inakaribia cha moto mtakiona,WAPINZANI WAJITUME ZAID KATIKA KUHAMASISHA WANACHAMA NA WAFUASI WAO KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA ILI WAWEZE KUPIGA KURA KWA WINGI,UPEPO UNAZID KUWAVUMIA TOFAUTI CCM NA MAFISADI WOTE...
 
Tatizo la CCM wanafikiri watu wa vijini hwawpati habari za uhakika kupitia kwenye mitando na vyombo vingine vya habari. JF yenyewe ina wasomaji zaidi ya milioni moja. Jaribu kuona kila uzi utakuta memba 20 wageni zaidi ya elfu moja. Mjitathimini mbadilike propoganda haijengi chama . Tekelezeni ahadi zenu
Waambie chadema wabadilike na siasa zao za maji taka
 
Akaripoti polisi huyo Nepi kama ana uhakika na hili. Vinginevyo ni ccm wanapanga kufanya mauaji kama ilivyo kawaida yao ili wawasingizie CDM

Haya wanayosema CCM yanasadifiwa huko Arusha ambapo wanaokamatwa wakiwa na silaha na kutishia wananchi ni wa CDM. Kama sio wa CDM bali wanawasingizia basi tuendako hapafai
 
CCM Wakubali tuh kwamba zama zao sasa zimefikia ukingoni,kufeli kwa sera zao na wananchi walivyowachoka wao wanatupia lawama kwa wapinzani,

Haya sasa mauaji yaliyofanyika huku Mtwara ya kina mama na watoto tena kwa kupigwa risasi na polisi ikiwa na nyumba zao kuchomwa moto na polisi yamefanywa na harakati za chadema pia??,Upuuzi sana huu,na 2015 inakaribia cha moto mtakiona,WAPINZANI WAJITUME ZAID KATIKA KUHAMASISHA WANACHAMA NA WAFUASI WAO KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA ILI WAWEZE KUPIGA KURA KWA WINGI,UPEPO UNAZID KUWAVUMIA TOFAUTI CCM NA MAFISADI WOTE...
Mkuu, hata kama chadema wanaendesha siasa chafu, ccm wakae tu kimya?
 
Back
Top Bottom