Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nape aja na Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Nepi ni mpumbavu na mwanasiasa mjinga kabisa,jana nimehudhuria mkutano wa CHADEMA na ulikuwa wa amani kabisa,Hivi hawa watu wa CCM ukomo wao wa kufikiri ndio umeishia hapa?Sina cha kuongea zaidi ila ukweli ni kwamba CCM haina Viongozi wenye mawazo makubwa.Poleni!
 
Duh CHADEMA wanatisha,wanawatumia polisi kuua na wakishaua serikali inawapandisha vyeo polisi waloua(this is ridiculous)
 
nape ni kiboko yao chadema anawapa kiwewe ile mbaya we unaFikiri kwa nini babu slaa alimkimbia pale itv?
CDM wakisikia jina la Nape na Mwigulu huwa macho yanawatoka na kuweweseka. Acha waendelee kutukana na kuweseka, wakati CCM inafanya kazi iliyotumwa kuifanya na watanzania wengi 2010.
 
Nepi ni mpumbavu na mwanasiasa mjinga kabisa,jana nimehudhuria mkutano wa CHADEMA na ulikuwa wa amani kabisa,Hivi hawa watu wa CCM ukomo wao wa kufikiri ndio umeishia hapa?Sina cha kuongea zaidi ila ukweli ni kwamba CCM haina Viongozi wenye mawazo makubwa.Poleni!
Utawezaje kuona kama CCM ina viongozi wenye mawazo makubwa wakati macho yako yamezibwa na bendera ya CHADEMA inayopepea mbele ya macho yako.

Wewe endelea kufikiri hivyo hivyo kwa vile unatimiza haki yako ya kikatiba!.
 
Du kama maneno yenyewe ni ya nape wala sichangii maana akili za nape kwanza za kimirembemirembe
Hizi kweli ni akili za bavicha.

Kwa taarifa yako, kusoma thread ni zaidi ya kuchangia pamoja na kwamba kuandika tu hapa, umeishachangia.
 
Huyu Nape Nnauye ni mliberali na mpangamaujaji tu kisha kusingizia wengine hana lolote. Amekua kama pepo na mwenzake Mwigulu wanatumwa bila kujua impact ya wanachofanya, ila mwisho wao umekaribia na uzandiki wao utaisha
Ni impact gani anayoifahamu ambayo Nape na Mwigulu hawaifahamu. Hebu nieleweshe mimi ambaye hata gwanda silifahamu.
 
Niliposoma tu title, nikajiridhisha kwamba hiyo habari lazima iwe imeandikwa na gazeti la Mtanzania. Sasa gazeti la Mtanzania linaendesha harakati za kutisha dhidi ya CHADEMA, kiasi cha kwamba hata magazeti ya uhuru na Mzalendo hivi sasa yanaonakana si kitu wala si chochote mbele ya mtanzania kwa propaganda za kusadikika.
 
Akaripoti polisi huyo Nepi kama ana uhakika na hili. Vinginevyo ni ccm wanapanga kufanya mauaji kama ilivyo kawaida yao ili wawasingizie CDM

Safi, kwa sababu kiongozi mkubwa kama huyu kwa nini alalame kwenye mikutano asiripoti polisi. huu ni uzushi na propaganda chafu
 
Ni impact gani anayoifahamu ambayo Nape na Mwigulu hawaifahamu. Hebu nieleweshe mimi ambaye hata gwanda silifahamu.
Kwa hiyo hata walipokuwa wanaeneza sera ya udini na ukabila pia walijua kwamba yatatokea haya yanayotokea hivi sasa ya watu kuanza kuchinjana? Kwahiyo mipango ya kuwagawa watanzania ili wachinjane na kuuana inafanyika kwa makusudi huku mkiwa mnajua kabisa impact zake? Na tukisema CCM ipo tayari kumwaga damu za watanzania ilimradi tu yenyewe ibaki ikulu tutakuwa tumekosea?
 
iv zile za ukabila, then udini na sasa ugaid..... nape cjui anawaonaje hao wa2.. kat ya cdm na ccm nani ana dola? kaz ya polic ni nini? TUENDELEE KUFUMBIA MACHO IZ PROPS.. yakfikia level ilpofkia udin tuseme mkono wa nje..,.!
 
Josephine Mushumbusi anamfanya Dr.Slaa awe too desperate.

Siasa za mauaji hazifai...

Kifo cha Amina Chifupa na mmewe Mupakanjia hukumu ya Babu Seya vipi,KJ hausiki?. (Atakaenitoa ni Kikwete. by. Babuseya)
 
*Ni kuhusu mauaji, Chadema, CCM vyashikana uchawi

*Mpango wa Nchimbi na Kinana kukutana waandaliwa

WAKATI Chadema wakikishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inakihujumu, tuhuma nyingine nzito zimeibuliwa dhidi yake. Tuhuma hizo ni zile za mipango ya mauaji, ambako CCM kinadai kuwa kimebaini mpango wa siri unaoratibiwa na chama hicho kwa kuwahusisha askari Polisi na wananchi wa kawaida.

Hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa nchini kushutumiana hadharani juu ya tuhuma nzito kama hizo. Wakati CCM ikidai kuwa na ushahidi juu ya tuhuma za sasa, Chadema wamekuwa wakidai kuwa tuhuma kama hizo na nyingine ni mpango wa kutaka kukidhoofisha baada ya kuona kuwa ni tishio kwake.

Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, aliibua tuhuma nyingine nzito alizodai kuwa na ushahidi nazo dhidi ya Chadema mbele ya mamia ya wananchi aliokuwa akiwahutubia mjini Makambako na vitongoji vyake.

Katika mkutano huo, Nape alisema kuwa kumekuwa na mipango inayoratibiwa na CHADEMA kwa takribani mwezi mmoja sasa ya kufanya maandamano ambayo yataambatana na mauaji dhidi ya askari Polisi na wananchi wa mji huo na maeneo tofauti.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa CCM imedhamiria kukishughulikia Chadema dhidi ya tuhuma hizo, Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana, anaelezwa kupanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mkoani Ruvuma kuangalia jinsi ya kushughulikia tuhuma hizo.

Nape akizungumza na wananchi hao, alidai kuwa mpango huo unawahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho cha upinzani.

“Ninapenda kuweka wazi jambo moja kwa mujibu wa taarifa za siri ambazo CCM imezinasa kutoka ndani ya Chadema, ni kwamba hivi sasa chama hiki kipo katika mikakati ya kufanya maandamano katika miji minne, ikiwemo Makambako.

“Lengo la maandamano hayo ni kuibua vurugu zitakazosababisha mauaji dhidi ya askari Polisi na raia wa kawaida, ili kutafuta umaarufu wao ambao umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni.

“CCM inapenda kuwaambia Watanzania popote pale walipo, wajue kuwa CHADEMA si chama cha siasa, bali ni genge la watu ambalo limejikusanya kwa lengo la kuua na kung’oa kucha watu. CCM haiko tayari kuona nchi inaingia katika shimo la mauaji ya kupanga hata kidogo.

“Kwa wiki moja sasa wamekuwa wakichagua miji ya kufanya maandamano yao ambayo yataambatana na mauaji na wamepanga kufanya katika miji ya Makambako, Songea pamoja na miji ya Ilula wilayani Kilolo pamoja na mji wa Ruaha, wilayani Kilombero,” alisema Nape, huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alisema kwa muda mrefu chama chake kimekuwa kimya na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitaka kulitumbukiza taifa katika machafuko kwa kivuli cha siasa.

Alisema kutokana na hali hiyo, chama chake hakitakuwa tayari kuona kile alichodai kuwa mauaji yakitokea tena nchini, kama ilivyokuwa katika miji ya Arusha, Morogoro na Iringa.

“Ni wazi siku tatu kabla ya maandamano ya Morogoro yaliyosababisha kifo cha kijana mmachinga asiye na hatia, CCM ilijitokeza mbele ya umma wa Watanzania na kuwaambia kuwa kuna mipango ya mauaji inayopangwa na Chadema kwa kutoa watu jijini Dar es Salaam.

“Ilipotimu siku hiyo walifanya hivyo kwa kutoa magari kila kona ya jiji la Dar es Salaam na kwenda kuwaingiza vijana maskini wa Morogoro katika maandamano ambayo yalipigwa marufuku na Polisi.

“Haikupita muda alikufa kijana wa Kitanzania bila hatia, huku Mbowe na babu Slaa wakiwa Dar es Salaam wakiendelea na kazi zao, huku wakifanya mashauri na familia zao. Kama wao kweli wana uchungu na nchi hii, kwa nini hatuwaoni wakiwa mbele ya maandamano,” alisema Nape.

Kutokana hilo Nape, alisema kuwa moja ya kazi anayoifanya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa sasa ni kwenda mjini Songea ambako atafanya kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kumueleza juu ya mipango hiyo michafu inayolenga kuharibu sifa ya Tanzania.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, MTANZANIA Jumapili ilimtafuta Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa ili atoe ufafanuzi wa shutuma hizo, lakini simu yake iliita bila majibu, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake hiyo ya kiganjani pia hakujibu.

Alipotafutwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, naye hakujibu chochote.

Habari kutoka Mtanzania Jumapili.


Sasa kweli Tanzania ni nchi ya maajabu, katibu mwenezi wa chama tawala anataarifa nyeti kiasi hiki anaishia kutoa kwenye mikutana ya jukwaani badala ya kuwajulisha vyombo vya dola na kuwapa ushahidi!!!!!!!!. Watanzania hapa kweli tuna viongozi? Hawa tukiwaita matapeli tunachochea? Tukiwaita hamnazo tumetukana? Haya tutaona huko mbele tuendako.
 
ha ha haaa!

Ati nini?

Source yenyewe ni gazeti la mtanzania. Ndio mwanzo wa kuwa na mashaka na habari yenyewe!
 
Kweli nimeamini kinana noma mtu kaua tembo kasafirisha meno yake na bado anaenda kuongea na waziri wa mambo ya ndan? Ayse nchi hii kuna watu wamejipanga .
 
Kwa hiyo hata walipokuwa wanaeneza sera ya udini na ukabila pia walijua kwamba yatatokea haya yanayotokea hivi sasa ya watu kuanza kuchinjana? Kwahiyo mipango ya kuwagawa watanzania ili wachinjane na kuuana inafanyika kwa makusudi huku mkiwa mnajua kabisa impact zake? Na tukisema CCM ipo tayari kumwaga damu za watanzania ilimradi tu yenyewe ibaki ikulu tutakuwa tumekosea?
Hatujadili hisia za watu hatu, hayo majadiliano waachie Tanzania Daima na wadau wake, lakini kama na wewe ni mdau wa Tanzania Daima, basi sitakuwa na nguvu za majadiliano.

Katiba gani hiyo ya CCM unayoisoma ambayo imeandikwa sera za udini na ukabila?.

Sitashangaa kufahamu kama hujui maana ya sera za vyama na taratibu zake katika mikono ya sheria za vyama vya siasa na sheria za nchi.
 
Sasa kweli Tanzania ni nchi ya maajabu, katibu mwenezi wa chama tawala anataarifa nyeti kiasi hiki anaishia kutoa kwenye mikutana ya jukwaani badala ya kuwajulisha vyombo vya dola na kuwapa ushahidi!!!!!!!!. Watanzania hapa kweli tuna viongozi? Hawa tukiwaita matapeli tunachochea? Tukiwaita hamnazo tumetukana? Haya tutaona huko mbele tuendako.
Ina maana hujasoma katibu mkuu wa CCM amepanga kukutana na waziri wa mambo ya ndani. Mbona unakuwa kama unasoma kichwa cha habari pekee. Usiwe kati ya wavivu wa kusoma kama walivyo watanzania wengi.

Please, Soma habari yote.
 
Kumbe ccm wana intelijensia zaidi ya intelijensia ya taifa hili..,wao wamenasaje habari hizi? Wapi usalama wa taifa na vyombo vingine vya sheria? Imekuaje ccm wawe na habari hizi,waziri usika asiwenazo?..upangaji wao wa propaganda bado uko chini sana.wajipange upwa tena.
 
kama hizo tuhuma za nape ni kweli kwa nini hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyowasilishwa na Mh.Sugu iliyoitaka serikali kuchukua hatua kwa wauaji ikiwemo mauaji ya Mwangosi na kuteswa kwa akina Ulimboka mbona haikupata kuungwa mkono na ccm? Kama kweli muuaji na Mtasa watu ni CDM kwa nini ccm yenye dola haichukui hatua?
Mimi naona Nape anawapa tahadhari wakazi wa huko anakotembea kwamba wanajiandaa kuwaua pindi watakapohudhuria mikutano ya wakombozi wa nchi CDM.
Namshauri nape akimaliza kuhutubia awe anatoa nafasi ya kuulizwa maswali aone kama watu wanamuelewa.
Afu naona nape anakula matapishi yake,alimwandama EL kwamba ni gamba sasa atake asitake ajue wazi kuwa anampigia debe 2015.
 
Ipo cku mtakumbuka ccm,, uhuru uliopo ukitoweka na fursa zilizipo zikikosekana tusije laumu mtu maana tunawaunga mkono wenyewe cdm kwa mambo yao ya siasa z kihuni zisizo na tija
 
Back
Top Bottom