..Tanzania hatuthamini watu wa sanaa na wanamichezo.
..John Komba ana kipaji cha kuimba na amekitumia kufanikiwa kimaisha.
..tatizo ni mfumo wa maisha wa kifisadi na ujanja-ujanja uliopo Tanzania.
..John Komba angekuwa kwenye nchi za wenzetu angekuwa na maisha yake mazuri tu yaliyotokana na kipato halali.
..inawezekana wengine hapa wangefurahi kama John Komba angeishi maisha ya taabu na dhiki kama marehemu Mzee Mourice Nyunyusa.
NB:
..tuzingatie zaidi mchango wa mhusika ktk jamii yetu.
..kama mtu ni msomi basi tumhoji amechangia nini kwa jamii yake na taaluma yake.
..kwa wanamichezo/wasanii etc tuhoji mchango wao kwa jamii ktk michezo/sanaa etc.
..hii tabia ya kuulizana vyeti vyeti vyeti kila mara, tena hata mahali pasipohusika, sidhani kama inajenga, na ndiyo chanzo cha viongozi kutafuta vyeti feki.