Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Duu wewe mav. Kweli hivi hata mwenye akili kidogo wa chekechea anaweza kutambua hilo kuwa mfa maji haachi kutapatapa. Kipigo bado kitaendelea tu. Kaka hakuna kulala mpaka kieleweke.
duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

Kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

Why all this?. Why, why, why?.
 
*Ni kuhusu mauaji, Chadema, CCM vyashikana uchawi

*Mpango wa Nchimbi na Kinana kukutana waandaliwa

WAKATI Chadema wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inakihujumu, tuhuma nyingine nzito zimeibuliwa dhidi yake. Tuhuma hizo ni zile za mipango ya mauaji, ambako CCM kinadai kuwa kimebaini mpango wa siri unaoratibiwa na chama hicho kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.

Hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa nchini kushutumiana hadharani juu ya tuhuma nzito kama hizo. Wakati CCM ikidai kuwa na ushahidi juu ya tuhuma za sasa, Chadema wamekuwa wakidai kuwa tuhuma kama hizo na nyingine ni mpango wa kutaka kukidhoofisha baada ya kuona kuwa ni tishio kwake.

Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, aliibua tuhuma nyingine nzito alizodai kuwa na ushahidi nazo dhidi ya Chadema mbele ya mamia ya wananchi aliokuwa akiwahutubia mjini Makambako na vitongoji vyake.

Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa CCM imedhamiria kukishughulikia Chadema dhidi ya tuhuma hizo, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, anaelezwa kupanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mkoani Ruvuma kuangalia jinsi ya kushughulikia tuhuma hizo.

Nape akizungumza na wananchi hao, alidai kuwa mpango huo unawahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.

“Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya Chadema, ni kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika miji minne, ikiwemo Makambako.

“Lengo la maandamano hayo ni kuibua vurugu zitakazosababisha mauaji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida, ili kutafuta umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.

“CCM inapenda kuwaambia Watanzania popote pale walipo, wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung’oa kucha watu. CCM haiko tayari kuona nchi inaingia katika shimo la mauaji ya kupanga hata kidogo.

“Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua miji ya kufanya maandamano yao ambayo yataambatana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako, Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha, wilayani Kilombero,” alisema Nape, huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakuwa tayari kuona kile alichodai kuwa mauaji yakitokea tena nchini, kama ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.

“Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano ya Morogoro yaliyosababisha kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya mauaji inayopangwa na Chadema kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.

“Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingiza vijana maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.

“Haikupita muda alikufa kijana wa Kitanzania bila hatia, huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao, huku wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao kweli wana uchungu na nchi hii, kwa nini hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano,” alisema Nape.

Kutokana hilo Nape, alisema kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa sasa ni kwenda mjini Songea ambako atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kumueleza juu ya mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa ili atoe ufafanuzi wa shutuma hizo, lakini simu yake iliita bila majibu, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake hiyo ya kiganjani pia hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, naye hakujibu chochote.

Habari kutoka Mtanzania Jumapili.

tuhuma za kitoto kama hizi akawadangadanganye mabwege wenzake.inaonekana chadema imewashika pabaya maaana yake hamuishi kutapatapa.
ushauri:acheni siasa mfu.
 
Morogoro Slaa kawavuruga magamba vibaya kinana atakufa kwa presha mfungwa mtarajiwa huyu
 
Nape again, huyu jamaa yuko obsessed na chadema, nadhani ameitamka CDM mara nyingi kuliko alivyoitamka CCM na hata kuliko mwenyekiti wa CDM alivyoitamka CHADEMA!
 
Nape kawaambie serikali yako morogoro ajali kila siku wabakufa watu wawili mpaka wa tano kwa ajali ya malori achana na cdm ....hangaika na ilani watanzania tunateseka maisha magumu...ndugu zetu wanakufa kwa kukosa dawa na misaada ya uokozi hizo pesa mnazozurura kundi la watu mia zingetosha kutuokoa
 
Kwa kweli hawa ccm mafisadi mwisho wao umegota!
Chama imepoteza network sasa imebaki kutoa mapofu tu!
 
Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.

Nape asiwafanye watanzania kuwa ni wajinga. Mauaji ya Morogoro yaliwahusisha polisi, mauaji ya Iringa yaliamriwa moja kwa moja na RPC ambaye sasa amepandishwa cheo kwa kazi 'mzuri' aliyoifanyia ccm. Mauaji ya Arusha vile vile yalihusisha polisi walio chini ya serikali ccm. Sasa hapa muuaji ni nani? Kama CDM wanahusika kwa nini serikali ya ccm imekataa kuunda tume huru ya kuchunguza haya mauaji? Mimi ni mwana ccm lakini siungi mkono hoja za kipuuzi zinazotolewa na Nape.
 
Yeye ana tuhuma nzito za kutumia jina la watu pasi na rukhsa na hajajibu hata leo hii

BrigGen+NnauyeKisw.jpg


45722_10200382772425953_1346694315_n.jpg
 
Chama kinapokosa hoja za kuwaeleza watanzania kwa nini watz bado ni maskini, kwa nini wanafunzi wanapewa maksi ili waende form v, kwa nini huduma za afya ni mbovu, kwa nini kati ya barabara 86 elfu nchi nzima wamejenga 6 elfu tu tangu 1961 hadi sasa, kwa nini madini yao hayawafaidishi, kwa nini wakenya, wamalawi, wazambia, waganda na sasa wanyarwanda ndo wanaoajiriwa katika sekta ya utalii na sekta nyingine binafsi na si wao watz, kwa nini hakuna huduma ya uhakika ya maji safi na salama n.k na kuanza kushutumu chama cha upinzani ni MMOMONYOKO WA UBONGO,
 
mkuu huna unachokijua ni kama unakimbia kivuri chako chadema wametuletea siasa za kuuwa watu ambazo hapo awali hazikuwepo.

Majuzi tu hapa Watoto wa Sokoine wanataka baba yao afukuliwe na afanyiwe uchunguzi, je enzi hizo CDM ilishazaliwa. Refer na la Horace Kolimba. Hivyo ukatili huo ulikuwapo tangu enzi.
 
Nape haangilii alama za nyakati! Mtanzania wa leo utamdanganya kwa propaganda za kitoto namana hiyo! Morogoro CDM walipanga mauaji, Iringa CDM walipanga mauaji, Arusha CDM walipanga mauaji na sasa wanapanga Makambako.....! Hapa alikuwa anaidhalilisha serikali ya chama cha mapinduzi au hakujua anachoongea!? Ina maana nchi hii haina uslama wa taifa!? Wenye dola ni CDM au CCM? Kama kweli CDM wamefanya yote hayo polisi na mahakama ni kwa ajiri ya nani! CCM wanachotakiwa ni kujidhihirisha kuwa wanataka bado kubaki madarakani kwa kuchapa kazi ili watanzania wakikubari, sasa ndugu zangu hawa wanatumia muda na nguvu nyingi sana kuchafua chama ambacho hakina dola.....Kwa wakiristo ni kwamba Mchungaji mzuri ni yule anaetumia muda mwingi kueleza uzuri wa YESU na si kutumia muda mrefu na nguvu nyingi kueleza ubaya wa shetani! Mtu akijua uzuri wa Yesu hatatenda dhambi na automatic atajiepusha na shetani! CCM watueleze na kutuonyesha kwa vitendo uzuri wao na automatically watanzania wataachana na vyama vya upinzani lakini kama Nape ataendeleza hizi zilipendwa watakuwa wanaijenga CDM kwa gharama za CCM! Nimekuwa nikimwona Nape kila mkutano anatoa mapovu na kutokwa na jasho jingi akihangaika na CDM badala ya kuelezea CCM wamewafanyia nini watanzania! Kina mama wa tanzania hawajifungui kwa kulipia au kununua gloves, wazee wanatibiwa bure, ufaulu wa watoto wetu umeongezeka, walimu wanalipwa madai yao na kujengewa nyumba, shule za kata zina walimu wa kutosha. Wawekezaji wamebanwa na serikali na kulipa kodi na kodi kutumika kuleta maendeleo ya watanzania. Umeme vijijini imekuwa si hadithi ya kufikirika! Maji vijijini si tatizo tena baada ya miaka zaidi ya hasini ya uhuru. Ahadi ya makamu wa mwenyekiti wa CCM kuwashughulikia mafisadi baada ya yeye Nape kushindwa imetimizwa! Kwa sababu Nape hana majibu ya hoja za msingi amejikita kuleta propaganda za kipuuzi kabisa kwa watanzania....nafasi hiyo alipewa lakini ni kiatu kikubwa mno kwa mguu mdogo wa Nape! Haya kaka endelea kukiimarisha CHADEMA kwa aday ya wana CCM sijui ndo ulichotumwa kusema!
 
Taifa la Tanzania linaangamia kwa sababu Taifa linaongozwa kijinga na wajinga wanawaelekeza wananchi mambo ya kijinga badala ya kubadilisha maisha yao!
 
mfa maji haachi kutapatapa , kwa jinsi ilivyo inaonenekana sifa ya ccm katika mauaji imewachosha wananchi, wameamua ku geuza ubao kwa cdm
 
Back
Top Bottom