Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
*Ni kuhusu mauaji, Chadema, CCM vyashikana uchawi

*Mpango wa Nchimbi na Kinana kukutana waandaliwa

WAKATI Chadema wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inakihujumu, tuhuma nyingine nzito zimeibuliwa dhidi yake. Tuhuma hizo ni zile za mipango ya mauaji, ambako CCM kinadai kuwa kimebaini mpango wa siri unaoratibiwa na chama hicho kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.

Hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa nchini kushutumiana hadharani juu ya tuhuma nzito kama hizo. Wakati CCM ikidai kuwa na ushahidi juu ya tuhuma za sasa, Chadema wamekuwa wakidai kuwa tuhuma kama hizo na nyingine ni mpango wa kutaka kukidhoofisha baada ya kuona kuwa ni tishio kwake.

Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, aliibua tuhuma nyingine nzito alizodai kuwa na ushahidi nazo dhidi ya Chadema mbele ya mamia ya wananchi aliokuwa akiwahutubia mjini Makambako na vitongoji vyake.

Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa CCM imedhamiria kukishughulikia Chadema dhidi ya tuhuma hizo, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, anaelezwa kupanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mkoani Ruvuma kuangalia jinsi ya kushughulikia tuhuma hizo.

Nape akizungumza na wananchi hao, alidai kuwa mpango huo unawahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.

“Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya Chadema, ni kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika miji minne, ikiwemo Makambako.

“Lengo la maandamano hayo ni kuibua vurugu zitakazosababisha mauaji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida, ili kutafuta umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.

“CCM inapenda kuwaambia Watanzania popote pale walipo, wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung’oa kucha watu. CCM haiko tayari kuona nchi inaingia katika shimo la mauaji ya kupanga hata kidogo.

“Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua miji ya kufanya maandamano yao ambayo yataambatana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako, Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha, wilayani Kilombero,” alisema Nape, huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakuwa tayari kuona kile alichodai kuwa mauaji yakitokea tena nchini, kama ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.

“Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano ya Morogoro yaliyosababisha kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya mauaji inayopangwa na Chadema kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.

“Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingiza vijana maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.

“Haikupita muda alikufa kijana wa Kitanzania bila hatia, huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao, huku wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao kweli wana uchungu na nchi hii, kwa nini hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano,” alisema Nape.

Kutokana hilo Nape, alisema kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa sasa ni kwenda mjini Songea ambako atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kumueleza juu ya mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa ili atoe ufafanuzi wa shutuma hizo, lakini simu yake iliita bila majibu, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake hiyo ya kiganjani pia hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, naye hakujibu chochote.

Habari kutoka Mtanzania Jumapili.
 
*Ni kuhusu mauaji, Chadema, CCM vyashikana uchawi
*Mpango wa Nchimbi na Kinana kukutana waandaliwa

WAKATI Chadema wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inakihujumu, tuhuma nyingine nzito zimeibuliwa dhidi yake. Tuhuma hizo ni zile za mipango ya mauaji, ambako CCM kinadai kuwa kimebaini mpango wa siri unaoratibiwa na chama hicho kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.

Hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa nchini kushutumiana hadharani juu ya tuhuma nzito kama hizo. Wakati CCM ikidai kuwa na ushahidi juu ya tuhuma za sasa, Chadema wamekuwa wakidai kuwa tuhuma kama hizo na nyingine ni mpango wa kutaka kukidhoofisha baada ya kuona kuwa ni tishio kwake.

Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, aliibua tuhuma nyingine nzito alizodai kuwa na ushahidi nazo dhidi ya Chadema mbele ya mamia ya wananchi aliokuwa akiwahutubia mjini Makambako na vitongoji vyake.

Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa CCM imedhamiria kukishughulikia Chadema dhidi ya tuhuma hizo, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, anaelezwa kupanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mkoani Ruvuma kuangalia jinsi ya kushughulikia tuhuma hizo.

Nape akizungumza na wananchi hao, alidai kuwa mpango huo unawahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.

"Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya Chadema, ni kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika miji minne, ikiwemo Makambako.

"Lengo la maandamano hayo ni kuibua vurugu zitakazosababisha mauaji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida, ili kutafuta umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.

"CCM inapenda kuwaambia Watanzania popote pale walipo, wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung'oa kucha watu. CCM haiko tayari kuona nchi inaingia katika shimo la mauaji ya kupanga hata kidogo.

"Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua miji ya kufanya maandamano yao ambayo yataambatana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako, Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha, wilayani Kilombero," alisema Nape, huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakuwa tayari kuona kile alichodai kuwa mauaji yakitokea tena nchini, kama ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.

"Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano ya Morogoro yaliyosababisha kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya mauaji inayopangwa na Chadema kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.

"Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingiza vijana maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.

"Haikupita muda alikufa kijana wa Kitanzania bila hatia, huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao, huku wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao kweli wana uchungu na nchi hii, kwa nini hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano," alisema Nape.

Kutokana hilo Nape, alisema kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa sasa ni kwenda mjini Songea ambako atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kumueleza juu ya mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa ili atoe ufafanuzi wa shutuma hizo, lakini simu yake iliita bila majibu, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake hiyo ya kiganjani pia hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, naye hakujibu chochote.

Source: Mtanzania la leo 2/6/2013
 
Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.
 
Asante kwa taarifa @Nape hakika Chadema ni janga la Taifa.
 
hawa wamechanganyikiwa jamani wanatapa tapa Mungu wangu inusuru tanzania na hawa ambao wanajianda kutokabidhi dola kwa chadema
 
----- mtupu,mtaongea sana lakn angalia hii ya Moro jana chini ya Dr Slaa
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1370168986107.jpg
    uploadfromtaptalk1370168986107.jpg
    94.8 KB · Views: 808
  • uploadfromtaptalk1370169024889.jpg
    uploadfromtaptalk1370169024889.jpg
    68.3 KB · Views: 872
Ukishakuwa mtoto wa HARAMU ni tatizo kubwa sana...
 
mbona umbea tu..................M4C inawachanganya CCM
 
Kuna siku moja nikiwa chuoni pale UDSM nilisikia kada muumini mmoja wa CHASO akisema kuwa yeye ni chadema damu, lakini mbinu wanazoziandaa za kuwahandaa watanzania zinaweza kuhatarisha amani ya nchi. Inawezekana mbinu zenyewe ndo hizi nini? ee mungu tuepushe na balaa hili.
 
Source: gazeti la Mtanzania Jumapili.

Asante kwa taarifa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Katibu mkuu wa itikadi na uenezi wa CCM, NAPE Hnauye amesema kuwa kumekuwepo na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari polisi na WAnanchi katika mji wa MAKAMBAKO na maeneo mengine huku nape akiwasihi watanzania wanaoishi maeneo ambayo CHADEMA watafanya maandamano kuchukua tahadhari.

Source: Mtanzania la leo 2/6/2013
Uko sahihi ni tuhuma tu kama zingine zilizoishia kwa kauli za utani. CCM watulie tu, kwa sababu kila wakifurukuta dawa inakolea.
 
hapa hakuna mpya huu ni uzushi mwingine baada ya movie ya lwakatare kubuma. kaazi kwelikweli.
 
mbona umbea tu..................M4C inawachanganya CCM
Hii habari imeenea sana vyo vikuu tangu siku nyingi na inaonekana CCM ndo wanaipata leo, na inasemekana na mambo ya kweli, kwa wale ambao hamshabikii mambo kuna haja ya kuchukkua tahadhari kuliko kutanguliza ushabiki.
 
Too poor.
Ni ujinga mtupu Nape anasema.
Hizo propaganda zimeshachuja kitambo sana.
CCM mlianza na propaganda za Ukabila, Ukanda, Udini zikashindikana, mkaja na Ndoa ya Dr.Slaa bado mkashindwa, mkahamia kadi ya CCM ya Dr.Slaa watu wakawacheka sana, mwisho mkaibukia Ugaidi nao umeshachuja.
Sijui mtakuja na single gani mpya?
 
hapa hakuna mpya huu ni uzushi mwingine baada ya movie ya lwakatare kubuma. kaazi kwelikweli.

Mkuu sasa inavyosemekana ni kwamba kumbe LWAKATARE ndiye alikuwa aongoze kazi hiyo na baada ya kukamatwa ikabidi warudi kujipanga na kutafuatwa kijana ambaye anaweza kusimamia vizuri kazi hiyo, mpaka sasa inasemkana yule jamaa aliyejiengua CCM kule tanga na kujiunga na CHADEMA ndiye aliyekabidhiwa jukumu hilo wakati ambapo LWAKATARE bado hajatoka lupango
 
Jambo ambalo halijatukia unaliitaje tuhuma?
 
Back
Top Bottom