Kweli unatia huruma hivi katika maandamano ya Chadema wewe kama msomi nani anaua raia??Hapa ondoa mambo ya siasa na ushabiki usio na maana nani kauwa raia Arusha,Morogoro na Iringa??Hapa huhitaji Master au kuwa msomi.Je kama mikutano na maandamano ya Chadema italindwa vizuri na Police wasiingilie na kuripua mabomu na risasi za moto kweli kutatokea mauaji?Je maandamano na mikutano iliyofanya na Chadema pasipo kuingiliwa na Police kulitokea vifo???Kwenye picha ya mauaji ya mwandishi wa habari uliwaona wanachama wa Chadema wakimshambulia Daud Mwangosi???Mbona tunapenda kudanganyana bana,Hii habari ya Nape mbona atakuwa ameongelea chama chake CCM kwani wao si ndio wanatumia Police kukandamiza Demokrasia au Nape anataka kuwaona wananchi wajinga?Kama Chadema ndio wanang'oa watu kucha na kuuwa waandishi wa habari kwa nini wasiwakamate wakati wanawafahamu nkuwa ndio wauaji?Mbona Dr Ulimboko alimtaja ofisa wa Ikulu na hadi leo hajahojiwa pia Dr Ulimboka mwenyewe hajahojiwa hapa kuna nini?Je serikali na vyombo vyake vya dola inawalinda Chadema??Amka/amkeni Watanzania CCM inawahadaa kila kukicha na nyie mnazidi kulala ooh!!Poor Tanzanian