Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,288
- 5,762
Ukifuatilia historia yako...Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaid ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mktisto mama yangu ndiyo muislam, bahat mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielew kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasabu dini ya kiislam naijua nimesama madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zaman nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.
Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipend kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumban na natumia maji ya baraka wakat mwingi nahis kabisa yananisaidia, halaf nikiwa kanisani nina aman zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubir ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumban redio nasikiliza redio maria tu na naifurahia.
Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sahiv ndiyo nazid kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu nataman waanze mafundisho, au kuna sehem sijielewi?
Umezaliwa kwenye Familia ya Kiislam na kupata ile basic knowledge ya kusoma ( kama Nursery) ambapo kule ni mambo basic na pale ambapo ungetakiwa Usome Quran na kuelewa kilicho andikwa na kilichokusudiwa namaanishwa kuanzia umri wa miaka 13 hivi (ukiwa matured) ukawa umeenda kwenye Shule ya Kikatoliki
Ulipo kwenda sekondary ya wakatoliki, hapo ndio uliweza kupata Mafundisho ya Dini (Kikatoliki) ambapo ukawa ndio mwanzo wako wa kupata mafundisho ya Dini kwa undani na kuelewa kwani pale umekua (matured). Nimeandika hivyo ili ujue kuwa, hakuna kitu cha ajabu sana hapo.
Kwa mtu mwenye hekima nilitegemea uulize kuwa; nimepata mafundisho ya kikatoliki shuleni na natamani Kusoma Elimu ya Kiislam tofauti na ile ya Chekechea ya Kufundishwa/ku kremu kusoma na kuandika; namaanisha mwanafunzi wa Chekechea hawezi kujisifia eti na yeye ameelimika kisa tu amejua kusoma na kuandika
Kwa kufanya hivyo ungeweza kusoma indetail sio ile ya kukremu hata mimi nilisoma hiyo pia ila baadae nikajiona nilipata pengine kama 6% ya nilichotakiwa kujua; baada ya hapo ungeweza kufanya uamuzi sahihi
KWA ELIMU YAKO YA UISLAM LEVO YA CHEKECHEA USIJIWEKE KWENYE KUNDI LA WATU WANAOJUA UISLAM; SOMA!