Hili alitakiwa aliseme Mola mwenyewe au aseme Yesu mwenyewe, siyo nyinyi wala wanafunzi wake.
Nanukuu :
“Siwezi kufanya lolote peke yangu. Chochote ninachosikia, Ninahukumu na hukumu yangu ni ya haki. sitafuti mapenzi yangu mwenyewe bali mapenzi yake aliyenituma.” [Yohana 5:30]
Andiko lenu hapo juu linaonyesha wazi ya kuwa si kweli kwamba Mola alijihihirisha katika umbile la ubidamu, sababu hapo ameonyesha udhaifu na Mola si mdhaifu. Kinyume chake mnachokidai nyinyi ni uzushi na kumzulia nabii wa Mola.
"Yesu anazungumza juu ya Mungu kama kiumbe tofauti kwake mwenyewe:
Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu. [Yohana 20:17]"
Hapo Yesu anaonyesha kwa vyovyote vile hawezi kuwa Mola, sababu amekiri kwa wazi kabisa yeye ni kama wewe tu. Kadhalika ana muabudu mnaye paswa kumuabudu nyinyi.
"Katika mstari huu anathibitisha kwamba alitumwa na Mungu:
"Huu ndio uzima wa milele: Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. [Yohana 17:3]"
Hapo Yesu anakiri kabisa ya kuwa Mola ni wa pekee, hana mwenza wala mshirika ndiyo maana hupati andiko ambalo Yesu anasema yeye ni Mungu.
Tuanzie hapa..
wewe unachagua mistari mingine unairuka makusudi,
inabidi nikufundishe kwa kutumia Koran ili kichwa yako ngumu ielewe
Katika Koran tunaona Allah akimtaja Yesu na kutoa sifa za Mungu
Koran 57:3. Yeye ndiye wa
Mwanzo na ndiye wa Mwisho,
Rev 22:12.“Sikiliza!”
Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.
13Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.”
Koran 24:35.
Mwenyezi Mungu ni Mwanga wa Mbingu na Ardhi....
John 8:12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “
Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu.
Koran 20:114. Ametukuka
Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki....
Itim 6:15 Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao uliopangwa na Mungu mwenye heri na aliye Mtawala pekee,
Mfalme wa
wafalme,
Koran 22:62. Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi
Mungu ndiye Wa Kweli,....
John 14: 6
Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na
ukweli na uhai.
102. Huyo ndiye
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye,
Muumba wa kila kitu...
John1: 3 Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa;
hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye.
Koran 3:135.....na nani
anaye futa dhambi isipo kuwa
Mwenyezi Mungu?........
Math 9:6Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu
anao uwezo duniani wa kuwasamehe watu dhambi.”....
Koran 22:69. Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu...
Math25:32 Mataifa yote yatakusanyika mbele yake,
naye atawatenganisha watu kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
Koran 59:23. Yeye ndiye
Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme,
Mtakatifu, ....
Luke 4:34“Una nini nasi, wewe
Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni
Mtakatifu wa Mungu!”