Labda nikufafanulie kidogo ili twende sawa
Mwanadamu anaundwa na vitu viwili vikuu
1.roho(pumzi)
2.mwili
Roho ya mwanadamu haina uwezo wa kujigawa mara mbili.
Yohana alibeba roho ya elia(maana yake roho ya elia imewahi kukaa kwenye miili miwili ya kibinadamu)
Wakati musa na elia wamekuja bado yohana alikua yupo hai
Mwanadamu haundwi na Vitu 2.
Mwanadamu anaundwa na Vitu 3.
1. Roho - Spirit.
2. Soul - Nafsi.
3. Mwili - Body.
Na Kila kimoja kinafanya kazi tofauti. Unaonekana unapenda mambo ya Dini, ila unatumia Akili Yako ya kawaida kutaka kuelewa Biblia na mambo ya Kiroho Kwa ujumla.
Maisha ni Roho, na Biblia ni mwongozo wa kuishi Maisha yanayompendeza Mungu kimwili na kiroho.
Kwa Vile Mungu ni Roho na Kila kitu kinachohusiana naye kina Roho, Sasa Kwa Akili tu mtoto mdogo, basi ili kumwelewa Mungu inabidi uingie kwenye Anga zake, uwe mtu wa Kiroho, kuwa mtu wa Kiroho sio kusoma Biblia.
Ndiyo maana Kwa vile Mungu ni Roho, na sisi Binadamu tu Mwili, Nafsi na Roho, na ili Mungu aingie kwenye Anga zetu tuweze kuelewana ama twende sawa, ilibidi ajivue Uungu wake, ashuke Duniani kama Binadamu kupitia Yesu Kristo....!
Ushauri wangu kwako kama unataka kuelewa Mambo ya kwenye Biblia na Ulimwengu wa Roho Kwa Ujumla, alika Roho nyingine iingie ndani Yako, soon Ile Roho ikiingia ndani Yako, itakusaidia kuelewa yote haya, wakati mwingine utashangaa unajiuliza tu jambo ndani Yako, na ghafla tu, ukajikuta unapata majibu ndani Yako, unajikuta unaelewa mambo ya Kiroho bila kufundishwa na Binadamu, Ile Roho unayotakiwa kuikaribisha inaitwa Roho Mtakatifu.
Mimi pia ni Mkatoriki Kwa Asili, lakini kwenye Ukatoriki Kazi za Roho Mtakatifu zimefinywa sana hivi, so Kuna Vitu nikaanza kubadirisha Mimi mwenyewe, mambo za kwenda Kwa Padre kutubu nikaondoa, nikawa nafanya toba straight Kwa Mungu na vitu vingine nikaongeza, zile sala za kukariri nikazitoa, nikaanza kufanya maombi kufunga mfululizo n k...... Kwa Nia kabisa... Then one day....... boom....!
Nikajikuta tu naanza kuelewa Mambo ya kiroho bila kufundishwa, nikajikuta naona vitu ambavyo macho ya kawaida hayawezi kuona, nikajikuta naanza kupata majibu ya maswali mengi niliyokua najiuliza, nikaanza kusikia Sauti ya ndani, Kuna Sauti ikaanza kuongea ndani yangu, nasikia mwenyewe Kwa ndani....!
Ikinikumbusha Kuomba nikisahau, ikinipa vifungu vya kusoma vya Biblia etc.
So kama Lengo lako ni kuijua kweli na sio kuja hapa ili Ubishane, badirisha Mentality Yako, tumia muda wako kumtafuta Mungu, naye atajifunua kwako Wazi Wazi.