Naomba ushauri kuhusu dini

Naomba ushauri kuhusu dini

Source doesn't matter. Pale mtu anapokuwa na hamu ya kuutafuta ukweli hujikuta aki'resonate'/akiitikia na kukubaliana na ukweli toka katika source mbalimbali.

Well unajuaje kama huu ni ukweli? Ni roho wa Mungu anatuongozaga. Mungu atusaidie sana. We unadhani kwa nini watawala wale na majini yaliposikia aya za Quran yakasema hakika tumeamini? Ukweli una namna ya kujipambanua wenyewe. Kinakuwa kama kitu hai hivi: Na katika kila kitabu/msahafu yapo ya kweli na ya uongo!! Uking'angana na source tu unapotea. Kila kimoja kimeandikwa baada ya wahusika wakuu kuwa walishajiondokea. Kwa hiyo hata kama wao tunawaamini, je vipi kuhusu hawa waliowaacha? Je hawawezi kupitiwa, hawawezi kukosea hata kama si kimakusudi....na je hawawezi kujiongeza kimakusudi kwa lengo jema? Na worst case scenario, kujiongeza kwa lengo baya?

Hujajibu swali , jee wewe utaifuata biblia yoyote Tu kwa vile umeambiwa ni maneno ya Mungu. ?
 
Sio kuambiwa ni pale nitakapojionea mwenyewe hayo maneno, iwe biblia uwe msahafu haijalishi
 
Kwa hivyo wewe unaikubali biblia ipi au zote unaziona ni maneno ya Mungu ?
Nikwambie kosa la kimantiki unalolifanya kila mara? Umeegemea sana kwenye mamlaka 'appeal to authority'. Ungeegemea kwa mtu fulani tungesema 'ad hominem' appeal to a person.

Vizuri ukakikubali kitu kwa kuangalia je? hoja yake ni ya ukweli hoja zisimame kama hoja mkuu.

Kwa hiyo tukirudi kwenye swali lako mimi sikubali biblia fulani, sikubali msahafu fulani bali nakubaliana na hoja moja baada ya nyingine katika hizo biblia au elimu yoyote husika.
 
Tafsiri ya Neno Uisilamu ni kunyenyekea au kujikabizisha kwa Mwenyezi Mungu,kwa hiyo Mitume wote na Manabii walijikabidhisha kwa mwenyezi Mungu,na Uisilamu unamuamini Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wala msaidizi,kila unachoomba na kutubu inabidi Umuombe yeye, sasa jiulize wewe uko wapi hapo?
Una hakika walikua wanamnyenyekea Mungu unayemtaja wewe
 
Nikwambie kosa la kimantiki unalolifanya kila mara? Umeegemea sana kwenye mamlaka 'appeal to authority'. Ungeegemea kwa mtu fulani tungesema 'ad hominem' appeal to a person.

Vizuri ukakikubali kitu kwa kuangalia je? hoja yake ni ya ukweli hoja zisimame kama hoja mkuu.

Kwa hiyo tukirudi kwenye swali lako mimi sikubali biblia fulani, sikubali msahafu fulani bali nakubaliana na hoja moja baada ya nyingine katika hizo biblia au elimu yoyote husika.
Kwa hivyo unakubali biblia zote zimetoka kwa Mungu ?
 
Tatizo lako sio kwamba huelewi. La. Hiyo itakuwa ni kukushusha kiwango [understatement]!

Ukweli ni kwamba hun'gamui ninachokisema kila muda hapa.

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi. Vitabu ni mkusanyiko wa hoja mbalimbali......nakubali kuwa kuna hoja za biblia zimetoka kwa Mungu. Nakubali pia kuwa kuna hoja za Quran zimetoka kwa Mungu. Nakubali pia kuwa kuna hoja za kisayansi zimetoka kwa Mungu. Chochote cha ukweli kimetoka kwa Mungu.
 
Unayo haki ya kunishusha daraja upendavyo. Ni haki yako

Mimi siongelei vitabu vya biblia , nakuuliza biblia zenyewe , KJV, RSV , Douay nk. Jee kwa ulivyoandika mwenyewe unakubali vyote ni maneno ya Mungu ??

Au kiswahili kinakupiga chenga?
 
Ndugu yangu nimekubali kununua nyanya za mia tatu katika soko, duka etc. Usilazimishe kuniambia kwamba wewe nyanya unanunua wapi? Sokoni au dukani. Kwamba nikikubali kununua nyanya ya dukani ina maana nimekubali kila kitu dukani kimetoka kwa mkulima bustanini!, hadi balbu, hadi mabati na tochi. Kisa tu zipo dukani?

Ila popote nitakapoikuta nyanya mimi nitajua fika imetoka bustanini kwa mkulima😂. Na ntainunua bila ubishi. Hoja hapa ni nyanya sio nimeikuta wapi
 
Ndiyo kuna maneno ya Mungu katika KJV,RSV etc
 
Sijakuuliza habari ya nyanya sokoni , tunaongelea biblia Na swali ni jee wewe unaziamini zote ni maneno ya Mungu?
 
Kwa hivyo wewe unaikubali biblia ipi au zote unaziona ni maneno ya Mungu ?
Uwa nacheka sana 😂😂😂😂 mnaposema biblia ipi, biblia ni kitabu Cha vitabu unachotakiwa kusema kitabu kipi

Mfano Mimi nasoma Koran Kuna translation mpaka unaogopa watu wanavyodanganya , ila uzuri siku izi unaweza soma lugha ya hasili na ukapata wanacho kificha

Leo nilikuwa nasoma jibril alishuka na kamba kwa Muhammad hiyo ndio lugha ya asili ila soma translation uongo mtupu hakuna kamba wameficha yote
 
hakuna aliyekufa akafufuka akaeleza aliyoyakuta huko! Hata yesu sijui kama alisema kwa mungu kukoje au unielekeze
Yesu pekee ndiye anajua. Kwa sababu ni Mungu then anajua kuliko wanadamu wote. Na kwa sababu aliuvaa mwili ni Mungu pekee anayejua matatizo yetu kwa experience.

Na kwa sababu alikufa akafufuka anaweza kutuambia kifo kikoje, kwa experience kabisa na kufufuka kukoje. Kwa kuwa ni Mungu na Mwanadamu vyote kwa 100% anaweza kutupa experience ya mwanadamu kuishi mbinguni.

Kuu kuliko yote kwa sababu alikufa kulipa deni ya hatia yetu basi anaweza kutusamehw deni zetu kama tukimwendea kwa imani.

Hakuna Mungu aliyelipa deni za wanadamu isipokuwa Yesu pekee!
 
Uwa nacheka sana 😂😂😂😂 mnaposema biblia ipi, biblia ni kitabu Cha vitabu unachotakiwa kusema kitabu kipi

Mfano Mimi nasoma Koran Kuna translation mpaka unaogopa watu wanavyodanganya , ila uzuri siku izi unaweza soma lugha ya hasili na ukapata wanacho kificha

Leo nilikuwa nasoma jibril alishuka na kamba kwa Muhammad hiyo ndio lugha ya asili ila soma translation uongo mtupu hakuna kamba wameficha yote
Afadhali brother umekuja. Huyu hapa Jagina nakukabidhi mchukue. Mimi amenishinda tabia.

Anapenda sana vifungu nadhani mtaelewana vizuri zaidi
 
Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaidi ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya Kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mkristo mama yangu ndiyo Muislam.

Bahati mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielewi kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasababu dini ya Kiislam naijua nimesoma madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zamani nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.

Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipendi kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumbani na natumia maji ya baraka wakati mwingi nahisi kabisa yananisaidia, halafu nikiwa kanisani nina amani zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubiri ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumbani redio nasikiliza redio Maria tu na naifurahia.

Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sasa hivi ndiyo nazidi kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu natamani waanze mafundisho, au kuna sehemu sijielewi?
Din so shda ila iman
 
Fuata haja ya moyo wako inavyokuongoza, na uone mwenyewe ni wapi unapata amani, mambo ya imani ni magumu sana lkn pia siku hukumu utasimama wewe kama wewe.....
 
Uwa nacheka sana 😂😂😂😂 mnaposema biblia ipi, biblia ni kitabu Cha vitabu unachotakiwa kusema kitabu kipi

Mfano Mimi nasoma Koran Kuna translation mpaka unaogopa watu wanavyodanganya , ila uzuri siku izi unaweza soma lugha ya hasili na ukapata wanacho kificha

Leo nilikuwa nasoma jibril alishuka na kamba kwa Muhammad hiyo ndio lugha ya asili ila soma translation uongo mtupu hakuna kamba wameficha yote

Cheka zaidi , unajifanya kama hujui kuwa biblia ya

King James Version

New King James version

New International version

Revised Standard version

American Standard version

NK

Hizi ni biblia tofauti wala si moja ??????

Hivi unaelewa maana ya Version ???
 
Back
Top Bottom