Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nilitegemea kuona chama kikongwe kikinadi sera zao, lakini sasa hivi kinajihangaisha na kuchonga cd na kuzitafutia uhalisia huku kikisahau hakina nyenzo za kufyatulia teknolojia.
CDM hawana maji taka, Kazi wanazo wale wanaojaribu kuficha mambo ya ufisadi mchana kweupe. Wakati wao wakiongea kwa hisia za intelgensia ambazo hazina ushahidi CDM wanaweka wazi mpaka mawasiliano wanayoyafanya CCM juu ya kuwachafua wenzao.
Sisi MATOMASO tunaamini zaidi yanayosemwa na CDM kwa kuwa yana ushahidi wa dhahiri sio ule unaotolewa na CCM kwa nadharia.
mkuu huna unachokijua ni kama unakimbia kivuri chako chadema wametuletea siasa za kuuwa watu ambazo hapo awali hazikuwepo.
 
Kwani mzee slaa anapokaa na kutunga uongo anapata nini yeye alipaswa awafundishe wanasiasa wadogo lakini yeye ndo anaongoza kwa tabia mbovu.
 
Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.

Muulize kinana Na nape why, why , why wanapanga hayo mauaji.
Kama yakipangwa Na Chadema Na ccm ikajua itatumia Polisi kuzuia mauaji. Ukiona ccm wanajua Mipango ya mauaji lakini ikatekelezwa wakati kuna Polisi we utakuwa Na akili za ajabu kuamini kuwa Mipango hiyo Polisi yetu haiwezi kuizuia
 
CCM imeishiqa mbinu,ilifhani CHADEMA ni upepo tu kwamba unapita kama walivyotabiri mwaka 2010,badala yake imekuwa tofauti,wameamua na wao wafanye mikutano ili kukinusuru chama but its too late.
 
Kwani mzee slaa anapokaa na kutunga uongo anapata nini yeye alipaswa awafundishe wanasiasa wadogo lakini yeye ndo anaongoza kwa tabia mbovu.

Kwahiyo Nape katunga uongo coz Dr.Slaa anasema uongo? Tofauti ya ccm na cdm wao huwa wanaweka ushahidi je Gatwick wako huko Wapi nape?
 
Propaganda tu hizo za kuwahadaa Wananchi, kila siku Nape ana siri nzito za CDM, lakini hatuoni hatua zozote anazochukua! Gahalaghabhao!
 
Mwenzie Dr Slaa jana alipoibua tuhuma za Kinana kutaka kuwahonga majaji wa Mahakama ya rufaa ili wafufue kesi ya uchaguzi dhidi ya TUNDU LISSU kwa mlango wa nyuma, alitoa na barua walizoandika wenyewe kuandaa njama hizo!!...

Yeye inakuwaje anakuja na anazoziita tuhuma bila ya kuonesha ushahidi huo anaosema anao ili hadhira ikamwelewa na kumwamini ingalau kidogo?..Hofu yangu ni moja ukiona Nape au Nchemba au Wassira anapiga kelele jukwaani na kukituhumu CHADEMA, tambua mara moja kuwa wao ndo wanajiandaa kuua mtu,au kumtoa kucha na macho!!....kisha..........hawa ni... iwe .....si mnaona wananchi...

Hawa jamaa, defenetely ni wapuuzi,wapumbavu na ni washenzi tu, wanatuandalia machafuko tu ktk nchi yetu!!..Haingii akilini kubwabwaja jukwaani na kujaribu kuwaaminisha watu wanaofikiri kwa vichwa eti CHADEMA wanaandaa mkakati wa kuua polisi katika mikutano yao!!....Nionavyo na tafsiri yangu mimi ni moja tu kuwa CHADEMA wanaandaa jeshi lao kupambana na kuua polisi wa Tz!!..Hizi ni tuhuma za kipuuzi na za kishenzi kabisa

Ni wazi tungekuwa na TISS na POLISI wanaojua kufanya kazi yao Nape alipaswa kuwa amekamatwa na kutoa maelezo mara baada ya kushuka tu jukwaani!!!
 
KIfo cha uandihi wa habari.....nimesoma hilo gazeti nikaona jinsi CCM walivyo busy ktk kila idara ili kupambana na CDm na si na shida za wananchi.
 
Nape nilishakuambia unasoma vitabu vya propaganda za kizamani kutoka baba yako marehemu.Ninakusahuri nenda shule.kwani unatia huruma hapa JF.au sivyo tumeanzisha jamiiforums za watoto.naomba jiunge huko.
 
Daktari Augustine. Wacha huu upuuzi wa CCM tusiupuuze kdg. Kuna upuuzi wa kupuuzwa, mwingine unapaswa kujadiliwa ili uzidi kuonekana na kuwekwa wazi ni upuuzi wa kiwango gani na walioutoa wazidi kupuuzwa na kuonekana daraja la kutojua kwao ni la ngapi!

Aiseee this is very serious.

Imefikia hatua chama tawala hakiwezi tena kuzungumzia shughuli za maendeleo, hakiwezi kusema sera zake (zimeshindwa) zimefikia wapi, hakiwezi kusema kwa wananchi kuwa in next 50 or so years sera hizo zitalifikisha taifa mahali gani, hakiwezi kusema hadi sasa kimefanyika 1, 2, 3 (tangible)...this is getting more serious.

Kwamba CCM imefikia mahali haiwezi kabisa hata kuzungumzia topical issue (zilizoko) kwenye maisha ya kila siku ya wananchi, zinazohusu maendeleo yao, mathalani hata kuzungumzia namna rasilimali za nchi zinavyoporwa na uhusiano huo kwa ugumu wa maisha unaowakabili wananchi, mismanagement ya uchumi na athari zake kwa ugumu wa maisha unaozidi kudhihirika kupitia 'mkate' wa kila siku na masuala mengine kama usafiri!

Kila wakilala, wakiamuka, wakikutana, kila wakisema, kila wakipayuka, ni CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA...dude! Who are these CHADEMA ambao wanaweza kuifikisha serikali ya CCM kwenye defensive mechanisim ya kichovu kama hii ambayo inaashiria serikali kusarenda na chama tawala kujiandaa kuondoka, ofcoz baad ya kumwaga damu za watu kwa kujaribu kuzuia 'mvua kunyesha!'.

Imefikia mahali CCM wakishinda hata kitongoji au kijiji, wanalazimika kukimbiza mwenge kutangaza kuwa wamewashinda CHADEMA mahali fulani! Haikuwahi kutokea. Inatokea sasa na hali hii inaonekana kuchemka kadri zinavyosogea siku.

Vitu kadhaa tungependa Nape's na Kinana's crew huko waliko kwenye ziara ambao wanazidi kushuhudia namna ambavyo wananchi wamewaasi sirini na hadharani, wenzao wengine walioko sehemu zingine na ndani ya serikali, wajue;

1. CHADEMA haitafanya siasa kwa hisani ya CCM. Hii ni kwa sababu kauli za Nape kama zilivyonukuliwa na jamaa zao hawa kuanzia jana na leo, mbali ya kutaka kupotosha, zinalenga upotoshaji huo ufanyiwe kazi na vyombo vya dola (kwa maelekezo) kama walivyozoea. Itaendelea kufanya kazi za kisiasa kama wajibu na haki ya kikatiba. Period.

2. Hizi kauli za kila siku za Nape ambazo hazina ushahidi hata wa kimazingira, hasa akiwataja viongozi wakuu ili eti apate attention yao, hatafanikiwa. Let him mark my words, viongozi makini wa taasisi makini kama CHADEMA hawataweza kupoteza muda na mtu wa sampuli hii.

Kwa kushirikiana na Watz wengine wenye moyo na akili njema za kujenga nchi yao, wanayo mambo mengi ya msingi kwa ajili ya kufikiria next 50-100 years ya taifa letu. In its store, CHADEMA has a lot to fit Nape. Tena ajiandae, asishangae siku moja atajibiwa na mabalozi wa nyumba kumi kumi.

Maana tunajua amekuwa akifanya makusudi kwenye kila kauli yake anayotoa lazima ataje Dkt. Slaa au Mwenyekiti Mbowe...hatafanikiwa. Bila shaka na watu wao wanaowatumia kuandika stories kama hizi watatusaidia kujua hili vizuri. Eti walimtafuta Mbowe na Dkt. Slaa kwa ufafanuzi...wa kauli za Nape?!?!? What a waste of time for Mwenyekiti Mbowe or Dkt. Slaa responding to Nape!

Tuje kwenye huu uzushi wake ambao kama alivyosema Mohamed, ulishakuwa pre-empted. Mwanzoni walipanga anukuliwe mtu mmoja aliyehamiwa kwao miaka zaidi ya miwili iliyopita. Akutane na watu wao, wawalishe maneno. Kisha stori iwe kwamba huyo mtu aliwahi kuwa mjumbe eti wa kamati ya ulinzi ya chama (sijui imeanzishwa lini) hivyo wakati akiwa bado CHADEMA waliwahi kukaa kikao na kupanga mipango...ilivyokuwa preempted, wakaahirisha.

Wakaamua kutoka leo kivingine kidogo. Kutokea jukwaani.

Itoshe tu kuonesha vitu kadhaa, ambavyo viko kwenye kauli hizi hii ambavyo vitamfanya aliyezitoa azidi kuonekana kwamba ni mpuuzi na alichosema ni maneno yao ya siku yote ya kutunga eti ikiwa ndiyo mikakati ya timu mpya ya sekretarieti kupambana na wimbi kubwa la mabadiliko.

Wakati wa shughuli za mikutano ya M4C Morogoro, Mwenyekiti Mbowe kwa sehemu kubwa alikuwa bungeni, kabla ya kusafiri kikazi kwenda nje ya nchi. Siku ya mapokezi yaliyovurugwa na polisi kwa maelekezo ma faida ya CCM, kisha polisi wakamuua ndugu Ally Singano Zona, Mwenyekiti Mbowe hakuwepo kabisa Dar es Salaam. Kusema kuwa alikuwa Dar es Salaam ni uongo. Mtu kijana hawezi hata kutafiti kidogo kabla hajasema. Akiwa muongo kwenye umri wa namna hii, sijui akizeeka itakuwaje...

Katibu Mkuu, Dkt. Slaa alikuwepo kwenye M4C ya Morogoro. Wakati polisi wakimuua yule kijana kwa kitu kizito chenye ncha kali, Dkt. Slaa alikuwepo Morogoro. Na baadae siku hiyo hiyo baada ya polisi kuvuruga mapokezi, alihutubia mkutano mkubwa sana wa kihistoria mjini Morogoro, ambao ulikuwa na simanzi ya kumpoteza binadamu mwenzao kwa hujuma za CCM inayoogopa mikutano na operesheni za CHADEMA kwa kiwango kisichofananishwa!

Hakukuwa na maandamano yoyote siku hiyo. Kulikuwa na mapokezi ya wanachama wa CHADEMA wa Morogoro pamoja na wananchi wengine kuwalaki viongozi wengine waliokuwa wanatokea Dar es Salaam kwenda Morogoro. Polisi wakaingilia. Wakapiga mabomu, wakafyatua risasi za moto. Wakajeruhi. Mtu mmoja akafa. Wakajichunguza wao, wakajiundia mashtaka, wakajisikiliza na kujifutia tuhuma za mauaji ya huyo mtu mmoja. Lakini hadi leo wananchi wanajua walioua ni polisi.

Kuna mtu yeyote anaweza kuwaambia Watz kuwa CHADEMA walivunja sheria ipi au kifungu kipi cha katiba kuwapokea viongozi wao kisha waende kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umeshatolewa taarifa polisi kama inavyotakiwa?

Sasa kwa nini mtu aseme uongo kiasi hiki unaomfanya aonekane ni mtu wa kupuuzwa hata na mtu aliye tabulalasa!

Hivi ni lini CCM waliwahi kukiri hadharani (tunajua wanafanya hivyo sirini) kuwa umaarufu wa CHADEMA umekua? Kama hawajawahi kukiri hivyo au kusema hadharani, sasa wanapata wapi uhalali au ujasiri wa kusema umaarufu wa CHADEMA umepungua?

Hofu yao inayowafanya watunge maneno kama haya inadhihirisha namna wanavyotishika na umaarufu huo wa CHADEMA ambao wanaukiri kwa kusema kinyume chake hadharani na kuusema kwa dhati wakiwa kwenye vikao vya ndani.

Mipango ya operesheni kwenye miji gani sijui (labda maana ya mji ni nyingine) maana labda kijiji cha Ruaha kimepewa hadhi ya kuwa mji, Ilula nayo siku hizi imekuwa mji, Makambako nayo siku hizi ni mji? Songea.

Hakujapangwa kufanyika shughuli rasmi za chama kuhusisha ngazi ya taifa. Lakini mamlaka nyingine kama kanda za chama (mikoa, wilaya, majimbo, kata, vijiji, matawi na misingi) zinayo mamlaka ya kufanya siasa na kusimamia utendaji wa chama katika maeneo husika kwa kila siku. Wanaweza kufanya shughuli za kisiasa wakati wowote, mahali popote, kama wajibu wao na haki yao ya kikatiba.

Inajulikana. Wananchi wa Ruaha wamekataa dhuluma wanayotaka kufanyiwa na utawala wa CCM. Kusimikiwa kiongozi asiyetokana na matakwa yao. Wanao ujasiri wa kusema hapana. Ndiyo maana walimuuliza maswali Katibu Mkuu wa CCM juu ya tuhuma za "weka mbali na tembo", wakiwa pamoja na Nape, wakafunga mkutano na kukimbia, wakisema wananchi wale wametumwa na CHADEMA.

Wananchi wa maeneo mengine vivyo hivyo wanaweza kuwa na harakati zao za kudai haki, maana dhuluma za CCM sasa ni kila mahali. Nape asiwatishe.

Kama CCM wangelikuwa wanawajali wnananchi, au basi wangejali maisha ya Watanzania, wakiwemo hao wa Songea ambao leo wanajifanya eti kuwapatia tahadhari, basi angehakikisha Michael Kamuhanda aliyesababisha watu kadhaa wa mji huo, wakiwemo vijana, wapigwe risasi na kufa papo hapo, anawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na kushtakiwa.

Mtu huyo huyo amekwenda Iringa na kusimamia mauaji ya Daudi Mwangosi. Kwa sababu ya kutekeleza kwa ufanisi kazi ya mauaji anayotumwa kutokana na mipango ya CCM, juzi Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete kampandisha cheo!

Waache uongo. Watu wanawajua na kuwaona. Hiyo huruma wanaotaka kujipachika hawana. huo ubinadamu wananoyaka kuigiza, ulishawatoka. Hawana. Wangeanzia kwa kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali zao. Wangeweza basi kuwahurumia tembo wanaokatiliwa maisha kwa ukatili wa hali ya juu na na twiga wanaokunjwa shingo na kuwekwa kwenye ndege.

Wangeweza hata kuepusha vifo vya watu vinavyosababishwa na serikali hii hii na chama hiki hiki, kila mahali sasa! Kuanzia kwenye elimu, kilimo, mifugo, viwanja, afya, maji machafu, barabara mbovu, uvunjwaji wa sheria, ukiukwaji wa katiba, kulindana!

Kama wana ujasiri wa kuweza kusema kuna hata tukio moja la mauaji limesababishwa na CHADEMA, kwa nini Rais Kikwete ameshindwa kutekeleza walau hata kujibu barua ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe, juu ya azimio la Kamati Kuu, kumtaka Rais aunde Tume Huru ya Kimahakama/Kijaji kuchunguza matukio yote, walau walitajiwa matano, likiwemo moja lililomhusisha kiongozi wa CCM kule Ndago, Iramba, Singida?

.
 
Source: gazeti la Mtanzania Jumapili.

Asante kwa taarifa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
It seems Lowasa alishaona kuwa kizingiti kikubwa kwake sasa ni CDM na sio membe tena. Hata hivyo kutokana na ile kauli ya Sitta juzi juzi tutarajie Mtanzania kuanza tena kumuandama hivi karibuni. Lowasa aachane na mambo ya kutaka uraisi. Atakufa kwa presha...
 
Mzee Nape eeeeh....!!!
Wananchi wa sasa Sio kama wa Enzi zileeeee...!!
MaJF uwo ni upepo na unapita Tu.
 
Kama CCM wanasema kweli kwa nini wasiripoti polisi, kama wana uhakika wa tuhuma hizo?
Ndugu zangu hata wakoloni waliopozidiwa na vuguvugu la harakati za ukombozi walianza kuwabambikiza kesi na tuhuma kama za leo, ndo maana unasikia akina Nyerere, Kenyatta, Mandela wote waliswekwa ndani, hivyo watanzania wenye aliki timamu nawaomba wasikate tamaa saa ya ukombozi ni sasa ukiona watawala wanaanza kupiga kelele hizo ujue sasa mwisho wa safari yao uko karibu sana.

Wao ndo watawala halafu wanavyo vyombo vya dola kwa nini wasichukue hatua ya kwenda polisi na kwa nini wasemee majukwaani.Hawajifunzi kwenye single ya Mwigulu etu kiongoziwa CHADEMA alimplelekea mkanda wa ugaidi? yeye ni nani mbona mahakamani kaangukia pua, Ikumbukwe kwamba UFISADI ukushafikia umri mkubwa kama ulivyo wa CCM sasa hofu ya kusema uongo, kuua, kupotosha ukweli, kupandisha vyeo watuhumiwa wanaona nikawaida kama njia na kinga yao.

Nitumie fursa hii kuwaomba wote wenye kumwabudu mwenyezi MUNGU waendelee kuwaombea wakombozi wetu wasikwame popote mpka watufikishe kwenye nchi ya ahadi ambayo Mungu alitupenda upeo akaiumba Tanzania akaiwekea dhahabu Tanzanite, Almasi, Uranium, Makaa ya mawe, gesi asilia, mafuta samaki, milima, maziwa mifugo lakini kwa sababu zisizoelewka sasa tumewapata makuwadi wa wawekezaji wanatupiga nada mchana kweupe kwa kuingia mikataba ya kitapeli, mingine ikisainiwa nje mingine hapahapa usiku bila hata ya kuisoma.

Alisema Mchg. Mtikiala SAA YA UKOMBOZI NI SASA
Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Je Nape kesha mtambua Baba yake? Shida ya wanaolelewa na single parents ndo hiyo sasa.
 
Hii habari imeenea sana vyo vikuu tangu siku nyingi na inaonekana CCM ndo wanaipata leo, na inasemekana na mambo ya kweli, kwa wale ambao hamshabikii mambo kuna haja ya kuchukkua tahadhari kuliko kutanguliza ushabiki.

Kwa hiyo nape kaambiwa na wewe?!

Mkuu sasa inavyosemekana ni kwamba kumbe LWAKATARE ndiye alikuwa aongoze kazi hiyo na baada ya kukamatwa ikabidi warudi kujipanga na kutafuatwa kijana ambaye anaweza kusimamia vizuri kazi hiyo, mpaka sasa inasemkana yule jamaa aliyejiengua CCM kule tanga na kujiunga na CHADEMA ndiye aliyekabidhiwa jukumu hilo wakati ambapo LWAKATARE bado hajatoka lupango

Inasemekana --- Hisia za LUMUMBA.

Kuna siku moja nikiwa chuoni pale UDSM nilisikia kada muumini mmoja wa CHASO akisema kuwa yeye ni chadema damu, lakini mbinu wanazoziandaa za kuwahandaa watanzania zinaweza kuhatarisha amani ya nchi. Inawezekana mbinu zenyewe ndo hizi nini? ee mungu tuepushe na balaa hili.

Unashuhudia uongo, baadaye unajifanya muumini safi!

Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.

Haya ni mambo makubwa!... Kwa hiyo akiamka mtu nyumbani kwake na kukuita wewe jambazi basi wewe ni mtu unayetafuta riziki kwa njia haramu?
 
Hii habari imeenea sana vyo vikuu tangu siku nyingi na inaonekana CCM ndo wanaipata leo, na inasemekana na mambo ya kweli, kwa wale ambao hamshabikii mambo kuna haja ya kuchukkua tahadhari kuliko kutanguliza ushabiki.

Mkuu sasa inavyosemekana ni kwamba kumbe LWAKATARE ndiye alikuwa aongoze kazi hiyo na baada ya kukamatwa ikabidi warudi kujipanga na kutafuatwa kijana ambaye anaweza kusimamia vizuri kazi hiyo, mpaka sasa inasemkana yule jamaa aliyejiengua CCM kule tanga na kujiunga na CHADEMA ndiye aliyekabidhiwa jukumu hilo wakati ambapo LWAKATARE bado hajatoka lupango

Kuna siku moja nikiwa chuoni pale UDSM nilisikia kada muumini mmoja wa CHASO akisema kuwa yeye ni chadema damu, lakini mbinu wanazoziandaa za kuwahandaa watanzania zinaweza kuhatarisha amani ya nchi. Inawezekana mbinu zenyewe ndo hizi nini? ee mungu tuepushe na balaa hili.

Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.

* Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Ukabila umefeli, Udini umefeli, Ugaidi umefeli. sasa ni mauaji ya Polisi. Kwa hiyo CCM wataua polisi na kuutangazia umma kuwa CDM wameua? Wameshasahau kuwa mauaji ya Mwangosi yalikuwa na lengo hili?... Leo hii RUNGWE inasubiri ripoti ya kweli kuhusu MAUAJI ya Mwangosi!!!.. PROPAPANDA HIZI ZIKIENDELEA mauaji ya akina Mwangosi na Ally Zona yatakuwa ajenda za mikutano. Picha za kuuliwa Mwangosi na kupandishwa cheo Kamuhanda zitafika kila mahali.
 
Duh, hii inatia hofu. Kwa nini vyama visiendeshe siasa safi kwa manufaa na mstakabali wa Taifa.

Kuna faida gani kupata madaraka kwa njia za kishetani?.

Why they are so desperate for power?.

kwani hawafahamu kama nchini kuna demokrasia ya kupata viongozi kwa njia ya kura?.

why all this?. Why, why, why?.

No sense,no sense at all

Unatuletea habari tuchangie then unakuwa wa kwanza kutoa hukumu!

No sense Magamba tulieni mnyolewa kwenye chaguzi hizi za madiwani June 16!Polisi ni wenu CHADEMA hawana dola!!Acheni uzushi!

No sense!
 
Tishio kubwa kuliko yote la amani nchini Tanzania kwa sasa ni hii desperation ya CCM. Kiko tayari kuleta machafuko ili kibaki madarakani. Bu it will not work.

Awamu hii imekuwa janga. Hadi sasa fanikio lake kubwa ni kutumia polisi kuuwa Watanzania wengi kuliko awamu zote zilitongalia, combined. And they are not done yet. Maneno ya sasa ya Nape bila shaka ni matayarisho tu ya wao kuuwa tena na tena.
 
Daktari Augustine. Wacha huu upuuzi wa CCM tusiupuuze kdg. Kuna upuuzi wa kupuuzwa, mwingine unapaswa kujadiliwa ili uzidi kuonekana na kuwekwa wazi ni upuuzi wa kiwango gani na walioutoa wazidi kupuuzwa na kuonekana daraja la kutojua kwao ni la ngapi!

Aiseee this is very serious.

Ukweli ni kama tanuru la moto. Ukweli huunguza pole pole hata kama ukiamua kujifanya unaweza kuuhimili.

Bandiko hili limewaunguza polepole mpaka mmeanza kuibuka mkipiga kelele huku mkitaka kuwaaminisha watu kuwa hizi ni kelele za kishujaa wakati tunazisikia ni kelele za kutaka msaada kutoka kwa wanajanvi.

Hivi kweli unaweza kuwahadaa watu wenye uelewa mpana kuwa hiki ulichojaribu kukijibu kutoka kwa Nape Nnauye ni empty talk and garbage wakati majibu yako karibia yamejaza screen interface. You're just fooling yourself.

Huwezi kujibu majibu yanayojaza screen interface ukataka kuwaaminisha watu hicho unachokijibu ni utumbo bila kuonekana pia kile unachokiandika ni utumbo. Umejaribu lakini ukweli haufutwi kwa spinning and slant.

Sitashangaa kumuona yule aliyesikika akisema hawezi kujibu kwa vile ukweli ni kidogo.

You can't springboard the truth. Watu wenye upeo wa juu watanielewa nina maanisha nini.

What's the point of filling the whole screen interface with words answering garbage kama siyo kudhihirisha kuwa, ukweli umewachoma.

Kama hamtaki kuunguzwa na tanuru la ukweli. Fanyeni siasa safi, apart from that, tutaendelea kuwakumbusha.
 
Back
Top Bottom